Monday, October 9, 2023

TANZANIA NA INDIA ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Tanzania na India zimekubaliana kuimarisha ushirikiano kwenye maeneo ya kimkakati ambayo yana manufaa  kwa wananchi wa pande zote mbili ikiwemo maji, kilimo, nishati, teknolojia, afya, ulinzi na usalama, utamaduni na michezo, uchukuzi  na biashara na uwekezaji.

 

Hayo yamebainishwa wakati wa mkutano wa pamoja na Waandishi wa Habari  mara baada ya mazungumzo ya faragha kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi yaliyofanyika katika jengo la kupokelea wageni wa kitaifa la Hyderabad House jijini New Delhi tarehe 09 Oktoba 2023.

 

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhe. Rais Dkt. Samia ameipongeza Serikali ya India kwa kuendelea kuwa mshirika muhimu na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya Tanzania hususan kwenye maeneo ya kimkakati kama maji, afya, kilimo, teknolojia, ulinzi na usalama, na baiashara na uwekezaji.

 

Pia amesema Tanzania inapongeza uamuzi wa Serikali ya India wa kuanziasha kampasi ya kwanza la Taasisi ya Teknolojia ya India nje ya nchi hiyo ambayo itaanzishwa hivi karibuni Zanzibar na kuutaja uamuzi huo kama heshima na upendeleo kwa Tanzania kwani utawanufaisha watanzania, Afrika Mashariki na Kati.

 

Akizungumzia biashara baina ya nchini hizi, Mhe. Rais Samia amesema, thamani ya ufanyaji biashara kati ya Tanzania na India imeendelea kuongezeka ambapo kwa takwimu zilizopo nchini biashara kati ya nchi hizi mbili imeongezeka hadi kufikia Dola za Marekani  Bilioni 3.1 mwaka 2022 kutoka Dola za Marekani Bilioni 2.6 mwaka 2017.

 

Kwenye medani za ushirikiano wa kimataifa, Mhe. Rais Samia amempongeza Waziri Mkuu Modi kwa kuandaa kwa mafanikio Mkutano wa Wakuu wa Nchi za G20 uliofanyika nchini hapa mwezi Septemba 2023 ambapo Afrika kupitia Umoja wa Afrika imefanikiwa kuwa mwanachama wa kudumu wa Umoja huo.  

 

“Siwezi kusita kuipongeza India kwa kufanikiwa kuandaa Mkutano wa G20 ambao ulishuhudia Afrika inakuwa mwanachama kamili wa G20, nampongeza Waziri Modi kwa kutetea mpango wa kupunguza madeni kwa mataifa madogo na kutangaza mpango wa dharura wa kuhamasisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya nchi zinazoendelea ili kuwezesha upatikanaji wa teknolojia ya nishati safi ifikapo mwaka 2050” amesema Mhe. Rais Samia.

 

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Modi ameitaja Tanzania kama mshirika wake wa karibu na  mkubwa katika  maendeleo barani Afrika na kwamba nchi hizo zimekubaliana kuupeleka ushirikiano uliopo katika viwango vya juu kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na India.

 

Amesema India itaendelea kushirikiana na Tanzania kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo ya kukuza ujuzi, usambazaji maji, teknolojia ya habari na mawasiliano na uhusiano wa watu wa India na Tanzania, nishati safi na ulinzi na usalama.

 

Pia ameongeza kusema nchi hizo zimekubaliana kuwa na mpango wa miaka mitano wa ushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama hususan katika maeneo ya kujenga uwezo, mafunzo na ulinzi baharini.

 

Akizungumzia ushirikiano katika biashara, Mhe.  Modi amesema nchi hizo zimekubaliana kuangalia uwezekano wa kuongeza biashara kwa kutumia sarafu za nchi zao kwa lengo la kupunguza gharama na matumizi ya Dola za Marekani.

 

Wakati wa Mkutano huo, Mhe. Rais Samia na Mhe. Modi walishuhudia ubadilishanaji wa Hati Sita za Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Hati 14 na Mkataba mmoja zilizosainiwa kati ya Tanzania na India wakati wa ziara hii. Hati hizo zinagusa sekta za Uchukuzi, Utamaduni, Michezo, Uwekezaji, TEHAMA na Elimu.

 

Mhe. Dkt. Rais Samia yupo nchini India kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu kuanzia tarehe 8 hadi 11 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya faragha kati yao  yaliyofanyika katika jengo la kupokelea wageni wa kitaifa la Hyderabad House jijini New Delhi, India tarehe 09 Oktoba 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya faragha kati yake na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi yaliyofanyika katika jengo la kupokelea wageni wa kitaifa la Hyderabad House jijini New Delhi, India tarehe 09 Oktoba 2023

Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi  akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya faragha kati yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  wa India, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yaliyofanyika katika jengo la kupokelea wageni wa kitaifa la Hyderabad House jijini New Delhi, India tarehe 09 Oktoba 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa pamoja na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi, wakiwashuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba  na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Dkt. Subrahmanyam Jaishankar wakibadilishana moja ya Hati za Makubaliano ya Ushirikiano zilizosainiwa wakati wa ziara ya Mhe. Rais Dkt. Samia nchini India
Uadilishanaji wa Hati za Makubaliano ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (kulia) akiwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega wakifuatilia Mkutano wa Mhe. Rais Dkt. Samia na Mhe.Modi na waandishi wa habari uliofanyika jijini New Delhi wakati wa ziara ya Mhe. Rais Dkt. Samia nchini India

Mhe. Rais Samia akiwa na Mhe. Modi mara baada ya kuwasili katika jengo la kupokelea wageni wa kitaifa la Hyderabad House jijini New Delhi, India tarehe 09 Oktoba 2023

Mhe. Rais Samia akiwa na Mhe. Modi mara baada ya kuwasili katika jengo la kupokelea wageni wa kitaifa la Hyderabad House jijini New Delhi, India tarehe 09 Oktoba 2023



 

Sunday, October 8, 2023

MTENDAJI MKUU WA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA OMAN ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA KAOLE- BAGAMOYO



Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi akiangalia mabaki ya vitu mbalimbali vilivyohifadhiwa katika  Makumbusho ya Kaole mjini Bagamoyo Mkoani Pwani alipotembelea kujionea historia ya mabaki ya mawe ya zamani, magofu na vitu vingi vya kale yakiwemo makaburikatika makumbusho hiyo


Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal Al-Moosawi akiangalia mabaki ya vitu mbalimbali vilivyohifadhiwa katika makumbusho ya Kaole mjini Bagamoyo


Mhifadhi wa makumbusho katika Makulbusho ya Kaole mjini Bagamoyo akimuelezea Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal Al-Moosawi historia ya vitu vivyohifadhiwa katika Makumbusho hiyo


Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akiangalia gofu lenye mnara mrefu alipotembelea Makumbusho ya Kaole mjini Bagamoyo


Balozi wa Oman nchini Mhe. Saud bin Hilal Alshaidani akisoma  historia ya watu na mabaki ya vitu mbalimbali vilivyohifadhiwa katika Makumbusho ya Kaole mjini Bagamoyo alipotembelea makumbusho hiyo

Balozi wa oman nchini Mhe. Saud bin Hilal Alshaidani akinawa maji maarufu yanayopatikana katika kisima kinachoaminika kuchimbwa katika karne ya 13 mjini Bagamoyo katika Makumbusho ya Kaole  alipotembelea makumbusho hiyo

Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akiangalia Kisima cha maji maarufu yanayopatikana katika kisima kinachoaminika kuchimbwa na kutumika katika karne ya 13 mjini Bagamoyo katika Makumbusho ya Kaole  alipotembelea makumbusho hiyo


Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akinawa maji ya kisima maarufu ya kaole alipotembelea makumbusho hayo
Mmoja wa wageni kutoka Makumbusho ya Taifa ya Oman akinawa maji maarufu yanayopatikana katika makumbusho ya kaole mjini Bagamoyo walipotembelea makumbusho hayo mjini Bagamoyo mkoani Pwani

 

Ujumbe wa Makumbusho ya Taifa ya Oman ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi umetembelea Makumbusho ya Kaole yaliyoko Bagamoyo Mkoani Pwani na kujionea mabaki ya mawe ya zamani, magofu na vitu vingi vya kale yakiwemo makaburiambayo ni sehemu ya historia ya kale vilivyotumiwa na Waarabu katika karne ya 13 mpaka karne ya 16.
 

Ujumbe huo kutoka Oman ambao uko nchini kukutana na wenzao wa Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Oman ulihudhuria Mkutano wa Kwanza wa Pamoja wa Wataalamu kati ya Makumbusho ya Taifa ya Tanzania na Makumbusho ya Taifa ya Oman.
 

Ujumbe huo uliambatana na Balozi wa Oman nchini Tanzania Mheshimiwa Saud bin Hilal Alshaidani Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Dkt. Oswald Masebo na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga.

Ujumbe huo kutoka Makumbusho ya Taifa ya Oman unatarajia kwenda katika Visiwa vya Zanzibar ambako utatembelea Mji Mkongwe, Makumbusho ya amani na historia ya Mnazi Mmoja, Jumba la Kibweni na Magofu ya Mtoni. 

