Na Mwandishi Wetu, Dar
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeipiga msasa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) kwa kuipatia mafunzo maalumu
yenye malengo mbalimbali hasa katika kutetea maslahi ya Taifa.
Pamoja
na mambo mengine, mafunzo hayo pia yatajikita
katika masuala ya Itifaki, mawasiliano ya Kidiplomasia, usalama wa
Kimtandao na Diplomasia ya Uchumi ili
kuwajengea uwezo wabunge wa kamati hiyo katika kutekeleza majukumu yao ya
Kamati na Bunge kikamilifu.
Akifungua mafunzo
hayo ya siku tano Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema kuwa kupitia mafunzo
hayo kamati itapata ujuzi juu ya masuala mbalimbali yanayohusu Kamati maslahi
ya Taifa, masuala ya Itifaki, mawasiliano ya Kidiplomasia, usalama wa Kimtandao
na Diplomasia ya Uchumi ili kuwajengea
uwezo katika kutekeleza majukumu yenu ya Kamati na Bunge kikamilifu.
“Ninayo furaha
kuwajulisha kuwa mtapata fursa ya kuelimishwa juu ya mambo Uchumi wa Buluu,
mada itakayotolewa na Wizara yenye dhamana ya usimamizi wa uchumi wa buluu
kutoka Zanzibar ambayo imepiga hatua katika utekelezaji wake,” Amesema Balozi
Mulamula.
Balozi Mulamula
ameongeza kuwa, Wizara inaamini kuwa wajumbe wa Kamati na washiriki wote wa
mafunzo wataendelea kutumia ujuzi watakaoupata kuishauri Wizara na kuwa
Mabalozi wazuri ndani na nje ya Bunge katika kulinda taswira ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
“Niihakikishie
Kamati kuwa Wizara itaendelea kushirikiana nanyi kikamilifu hasa katika kipindi
hiki tunapoandaa Sera yetu ya Mambo ya Nje. Tunaamini kuwa ushiriki wenu
utaiwezesha nchi yetu kuwa wa sera iliyosheheni masuala muhimu yatakayoiwezesha
nchi kunufaika,” ameongeza Balozi Mulamula
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
(NUU) Bw. Mussa Zungu amesema kamati anayoiongoza inafanya kazi kuwa kwa maslahi
mapana ya nchi na kuahidi kuwa vichocheo vya maslahi ya nchi vinalindwa kwa
maslahi mapana ya nchi.
“Kamati inatoa
ushauri ‘cross-cutting’ kwa maana inagusa kila eneo kwa taifa letu, jambo
lolote lile linalohusiana na masuala ya foreign huwa tunashauri, mambo ya
ulinzi na usalama…..kwa hiyo inatoa mambo yak echini kwa chini kwa malengo ya
kuisaidia serikali,” Amesema Bw. Zungu
Mafunzo haya muhimu
kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
(NUU) yameandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
kwa kushirikiana na Chuo cha Diplomasia na yatafanyika kuanzia tarehe 13 – 17
Septemba 2021 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akijadili
jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama (NUU) Bw. Mussa Zungu (Mb) Jijini Dar es Salaam
|
Sehemu
ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
(NUU) wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Liberata Mulamula (Mb) hayupo pichani |
Mkurugenzi wa Idara
ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Bibi. Agnela Nyoni akitoa hotuba kabla ya kumkaribisha Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kuongea
na wajumbe wa Kamati ya NUU
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwasilisha
hotuba ya ufunguzi wa mafunzo maalum ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha
ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
(NUU) Jijini Dar es Salaam