Monday, November 13, 2023
WAZIRI MAKAMBA AWASILI UHOLANZI KWA ZIARA YA KIKAZI
Sunday, November 12, 2023
TANZANIA NA FINLAND KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO KUMUENZI HAYATI AHTISAARI
Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano na Finland ili kuenzi misingi mizuri ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili iliyowekwa na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Hayati Martti Ahtisaari.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipozungumza katika hafla
ya kumbumbuku ya kumuenzi Hayati Ahtisaari iliyofanyika jijini Helsinki
Finland tarehe 11 Novemba 2023.
Amesema Hayati Ahtisaari ambaye dunia inamtambua kwa mchango wake mkubwa katika
kutetea amani, Tanzania itaendelea kumuenzi na kutambua mchango wake mkubwa
alioutoa katika kuimarisha ushirikiano na Tanzania tangu akiwa Balozi wa
Finland nchini Tanzania mwaka 1973 hadi 1976 na alipokuwa Rais wa nchi hiyo
mwaka 1994 hadi 2000.
Amesema kupitia misingi hiyo, Finland imekuwa mshirika mzuri wa
Tanzania katika kutekeleza agenda mbamlimbali za maendeleo na kwamba
mchango wa nchi hiyo kwenye sekta mbalimbali za maendeleo utaendelea
kubaki kama alama ya kukumbukwa tangu Tanzania ilipotoka na ilipo sasa.
“Ninayo furaha kusema kwamba, Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuhakikisha uhusiano mzuri uliopo kati ya
nchi hizi mbili na watu wake unaimarika siku hata siku” alisisitiza Mhe. Balozi
Mbarouk.
Vilevile amesema kuwa, mtazamo wa Tanzania na Filand katika agenda
mbalimbali za kimataifa unafanana, hivyo Tanzania itaendelea kushirikiana na
nchi hiyo kuhakikisha agenda hizo ikiwemo kuleta maendeleo ya kiuchumi
duniani, ulinzi wa amani na mapambano dhidi ya umaskini zinatekelezwa ili
kuifanya dunia mahali salama pa kila mmoja kuishi.
Kadhalika Mhe. Balozi Mbarouk amepongeza kuwepo kwa Mfuko wa Amani wa Martti
Ahtisaari (CMI) ambao una jukumu kubwa la kuendelea kuenzi urithi mwema
aliouacha Hayati Ahtisaari ambaye anatambulika kama mtetezi bingwa wa Amani
duniani.
Mhe. Balozi Mbarouk alitoa hotuba hiyo kwa niaba ya Rais Mstaafu,
Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya kitaifa ya Hayati
Ahtisaari yaliyofanyika jijini Helsiknki tarehe 10 Novemba 2023.
Mhe.
Balozi Mbarouk akiendelea na hotuba yake, ambapo pamoja na mambo
mengine alisema Tanzania itaimarisha ushirikiano na Finland kumuenzi
Hayati Ahtisaari |
Mhe. Balozi Mbarouk akihutubia |
Saturday, November 11, 2023
KIKWETE AMWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE MAZISHI YA RAIS WA ZAMANI WA FINLAND
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete akimpa pole Mjane wa Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari |
Hafla ya Mazishi ya Kitaifa ya Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari ikiendelea Helsinki tarehe 10 Novemba 2023 |
Thursday, November 9, 2023
Wednesday, November 8, 2023
MAPENDEKEZO YA TUME YA HAKI JINAI NCHINI YAANZA KUTEKELEZWA
Kamati ya Kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Kurekebisha Mifumo ya Haki Jinai nchini imekutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wanaowakilisha nchi na taasisi zao nchini.
Kamati hiyo imewahakikishia Mabalozi na wawakilishi hao kuwa baadhi ya mapendekezo yameanza kufanyiwa kazi na Serikali.
Akizungumza na mabalozi na wawakilishi hao kuwapa mrejesho wa taarifa ya tume ya kuboresha muundo wa taasisi za haki jinai Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Kurekebisha Mifumo ya Haki Jinai, Jaji Mstaafu Mhe. Othman Chande amesema Serikali imeanza kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyowasilishwa na tume hiyo.
