Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa rai
kwa nchi za Afrika kuwekeza zaidi katika kuboresha afya, elimu na lishe kwa
watu wake ili kutengeneza rasilimali watu inayoweza kuchangia maendeleo na
ukuaji wa uchumi barani Afrika.
Rai
hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam leo tarehe 26 Julai 2023 wakati akifungua rasmi
Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu uliofanyika katika
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere.
Amesema
Mkutano huu umetoa fursa kwa nchi za Afrika kujadili na kupanga mikakati mipya
ya namna ya kutumia Rasilimali Watu ambayo Afrika imejaliwa kuwa nayo kama nyenzo
muhimu katika kuchangia maendeleo na mafanikio ya Bara la Afrika.
Ameongeza
kusema kwa upande wa Tanzania tayari mikakati mbalimbali imewekwa ya kuendeleza
Rasilmali Watu ikiwemo kutenga fedha kwa ajili ya kuongeza afua za lishe na
huduma za afya ya mama na mtoto ambapo amesema ameingia mkataba na Wakuu wa
Mikoa kuhakikisha wanasimamia suala hili katika mikoa yao.
Amesema
ifikapo mwaka 2050 Afrika itakuwa na asilimia 42 ya vijana duniani kote hivyo
uwekezaji kwenye rasilimali watu yenye tija unahitajika ili kuwa na hatima
nzuri. Amesema jitihada zaidi zinahitajika ili kuepuka kuzalisha vijana wasio
na ujuzi, wasio ajirika na vijana wenye kujiingiza kwenye vitendo viovu vya
kihalifu na uvunjifu wa amani.
Ameongeza
kusema uwekezaji kwenye rasilimali watu unaanza tangu mtoto anapozaliwa kwa
kumpatia lishe bora na chanjo stahiki ili kuondoa udumavu ambao husababisha
upungufu wa uelewa na uwezo wa kusoma vizuri kwa watoto. Pia amesisitiza
kuwekeza katika elimu ya awali ambayo ni msingi wa kuwaandaa watoto kimwili,
kiakili, kihisia na kiubunifu.
Kadhalika
ameeleza kuwa Tanzania inaendelea kuboresha utoaji huduma za jamii na kufanya maboresho
ya miundombinu kama madarasa, vituo vya afya, kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa
sekta ya elimu na afya na kutekeleza mpango wa elimu bure kwa shule za msingi
hadi sekondari.
Awali
akizungumza, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuridhia Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano huo
muhimu ambao amesema umehudhuriwa na zaidi ya Washiriki 2,500. Pia ameipongeza
na kuishukuru Benki ya Dunia kwa kuandaa mkutano huo kwa kushirikiana na
Serikali ya Tanzania.
Amesema
Mkutano huo ni jukwaa kwa nchi za Afrika kupanga mikakati bora zaidi ya
kuendeleza rasilimali watu kwa maendeleo endelevu ya Bara la Afrika.
Naye
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa
Afrika, Bi. Victoria Kwakwa amesma Benki hiyo itaendelea kushirikiana na kuunga
mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na Nchi za Afrika katika kuendeleza
rasilimali watu ili hatimaye kuwa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Mkutano
huo ambao umehudhuriwa na Wakuu wa Nchi kutoka Nchi sita za Kenya, Madagascar,
Sao Tome na Principe, Sierra Leone, Malawi na Msumbiji na wadau mbalimbali
kutoka sekta binafsi naza umma umemalizika kwa kupitishwa kwa Azimio la Dar es
Salaam ambalo limeainisha mikakati ya kuboresha maendeleo ya rasilimali watu
barani Afrika.
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua rasmi Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Afrika Kuhusu Rasililmali Watu uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai 2023
|
|
Mhe. Rais Samia akihutubia mkutano
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akitoa neno la utangulizi wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu kabla ya kumkaribisha Mhe. Rais Samia kufungua rasmi mkutano huo.
|
|
Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa
Afrika, Bi. Victoria Kwakwa akizungumza wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu
|
|
Marais kutoka Nchi za Afrika ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. Kutoka kushoto ni Rais wa Kenya, Mhe. William Ruto, Rais wa Malawi, Mhe. Lazarus Chakwera na Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi
|
|
Mhe. Rais Dkt. Samia (wa nne kushoto) akiwa na Marais walioshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. Kutoka kushoto ni Mhe. Rais Ruto, Mhe. Rais Chakwera, Mhe. Rais Nyusi, Mhe. Rais Andry Rajoelina wa Madagascar, Mhe. Rais Carlos Vila Nova wa Sao Tome na Principe na Mhe. Rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone
|
|
Mhe. Dkt. Tax akiteta jambo na Mhe. William Lukuvi
|
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akifurahia jambo kwa pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliani Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu.
|
|
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Agnes Kayola wakati wa
Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. |
|
Mkutano ukiendelea
|
|
Wageni waalikwa wakishiriki
Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. |
|
Katibu Mkuu, Balozi Dkt. Shelukindo akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Mathew Mkingule wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. Anayeshuhudia katikati ni Balozi Kasiga
|
|
Balozi wa Afrika Kusini nchini, Mhe. Noluthando Mayende-Malepe akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. |
|
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme (kushoto) akiwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Mteule, Iman Njalikai wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. |
|
|
Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. |
|
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Caesar Waitara akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. |
|
Picha ya pamoja
|
|
Picha ya pamoja
|
|
Picha ya pamoja
|