Balozi wa Tanzania nchini
Japan, Mhe. Baraka Luvanda amewahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Japan kuja kuwekeza
nchini kwenye zao la kahawa na mazao mengine ya kimkakati.
Rai hiyo ameitoa hivi karibuni wakati akifungua semina maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya
Tanzania ikiwa ni siku ya pili ya Maonesho ya Kimataifa ya Kahawa yaliyofanyika
kwa siku tatu nchini Japan kuanzia tarehe 27 hadi 29 Septemba 2023.
Semina
hiyo ilipata mwitikio mkubwa kwa kuhudhuriwa
na wadau wa kahawa wapatao
80 wa ndani na nje ya Japan ambapo
Tanzania ilitumia fursa hiyo kutangaza kahawa ya Tanzania na zoezi la uonjaji wa sampuli za kahawa ya Tanzania kutoka kampuni 30 zilizopo
nchini lilifanyika. Sampuli hizo ni za kahawa ya
Arabica laini Arabica ngumu na kahawa ya Robusta.
Tanzania
inasifika Japan kwa kutoa kahawa bora aina ya Arabica inayolimwa katika mikoa
ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara,
Mara, Tanga, Morogoro, Njombe, Iringa, Katavi, Rukwa, Ruvuma, Kigoma, Songwe na Mbeya; na kahawa
ya Robusta inayolimwa mkoani Kagera.
Mbali
na kuinadi Tanzania pamoja na vivutio
vyake nchini Japan, kahawa ya Tanzania
ni miongoni mwa vivutio hivyo ambapo imeweza kujipatia umaarufu mkubwa kutokana
na ladha ya kipekee na kupewa Jina la
Kibiashara la Tanzania Kilimanjaro Coffee.
Jina hili hutumika nchini Japan kwa
kahawa zinazozalishwa Tanzania pekee, kwa kutambua kivutio kikubwa cha Mlima Kilimanjaro uliopo nchini Tanzania.
Kadhalika, Tanzania imeshiriki Maonesho hayo ya Kimataifa ya Kahawa kama mdau mkubwa wa kahawa duniani ambapo kwa
mwaka huu yametimiza miaka 20 tangu kuanzishwa
kwake mwaka 2003. Maonesho ya mwaka huu, yameshirikisha makampuni na taasisi zinazohusika na kahawa zipatazo 250 kutoka
nchi zinazozalisha kahawa duniani na kuhudhuriwa na wadau wa kahawa wapatao 45,000
wakiwemo, wazalishaji na wanunuzi.
|
Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Baraka Luvanda (mwenye scarf ya bendera ya Tanzania) akifungua semina maalum iliyoandaliwa wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Kahawa yaliyofanyika kwa siku tatu nchini Japan kuanzia tarehe 27 hadi 29 Septemba 2023. Semina hiyo pamoja na mambo mengine ililega kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana kwenye sekta ya kilimo hapa nchini ikiwemo kilimo cha kahawa |
|
Washiriki wa Semina wakifuatilia hafla ya ufunguzi |
|
Zoezi la uonjaji wa kahawa ya Tanzania likiendelea wakati wa maonesho ya kimataifa ya Kahawa yaliyofanyika Japan kuanzia tarehe 27 hadi 29 Septemba 2023 |
|
Balozi Luvanda katika picha ya pamoja na washiriki na wadau wa kahawa kutoka Tanzania na Japan |
|
Picha ya pamoja |