Wednesday, July 26, 2023

MHE. MARIAM CHABI TALATA AREJEA BENIN

Makamu wa Rais wa Benin, Mheshimiwa Mariam Chabi Talata ameondoka nchini na kurejea Benin baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu (Africa Human Capital Heads of State Summit) ulianza tarehe 25 na kumalizika tarehe 26 Julai 2023.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, Mhe. Mariam Chabi amesindikizwa na Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso (Mb.), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.

Makamu wa Rais wa Benin, Mheshimiwa Mariam Chabi Talata akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kuondoka nchini Tanzania na kurejea Benin baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu (Africa Human Capital Heads of State Summit) ulianza tarehe 25 na kumalizika tarehe 26 Julai 2023


Makamu wa Rais wa Benin, Mheshimiwa Mariam Chabi Talata akizungumza na Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila kabla ya kuondoka nchini na kurejea Benin baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu (Africa Human Capital Heads of State Summit) ulianza tarehe 25 na kumalizika tarehe 26 Julai 2023










RAIS NYUSI AREJEA NCHINI MSUMBIJI

Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi ameondoka nchini baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Rasilimali Watu (Africa Human Capital Heads of State Summit) uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 na 26 Julai, 2023.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam , Mhe. Rais Nyusi amesindikizwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Faustine Kasike.

Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akisindikizwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakati wa kuondoka nchini na kurejea Msumbiji mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Rasilimali Watu (Africa Human Capital Heads of State Summit) uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 na 26 Julai, 2023



Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakati wa kuondoka nchini na kurejea Msumbiji baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Rasilimali Watu (Africa Human Capital Heads of State Summit)

Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakati wa kuondoka nchini na kurejea Msumbiji baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Rasilimali Watu (Africa Human Capital Heads of State Summit)

Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akiwaaga watanzania wakati wa kuondoka nchini na kurejea Msumbiji baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Rasilimali Watu (Africa Human Capital Heads of State Summit)

Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akiwaaga watanzania wakati wa kuondoka nchini na kurejea Msumbiji baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Rasilimali Watu (Africa Human Capital Heads of State Summit)

Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stergomena Tax wakimuaga Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi


MHE. RAIS SAMIA AFUNGUA RASMI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA KUHUSU RASILIMALI WATU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa nchi za Afrika kuwekeza zaidi katika kuboresha afya, elimu na lishe kwa watu wake ili kutengeneza rasilimali watu inayoweza kuchangia maendeleo na ukuaji wa uchumi barani Afrika.

 

Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam leo tarehe 26 Julai 2023 wakati akifungua rasmi Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere.

 

Amesema Mkutano huu umetoa fursa kwa nchi za Afrika kujadili na kupanga mikakati mipya ya namna ya kutumia Rasilimali Watu ambayo Afrika imejaliwa kuwa nayo kama nyenzo muhimu katika kuchangia maendeleo na mafanikio ya Bara la Afrika.

 

Ameongeza kusema kwa upande wa Tanzania tayari mikakati mbalimbali imewekwa ya kuendeleza Rasilmali Watu ikiwemo kutenga fedha kwa ajili ya kuongeza afua za lishe na huduma za afya ya mama na mtoto ambapo amesema ameingia mkataba na Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanasimamia suala hili katika mikoa yao.

 

Amesema ifikapo mwaka 2050 Afrika itakuwa na asilimia 42 ya vijana duniani kote hivyo uwekezaji kwenye rasilimali watu yenye tija unahitajika ili kuwa na hatima nzuri. Amesema jitihada zaidi zinahitajika ili kuepuka kuzalisha vijana wasio na ujuzi, wasio ajirika na vijana wenye kujiingiza kwenye vitendo viovu vya kihalifu na uvunjifu wa amani.

 

Ameongeza kusema uwekezaji kwenye rasilimali watu unaanza tangu mtoto anapozaliwa kwa kumpatia lishe bora na chanjo stahiki ili kuondoa udumavu ambao husababisha upungufu wa uelewa na uwezo wa kusoma vizuri kwa watoto. Pia amesisitiza kuwekeza katika elimu ya awali ambayo ni msingi wa kuwaandaa watoto kimwili, kiakili, kihisia na kiubunifu.

