Tuesday, April 25, 2023

UJUMBE WA TANZANIA ULIVYOSHIRIKI MAANDALIZI YA MKUTANO MAALUM WA 48 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA EAC

Mkutano Maalum wa 48 wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki kwa ngazi ya Makatibu Wakuu umefanyika kwa njia ya mtandao tarehe 25 Aprili 2023 huku ujumbe wa Tanzania ukishiriki kutokea Dodoma.

 

Mkutano huo  ambao ulianza  kwa ngazi ya Wataalam tarehe 24 Aprili 2023 umejadili pamoja na mambo mengine Taarifa ya Mkutano wa Kamati ya Fedha na Utawala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mwezi Machi 2023 pamoja na  Taarifa ya Kamisheni ya Ukaguzi wa Fedha za Jumuiya kwa kipindi kilichoishia tarehe 30 Juni 2022.

 

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Mkatibu Wakuu umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi.

 

Vilevile, mkutano huo umehudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote Wanachama wa Jumuiya ambazo ni Burundi, Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na Sekretarieti ya Jumuiya hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 25 Aprili 2023 kuandaa Mkutano Maalum wa 48 wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki.
Mkutano ukiendelea
Balozi Mbumdi akiwa na Wajumbe wengine wa Tanzania kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mkutano ukiendelea

Wajumbe kutoka Tanzania katika Mkutano wa Makatibu Wakuu

Mkutano ukiendelea

Makatibu Wakuu kutoka Nchi wanachama wakishiriki Mkutano kwa njia ya mtandao

 

 

 


SERIKALI YAENDELEA KUWAREJESHA WATANZANIA KUTOKA SUDAN

 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Monday, April 24, 2023

CALL FOR APPLICATION: QUEEN'S COMMONWEALTH ESSAY COMPETITION 2023


 

NJE SPORTS HOI MBELE YA WAKUSANYA MAPATO


Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuingia dimbani kuwakabili wapinzani wao timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) kwa mara nyingine jana tarehe 23 Aprili 2023 ilishuka dimbani kucheza na timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika hatua ya timu 16 bora kwenye michuano ya kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) yanayoendelea mjini Morogoro 

Katika mtanange huo ulionza majira ya saa 10.30 jioni kwenye uwanja uliopo Solomon Mahlangu Kampas – Mazimbu, Nje Sports ambayo ilipewa nafasi kubwa ya ushindi kabla mchezo ilipoteza kwa goli 1-0 liliofungwa na mshambuliaji Erick Mwita katika dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza, na kudumu hadi dakika ya mwisho wa mchezo. 

Katika hatua hiyo ya mashindano ya timu 16 bora ilihusisha timu ya TAMISEMI, Morogoro DC, Uchukuzi, Afya, Mahakama, TANROADS, HAZINA, Maliasili, TRA, Nje Sports, TANESCO, Kilimo, CRDB, Mambo ya Ndani, Wizara ya Ulinzi na TPDC.

Baada ya kufungwa katika mchezo huo Nje Sports imepoteza nafasi ya kuendelea kushiriki katika mashindano ya mpira wa miguu, hivyo wanamichezo wake wataendelea kushiriki katika mashindano ya michezo mingine ikiwemo kuvuta kamba, bao na drafti.

Mashindano hayo yanayohusisha michezo mbalimbali kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Dunia (Mei Mosi), itakayo adhimishwa kitaifa mjini Morogoro tarehe 1 Mei 2023.

Wachezaji wa Nje Sports na TRA wakiwania mpira katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja uliopo Solomon Mahlangu Kampas – Mazimbu.
                                           Mchezo ukiendelea
Safu ya ulinzi ya Nje Sports ikiwa imejipanga kuzima moja ya shambulizi lililofanywa na TRA 
Mshambuliaji wa Nje Sports akiwatoka walinzi wa TRA katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja uliopo Solomon Mahlangu Kampas – Mazimbu

Saturday, April 22, 2023

NJE SPORTS KUSONGA MBELE KWENYE MICHUANO YA MEI MOSI LICHA YA KUKUBALI KISASI CHA MAAFANDE

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) leo terehe 22 Aprili 2023, imeingia dimbani kucheza dhidi ya mpinzani wake timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa Sekondari ya Morogoro kuanzia majira ya saa 3.00 asubuhi.

