Monday, September 19, 2022

DKT. MPANGO KUMWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA UNGA77

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akiwasili katika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani alipowasili jijini humo kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA77).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani alipowasili jijini humo kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA77).


 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (wa kwanza kulia) na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania  Umoja wa Mataifa Mhe. Prof. Kennedy Gaston (katikati) alipowasili katika Ofisi za Ubalozi jijini New York kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA77).


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akizungumza na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA77) alipowasili katika Ofisi za Ubalozi jijini New York kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano huo
Baadhi ya  wajumbe wa timu ya Tanzania unaoshiriki Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA77) ukimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango alipowasili katika Ofisi za Ubalozi jijini New York kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano huo

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango amewasili Jijini New York nchini Marekani kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA77).

Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika Ukumbi wa Mikutano wa Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani tarehe 22 Septemba 2022.

Makamu wa Rais pia akiwa Jijini humo ataongoza Ujumbe wa Tanzania katika mikutano mbalimbali ya ngazi za juu na ya pembezoni inayohusu Uchumi, Elimu, Afya, Demokrasia na Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo imeandaliwa na Umoja wa Mataifa.

Mkutano huo wa UNGA wa 77 unatarajiwa kujadili masuala mbalimbali ya kimataifa ambayo yameikumba dunia kwa wakati huu kama vile mlipuko wa ugonjwa wa COVID 19, Vita ya Urusi na Ukraine, mabadiliko ya tabia nchi na athari zake katika uchumi wa dunia.

Katika mkutano huo, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.), Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Zanzibar Mhe. Masoud Ali Mohamed na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa

Friday, September 16, 2022

BALOZI SOKOINE AKUTANA NA BALOZI WA CUBA NCHINI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Joseph Sokoine afanya mazungumzo na Balozi wa Cuba hapa nchini, Mhe. Yordenis Despaigne walipokutana katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi Joseph Sokoine akiongea na Mhe. Yordenis Despaigne

Balozi Joseph Sokoine akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Yordenis Despaigne 

 

BALOZI MINDI ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA WANAWAKE WA AFRIKA KATIKA UONGOZI

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga ameelezea uzoefu wa Tanzania kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia na uongozi wakati akiwasilisha mada katika Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Afrika katika Uongozi (African Women in Leadership International Conference) unaoendelea jijini Durban, Afrika Kusini. 

Mkutano huo ambao umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 15-17 Septemba 2022, chini ya wenyeji wa kiongozi wa Jimbo la KwaZulu-Natal Bi. Nomusa Dube-Ncube, hufanyika kila mwaka kwa kuwaleta pamoja viongozi wanawake kutoka Bara la Afrika ili kujadili masuala yanayohusu usawa wa kijinsia na uongozi. 

Miongoni mwa waliohuduhuria mkutano huo ni pamoja na viongozi mashuhuri katika siasa, Sekali na makampuni binafsi kutoka nchini. Liberia, Nigeria, Tanzania, Cameroon, Rwanda, na wenyeji Afrika Kusini. 

Kongamano lijalo linatarajiwa kufanyika Agosti 2023 jijini Arusha, Tanzania.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga akielezea uzoefu wa Tanzania kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia na uongozi katika Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Afrika katika Uongozi (African Women in Leadership International Conference) unaoendelea jijini Durban, Afrika Kusini. 
Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Afrika katika Uongozi (African Women in Leadership International Conference) ukiendelea jijini Durban, Afrika Kusini.
Kutoka kushoto ni Prof. Fortunata Makene Mkuu wa Sera na Utafiti kutoka Taasisi ya Uongozi Tanzania; Mkunde Senyagwa Mkurugenzi wa Mikutano na Masoko katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha; Festo Mramba kutoka AICC, Balozi Mindi Kasiga kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, mwanzilishi wa AWLO Dkt Elisha Attai , Bibi Happiness Godfrey kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini na Bi. Maria Mafie kutoka Bodi ya Utalii Tanzania.

