Mazungumzo yakiendelea |
Thursday, September 9, 2021
UINGEREZA IMEIPONGEZA TANZANIA KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA, UWEKEZAJI, HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Wednesday, September 8, 2021
Monday, September 6, 2021
SERIKALI YAAINISHA VIPAUMBELE SEKTA YA AFYA
Na Mwandishi Wetu, Dar
Serikali imeainisha vipaumbele vitakavyonufaika na mradi wa sekta ya
afya kwa kipindi cha miaka mitatu kwa ufadhili wa Serikali ya Italia.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee Prof. Abel Makubi amevitaja hivyo alipokutana na madaktari kutoka Italia leo Jijini Dar es Salaam ambavyo ni mafunzo kwa wataalamu wa afya katika hospitali za mkoa, kanda na Taifa kwa ujumla, kununua vifaa vya matibabu vya kisasa, kujenga na kukarabati hospitali za kanda na taifa.
“Vipaumbele vingine ni kuanzisha na kuendeleza ushirikiano katika sekta
ya afya kati ya Tanzania na Italia, kuimarisha mifumo ya maabara katika
hospitali na kuendelea kupambana na ugonjwa wa Uviko 19 ikiwa ni pamoja na
kuelimisha umuhimu wa chanjo” amesema Prof. Makubi.
Kwa upande wake Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Marco Lombardi amelipongeza
Shirika la Maendeleo la Italia kwa kutenga Euro 1,250,000 za msaada wenye
manufaa kwa sekta ya afya nchini.
“Ushirikiano baina ya Tanzania na Italia ni wa muda mrefu na imara,
naomba nikuhakikishie kuwa Italia itaendelea kushirikiana na Serikali ya
Tanzania katika sekta ya afya pamoja na sekta nyingine kwa maslahi ya pande
zote mbili na kwetu sisi kama Italia huu ni mwanzo na tunaamini kuwa kupitia
mradi huu uhusiano wetu utaendelea kuimarika zaidi,” amesema Balozi Lombardi.
Nae Dkt. Davide Bonechi, Daktari kutoka Kituo cha Taifa la Italia cha
Afya Duniani amesema kuwa kupitia mpango wao wa kuboresha na kuimarisha sekta
ya afya katika ukanda wa Afrika, mbali na Tanzania nchi nyingine zitakazo nufaika
na mpango huo ni Kenya na Uganda.
“Lengo letu ni kuboresha sekta ya afya kwa ujumla pamoja na kuwaongezea
uwezo wataalamu wa afya ili waweze kukabiliana na magonjwa mbalimbali
yanayowapata binadamu,” amesema Dkt. Bonechi
Tarehe 3 September ujumbe wa wataalam wa afya kutoka nchini Italia uliwasili
Tanzania kwa ziara maalum ya kutathmini na kufahamu mahitaji na vipaumbele vya Tanzania
katika ya afya kwa hospitali zilizopo nchini.
Ujumbe wa wataalam wa afya kutoka nchini Italia unaongozwa na Dkt.
Davide Bonechi, Dkt. Giulia Dagliana, pamoja na Dkt. Beatrice Borchi, wote
wakitoka katika Kituo cha Taifa la Italia cha Afya Duniani.
Tanzania imekuwa
ikishirikiana na Italia katika miradi mbalimbali ya afya hapa nchini ambapo ushirikiano
rasmi katika sekta ya afya ulianza mwaka 1968 kupitia Shirika la Madaktari wa
Italia-CUAMM-Doctors with Africa. Kuanzia wakati huo, Serikali ya Italia
imekuwa ikifadhili miradi mbalimbali ya afya hapa nchini kama vile miradi ya kupambana na utapiamlo, afya ya watoto wachanga, afya ya
uzazi na kupunguza maambizi ya virusi vya ukimwi.
Serikali ya Tanzania imekuwa
ikipokea madaktari wa binadamu na wataalamu wa dawa za binadamu kutoka Italia
ikiwa ni sehemu ya ushirikiano wa kutoa huduma za matibabu.