Katika mchezo huo Nje Sports imepoteza kwa goli 1-0, lililofungwa katika dakika ya 37 ya kipindi cha pili (katika mashindano haya ya Mei Mosi mpira wa miguu unachezwa kwa dakika 60 badala 90 kama ilivyozoeleka) na kudumu hadi mwisho wa mchezo.

Hata hivyo licha ya kupoteza mchezo huo mbele ya Maafande, Nje Sports inasongo mbele kucheza hatua ya timu 16 bora ambazo zimefuzu katika hatua ya makundi baada ya kujikusanyia alama 7 katika kundi C, na kuwa miongozi mwa timu nne zilizofuzu katika kundi hilo. 

Kundi C lilijumuisha timu sita ambazo ni Wizara ya Ulinzi ambayo imejikusanyia alama 12 (kinala wa kundi), Wizara ya Fedha na Mipango –Hazina FC alama 10 (nafasi ya pili), Wizara ya Mambo ya Ndani alama 9 (nafasi ya tatu) Nje Sports alama 9 (nafasi ya nne) 21st Century alama 5 (nafasi ya 5) Ushirika alama 0 (nafasi ya 6)

Akizungumza muda mfupi baada ya mchezo huo Mwalimu wa Nje Sports Bw. Shaaban ameushukuru Uongozi wa Wizara kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa kikosi chake, ambao umewezesha kufunzu hatua ya 16 bora. Vilevile ametoa pongezi kwa wachezaji na uongozi wa timu kwa kufuzu hatua inayofuata katika mashindano hayo ya kuelekea Kilele cha Maadhimisho Mei Mosi yanaoyondelea mjini Morogoro.

Nje Sports inatarajiwa kushuka tena dimbani kucheza dhidi ya Mamlaka ya Pato Tanzania (TRA) siku ya Jumapili tarehe 23 Aprili 2023 saa 10.00 jioni. 
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuingia dimbani kuwakabili wapinzani wao Wizara ya Mambo ya Ndani 
Mechi ikiendelea
 Penati ikipigwa kuelekea lango Nje Sports. Penati hiyo haikufanikiwa kutengeneza goli baada ya kudakwa na kipa mahiri wa Nje FC.
Mlinzi mahiri wa Nje Sports Bw. Abbas Abdallah shuti lililoelekezwa langoni kwake.
Mchezaji wa Nje FC akiwatoka walinzi wa timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwenye mechi iliyochezwa katika uwanja wa Morogoro Sekondari.
Baadhi ya wachezaji wa Nje Sports wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mchezo wao dhidi ya Wizara ya Mambo ya Ndani

Friday, April 21, 2023

NJE SPORTS YA VUTWA SHATI MOROGORO

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) leo tarehe 21 Aprili 2023 imeshuka dimbani kucheza mchezo wake wa wanne dhidi ya timu ya Wizara ya Fedha na Mipango (Hazina FC) ambapo imepoteza kwa goli 1-0. 

Mchezo huo ulioanza majira ya saa 3.00 asubuhi katika uwanja wa Ujenzi uliopo mjini Morogoro, Nje Sports iliruhusu goli la mapema katika dakika ya 2’ ya kipindi cha kwanza cha mchezo ambapo lilidumu hadi mwishoni mwa mchezo. 

Baada ya kupoteza mchezo huo Nje Sports inasalia na alama zake 7 katika kundi C huku ikishika nafasi ya pili katika kindi hilo nyuma ya Ulinzi FC yenye alama 9.