 

Kadhalika ameeleza kuwa Tanzania inaendelea kuboresha utoaji huduma za jamii na kufanya maboresho ya miundombinu kama madarasa, vituo vya afya, kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa sekta ya elimu na afya na kutekeleza mpango wa elimu bure kwa shule za msingi hadi sekondari.

 

Awali akizungumza, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuridhia Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano huo muhimu ambao amesema umehudhuriwa na zaidi ya Washiriki 2,500. Pia ameipongeza na kuishukuru Benki ya Dunia kwa kuandaa mkutano huo kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

 

Amesema Mkutano huo ni jukwaa kwa nchi za Afrika kupanga mikakati bora zaidi ya kuendeleza rasilimali watu kwa maendeleo endelevu ya Bara la Afrika.

 

Naye Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa amesma Benki hiyo itaendelea kushirikiana na kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na Nchi za Afrika katika kuendeleza rasilimali watu ili hatimaye kuwa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

 

Mkutano huo ambao umehudhuriwa na Wakuu wa Nchi kutoka Nchi sita za Kenya, Madagascar, Sao Tome na Principe, Sierra Leone, Malawi na Msumbiji na wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi naza umma umemalizika kwa kupitishwa kwa Azimio la Dar es Salaam ambalo limeainisha mikakati ya kuboresha maendeleo ya rasilimali watu barani Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua rasmi Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Afrika Kuhusu Rasililmali Watu uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 26 Julai 2023

Mhe. Rais Samia akihutubia mkutano
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akitoa neno la utangulizi wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu kabla ya kumkaribisha Mhe. Rais Samia kufungua rasmi mkutano huo.
 
Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Victoria Kwakwa akizungumza wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu
 
Marais kutoka Nchi za Afrika ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. Kutoka kushoto ni Rais wa Kenya, Mhe. William Ruto, Rais wa Malawi, Mhe. Lazarus Chakwera na Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi
 
Mhe. Rais Dkt. Samia (wa nne kushoto) akiwa na Marais walioshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. Kutoka kushoto ni Mhe. Rais Ruto, Mhe. Rais Chakwera, Mhe. Rais Nyusi, Mhe. Rais Andry Rajoelina wa Madagascar, Mhe. Rais Carlos Vila Nova wa Sao Tome na Principe na Mhe. Rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone

Mhe. Dkt. Tax akiteta jambo na Mhe. William Lukuvi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akifurahia jambo kwa pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliani Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Mohammed Rajab akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Agnes Kayola wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu.
Mkutano ukiendelea
Wageni waalikwa wakishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu.

Katibu Mkuu, Balozi Dkt. Shelukindo akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Mathew Mkingule wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu. Anayeshuhudia  katikati ni Balozi Kasiga

Balozi wa Afrika Kusini nchini, Mhe. Noluthando Mayende-Malepe akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu.

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme (kushoto) akiwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Mteule, Iman Njalikai wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana akishiriki  Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu.

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Caesar Waitara akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu.

Picha ya pamoja

Picha ya pamoja

Picha ya pamoja




 

Tuesday, July 25, 2023

VIONGOZI AFRIKA WAENDELEA KUWASILI NCHINI KUSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI KUHUSU RASILIMALI WATU

Viongozi kutoka mataifa mbalimbali Barani Afrika wameendelea kuwasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023.

Viongozi waliowasili alfajiri ya Leo tarehe 25 Julai 2023, ni Makamu wa Rais wa Zambia, Mhe. W.K. Mutale Nalumango,  Makamu wa Rais wa Benin, Mhe. Madam Mariam Chabi Talata, Waziri Mkuu wa Eswatini, Mhe. Cleopas Sipho Dlamin, Waziri Mkuu wa Somalia, Mhe. Hamze Abdi Barre.

