Sunday, November 19, 2023

RAIS SAMIA AMUAGA RAIS WA ROMANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemuaga Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini leo tarehe 19 Novemba 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Pamoja na Rais Samia viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali wameshiriki kumuaga kiongozi huyo ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.).

Viongozi wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Mgeni wake Rais wa Romania Mheshimiwa Klaus Iohannis wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa katika hafla fupi ya kumuaga Rais Iohannis Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Romania Mheshimiwa Klaus Iohannis akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) baada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya kumuaga Rais Iohannis Ikulu Jijini Dar es Salaam


Rais wa Romania, Mheshimiwa Klaus Iohannis akiagana na viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini leo tarehe 19 Novemba 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam
No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.