Amesema baadhi ya mapendekezo yaliyoanza kutekelezwa ni pamoja na kufunguliwa kwa Ofisi 50 za Mkurugenzi wa Mashitaka katika ngazi ya wilaya nchini ili kusaidia upatikanaji wa haki nchini ikiwa ni moja ya mapendekezo ya kuboresha mfumo wa haki jinai nchini.
Amesema kufunguliwa kwa ofisi hizo za mashitaka katika wilaya 50 nchini ni jambo lililopendekezwa na tume tangu awali.
Mhe. Jaji Mustafa Chande alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliunda tume hiyo mwezi Januari 2023 ikiwa na wajumbe tisa na kuipa kazi ya kupitia na kutoa mapendekezo ya kuboresha mfumo wa taasisi za haki jinai nchini kazi iliyokamilika na kuwasilishwa mwezi Julai 2023.
Aliongeza kuwa baada ya kupokea mapendekezo zaidi ya 360 ya tume hiyo yaliyolenga kuboresha taasisi za haki jinai, aliibadilisha tume hiyo na kuwa Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa mapendekezo hayo na kusaidia Serikali kuandaa mpango wa utekelezaji wa mapendekezo hayo.
Akizungumza katika kikao hicho, Kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Balozi wa Visiwa vya Comoro, Dkt. Ahamada El Badaoui alisema kazi iliyofanywa na tume ni njema na wao kama mabalozi wanaunga mkono juhudi za serikali katika kutoa haki na kuahidi kuendelea kutoa mchango wao wa ushirikiano na Tanzania.
Naye Balozi wa Nigeria nchini, Mhe. Hamisu Umar Takamawa ameipongeza Kamati kwa kufanya kazi ndani ya muda mfupi na kuja na mapendekezo ambayo ni mazuri na kusema Tanzania ikiyatekeleza itapiga hatua zaidi na kusema Nigeria wana cha kujifunza kupitia tume hiyo.
“Tumefarijika na taarifa hii, kwa kweli Nigeria tutakuja kuiga mfano huu wa kutekeleza haki jinai hapa Tanzania,” Alisema Balozi Takamawa
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), Bi. Shalini Bahuguna ameipongeza tume kwa kuweka mapendekezo ya kuboresha haki za mtoto na kueleza kuwa UNICEF ipo tayari kuendeleza ushirikiano na Tanzania katika kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa na kuimarishwa zaidi.
Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia kikao |
Balozi wa Indonesia nchini, Mhe. Tri Yogo Jatmiko akichangia jambo wakati wa Mabalozi wakipatiwa taarifa ya tume ya kuboresha muundo wa taasisi za haki jinai Jijini Dar es Salaam |
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akizungumza kwenye kikao hicho |
BALOZI MBAROUK AMUAGA BALOZI WA AUSTRALIA
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) amemuaga Balozi wa Australia nchini mwenye makazi yake nchini Kenya, Mhe. Luke Williams baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi.
Akizungumza na Mhe. Balozi Williams walipokutana katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Waziri Mbarouk amesema Tanzania na Australia zimekuwa na uhusiano mzuri uliowezesha mataifa hayo kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta za elimu, utalii, madini, nishati, mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na biashara na uwekezaji.
Waziri Mbarouk ameongeza kuwa ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Australia ni jambo lililochochewa na kazi nzuri iliyofanywa na Balozi Williams wakati akitekeleza majukumu yake ya kibalozi.
“Katika kipindi chako umeiwakilisha vyema Australia na kuonesha mafanikio makubwa ambayo yamefikiwa kati ya Tanzania na Australia.
Kazi yako imechochea uboreshaji wa sekta za elimu, utalii, madini, nishati, uchumi wa buluu na kuchangia ukuaji wa sekta ya biashara uwekezaji katika nchi zetu, ni matumaini yangu kuwa utaendelea kuwa Balozi mwema kwa Tanzania nchini Australia na kokote uendako Duniani,” amesema Balozi Mbarouk.