Wengine ni Waziri wa Elimu wa Misri, Mhe. Reda Hegazy, Waziri wa Fedha wa Djibouti, Mhe. Ilyas Moussa Dawaleh pamoja na Waziri Ofisi ya Rais  - Namibia, Mhe. Christine Hoebes.
Makamu wa Rais wa Zambia, Mhe. W.K. Mutale Nalumango akisalimiana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023

Makamu wa Rais wa Zambia, Mhe. W.K. Mutale Nalumango akizungumza na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023

Makamu wa Rais wa Benin, Mhe. Madam Mariam Chabi Talata akipokelewa na Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam  kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023

Makamu wa Rais wa Benin, Mhe. Madam Mariam Chabi Talata katika mazungumzo na Waziri wa Maji, Mhe. Juma Aweso baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam  kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023

Waziri Mkuu wa Eswatini, Mhe. Cleopas Sipho Dlamin akizungumza na Waziri wa nchi Afisi ya Rais Ikulu - Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam  kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023

Waziri Mkuu wa Somalia, Mhe. Hamze Abdi Barre akifurahia jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega baada ya kuwasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023

Waziri wa Elimu wa Misri, Mhe. Reda Hegazy akiwa na Balozi wa Misri nchini, Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail baada ya kuwasili kuwasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu kuanzia tarehe 25 - 26 Julai, 2023 





Monday, July 24, 2023

VIONGOZI MBALIMBALI WAENDELEA KUWASILI NCHINI KUSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI KUHUSU RASILIMALI WATU

Viongozi mbalimbali kutoka Barani Afrika wameendelea kuwasili nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu utakayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam, tarehe 25 - 27 Julai 2023. 

Leo tarehe 24 Julai 2023, kwa nyakati tofauti viongozi mbalimbali wamewasili nchini kushiriki Mkutano huo. Viongozi waliowasili leo ni mke wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Mama Graca Machel, Balozi wa Ivory Coast nchini Afrika Kusini, Mhe. Sakaria Kone.

Wengine ni Waziri wa Fedha wa Kenya, Mhe. Prof. Njuguna Ndug’u, Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini, Mhe. Dr. Bonginkosi Nzimande pamoja na Waziri wa Elimu wa Togo, Mhe. Prof. Dodzi Komla Kokoroko.

Mbali ya Wakuu wa Nchi na Serikali, mkutano huo utawahusisha Mawaziri wa Fedha, Mawaziri wa Sekta nyingine zinazohusika na maendeleo ya Rasilimaliwatu, Watendaji Wakuu wa Benki ya Dunia na watu mashuhuri.
 
Mke wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Mama Graca Machel akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mama Machel yupo nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu utakayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam, tarehe 25 - 27 Julai 2023.  

Mke wa Rais wa zamani wa Msumbiji, Mama Graca Machel akizunguza na Waziri wa Nchi Utawala na Utumishi wa Umma - Msumbiji, Mhe. Ana Comoane baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Ivory Coast nchini Afrika Kusini, Mhe. Sakaria Kone akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu tarehe 25 - 27 Julai 2023 
Balozi wa Ivory Coast nchini Afrika Kusini, Mhe. Sakaria Kone akizungumza na mmoja kati ya wajumbe alioambatana na kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu tarehe 25 - 27 Julai 2023 

Waziri wa Elimu wa Togo, Mhe. Prof. Dodzi Komla Kokoroko  akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu tarehe 25 - 27 Julai 2023 
Waziri wa Elimu wa Togo, Mhe. Prof. Dodzi Komla Kokoroko  pamoja na ujumbe wake wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Viongozi hao wapo nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu tarehe 25 - 27 Julai 2023 

Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini, Mhe. Dr. Bonginkosi Nzimande akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusu Rasilimali Watu tarehe 25 - 27 Julai 2023 
Waziri wa Elimu wa Afrika Kusini, Mhe. Dr. Bonginkosi Nzimande akizungmza na Balozi wa Afrika Kusini nchini, Mhe. Noluthando Mayende-Malepe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Fedha wa Kenya, Mhe. Prof. Njuguna Ndug’u (kushoto) akizungumza na mmoja kati ya wajumbe wake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam