Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa (TCM) ukiendelea jijini Bujumbura, Burundi |
Friday, February 10, 2023
TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA 18 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA UCHUKUZI, MAWASILIANO NA HALI YA HEWA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Thursday, February 9, 2023
TANZANIA YAJIZATITI KUTUMIA FURSA ZINAZOPATIKANA NDANI NA NJE YA NCHI KUKUZA UCHUMI
Serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa kushirikiana
na nchi mbalimbali duniani ili kukuza uchumi
wa nchi kupitia fursa za biashara, uwekezaji na utalii zilizopo ndani na nje ya
nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Bungeni leo tarehe 09
Februari,2023 wakati akijibu swali la Mhe.
Felista Njau, Mbunge wa Viti Maalum kuhusu umuhimu
wa Serikali wa kuainisha nchi zenye fursa za biashara na uwekezaji ili kukuza
pato la Taifa.
Amesema Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa
kushirikiana na Wizara za kisekta na Balozi za Tanzania imeendelea kutangaza
fursa za biashara na uwekezaji zenye manufaa kwa Taifa na kwamba Wizara
inaandaa Mpango wa Kitaifa wa kutekeleza Diplomasia ya Uchumi utakaojumuisha
Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kufikia malengo tarajiwa.
Amesema Mpango huu ambao unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Desemba
2023, pamoja na mambo mengine unalenga kuhakikisha fursa za biashara, uwekezaji
na utalii zinakuwa na tija zaidi kwa wananchi wa Tanzania. Pia Mpango huo
utajumuisha Sekta zote husika ikiwa ni pamoja na kuainisha maeneo muhimu ya
kisekta yatakayo changia katika kukuza uchumi na pato la Taifa.
Akichangia hoja kuhusu mkakati wa utoaji elimu kwa wananchi kuhusu dhana ya Diplomasia ya Uchumi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, amesema Wizara inaendelea kutoa elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali na kufafanua kwamba Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi unaoandaliwa pia utajumuisha Mpango wa kutoa elimu kwa umma kuhusu dhana hiyo ili kuwawezesha wananchi kuielewa dhana hii na kuwawezesha kutumia fursa mbalimbali zinazotokana na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali.
Kuhusu taarifa hasi zinazotolewa na vyombo vya kimataifa dhidi ya Tanzania, Mhe. Dkt. Tax amesema tayari Wizara imeanza kushirikiana na vyombo vya habari vya Nje hususan vile vinavyorusha matangazo yake kwa Kiswahili ili kupitia vyombo hivyo fursa na taarifa chanya kuhusu Tanzania zitangazwe duniani kote.
Wednesday, February 8, 2023
Wednesday, February 1, 2023
BALOZI LUVANDA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO, NEW ZEALAND
Tuesday, January 31, 2023
UBALOZI WA UFARANSA WAFUNGUA OFISI NDOGO JIJINI DODOMA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi ya Uwakilishi ya Ubalozi wa Ufaransa jijinii Dodoma |
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa ofisii ya Uwakilishi ya Ubalozi wa ufaransa wakifuatilia tukio hilo |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) ameupongeza Ubalozi wa Ufaransa nchini kwa kufungua Ofisi Ndogo ya Uwakilishi jijini Dodoma na kuzihamasisha Balozi nyingine kuendelea kuitikia wito wa kuhamia Makao Makuu ya Nchi.
Akizungumza katika ufunguzi wa Ofisi hiyo, Mhe. Dkt. Tax amesema anaupongeza ubalozi huo kwa kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alioutoa mwanzoni mwa mwaka 2023 wa kuwasihi Mabalozi kuhamia Makao Makuu ya Serikali jijini Dodoma.
“Tuko hapa kwa ajili ya kufungua Ofisi ndogo za Uwakilishi za Ubalozi wa Ufaransa nchini, baada ya Serikali kuhamia rasmi Dodoma, ofisi hii ni ya tatu baada ya zile za Ujerumani na China, niwapongeze sana kwa uamuzi wenu huu, mmeiunga mkono Serikali katika kuhamia kwake hapa Dodoma’, alisema Dkt. Tax.
Dkt. Tax ameuhakikishia na kuuahidi Ubalozi huo kuwa, Serikali itatoa msaada wowote watakaouhitaji ili kuiwezesha ofisi hiyo kufanya kazi zake kwa ufanisi na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha ndoto ya kuwa na ubalozi kamili inakamilika.