Balozi Mbarouk ameongeza kuwa Australia imekuwa ikitoa fursa za ufadhili wa masomo katika sekta mbalimbali, ila kwa sasa Tanzania inaomba fursa hizo zijikite zaidi katika sekta ya nishati.
Pamoja na mambo mengine, Balozi Mbarouk amemueleza Balozi Williams kuwa kwa sasa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa kiasi kikubwa na kuwaalika wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Australia kuja kuwekeza kwa wingi nchini.
DIPLOMASIA YA UCHUMI NI UTEKELEZAJI WA SERA YA MAMBO YA NJE- BYABATO
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato akifafanua jambo wakati akijibu swali Bungeni |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato akijibu swali Bungeni |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato akisikiliza swali Bungeni |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato akifafanua jambo wakati akijibu swali Bungeni |
Saturday, November 4, 2023
RAIS SAMIA APONGEZA UAMUZI WA SADC KUPELEKA MISHENI YA ULINZI WA AMANI NCHINI DRC
Friday, November 3, 2023
TANZANIA YANUFAIKA KUTOA WALINZI WA AMANI KATIKA MISHENI ZA UMOJA WA MATAIFA
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) akijibu swali Bungeni |
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) ameliambia Bunge kuwa ushiriki wa Tanzania katika Misheni za Ulinzi wa Amani umekuwa na manufaa mbalimbali kwa Taifa ikiwemo mafunzo ya ziada na ajira za kiraia kwa watanzania.
Mhe. Balozi Mbarouk alitoa kauli hiyo Bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi aliyetaka kujua Tanzania inanufaika kiasi gani katika uuzaji wa bidhaa na huduma katika maeneo ambayo Jeshi la Tanzania linafanya ulinzi wa amani.
Balozi Mbarouk amesema kuwa Tanzania imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kushiriki kwenye jitihada mbalimbali za kutafuta amani duniani kama ilivyoainishwa katika Sera ya Mambo ya Nje 2001 na yapo manufaa makubwa katika ushiriki huo.
“Ushiriki wa Tanzania katika Misheni za Ulinzi wa Amani umekuwa na manufaa mbalimbali ikiwemo; Walinda amani wetu kufaidika na mafunzo ya ziada ambayo yanawajenga na kuwaimarisha,” alisema Balozi Mbarouk
Ametaja faida nyingine nchi inayopata kuwa ni pamoja na ajira za kiraia kwa watanzania na kudumisha utamaduni hususan kukua kwa lugha ya Kiswahili na kutolea mfano katika eneo la DRC, Lebanon na Darfur kumekuwa na ongezeko la matumizi ya lugha ya Kiswahili.
Mhe. Balozi Mbarouk amesema mbali na manufaa yaliyoainishwa, zipo fursa za kiuchumi ambazo nchi inazipata katika shughuli za ulinzi wa amani.
Balozi Mbarouk ametaja fursa hizo kuwa ni biashara ya bidhaa zinazotumiwa na vikosi vilivyopo katika Misheni kama chakula, mavazi, vinywaji, vifaatiba na dawa.
“Fursa nyingine ni usafirishaji wa mizigo, ujenzi wa majengo yanayohamishika, vifaa na huduma za TEHAMA na kuongeza kuwa Tanzania inaweza pia kuuza teknolojia ya kutumia panya katika kubaini na kutegua mabomu yaliyotegwa ardhini kama fursa za kiuchumi”, alisema Mhe. Balozi Mbarouk.
Wednesday, November 1, 2023
UJERUMANI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUBORESHA MAKUMBUSHO YA MAJIMAJI
Serikali ya Ujerumani imeahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuboresha Makumbusho ya Majimaji ili kuhifadhi kumbukumbu sahihi kwa ajili ya wakati huu na kwa vizazi vijavyo.
Ahadi hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier alipotembelea Makumbusho ya Vita vya Maji Maji Songea Mkoani Ruvuma.