Balozi wa Italia nchini,
Mhe. Marco Lombardi (kushoto) akielezea jambo katika kikao cha Katibu Mkuu
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi
kilichofanyika Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara
ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi (kulia) akiwaelezea
vipaumbele vya Serikali sekta ya afya madaktari kutoka Italia. Madaktari hao
wameambatana na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi.
Mmoja kati ya
madaktari kutoka Italia akieleza jambo wakati wa kikao
Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao
Kikao kikiendelea
Friday, September 3, 2021
TANZANIA, UFARANSA NI UJUMBE WA UTULIVU NA AMANI DUNIANI
Na Mwandishi wetu, Dar
Tanzania
na Ufaransa zimetajwa kuwa ni ujumbe wa utulivu, amani na maendeleo duniani na
kwamba tukio la hivi karibuni katika ubalozi huo halikuathiri kwa namna yeyote
mahusiano baina ya Nchi hizo.
Balozi
wa Ufaransa hapa nchini mhe. Frederic Clavier ameyasema hayo Jijini Dar es
Salaam alipokutana kwa mazungumzo pamoja na kumuaga Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) baada ya kumaliza
muda wake wa uwakilishi hapa nchini na kuongeza kuwa katika kipindi chote cha
utumishi wake ameiona Tanzania kuwa ni ujumbe wa utulivu,amani na maendeleo kwa
Bara la Afrika na duniani kwa ujumla.
“Katika
kipindi chote cha uwakilishi wangu hapa Tanzania, nimeiona Tanzania kuwa ni
ujumbe wa utulivu, amani na maendeleo kwa Bara la Afrika na duniani kwa ujumla,”
Amesema Balozi Clavier.
Balozi
Clavier ameongeza kuwa ushirikiano kati ya Ufaransa na Tanzania katika nyanja
mbalimbali za maendeleo ikiwemo elimu, afya, miundombinu biashara na uwekezaji
umeendelea kukua kwa kiwango kikubwa na kwamba Ufaransa itaendela kukuza
mahusiano hayo ya kihistoria baina ya nchi hizo mbili.
Ameongeza
kuwa Ufaransa itaendelea kutoa kipaumbele katika kuendeleza uchumi wa buluu
ambao kwa sasa umewekewa mikakati mahususi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kama chanzo kipya cha kuongeza mapato ya serikali lakini pia kupunguza
umasikini kwa Watanzania wote na kwamba anaporejea Ufaransa atahamasisha
makampuni, wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Ufaransa kuja
kuwekeza Tanzania.
Kwa
upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula (Mb) amemshukuru Balozi Frederic Clavier kwa kuimarisha na
kuendeleza mahusiano baina ya Tanzania na Ufaransa.
Balozi
Mulamula amempa pole Balozi huyo kwa tukio la kihalifu lililotokea hivi
karibuni katika Ubalozi wa Ufaransa na kumhakikishia kuwa licha ya tukio hilo
ambalo lilidhibitiwa na vyombo vya dola,Tanzania ni salama.
Balozi
wa Ufaransa aliyemaliza muda wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Frederic Clavier
akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Maongezi
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula na Balozi wa Ufaransa aliyemaliza muda wa uwakilishi hapa
nchini, Mhe. Frederic Clavier yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini
Dar es Salaam
Maongezi
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula na Balozi wa Ufaransa aliyemaliza muda wa uwakilishi hapa
nchini, Mhe. Frederic Clavier yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini
Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula
(Mb) akitoa zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro kwa Balozi wa Ufaransa
aliyemaliza muda wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Frederic Clavier
Wednesday, September 1, 2021
BALOZI SOKOINE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CANADA NCHINI
Umoja wa Mataifa umetangaza nafasi ya kazi ya Katibu Mkuu Msaidizi atakayeshughulikia masuala ya Amani (Assistant Secretary General for Peacebuilding Support). Fursa hii iko wazi kwa nchi wanachama wote wa Umoja wa Mataifa.