Thursday, September 15, 2022

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR AFUNGA MKUTANO WA WANAWAKE NA VIJANA KATIKA BIASHARA WA AfCFTA


Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Masoud Othman akihutubia wakati wa hafla ya kufunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliomalizika tarehe 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake Mhe. Masoud Othman alisisitiza kuwa kauli mbiu ya mkutano huo isemayo "Wanawake na Vijana ni injini ya biashara katika Mkataba wa Eneo Huru Barani Afrika" ni kauli inayoishi na imekuja wakati sahihi ambapo biashara zinazofanywa na wanawake na vijana zimekuwa zikikua kwa kasi.

Pia amepongeza muamko mkubwa ulioneshwa na washiriki ambao wametoka maeneo mbalimbali barani Afrika kuja kushiriki mkutano huo na kufafanua kuwa mkutano huo ulikuwa na washiriki wasiopungua 5,000 pamoja na wafanyabiashara wapatao 100 walioshiriki maonesho ya biadhaa ambayo yalifanyika katika eneo la mkutano.

"Ni matumaini yangu kuwa kupitia kusanyiko hili kutatokea maafikiano na kuanzishwa kwa mawasiliano baina yenu na hivyo kuwawezesha kupeana uzoefu" alisema Mhe. Masoud Othman

Aidha, akaeleza mkutano huu umekuwa na manufaa mengi kwakuwa wanawake na vijana wanaojihusisha na masuala ya biashara wamepata nafasi ya kueleza hali halisi ya kuendesha biashara, biashara wanazozifanya, changamoto wanazokutana nazo na kushauri suluhisho la kila changamoto kwa uhalisia wake.

Vilevile akaeleza maarifa na michango yote iliyotolewa ina manufaa katika kuleta maboresho kwenye maeneo ya biashara na kuwezesha kutumia fursa zilizopo kikamilifu kwa maslahi ya Taifa na Afrika kupitia utajiri wa rasilimali zilizopo. 

Hivyo, akasistiza kuwa maoni na mapendekezo yaliyotolewa yatazingatiwa katika itifaki ya wanawake na vijana katika biashara ili kuwezesha fursa zilizopo kutumika kwa ustawi wa watu wake na kanda ya Afrika kwa ujumla.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifuatilia hotuba ya kufunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliofanyika tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Fatma Rajab akifuatilia hotuba ya kufunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliofanyika tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika, Mhe. Wamkele Mene (AfCFTA) akipongeza muitikio mkubwa wa washiriki na kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utayari wake wa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliomalizika tarehe 14 Septemba 2022  Jijini Dar es Salaam.

Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia, Bi. Upendo Mwasha (katikati) akifuatili hotuba ya kufunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliofanyika tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya kufunga mkutano huo.

Sehemu nyingine ya washiriki wakifuatilia hotuba ya kufunga mkutano huo.
Picha ya pamoja.

WAZIRI MULAMULA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA MABALOZI WATEULE WA FINLAND, CANADA NA HISPANIA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb.) amepokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wateule wa nchi za Finland, Hispania na Canada katika hafla iliyofanyika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini  Dar es salaam.

Mabalozi wateule waliowasilisha nakala za Hati za Utambulisho kwa Mhe. Waziri Mulamula  leo ni Balozi wa Canada Nchini, Mhe. Kyle Nunas, Balozi wa Finland Nchini, Mhe. Zitting Maria Theresa na Balozi wa Hispania, Mhe. Jorge Moragas Sanchez.

Akizungumza na mabalozi hao kwa nyakati tofauti Mhe. Waziri amewaahidi kuwapa ushirikiano ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu hapa nchini na kuwasihi kuendeleza kile ambacho mabalozi waliowatangulia wamekifanya katika nyanja mbalimbali za ushirikiano baina ya nchi zao na Tanzania.

 

Akizungumza baada ya kuwasilisha nakala ya hati zake kwa Mhe. Waziri, Balozi mteule wa Finland Mhe. Zitting Maria Theresa aliahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Finland na kuongeza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, masuala ya jinsia na kuwajengea uwezo wa kiuchumi wanawake. 

Naye Balozi Mteule wa Canada Mhe. Kyle Nunas amesema Canada itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuibua maeneo mapya ya ushirikiano yakiwemo biashara na uwekezaji, sekta ya madini,elimu , maji na ulinzi na usalama.

Naye Balozi Mteule wa Hispani Nchini, Mhe. Jorge Moragas Sanches amemuahidi Mhe. Waziri kuwa Hispania itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali kama vile kilimo, afya, michezo, maji, elimu na umeme vijijini ili kuleta tija nchini.

Katika hatua nyingine Balozi Mulamula amekutana na kuzungumza na Balozi wa Afrika Kusini nchini Mhe. Noluthando Mayende Malepe. Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamejadili jinsi ya kuendelea kushirikiana kwa kuzingatia makubaliano ambayo nchi hizi mbili ziliingia kwa lengo la kufungua maeneo zaidi ya ushirikiano kupitia fursa za kujengeana uwezo kati ya wananchi wa Tanzania na Afrika Kusini.

Balozi Mteule wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Zitting Maria Theresa akiwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula jijini Dar Es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Zitting Maria Theresa baaada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho jijini Dar Es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiendelea na mazungumzo na Balozi Mteule wa Finland nchini Tanzania, Mhe. Zitting Maria Theresa baaada ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho jijini Dar Es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Hispania nchini Tanzania, Mhe. Jorge Moragas Sanchez

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Hispania nchini Tanzania, Mhe. Jorge Moragas Sanchez

Balozi Mteule wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula alipowasili ofisini kwake kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Kyle Nunas

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimpokea Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Noluthando Mayende Malepe aliyekuja ofisini kwake kufanya mazungumzo kuhusu ushiikiano wa mataifa yao

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Noluthando Mayende Malepe 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiendelea na mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Mhe. Noluthando Mayende Malepe 




 

TANZANIA NA DRC ZAAHIDI UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA MKUTANO WA JPC


                                                                                

 
                            
    
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisoma hotuba ya kufunga Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) uliofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa meza kuu kwa ajili ya Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Wengine katika picha, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mtangamano wa Kikanda na Nchi zinazongumza Kifaransa wa DRC, Mhe. Zacharie Tshimbinda Bilolo. 

Waziri wa Mtangamano wa Kikanda na Nchi zinazozungumza Kifaransa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Didier Mazenga Mukanzu akisoma hotuba ya kufunga Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) uliofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022
Wajumbe wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa kufunga  Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula na Waziri wa Mtangamano wa Kikanda na Nchi zinazozungumza Kifaransa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Didier Mazenga Mukanzu wakisaini Taarifa ya Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) uliofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 

Wajumbe wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa kufunga  Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula na Waziri wa Mtangamano wa Kikanda na Nchi zinazozungumza Kifaransa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mhe. Didier Mazenga Mukanzu wakibadilishana Taarifa ya Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) uliofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimpa zawadi ya picha za kuchora za twiga Waziri wa Mtangamano wa Kikanda na Nchi zinazozungumza Kifaransa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ya Kongo (DRC), Mhe. Didier Mazenga Mukanzu

Picha ya pamoja ya viongozi Wakuu walioshiriki Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) uliofanyika jijini Dar Es Salaam


 

WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA BALOZI WA UFARANSA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui katika Ofisi Ndozo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Septemba 2022.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa yao katika sekta za uwekezaji, ujenzi na uboreshaji wa miundombinu, biashara, usafiri na uchukuzi, nishati, kilimo, uchumi wa blue, elimu na utamaduni.

Pia wamejadili umuhimu wa kuwa na kamati za kitaifa kwa ajili ya ufuatiliaji wa masuala ya msingi ya utekelezaji yaliyokubaliwa wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Ufarasa mwezi Februari 2022, pamoja na masuala mengine ya ushirikiano baina ya nchi zao.

