Na
Waandishi wetu, Arusha
Mamia ya watalii kutoka Israel waendelea kuja
nchini kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii licha ya changamoto ya Ugonjwa
wa UVIKO-19 ambao umeikumba dunia hivi sasa.
Kuja kwa watalii hao kunatokana na sio tu Tanzania
kubarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, bali pia hatua za tahadhali
zinachokuliwa na Serikali dhidi ya maambukizi ya virusi vya UVIKO-19.
Hatua hizo ambazo zimewejengea imani watalii kuendelea
kuja nchini zimetambuliwa na Baraza la Wasafiri na Utalii Duniani (World Travels
and Tourism Council-WTTC) ambapo Mwezi Agosti 2020 baraza hilo liliitangaza
Tanzania kuwa nchi salama ya kuitembelea.
Akizungumza Jijini Arusha, wakati wa hafla ya
kuwapokea watalii takribani 100 kutoka Israel na wengine 150 waliokuwa
wanaagwa, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemedi Mgaza amesema ujio wa
watalii hao umetokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Nje, kupitia
Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na wadau wengine wa utalii za kutangaza
vivutio vya utalii nchini humo.
Juhudi hizo ni pamoja na kushiriki maonesho ya
utalii yanayofanyika kila mwaka nchini Israel ambapo kwa mwaka huu yamepangwa
kufanyika mwezi Oktoba, kushiriki katika vyombo vya habari mbalimbali nchini
humo pamoja na kuwatumia mawakala wa utalii, kampuni za kuongoza watalii na
waandishi wa habari.
Mmoja wa watalii waliokuwa wanaagwa leo, Bw. Lior
Ziegler aliwahakikishia Watanzania kuwa Watalii kutoka Israel wataendelea kuja nchini
kwa sababu Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii, huduma bora
ikiwemo na mapokezi mazuri ya kuridhisha.
“Nimefurahia kutalii katika vivutio mbalimbali vya
utalii hapa Tanzania kwa kweli ni vizuri sana…..nitaendelea kuhamasisha
Waisrael kuja kutembea hapa na kujionea wenyewe vivutio hivyo adhimu,” Amesema
Bw. Ziegler
Kauli hiyo imeungwa mkono na Afisa Masoko Mkuu wa Mamlaka
ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Bw. Michael Makombe ambapo alieleza kuwa
watalii hao wamevutiwa na Bonde la Ngorongoro kutokana na mazingira yake ya
upekee, wanyama kuonekana kwa urahisi pamoja na historia ya Olduvai Gorge
ambapo ni eneo linaloaminika kuwa fuvu la mtu wa kale zaidi duniani limegunduliwa.
Kwa upande wa Kaimu Meneja Uhusiano wa Bodi ya
Utalii Tanzania (TTB), Bi. Christina Kamuzola amesema TTB kwa kushirikiana na
Serikali na wadau kutoka sekta binafsi itaongeza juhudi za kutangaza vivutio
vya utalii ili kufikia malengo ya Serikali ya kuleta watalii milioni tano na
mapato ya Dola za Marekani bilioni 600 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025 kama
ilivyoainishwa katika Ilani ya CCM ya
2020-2025.
Juhudi hizi ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa Tarehe 27
Julai, 2021 akiwaapisha mabalozi wapya 13 na kuwaagiza pamoja na mambo mengine,
kutangaza vivutio vya utalii, fursa za kiuchumi pamoja na uwekezaji
zinazopatikana nchini.
Baadhi ya watalii kutoka Israel wakipita kuangalia
kikundi cha utamaduni kutoka kabila la Wamasai katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kabla ya kuondoka kurejea Israel
Baadhi ya watalii kutoka Israel wakipita kuangalia
kikundi cha utamaduni kutoka kabila la Wamasai katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kabla ya kuondoka kurejea Israel
Baadhi ya watalii kutoka Israel wakipita kuangalia
kikundi cha utamaduni kutoka kabila la Wamasai katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kabla ya kuondoka kurejea Israel
Baadhi ya watalii kutoka Israel wakipita kuangalia
kikundi cha utamaduni kutoka kabila la Wamasai katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kabla ya kuondoka kurejea Israel
Baadhi ya watalii kutoka Israel wakiwa katika eneo
la kuondokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kabla ya
kuondoka kurejea Israel
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemedi Mgaza
akiongea na waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA) baada ya watalii kuondoka kuelekea Israel
|
Kaimu Meneja Uhusiano
wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi. Christina Kamuzola akiongea na waandishi
wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) baada ya
watalii kuondoka kuelekea Israel |
Afisa Masoko Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la
Ngorongoro, Bw. Michael Makombe akiongea na waandishi wa habari katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) baada ya watalii kuondoka kuelekea
Israel