Nje Sports kesho tarehe 22 Aprili 2023 inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa tano (5) dhidi ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Michezo hii ni muendelezo wa mashindano yanayoendelea mjini Morogoro kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) yatakayo adhimishwa Kitaifa mjini humo tarehe 1 Mei 2023.

Katika hutua nyingine timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeibuka na ushindi dhidi ya TAMISEMI katika mchezo uliochezwa saa 12.30 asuhuhi katika uwanja wa Jumhuri mjini Morogoro.

Wakati huohuo timu ya Wanawake inayoshiriki mashindano ya mpira wa pete ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki saa 1.00 asubuhi ilishuka dimbani kucheza dhidi ya mpinzani wake Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo imepoteza kwa magoli 47-5 kwenye mchezo iliochezwa Jamhuri mjini Morogoro.
Mshambuliaji machachari wa Nje Sports Bw. Mikidadi Magola akiwatoka walinzi wa Hazina FC katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Ujenzi mjini Morogoro
Timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla kuingia uwanjani kucheza dhidi ya Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Balozi James Bwana wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na baadhi wanamichezo wa Wizara alipowatembelea katika uwanja wa Ujenzi, mjini Morogoro kwa lengo la kuwahamashisha. 
Timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (mawasiliano) zikiwa zimejipanga tayari kwa mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
Moja ya goli lililofungwa kwenye mchezo kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 
Moja ya goli lililofungwa kwenye mchezo kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 
Mchezo kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mawasiliano ukiendelea
Winga machachari wa Nje Sports akipiga shuti baada ya kuwatoka walinzi wa Hazina FC katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Ujenzi mjini Morogoro
Mechi kati ya Nje na Hazina FC ikiendelea katika uwanja wa Ujenzi mjini Morogoro
Wachezaji wa Nje FC wakipata nasaha za kocha Bw. Shaaban Maganga wakati wa mapunziko

Thursday, April 20, 2023

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI YASHIRIKI UFUNGUZI WA MICHEZO YA MAADHIMISHO YA MEI MOSI


Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wanaoshiriki katika michezo inayoendelea mjini Morogoro wameungana na maelfu ya wafanyakazi wenzao kushiriki katika sherehe ya ufunguzi wa tamasha la michezo kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) yatakayofanyika Kitaifa mjini Morogoro.

Ufunguzi huo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro umefanywa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Fatma Abubakar Mwassa na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Wafanyakazi nchini.

Mhe. Mwassa akihutubua wafanyakazi waliojitokeza katika uwanja wa Jamhuri ametoa wito kwa Watumishi kuendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuongeza ukakamavu na kupunguza uwezekano wa kuugua magonjwa yasiyo ambukizwa kama inavyoshauriwa na Wataalamu wa Afya. 

“Michezo ni afya, michezo ni furaha, michezo ni urafiki hivyo naendelea kusisitiza Wafanyakazi kuendeleza utamaduni wa kufanya mazoezi kama ambavyo sera inavyohimiza ilikuongeza utimamu wa mwili na akili. Mfanyakazi anayezingatia michezo au mazoezi hata ufanisi wake kazini huwa nimzuri zaidi” ameeleza Mhe. Mwassa

Sherehe za ufunguzi wa tamasha hilo lilishindikizwa na michezo na burudani mbalimbali ambapo Viongozi waliohudhuria uwanjani hapo akiwemo Mhe. Prof. Joyce Ndalichako Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu walipata nafasi ya kujionea ujuzi, ukakamavu na umahiri wa watumishi katika michezo.