Vilevile wamejadili juu ya mchango unaotolewa na serikali ya Ufaransa katika masuala ya ulinzi wa amani pamoja na nafasi ya tanzania katika kusimamia masuala ya ulinzi na amani kikanda hususan katika  Nchi wanachama za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC), Nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na katika Umoja wa Afrika (AU).

Mhe. Nabil Hajlaoui akimweleza Mhe. Balozi Liberata Mulamula jitihada zinazofanya na Serikali yake katika kuunga mkono jitihada za kusaidia shughuli za maendeleo barani Afrika kwa kushirikiana na mataifa mengine ya Ulaya walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Septemba 2022.

 Mhe. Balozi Mulamula akiagana na Mhe. Nabil Hajlaoui baada ya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Septemba 2022.

Mazungumzo yakiendelea.

Picha ya Pamoja, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (wa pili kulia), Mhe. Nabil Hajlaoui (wa pili kushoto) na maafisa waliombatana nao katika mazungumzo yao.

 

TANZANIA YAPONGEZWA KWA KUWA MWANACHAMA HAI WA UMOJA WA AFRIKA

Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Monique Nsanzabaganwa alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula pembezoni mwa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) uliofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 Jijini Dar es Salaam.

Akifafanua shughuli za utekelezaji zinazofanywa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Nchi Wanachama Mhe. Nsanzabaganwa alieleza kuwa Tanzania ni miongoni mwa wadau muhimu katika Umoja wa Afrika ambapo, licha ya nafasi yake ya kuunga mkono uanzishwaji wa umoja huo pia imekuwa ikikamilisha michango yake ya uanachama kwa wakati.

"Ukamilishaji wa michango kwa wakati kutoka kwa Nchi wanachama unawezesha uendeshaji wa shughuli za Sekretarieti kutekelezeka kwa tija na kusaidia kupatikana kwa maslahi ya watumishi." alisema Mhe. Nsanzabaganwa.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amemuhakikishia Mhe. Nsanzabaganwa kuwa Tanzania itaendelea kuheshimu makubaliano yaliyokubaliwa katika Umoja wa Afrika sambamba na kuhakikisha inanufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana kama vile ajira na biashara.

Pia ameshukuru kwa jitihada zinazofanywa na Umoja wa Afrika kupitia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) kwa kumtambua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Kinara wa Uhamasishaji wa Masuala ya Wanawake na Vijana katika biashara, sambamba na heshima iliyotolewa kwa Tanzania ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika.

Aidha, Mhe. Waziri amesema kuwa mkutano huo ni muhimu sana kwakuwa umebeba agenda ya wanawake na vijana yenye lengo la kujenga haki na usawa wa kijinsia katika ajira, kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira, kuwajengea uwezo na kushirikishana uzoefu katika biashara na kuingia katika ushindani wa biashara kitaifa, kikanda na kimataifa.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Monique Nsanzabaganwa katika ofisi za Wizara jijini Da es Salaam tarehe 14 Septemba 2022. 

Mazungumzo yakiendelea

Picha ya pamoja baada ya mazungumzo.
 

Tuesday, September 13, 2022

BALOZI WA TANZANIA NCHINI INDONESIA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele mapema leo tarehe 13/09/2022 amewasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Indonesia Mhe. Joko Widodo katika hafla iliyofanyika kwenye Kasri la Merdeka jijini Jakarta. 

Katika hafla hiyo, wawili hao walipata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya biashara na uwekezaji. 

Hatua hiyo ya Mhe. Balozi Makocha Tembele kuwasilisha hati zake za utambulisho inaashiria kuanza rasmi kwa utumishi wake katika nchi hiyo. 
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akiwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Nchi hiyo Mhe. Joko Widodo
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akiwasili katika Kasri la Merdeka jijini Jakarta ambapo aliwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Indonesia Mhe. Joko Widodo
Balozi wa Tanzania nchini Indonesia Mhe. Macocha Tembele akisalimiana na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Joko Widodo