Tuesday, August 31, 2021
UYOGA WA TANZANIA KUPATA SOKO NCHINI UHOLANZI
| ||
Balozi Irene Kasyanju (kulia) akiangalia namna uyoga unavyofungashwa kwenye
makasha (packaging) tayari kwa kupelekwa sokoni huku akipatiwa maelezo ya mchakato
mzima wa ufungaji kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa LIMAX Group, Bw. Rob
Menheere (kushoto). Katikati ni Bw. Petro Mahuwi “intern” Mtanzania aliyeongozana
na Balozi Kasyanju kwenye ziara hiyo. |
Namna kitalu kimoja wapo cha uyoga uliopandwa na ambao unakaribia kuvunwa kinavyoonekana katika moja ya mashamba makubwa 4 ya LIMAX Group iliyoko Horst, Uholanzi. |
Balozi Kasyanju (kushoto) akiwa na Mkurugenzi na Mmiliki wa LIMAX Group,
Bw. Tom van WALSEM (wa kwanza kushoto); Mkurugenzi Mwendeshaji, Bw. Rob
Menheere (wa pili kushoto); na Meneja Biashara, Bw. Mark Duppen (wa tatu
kushoto) wakikamilisha mazungumzo yao baada ya zoezi la kutembelea mashamba ya uyoga
mjini Horst, Uholanzi kukamilika. ---------------------------- UYOGA WA TANZANIA KUPATA SOKO NCHINI UHOLANZI Kampuni maarufu
ya Uholanzi, LIMAX B.V. (LimaxGroup) imedhamiria kuwekeza kwenye Sekta ya Uyoga
nchini Tanzania kwa kujenga kiwanda cha kusindika na kukausha uyoga Mkoani
Iringa kwa thamani ya Euro milioni 2.1 ambazo ni sawa na Shilingi Bilioni 5.5
za Tanzania. Hayo yameelezwa kufuatia Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe.
Irene Kasyanju kutembelea kampuni hiyo tarehe 26 Agosti 2021 na kufanya
mazungumzo na Mkurugenzi na Mmiliki wa kampuni hiyo, Bw. Tom VanWalsem. Balozi Kasyanju alieleza kuwa uwekezaji huo utakapokamilika, Tanzania itafaidika kwa kiasi kikubwa kutokana na mtiririko wa biashara ya uyoga kukua kwa kasi duniani ambapo kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), biashara hiyo inakadiriwa kuongezeka hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 62.2 ifikapo mwaka 2023 kutoka Dola za Marekani bilioni 42.4 mwaka 2018.
Balozi Kasyanju akiwa katika kampuni hiyo alipata fursa ya kujionea mashamba ya kisasa ya uyoga unaozalishwa (sio wa asili) na namna zao hilo lenye faida kubwa kwa binadamu linavyosindikwa na kufungashwa (processed and packed) na kuelezea matumaini yake kuwa Tanzania itafaidika na uwezo, uzoefu na utaalam mkubwa wa biashara wa Kampuni hiyo. “Tanzania ni nchi yenye maeneo makubwa ya misitu yenye aina anuwai ya uyoga wa porini kwa ajili ya kula, na jamii zimekuwa zinategemea maarifa asilia kukusanya uyoga huo kwa matumizi na kuuza katika masoko ya ndani tu. Ni wakati muafaka sasa kufanya kazi pamoja kukuza ukuaji wa sekta hii kibiashara”., Balozi Kasyanju alisema. LIMAXGroup itatoa mafunzo ya kuhifadhi na kuvuna uyoga wa
porini kwa madhumuni ya biashara na kulinda mazingira pia. Aidha, ujenzi wa
kiwanda hicho mkoani Iringa kutawawezesha wakulima kuuza uyoga wanaozalisha moja
kwa moja kiwandani, kuongeza ajira kwa Watanzania na kukuza mnyororo wa thamani
wa kilimo cha uyoga nchini. |
Saturday, August 28, 2021
BALOZI LIBERATA MULAMULA KATIKA KIKAO KAZI NA MAAFISA WA UBALOZI WA KUDUMU KATIKA UMOJA WA MATAIFA - NEW YORK, MAREKANI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika kikao kazi na watumishi wa Uwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa New York,Marekani(hawapo pichani) |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika kikao kazi na watumishi wa Uwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa New York,Marekani; kushoto kwa Balozi Mulamula ni Balozi wa Tanzania katika umoja wa Mataifa Balozi Kennedy Gastorn. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika kikao kazi na watumishi wa Uwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa New York,Marekani |
