Tuesday, September 6, 2022

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NORWAY AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU TATU

Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim amewasili nchini leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 6 - 8 Septemba 2022 na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Akiwa nchini Mhe. Tvinnereim kwa nyakati tofauti, atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jaffo na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde.

Aidha, Mhe. Tvinereim pia anataraji kutembelea miradi ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF)  pamoja na Mji wa Serikali (Mtumba) Jijini Dodoma ili kujionea maendeleo ya miradi  sambamba na mikakati ya Serikali katika kufanikisha miradi hiyo. 

Tanzania na Norway zinashirikiana katika sekta za elimu, afya, kilimo, uwekezaji, miundombinu, nishati, madini, tehama, utafiti, maboresho kwenye mifumo ya ukusanyaji wa kodi, uchangiaji wa bajeti kuu ya Serikali, misitu, demokrasia, haki za binadamu, usawa wa jinsia, utunzaji wa mazingira na ukuzaji wa sekta ya biashara. 

Maeneo mengine mtambuka ya ushirikiano ni pamoja na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, utawala bora, usimamizi wa migogoro, amani na ulinzi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimpokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim alipowasili nchini leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 6 - 8 Septemba 2022
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam 



TANZANIA, NORWAY KUSHIRIKIANA KUIMARISHA UCHUMI


Serikali za Tanzania na Norway zimesisitiza kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo ili kukuza uchumi.

Msisitizo huo umetolewa wakati wa mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb.) na Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim walipokutana tarehe 06 Septemba 2022 katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar es Salaam.

Nchi hizo zinashirikiana katika masuala ya elimu, afya, kilimo, uwekezaji, miundombinu, nishati, madini, tehama, utafiti, maboresho kwenye mifumo ya ukusanyaji wa kodi, uchangiaji wa bajeti kuu ya Serikali, misitu, demokrasia, haki za binadamu, usawa wa jinsia, utunzaji wa mazingira na ukuzaji wa sekta ya biashara.

Balozi Mulamula alieleza kuwa Tanzania inathamini ushirikiano uliopo baina yake na Norway kwa kusimamia miradi ya maendeleo iliyo kwenye makubaliano na kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano kwa lengo la kujenga uchumi wa Wananchi.

“Norway ni mshirika wa maendeleo wa Tanzania wa muda mrefu na imesaidia kujenga uwezo katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji ikiwemo uboreshaji wa mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara, usimamizi wa mfumo wa ulipaji kodi,” alisema Balozi Mulamuala.

Kadhalika, Serikali ya Norway imeongeza muda wa miaka mitano ya utekelezaji wa makubaliano ya majadiliano ya kisiasa yaliyoingiwa kati yake na Tanzania yanaendelea ili kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya kipaumbele ya Serikali ya awamu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Doroth Gwajima alieleza kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na Norway katika utekelezaji wa pendekezo la mpango wa miaka mitano wa kujenga usawa na uwezo kwa wanawake, vijana na makundi maalum unaotegemewa kuinua uchumi na kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri katika kazi rasmi. 

Mpango huo pia umezingatia umuhimu wa afya ya uzazi kuwa agenda muhimu ili kuyafikia Malengo ya Mpango wa Maendeleo Endelevu.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Antony Mavunde alieleza kuwa kupitia sekta ya kilimo Tanzania inayo nia ya kushirikiana na Norway katika masuala ya kujenga uwezo katika vyuo vya kilimo na taasisi zake ili kuwezesha tafiti za sekta hiyo kwa lengo la kuinua uwezo binafsi wa kuzalisha mbegu za mazao, kusimamia usalama wa chakula nchini, kujenga mabwawa na kuimarisha miradi ya umwagiliaji.

Maeneo mengine ya ushirikiano ni pamoja na upatikanaji wa mbolea kwa gharama nafuu, uimarishaji na ujenzi wa miundominu ya kilimo ili kujenga uwezo wa kuzalisha kwa mwaka mzima badala ya kusubiri msimu wa mvua kama ilivyosasa.