Mhe., Dkt. Steinmeier amesema Ujerumani ipo tayari kufanya uchambuzi na mchakato wa historia ya vita vya Maji Maji kwakuwa kilichotokea zamani hakipaswi kusauhilka na mtu yoyote.
“Ili kuweka kumbukumbu sawa kwa sasa na kwa wakati ujao, Ujerumani tunaahidi kushirikiana na Tanzania kuboresha makumbusho hii,” alisisitiza Mhe. Rais Steinmeier.
Mhe. Dkt. Steinmeier alisema Ujerumani inatamani kufanya uchambuzi na mchakato wa historia ya ‘Vita vya Maji Maji’ na kuongeza kuwa mchakato huo utahusisha vijana, wanafunzi wa shule na vyuo vikuu, wasomi na wataalamu wa hifadhi na sehemu za kumbukumbu.
“Mwaka 2024, Ujerumani inampango wa kufanya maonesho kwa kushirikiana na Makumbusho ya Taifa ya Tanzania, maonesho hayo yatajulikana kwa jina la “Historia ya Tanzania”, alisema Mheshimiwa Steinmeier.
Awali Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Mb.) alisema historia ya Tanzania na Ujerumani ina sura mbili tofauti. Alifafanua kuwa sura ya kwanza ni kuhusu vita waliyopigana babu zetu na sura ya pili ni yale mazuri yaliyofanywa na Serikali ya Ujerumani Kama vile kujenga shule, hospitali na kutoa huduma nyingine za kijamii.
“Muhimu zaidi ni kukumbuka na kusahau yaliyopita na kuendelea kudumisha uhusiano mzuri uliopo na kusonga mbele kwa kuleta maendeleo kati ya mataifa yetu mawili, lakini pia katika mji wetu wa Songea ,” alisema Dkt. Ndumbaro
Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa Songea wanatamani kuona makumbusho ya kisasa ya ushirikiano kati ya Ujerumani na Tanzania yakijengwa Songea, “pia tunatamani Ujerumani itusaidie kuboresha chuo cha VETA Songea ili kuwawezesha vijana wetu kupata mafunzo mbalimbali,” alisema Dkt. Ndumbaro.
Waziri Ndumbaro pamoja na mambo mengine, ameiomba Serikali ya Ujerumani kushirikiana na Mji wa Songea kwa kuwawezesha kutembeleana, kushirikiana na kuendeleza utani kati ya Wangoni na Wajerumani.
Mheshimiwa Rais Stenmeier mbali na kutembelea Makumbusho ya Vita vya Maji Maji pia ametembelea Shule ya Msingi ya Majimaji.
Makumbusho ya Vita vya Maji Maji ni makumbusho pekee nchini Tanzania inayoonesha historia kubwa ya Vita vya Maji Maji katika harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wajerumani.
Mheshimiwa Rais Stenmeier amehitimisha ziara yake ya Kikazi ya siku tatu nchini leo tarehe 01 Novemba 2023.
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier akiweka shada la maua katika kaburi la walilozikwa mashujaa wa Vita vya Maji Maji |
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier akiweka ua katika kaburi la Chifu Nduna |
Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier akiwa amekaa na wanafunzi wa shule ya Msingi Maji Maji alipofanya ziara shuleni hapo |
Tuesday, October 31, 2023
BALOZI MBAROUK AMPONGEZA DKT. TULIA KWA USHINDI URAIS IPU
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
Balozi Mbarouk aliambatana na Mabalozi watatu (3) waliohusika kwenye Kampeni ya IPU walipoenda kumpongeza kwa ushindi huo na kumhakikishia Ushirikiano wa Wizara katika utekelezaji wa Majukumu yake Mapya.
Mabalozi watatu ni pamoja na Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Uwakilishi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Seiman Suleiman, Naibu Mwakilishi wa Kudumu, Uwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Geneva, Balozi Hoyce Temu pamoja na Balozi Robert Kahendaguza.
Picha ya Pamoja |