Baadhi ya Maafisa katika Ubalozi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa New York,Marekani wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) |
BALOZI MULAMULA AKIZUNGUMZA NA MHE. FLEMMING MOLLER MORTNSEN KWA NJIA YA MTANDAO KUHUSU UAMUZI WA KUFUNGA SHUGHULI ZA UBALOZI WA DENMARK
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza kwa nia ya mtandao (video conferencing) na Waziri Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Flemming Moller Mortensen kuhusu hamuzi wa Denmark kufunga shughuli za Ubalozi wake Nchini Tanzania |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza kwa njia ya mtandao (video conferencing) na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Flemming Moller Mortensen kuhusu uamuzi wa Denmark kufunga shughuli za Ubalozi wake Nchini Tanzania |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Swahiba Mndeme (kushoto kwa Balozi Mulamula) pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bi. Jean Msabila wakati wa mazungumzo kwa njia ya mtandao na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Flemming Moller Mortensen kuhusu uamuzi wa Denmark kufunga shughuli za Ubalozi wake Nchini Tanzania |
Friday, August 27, 2021
BALOZI SOKOINE AKUTANA NA BALOZI WA INDIA, ALGERIA NA SWEDEN
Na Mwandishi wetu, Dar
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Balozi Sokoine amekutana kwa nyakati tofauti na mabalozi hao ambao ni Balozi wa India hapa nchini Mhe. Binaya Pradhan, Balozi wa Algeria hapa nchini Mhe. Ahmed Djellal pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Anders Sjöberg.
Pamoja na Mambo mengine viongozi hao wamejadili masuala ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ulipo baina ya Tanzania na mataifa hayo ambapo awali Balozi wa India Mhe. Pradhan ameahidi kuendeleza na kudumisha uhusiano mzuri uliopo baina ya India na Tanzania.
“Nimemhakikishia Katibu
Mkuu, Mheshimiwa Balozi Sokoine kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia uliopo
baina ya mataifa yetu kwa maslahi ya pande zote mbili katika sekta mbalimbali
ikiwemo Utalii, elimu, gesi, biashara na uwekezaji,” amesema Balozi Pradhan
Kwa upande wake, Balozi wa Algeria hapa nchini, Mhe. Djellal amesema kuwa mazungumzo yao yaligusia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Algeria na Tanzania.
“Tumekubaliana kuendelea
kuimarisha diplomasia baina ya mataifa yetu kwa maslahi mapana……….na kwa
maendeleo ya wananchi wetu,” amesema Balozi Djellal
Nae balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Sjöberg amesema katika jitihada za kuendeleza uhusiano wa Sweden na Tanzania, Sweden itaendelea kushirikiana na Tanzania kuendeleza sekta mbalimbali kwa manufaa ya pande zote mbili.
Kwa upande wake, Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Sokoine
amewahakikishia mabalozi hao ushirikiano wa kutosha kutoka Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiongea
na Balozi wa India hapa nchini Mhe. Binaya Pradhan katika Ofisi Ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Algeria hapa
nchini Mhe. Ahmed Djellal akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi Ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Sweden nchini
Mhe. Anders Sjöberg akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine katika Ofisi Ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam