Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jaji Imani Aboud kutoka Tanzania ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa misaada inayoipatia mahakama hiyo ikiwemo ujenzi wa jengo la ofisi ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilikabidhi eneo la ujenzi kwa Mkandarasi CRJE jijini Arusha tarehe 02 Juni 2023.
Jaji
Aboud ametoa shukrani hizo wakati wa kikao na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb)
kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 15 Juni 2023.
Rais
wa Mahakama ya Afrika na watumishi wengine, wakiwemo Makamu wa Rais; Majaji na
Msajili wapo jijini Dodoma kwa ajili ya kikao (retreat) cha kutathmini
utekelezaji wa majukumu ya Mahakama hiyo ili kubaini mafanikio na changamoto
kwa ajili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Kwa
kutumia fursa ya kikao kufanyika Dodoma, Rais na ujumbe wake wametumia nafasi
hiyo kukutana na wadau mbalimbali ikiwemo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) ili kajadili utekelezaji wa majukumu ya chombo
hicho muhimu barani Afrika.
Kwa
upande wake, Mhe. Waziri Dkt. Tax alieleza kufurahishwa na uamuzi wa Mahakama
hiyo wa kufanya kikao chao jijini Dodoma ambapo ni makao makuu ya nchi. Aidha,
aliwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano unaohitajika ili
mahakama hiyo iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kukamilisha
ujenzi wa jengo la Ofisi.
Mhe. Waziri Dkt. Tax alihitimisha mazungumzo yake kwa kumpongeza Jaji Aboud kwa kuchaguliwa tena kwa kipindi cha awamu ya pili na cha mwisho cha miaka miwili kuwa Rais wa Mahakama hiyo. Jaji Aboud alichaguliwa wakati wa ufunguzi wa Baraza la 69 la Pan-Afrika lililofanyika Arusha tarehe 12 Juni 2023.
Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Jaji Imani Aboud akizungumza wakati wa Mkutano kati yake na Mhe. Dkt. Tax (hayupo pichani) |
Mkutano ukiendelea |
Afisa kutoka Kitengo cha Sheria, Bi. Elizabeth Bukwimba akichangia jambo wakati wa Mkutano kati ya Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Jaji Aboud hawapo pichani |
Mhe. Jaji Aboud akimpatia Mhe, Dkt. Tax zawadi ya nembo ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu mara baada ya kukamilisha mazungumzo yao |
Mhe. Dkt. Tax na Mhe. Jaji Aboud wakijadili jambo baada ya mazungumzo yao |
Picha ya pamoja |
Picha ya pamoja |