Amesema hatua ya kufunguliwa kwa Ofisi hiyo ni muhimu katika kuimarisha uhusiano na urafiki uliopo baina ya Tanzania na Ufaransa na kwamba ina dhamira ya kuupeleka uhusiano huo katika ngazi nyingine.
Ameeleza kuwa tayari Serikali imewapatia viwanja na hati Balozi zote na Taasisi za Kimatifa zenye uwakilishi nchini na kuongeza kuwa Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika jiji la Dodoma ili kuhakikisha Jiji hili linakuwa na miundombinu na huduma bora za kijamii zinazotosheleza mahitaji ya wakazi wake wote.
Ameongeza kusema ana imani kuwa wito wa Serikali wa kuhamia makao makuu ya nchi utaenziwa na kuungwa mkono na Balozi na Mashirika ya Kimataifa na kuihakikishia jumuiya ya wanadiplomasia nchini kuwa Serikali itatoa msaada wowote utakaohitajika ili kurahisisha uhamiaji wao jijini Dodoma.
Naye Balozi wa Ufaransa nchini Mheshimiwa Nabil Hajloui amesema Ufaransa imefungua Ofisi yake jijini Dodoma ikiwa ni hatua za kuunga mkono uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kuhamishia Makao Makuu yake jijini humo, lakini pia kurahisisha huduma mbalimbali za kibalozi kwa wananchi wa Dodoma na mikoa jirani.
Amesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha uhusiano kwa manufaa ya pande zote mbili na kuahidi kuwa Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo la AFD itaendelea kushirikiana na Serikali katika jitihada zake za kuboresha na kuinua maisha ya wananchi wa Tanzania kupitia Sekta za Maji, Nishati, Afya, Kilimo na Elimu kwa Tanzania Bara na Zanzibar
Kufunguliwa kwa Ofisi hizo kunafanya Dodoma kuwa na ofisi tatu za Ubalozi baada ya zile za Ujerumani na China. Ofisi hizo ambazo zipo eneo la Kilimani jijini Dodoma zitatoa huduma mbalimbali kwa Serikali na wananchi wote kwa ujumla na zinajumuisha pia Ofisi za Shirika la Msaada la Ufaransa la Agence Francaise de Development (AFD).
TANZANIA INASHIRIKIANA NA COMESA KUPITIA AfCFTA- BALOZI MBAROUK
Naibu Waziri Mmambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akijibu swali bungeni jijini Dodoma tarehe 31 Januari 2023
Tanzania inaendelea kushirikiana na nchi zinazounda Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) kupitia utekelezaji Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) na pia kupitia Utatu unaoundwa na nchi za COMESA, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Momba, Mhe. Condester Michael Sichalwe aliyetaka kujua kwa nini Tanzania haioni haja ya kujiunga tena na COMESA.
Amesema Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi 19 zilizokuwa waanzilishi wa Jumuiya ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) mwaka 1994. Hata hivyo, Tanzania ilijitoa katika COMESA mwaka 2000 kwa sababu ilikuwa ni mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambapo baadhi ya nchi za jumuiya hizo pia ni wanachama wa COMESA.
Ameongeza kusema Tanzania pia ilijitoa COMESA baada ya kujiridhisha kuwa nchi haitaathirika kiuchumi kwa kuwa bado ni mwanachama wa EAC na SADC na kwamba lengo ni kulipunguzia taifa gharama hasa michango ya uanachama kwenye Jumuiya hizo.
Pia amesema kitendo cha Bunge cha kuridhia kwa Mkataba wa kuanzisha Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA) hapo mwezi Septemba 2021, kunaifanya Tanzania kuendelea kushirikiana na nchi za COMESA.
“Ikumbukwe kuwa mwaka 2008 nchi za COMESA, EAC na SADC zilikubaliana kuanzisha Utatu na hivyo Tanzania inaendelea kushirikiana na COMESA kupitia Utatu huo wa COMESA–EAC-SADC,” alisema Mhe. Mbarouk.
TANZANIA NA FINLAND ZAAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA BIASHARA
Serikali za Tanzania na
Finland zimeahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta zenye maslahi
mapana ya kiuchumi kwa wananchi wa nchi hizi mbili ikiwemo biashara, utalii na
uwekezaji.
Ahadi hiyo imetolewa katika
mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Uchumi wa Finland, Mhe. Mika
Lintilä walipokutana katika ofisi za Wizara jijini Dodoma tarehe 31
Januari 2023.
Katika mazungumzo hayo
viongozi hao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara,
uwekezaji, utalii, teknolojia ya habari na mawasiliano, usafirishaji, afya,
kilimo, madini, nishati, elimu, mazingira na tafiti ili kupitia sekta hizo
wananchi hususan wa Tanzania wanufaike kiuchumi na kijamii.
Dkt. Tax ameeleza kuwa
amefurahishwa na ziara ya Mhe. Mika Lintilä na ujumbe wake
nchini ikiwemo ujumbe wa wafanyabiashara alioambatana nao kutoka katika sekta
za msingi kwa maendeleo ya pande zote mbili.
“Tanzania na Finland zina
ushirikiano wa kihistoria ulioasisiwa kati ya nchi hizo mara baada ya uhuru wa
Tanganyika mwaka 1962. Tupo tayari kuendelea kushirikiana na Finland katika
kujenga uchumi wa kidigitali ili kuyafikia mapinduzi ya viwanda” alisema Dkt.
Tax.
Vile vile, ametumia nafasi
hiyo kuishukuru Serikali ya Finland kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 19 wa Nchi
za Nordic na Afrika uliofanyika mwezi Juni 2022. Pia ameeleza kuwa Tanzania
itaendelea kushiriki kwenye majukwaa mbalimbali ili kuwasilisha mchango wake
katika masuala ya kikanda na kimataifa.
Kwa upande wake, Mhe. Mika
Lintilä ameeleza kuwa Umoja wa Ulaya umetenga fedha kiasi cha Euro
Billioni 300 kwa ajili ya kushirikiana na nchi zinazoendelea na zile za Kusini
mwa Jangwa la Sahara katika sekta za maendeleo.
Vile vile, ameongeza kuwa
tarehe 23 na 24 Februari 2023 kampuni za biashara zipatazo 40 kutoka
Finland zitashiriki katika Jukwaa la Wafanyabiashara wa Tanzania na Umoja wa
Ulaya litakalofanyika jijini Dar es Salaam.
Wakati huo huo,
Waziri Lintilä amekutana na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha
ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji ili kukuza uwiano wa
biashara kati ya nchi hizi mbili ambao bado ni mdogo.
Pia Dkt. Kijaji ameongeza
kuwa, Tanzania itaendelea kuongeza samani ya bidhaa zake kama mbao,
chakula na madini ili kuziwezesha kuingia katika soko la kimataifa ikiwemo
Finland.
Waziri Lintilä yupo
nchini kwa ziara ya siku nne (4) ambapo ameambatana na kundi la wafanyabiashara
wapatao 18 kutoka katika sekta mbalimbali za kiuchumi ili kujionea maeneo
mbalimbali ya uwekezaji na biashara.
Mazungumzo yakiendelea. |
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akisalimiana na Waziri wa Uchumi wa Finland, Mhe. Mika Lintilä alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 31 Januari 2023. |
Dkt. Tax akimkabidhi zawadi Mhe.Mika Lintilä |
Monday, January 30, 2023
DIPLOMATIC CORPS IN TANZANIA REMINDED TO OBSERVE THE VIENNA CONVENTION
Sehemu ya Mabalozi wa Wakifuatilia Mkutano |
Sehemu ya Mabalozi wa Wakifuatilia Mkutano |
Mkutano baina ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa waliopo nchini ukiendelea jijini Dodoma |
Mkutano baina ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa waliopo nchini ukiendelea jijini Dodoma |
Sehemu ya Mabalozi wa Wakifuatilia Mkutano |
Meza Kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Wizara |
Sunday, January 29, 2023
WAZIRI WA MASUALA YA UCHUMI WA FINLAND AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Waziri wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mhe. Mika Tapani Lintilä amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 29 Januari hadi tarehe 1 Februari 2023.
Lengo la ziara hiyo ni kujadili masuala yenye maslahi kwa Tanzania na Finland ili kuimarisha ushirikiano wa pande mbili kupitia Programu ya sasa ya Ushirikiano wa Maendeleo na biashara na kukuza ushirikiano wa kibiashara katika sekta ya biashara na uwekezaji.
Mhe. Lintilă akiwa nchini anatarajia kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Dkt. Stergomena Tax, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Pindi Chana, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf F. Mkenda.
Viongozi wengine ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC); Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Shirika la Umerne Tanzania (TANESCO).