Kwa upande wake Timu ya Wanawake ya mpira wa pete ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) ilicheza dhidi ya timu ya Mahakama ya Tanzania mbapo Timu ya Mahakama imeibuka na ushindi wa magoli 37 dhidi 3 

Timu ya mpira wa pete ya Nje Sports imeendelea kuwa na mwenendo wa kusua sua katika mashindano hayo ambapo Kiongozi wake Bi. Pili Rajabu ameeleza kuwa uwepo kwa majeruhi wengi katika kikosi chake kinaifanya timu hiyo kutokuwa katika nafasi nzuri ya ushindani hivyo kupoteza michenzo mingi wanayoshiriki.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maandamano wakati wa sherehe za ufunguzi wa michezo kuelekea maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wafanyakazi duniani yatakayofanyika Kitaifa mjini Morogoro

Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maandamano yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuelekea maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wafanyakazi duniani yatakayofanyika Kitaifa mjini Morogoro



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Abubakar Mwassa akihutubia watumishi waliojitokeza katika uwanja wa Jamhuri mkoani humo kwenye sherehe za ufunguzi wa michezo kuelekea maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi).
Bi. Pili Rajab (mwenye mpira) mchezaji wa Nje Sports akiwatoka walinzi wa  Time ya Mahakama ya Tanzania katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri.  Timu ya Mahakama iliibuka na ushindi wa magoli 37 - 3 katika mchezo huo.




Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakila kiapo cha utiifu katika michezo ya kuelekea maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wafanyakazi duniani yatakayofanyika Kitaifa mjini Morogoro 

TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA NCHI ZA EAC KULINDA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika tarehe 19, Aprili jijini Kampala, Uganda.

Makatibu Wakuu ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Uratibu ya Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika tarehe 19, Aprili jijini Kampala, Uganda.


Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu ukifuatilia Mkutano huo

Ujumbe wa Uganda (kushoto) na ujumbe wa Tanzania (kulia) katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu ukifuatilia Mkutano huo

Washiriki wa Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu wakifuatilia Mkutano huo.  

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu akipongezana na Kaimu Mkurugenzi Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Judith Ngoda baada ya kumalizika kwa Mkutano huo uliofanyika tarehe 19, Aprili jijini Kampala, Uganda.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu baada ya kumalizika kwa Mkutano huo uliofanyika tarehe 19, Aprili jijini Kampala, Uganda.


 

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha rasilimali za uvuvi katika Ziwa Victoria zinalindwa ili zinufaishe jamii zinazozunguka ziwa hilo na mataifa husika kwa ujumla.

 

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika tarehe 19, Aprili jijini Kampala, Uganda.

 

Prof. Shemdoe aliuhakikishia mkutano huo kuwa, Tanzania itaendelea kuchukua hatua madhubuti za kusimamia ziwa hilo kama nchi wanachama wa wa LVFO zilivyokubaliana. Alisisitiza pia kuwa Tanzania inaendelea kudhibiti matumizi ya zana haramu za uvuvi, kupiga marufuku uvuvi wa samaki wachanga, kudhibiti utoroshaji wa mazao ya uvuvi na kuhamasisha ufugaji wa samaki kwa vizimba katika Ziwa Victoria bila kuathiri mazingira.

 

Amesema pia, Tanzania imeimarisha udhibiti wa uingizaji wa zana za kuvulia samaki ili kuzuia uingizaji wa zana haramu nchini na kuendesha ukaguzi wa kina ili kuhakikisha uvuvi endelevu unafanyika kwa tija.

 

Pia Profesa Shemdoe alitanabaisha kuwa mchango wa Sekta za Uvuvi katika uchumi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mdogo sana kwakuwa mchango wake unahesabiwa katika maeneo ya uvuvi na ukuzaji bila kujumuisha mapato yanayotokana na shughuli zote zinazofanyika katika minyororo yake ya thamani.

 

“Mchango wa Sekta za Uvuvi katika uchumi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ni mdogo sana kwakuwa mchango wake unahesabiwa katika maeneo ya uvuvi na ukuzaji bila kujumuisha mapato yanayotokana na shughuli zote zinazofanyika katika minyororo yake ya thamaniBadala yake thamani hiyo inajumuishwa katika sekta zingine na hivyo kutokutoa picha halisi ya Sekta ya Uvuvi,” alisema.

 

Katika mkutano huo, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda, Dkt. Aziz Mlima, alimwakilisha Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo.

 

Kikao hiki kimehudhuriwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zilizopo katika Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa