Waziri wa Uchumi wa Buluu
na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Suleiman Masoud Makame ameongoza ujumbe wa Tanzania
kwenye Mkutano wa Tatu wa Mawaziri kuhusu Usalama na Ulinzi wa Bahari Magharibi mwa Bahari ya Hindi uliofanyika Balaclava
nchini Mauritius tarehe 16 Novemba 2023.
Mkutano huo ambao
umeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Biashara za
Kimataifa ya Mauritius kwa kushirikiana na Kamisheni ya Bahari ya Hindi, pamoja
na mambo mengine ulipokea taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya mikutano ya
aina hiyo iliyofanyika mwaka 2018 na 2019 pamoja na kujadili hatua za kuchukua
ili kuimarisha ulinzi na usalama wa bahari.
Kadhalika, wakati wa
Mkutano huo, Nchi mbalimbali, Mashirika ya Kimataifa na kikanda na wadau wa
maendeleo zilipitisha Azimio la Pamoja kuhusu umuhimu wa ushirikiano na nguvu ya pamoja katika kulinda watumiaji wa
Bahari ya Hindi dhidi ya changamoto mbalimbali zinazotokana na matumizi ya bahari
ikiwemo ongezeko la makosa yanayovuka mipaka, uharamia na uvuvi haramu.
Ujumbe wa Tanzania ulimjumuisha
pia Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Rosemary Jairo, Mwakilishi wa Heshima wa
Tanzania nchini Mauritius, Bw. Marday Venkatasamy na Maafisa Waandamizi kutoka Shirika
la Uwakala wa Meli Tanzania na Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe ambao
unawakilisha pia nchini Mauritius.
|
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Zanzibar, Mhe. Suleiman Masoud
Makame (wa pili kulia) akishiriki Mkutano wa Tatu wa Mawaziri kuhusu
Usalama na Ulinzi wa Bahari Magharibi mwa Bahari ya Hindi uliofanyika
Balaclava
nchini Mauritius tarehe 16 Novemba 2023. Mhe. Makame aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo.
|
|
Waziri
wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Suleiman Masoud Makame (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi
wa Heshima wa Tanzania nchini Mauritius, Bw. Marday Venkatasamy. Mhe. Makame aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye
Mkutano wa Tatu wa Mawaziri kuhusu Usalama na Ulinzi wa Bahari Magharibi mwa Bahari ya Hindi uliofanyika Balaclava
nchini Mauritius tarehe 16 Novemba 2023. |
|
Waziri wa Waziri
wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Suleiman Masoud Makame (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi
wa Heshima wa Tanzania nchini Mauritius, Bw. Marday Venkatasamy, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Rosemary Jairo (wa pili kulia) na Afisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe ambao unawakilisha pia Mauritius, Bi. Gwantwa Mwaisaka wakati wa
Mkutano wa Tatu wa Mawaziri kuhusu Usalama na Ulinzi wa Bahari Magharibi mwa Bahari ya Hindi uliofanyika Balaclava
nchini Mauritius tarehe 16 Novemba 2023. |
|
Mhe. Makame (wa nne kulia waliosimama) katika picha ya pamoja na Viongozi wengine walioshiriki Mkutano wa Tatu wa Mawaziri kuhusu Usalama na Ulinzi wa Bahari Magharibi mwa Bahari ya Hindi uliofanyika Balaclava
nchini Mauritius tarehe 16 Novemba 2023. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.