Ujumbe huo pia utatembelea Pango la Kuumbi la Jambiani na Makumbusho ya Unguja Kuu kwa ajili ya kujifunza na kujionea historia ya Zanzibar. 


Ujumbe huo kutoka nchini Oman uliwasili nchini tarehe 05 Oktoba, 2023 unatarajiwa kuondoka nchini tarehe 12 Oktoba 2023 kupitia Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

UJUMBE WA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA OMAN WATEMBELEA MAKUMBUSHO YA KUNDUCHI

 

Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi akisini kitabu cha wageni alipowasili katika  Makumbusho ya Kunduchi jijini Dar es Salam, kulia ni Balozi wa Oman nchini Mheshimiwa Saud bin Hilal Alshaidani


Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akitembelea magofu ya Makumbusho ya Kunduchi jijini Dar es Salaam alipotembelea makumbusho hiyo

Mtendaji Mkuu wa makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akiangalia mabaki ya magofu yanayopatikana katika Makumbusho ya Kunduchi jijini Dar es Salaam alipotembelea makumbusho hiyo

Mtendaji Mkuu wa makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi na ujumbe wake wakiangalia mabaki ya magofu yanayopatikana katika Makumbusho ya Kunduchi jijini Dar es Salaam walipotembelea makumbusho hiyo

Mtendaji Mkuu wa makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi na ujumbe wake wakiangalia mabaki ya magofu yanayopatikana katika Makumbusho ya Kunduchi jijini Dar es Salaam walipotembelea makumbusho hiyo



Ujumbe wa Makumbusho ya Taifa ya Oman ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mheshimiwa Jamal al-Moosawi umetembelea Makumbusho ya Kunduchi jijini Dar es Salam.


Katika Makumbusho hiyo yamehifadhiwa magofu ya Kale ambayo ni Makaburi ya masultani waliozikwa na binti vigori wakiwa hai ili kumsindikiza sultan katika safari yake hiyo ya kaburini na Msikiti uliotumika tangu karne ya 15.


Ujumbe huo kutoka Oman ambao uko nchini uliambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Abdallah Kilima na Balozi wa Oman nchini Tanzania Mheshimiwa Saud bin Hilal Alshaidani.


Ujumbe huo pia uliambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Dkt. Oswald Masebo na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga.

UJUMBE WA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA OMAN WATEMBELEA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO

Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Dkt. Oswald Masebo (wa Kwanza kushoto),  Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Abdallah Kilima (wa pili kushoto) na Balozi wa Oman nchini Mhe. Saud bin Hilal Alshaidani walipotembelea kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam 

 

Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akisaini kitabu cha Kumbukumbu ya wageni katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam alipotembelea makumbusho hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Oswald Masebo walipotembelea Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.


Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akipanda mti alipotembelea Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam


Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akiwa ndani ya nyumba iliyohifadhiwa katika  Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam alipotembelea makumbusho hiyo

Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa makumbusho alipotembelea  Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam

Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akiangalia ngoma ya utamaduni alipotembelea Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam

Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi wa makumbusho alipotembelea  Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam


Mtendaji Mkuu wa Makumbusho ya Taifa ya Oman Mhe. Jamal al-Moosawi katika picha ya pamoja na ujumbe wake walipotembelea  Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam



Ujumbe kutoka Makumbusho ya Taifa ya Oman ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Makumbusho hiyo Mheshimiwa Jamal al-Moosawi umetembelea Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujifunza na kujionea historia, mila na tamaduni za makabila mbalimbali ya Tanzania. 

 
Ujumbe huo kutoka nchini Oman ambao uko nchini umeambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Abdallah Kilima na Balozi wa Oman nchini Tanzania Mheshimiwa Saud bin Hilal Alshaidani.
Ujumbe huo pia uliambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa Dkt. Oswald Masebo na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Noel Lwoga.

 
Akiongea baaada ya kutembelea Kijiji cha Makumbusho Mhe. Al Moosawi alielezea kuridhishwa kwake na uhifadhi wa historia ya makabila ya Tanzania ambayo ameisikia na kuona jinsi nyumba za makabila hayo kama zilivyooneshwa katika eneo hilo na kupongeza jitihada za kuhifadhi historia hiyo kwa ajili ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.

Kijiji cha makumbusho ni eneo linalohifadhi mifano ya nyumba na vifaa vya makabila na tamaduni mbalimbali zinazopatikana Tanzania.
Eneo hilo lilianzishwa mwaka 1966 kwa ajili ya kuonyesha na kutunza tamaduni za asili, ngoma na tamaduni za makabila mbalimbali kama Wanyakyusa, Wamakonde, Wamasai, Wachagga, Wahaya, Wangoni, Wayao na mengine mengi.

 

PRESS STATEMENT