Vilevile Wizara ya Kilimo imeandaa mpango wa miradi ya kilimo kwa Wanawake na Vijana itakayotekelezwa katika mikoa ya Mbeya na Dodoma ambapo mradi huo utatumia jumla ya ekari 69 hivyo, kupitia ushirikiano uliopo Tanzania ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na Norway ili kuyafikia malengo ya uzalishaji yaliyowekwa katika kufanya kilimo cha biashara na kulifikia soko la kimataifa.

Naye Mhe. Tvinnereim ameeleza kuwa Norway imejenga uwezo mkubwa katika masuala ya uzalishaji wa mbegu hivyo itaendelea kushirikiana na Tazania katika eneo hilo na maeneo mengine yaliyoelezwa na mawaziri walioshiriki mazungumzo hayo kwa lengo la kuondoa umasikini, kuongeza nafasi za ajira na kujenga uwezo wa kiuchumi kwa wananchi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Kushoto) akizungumza na ujumbe wa Norway ulioongozwa na Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Doroth Gwajima (Kushoto) akizungumza na ujumbe wa Norway ulioongozwa na Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim (Kulia) akizungumza na ujumbe wa Tanzania  ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Norway anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa na nchi za Nordic, Mhe. Anne Beathe Tvinnereim akipokea zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam





Monday, September 5, 2022

TANZANIA, VENEZUELA ZASAINI HATI ZA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

Serikali ya Tanzania na Serikali ya Venezuella zimesaini Hati za Makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kisiasa na mkataba wa ushirikiano katika nyanja mbalimbali baina ya nchi hizo. 

Makubaliano hayo yamesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.), pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Yuri Pimentel Moura katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

“Tumesaini mikataba miwili ambapo mmoja unalenga kuendeleza majadiliano ya kisiasa (political consultation) lakini pia makubaliano ya kuwa na ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo kichumi, nishati, afya, elimu na kilimo,” amesema Balozi Mulamula.

Kusainiwa kwa mikataba hiyo ni ishara ya kuimarika kwa uhusiano kati ya Tanzania na Venezuela katika sekta za nishati, afya, elimu na kilimo kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Yuri Pimentel Moura amesema kusainiwa kwa mikataba hiyo miwili ni hatua muhimu ya kudumisha na kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali baina ya Venezuela na Tanzania.

Mhe. Moura amewasili nchini leo akitokea Venezuela na atakuwepo nchini kwa siku mbili kwa ziara ya kikazi. 

Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana na kupokea barua za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Kenya mwenye makazi yake Arusha, Bw. Dennis Mburu katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupokea barua za utambulisho kutoka kwa Bw. Mburu Balozi Mulamula amemuahidi ushirikiano kutoka Serikalini wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala ya biashara na uwekezaji pamoja na utalii.  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Yuri Pimentel Moura katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika (kushoto), Balozi Swahiba Mndeme pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Balozi Mindi Kasiga (kulia) wote kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao cha Mhe. Balozi Mulamula na Mhe. Moura katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Yuri Pimentel Moura kwa pamoja wakisaini Hati za Makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kisiasa na mkataba wa ushirikiano katika nyanja mbalimbali baina ya nchi hizo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Utiaji saini Hati hizo umeshuhudiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wengine ni  Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Swahiba Mndeme, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga wote kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea barua za utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Kenya mwenye makazi yake Arusha, Bw. Dennis Mburu katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Konseli Mkuu wa Kenya mwenye makazi yake Arusha, Bw. Dennis Mburu. wengine pichani niMkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga na Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Ubalozi wa Kenya nchini katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.



Sunday, September 4, 2022

WAJUUMBE WA KAMATI YA NUU WATEMBELEA MIRADI YA KIKANDA YA EAC



Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala, Mhandisi Steven Mlote akiongea jambo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) ilipotembelea Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mshariki jijini Arusha kabla ya kuanza kutembelea miradi ya miundombinu ya EAC inayotekelezwa mkoani humo. Mwingine katika picha ni Mwenyekiti wa Kamati ya NUU, Mhe. Vita R. Kawawa

Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC kwa wajumbe wa Kamati ya NUU jijini Arusha.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakifuatilia kwa makini mada kuhusu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakifuatilia kwa makini mada kuhusu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota.

