Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano na Finland ili kuenzi misingi mizuri ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili iliyowekwa na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Hayati Martti Ahtisaari.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk alipozungumza katika hafla
ya kumbumbuku ya kumuenzi Hayati Ahtisaari iliyofanyika jijini Helsinki
Finland tarehe 11 Novemba 2023.
Amesema Hayati Ahtisaari ambaye dunia inamtambua kwa mchango wake mkubwa katika
kutetea amani, Tanzania itaendelea kumuenzi na kutambua mchango wake mkubwa
alioutoa katika kuimarisha ushirikiano na Tanzania tangu akiwa Balozi wa
Finland nchini Tanzania mwaka 1973 hadi 1976 na alipokuwa Rais wa nchi hiyo
mwaka 1994 hadi 2000.
Amesema kupitia misingi hiyo, Finland imekuwa mshirika mzuri wa
Tanzania katika kutekeleza agenda mbamlimbali za maendeleo na kwamba
mchango wa nchi hiyo kwenye sekta mbalimbali za maendeleo utaendelea
kubaki kama alama ya kukumbukwa tangu Tanzania ilipotoka na ilipo sasa.
“Ninayo furaha kusema kwamba, Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi wa Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuhakikisha uhusiano mzuri uliopo kati ya
nchi hizi mbili na watu wake unaimarika siku hata siku” alisisitiza Mhe. Balozi
Mbarouk.
Vilevile amesema kuwa, mtazamo wa Tanzania na Filand katika agenda
mbalimbali za kimataifa unafanana, hivyo Tanzania itaendelea kushirikiana na
nchi hiyo kuhakikisha agenda hizo ikiwemo kuleta maendeleo ya kiuchumi
duniani, ulinzi wa amani na mapambano dhidi ya umaskini zinatekelezwa ili
kuifanya dunia mahali salama pa kila mmoja kuishi.
Kadhalika Mhe. Balozi Mbarouk amepongeza kuwepo kwa Mfuko wa Amani wa Martti
Ahtisaari (CMI) ambao una jukumu kubwa la kuendelea kuenzi urithi mwema
aliouacha Hayati Ahtisaari ambaye anatambulika kama mtetezi bingwa wa Amani
duniani.
Mhe. Balozi Mbarouk alitoa hotuba hiyo kwa niaba ya Rais Mstaafu,
Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya kitaifa ya Hayati
Ahtisaari yaliyofanyika jijini Helsiknki tarehe 10 Novemba 2023.
Mhe.
Balozi Mbarouk akiendelea na hotuba yake, ambapo pamoja na mambo
mengine alisema Tanzania itaimarisha ushirikiano na Finland kumuenzi
Hayati Ahtisaari |
Mhe. Balozi Mbarouk akihutubia |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.