Na Mwandishi wetu, Roma
Jukwaa
la kwanza la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Italia limefanyika
Jijini Roma kwa mafanikio makubwa, Italia na kuwakutanisha wafanyabiashara na
wawekezaji zaidi ya 250 kutoka nchi zote mbili hasa katika kipindi hiki cha
Uviko 19.
Pamoja
na mambo mengine, jukwaa hilo limewawezesha wafanyabiashara na wawekezaji
kujadili fursa, uwezekano wa ubia, changamoto zinazokabili mazingira ya
biashara na njia ya kuboresha mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na
Italia ambapo limendaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kwa kushirikiana
na Kituo cha Taifa cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Taifa ya
Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).
Ujumbe
wa Tanzania umeongozwa na Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya ambapo
Prof. Manya amewaeleza wawekezaji na wfanyabiashara kutoka Italia kuwa Tanzania
kwa sasa imejikita kuwekeza katika miundombinu wezeshi ya uwekezaji, na kwamba
hilo ndilo jambo ambalo Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mhe.
Rais Samia ameliweka suala la uwekezaji kama
kipaumbele katika kuhakikisha kuwa wawekezaji kutoka nje na ndani ya nchi
wanawekeza fedha na mitaji yao ili kukuza biashara na ajira kwa watanzania na
kuwezesha uchumi wa Tanzania kusonga mbele
“Tanzania
inathamini uwekezaji na sasa inapiga hatua kwa kuweka miundombinu wezeshi pia
Tanzania kama nchi tunamshukuru Mungu kwamba lengo la njozi yetu na maono yetu
ya Tanzania Development Vision (2020-2025) imeweza kufikia malengo yake miaka mitano
kabla muda uliokuwa umepangwa. Ambapo lengo kubwa lilikuwa ni kuifanya Tanzania
kwenda katika viwango vikubwa vya kiuchumi na mwaka 2020 Tanzania ilitangazwa
na Benki ya Dunia kuingia katika Uchumi wa kati,” amesema Prof. Manya.
Kadhalika,
Prof. Manya ameongeza kuwa katika miaka mitano inayokuja Tanzania inapoelekea
kumaliza njozi yake, inatamani kuendelea kukuza uchumi na ikiwezekana ihame
katika uchumi wa kati na kuhamia uchumi wa juu……na ndiyo maana imejikita
kuwekeza katika miundombinu ya reli ya kati itakayotumika kusafirisha mizigo
kwa umeme, ujenzi wa bwawa kubwa linaloweza kuzalisha umeme wa kutosha pamoja
na barabara za kusafiri kutoka mashariki kwenda magharibi na kaskazini kwenda
kusini.
Ameongeza
kuwa Tanzania inajivunia kuwa na hali ya amani na utulivu na katika nchi za
ukanda wa maziwa makuu Tanzania inajivunia kuwa na siasa safi yenye utulivu na
amani ndani yake.
“Mfano
tumeona mwekezaji aliyewekeza katika kilimo cha Pareto ameshuhudia kwa kusema
kuwa Tanzania ni nchi ya amani na utlivu na kuwasihi Waitaliano kuja kuwekeza
Tanzania,” ameongeza Prof. Manya.
Kupitia
jukwaa hili, tunaamini kuwa litachagiza chachu ya uwekezaji zaidi nchini
Tanzania na kukuza biashara kati ya Tanzania na Italia.
Mwitikio
ni mkubwa na wameonesha utayari wa kuja kuwekeza zaidi Tanzania pamoja na
kukuza biashara miongoni mwetu na tumewahahakikishia kuwa Tanzania ni sehemu
salama na yenye mazingira mazuri ya Uwekezaji na wameahidi kuwekeza zaidi
Tanzania.
Nae
Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo amesema kuwa
kufanyika kwa Jukwaa la biashara na uwekezaji lengo lake kubwa ni kuwavutia
wafanyabiashara na wewekezaji wa sekta mbalimbali kutoka Italia kuwekeza zaidi
Tanzania ili kukuza uchumi wa pande zote mbili.
“Mwitikio
ni mkubwa sana na tumeitikiwa na Serikali ya Italia vizuri sana pamoja na
jumuiya za Italia za kibishara na pia kwa upande wa Tanzania pia mwitikio ni
mkubwa pia,” amesema Balozi Kombo.
Mwenyekiti
wa Chama Wawekezaji wa Hoteli Zanzibar, Bw. Paulo Rosso amewasihi wawekezaji
kutoka Italia kuwekeza kwa wingi Tanzania kwa kuwa mazingira ya biashara na
uwekezaji ni tulivu na salama.
“Tanzania
ni sehemu salama kuwekeza, ni nchi ya amani, tulivu kwa uwekezaji, karibuni
sana kuwekeza Tanzania,” amesema Bw. Rosso
Katika
Jukwaa hilo, Kampuni mbalimbali za Kiitaliano zimeonesha nia ya kuwekeza
Tanzania ambazo ni pamoja na Kampuni ya utengenezaji Magari Ferari ambayo
imeonesha utayari wa kuwekeza katika Gereji nchini Tanzania na Shirikisho la Uwekezaji
katika Uchumi wa Buluu kutoka Italia pia limeonesha nia ya kuwekeza Tanzania.
|
Naibu
Waziri, Wizara ya Madini Prof. Shukrani Manya akihutubia Jukwaa la biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na Italia Jijini Roma. Jukwa hilo limefanyika tarehe
2 na 3 Disema 2021 |
|
Balozi
wa Tanzania Nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabiti Kombo akiongea na
wafanyabiashara waliojitokeza kushiriki Jukwaa la biashara na uwekezaji kati ya
Tanzania na Italia lililofanyika Jijini Roma |
|
Sehemu
ya Wafanyabiashara na Wawekezaji walishiriki katika Jukwaa la biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na Italia lililofanyika Jijini Roma |