Mwenyekiti wa Kamati ya NUU, Mhe. Vita R. Kawawa akichangia hoja baada ya kuwasilishwa mada kuhusu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya NUU, Mhe. Vicent Mbogo akichangia hoja baada ya kuwasilishwa mada kuhusu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC

Mjumbe wa Kmati ya NUU, Mhe. Janeth Masaburi akichangia jambo kuhsu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC

Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati ya NUU na wajumbe wengine wakisikiliza mada kuhusu utekelezaji wa miradi ya kikanda ya miundombinu ya EAC

Wajumbe wa Kamati ya NUU wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Vita Kawawa wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala, Mhandisi Steven Mlote pamoja na watumishi wengine wa Serikali mbele ya Jengo la Makao Makuu ya EAC.

Mwenyekiti wa Kamati ya NUU, Mhe. Vita R. Kawawa akipokelewa na watumishi wa Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga, mara baada ya kuwasili na kamati yake katika kituo hicho kwa ajili ya kuangalia utendaji wa Kituo.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato wa Mkoa wa Arusha, Bw. Paul Kamukulu akifafanua jambo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga kwa wajumbe wa Kamati ya NUU walipotembelea kituo hicho tarehe 03 Septemba 2022.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Lungido, Bw. Kamana Juma Simba akitambulisha ujumbe wa Wilaya yake ulioshiriki katika ziara ya wajumbe wa Kamati ya NUU katika Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga

Meneja wa Mamlaka ya Mapato wa Mkoa wa Arusha, Bw. Paul Kamukulu akisoma taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga kwa wajumbe wa Kamati ya NUU
Afisa kutoka Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Bw. Imail Abdalla akifanya majumuisho ya ziara ya Kamati ya NUU katika miradi ya miundombinu ya EAC iliyofanyika kuanzia tarehe 02 hadi 04 Septemba 2022 

Wajumbe wa Kamati ya NUU wakisikiliza majumuisho ya ziara yao kutoka kwa Afisa kutoka Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Bw. Imail Abdalla

Mjumbe wa Kamati ya NUU, Bw. Cosato Chumi akijumuika na wajasiriamali wanaofanya biashara maeneo ya kuzunguka Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga



Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mahariki, Bw. Justin Kisoka akijumuika na wajasiriamali wanaofanya biashara maeneo ya kuzunguka Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Namanga

Picha ya pamoja






 

Friday, September 2, 2022

BALOZI MULAMULA AIHAKIKISHIA JUMUIYA YA KIMATAIFA UTAYARI WA TANZANIA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akiwa katika meza kuu wakati wa hafla ya ufungaji wa Mkutano  wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam . Mkutano huo uliandaliwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na Uingereza na kushirikisha wajumbe kutoka nchi 20 . 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifunga Mkutano  wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam. 

 

Bw. Matt Toombs kutoka Uingereza  akizungumza katika hafla ya ufungaji wa Mkutano  wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri wa Nchi Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) akimpa mkono wa pongezi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula baada ya kufunga Mkutano  wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akishukuru baada ya kufunga Mkutano  wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

 

Baadhi ya washiriki wa Mkutano  wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya ufungaji wa mkutano huo iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamulahayupo pichani


Baadhi ya washiriki wa Mkutano  wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya ufungaji wa mkutano huo iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamulahayupo pichani


 

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula ameihakikishia jumuiya ya Kimataifa utayari na ushiriki thabiti wa Tanzania katika jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

 

Balozi Mulamula ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga Mkutano  wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo ulioandaliwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na Uingereza na kushirikisha wajumbe kutoka nchi 20 .

 

“Tanzania iko tayari na itaendelea kuwa mshiriki thabiti wa jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, na niwahakikishie kwamba Tanzania ni muumini wa ushirikiano wa kimataifa katika kulinda na kuhifadhi mazingira kama nguzo kanuni na miongozo ya Umoja wa Mataifa inavyosema,” alisema Balozi Mulamula.

 

 

Balozi Mulamula pia amesema Tanzania ni muumini wa ushirikiano wa kimataifa kama nguzo ya kulinda mazingira sambamba na maadili na miongozo ya Umoja wa Mataifa inavyosema.

 

Ametumia nafasi hiyo kuwasihi wajumbe wa mkutano huo na mikutano mingine kama hiyo kuhakikisha wanakuwa na ajenda moja itakayosaidia harakati za dunia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi duniani.

 

Awali akitoa maelezo mafupi kuhusu mkutano huo Bw. Matt Toombs kutoka Uingereza alisema washiriki wa mkutano huo wamejadili maeneo mblimbali yanayohusiana na  utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi na kukublina kuendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuona namna ya kuweza kukbiliana na changamoto hiyo.

  

Mkutano huo wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Serikali ya Uingereza na kushirikisha zaidi ya nchi 20 duniani ulianza tarehe 1 Septemba na kufunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango


VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE COMMONWEALTH SECRETARIAT


 

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA IOM




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Bw. Maurizio Busatti ambaye alifika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Bw. Maurizio Busatti ambaye alifika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Bw. Maurizio Busatti ambaye alifika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Bw. Maurizio Busatti ambaye alifika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Bw. Maurizio Busatti ambaye alifika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.



mazungumzo yakiendelea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Bw. Maurizio Busatti na maafisa walioshiriki mazungumzo hayo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.

 

 

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kuzungumza na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) Bw. Maurizio Busatti ambaye amejitambulisha rasmi kwa Mhe. Waziri katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza katika kikao hicho Waziri Mulamula ameipongeza IOM kwa kazi inazofanya nchini na amemuhakikishia Bw. Busatti kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kufanya kazi na Shirika hilo.

 

Amesema Shirika hilo (IOM limekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala ya wakimbizi, majanga ya asili na kuongeza kuwa ni matumaini yake kwamba Bw. Busatti ataendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na IOM kwa kuzingatia uzoefu wa muda mrefu alionao kwa kufanya kazi kwa muda mrefu ndani ya shirika hilo.

 

 

Balozi Mulamula ameipongeza IOM kwa kuendelea na shughuli za kuwarejesha nyumbani rai awa Ethiopia waliokuwa katika magereza nchini na kuongeza kuwa kitendo hicho kimesaidia Tanzania kukabiliana na msongamano wa watu katika magereza yake.

 

Ameipongeza IOM na jitihada zake za kukijengea uwezo kituo cha mafunzo cha maafisa Uhamiaji Kanda ya Afrika kilichoko ndani ya Kituo cha mafunzo cha Maafisa Uhamiaji cha mjini Moshi ambapo pia maafisa uhamiaji wa Tanzania wananufaika nacho.

 

Naye Bw. Busatti ameishukuru Serikali kwa jinsi inavyoshirikiana na Shirika hilo katika kutekeleza majukumu yake hapa nchini.

 

Bw. Busattia ameahidi kuendeleza ushirikiano mzuri ambao shirika hilo umekuwa na Serikali ya Tanzania kwani imekuwa mdau wake mkubwa katika kufanikisha majukumu yake.

 

Thursday, September 1, 2022

BALOZI FATMA: WATUMISHI FANYENI KAZI KWA BIDII, USHIRIKIANO

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab amewasihi watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na kwa ushirikiano mkubwa ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake iliyojiwekea. 

Balozi Fatma ametoa maelekezo hayo wakati alipokutana na watumishi wa Ubalozi katika kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za ubalozi Jijini Doha, Qatar na kuwataka kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, weledi na uaminifu kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.

"Nawasihi kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano pamoja na kuwa wabunifu wa kuitangaza lugha ya Kiswahili, pamoja na Filamu ya Roya Tour, pamoja na vipaumbele vya Serikali hasa katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi," amesema Balozi Fatma.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Bi. Patricia Kiswaga amemhakikishia Balozi Fatma kuwa watafanya kazi kwa umoja, bidii, weledi na ubunifu kwa maslahi mapana ya Taifa.

Pamoja na mambo mengine, Bi. Kiswaga ameongeza kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar ni mzuri na unaendelea kuimarika kila wakati.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akizungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar katika kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za ubalozi huo Jijini Doha, Qatar 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akizungumza na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar katika kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za ubalozi huo Jijini Doha, Qatar