Friday, October 25, 2013

Balozi wa India hapa nchini atembelea Wizara

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Omar Mjenga akizungumza na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Debnath Shaw kuhusu kuimarisha  ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na India. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 24 Oktoba, 2013.

Mhe. Shaw akichangia jambo wakati wa mazungumzo yao.
 
Bw. Mjenga akimsikiliza Mhe. Balozi Shaw wakati wa mazungumzo yao. Kushoto ni Bi. Deepa Sehgal, Afisa katika Ubalozi wa India na kulia ni Bw. Charles Faini, Afisa Mambo ya Nje.
 
Bw. Mjenga akiagana na Mhe. Shaw mara baada ya mazungumzo yao.

Balozi wa Pakistan hapa nchini aagwa

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Bibi Angela Kairuki akimkaribisha Balozi wa Pakistan hapa nchini, Mhe. Tajjamul Altaf kwenye hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kwa ajili ya kumuaga Balozi huyo baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini. Anayefuata nyuma ni Balozi Khalfan Mpango, Balozi wa Congo hapa nchini. Mhe. Kairuki alimwakilisha Mhe. Membe kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency.

Mhe. Altaf akishukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka kwa Serikali ya Tanzania katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini.

Mhe. Kairuki, Mhe. Altaf, Mabalozi na Wageni waalikwa wakimsikiliza Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa  alipokuwa akichangia jambo wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Altaf.

Mhe. Kairuki akimkabidhi Mhe. Balozi Altaf zawadi ya picha ya kuchora kama ukumbusho kwake.

Mhe. Kairuki katika picha ya pamoja na Balozi Altaf Mabalozi na Wageni waalikwa.




By Mkumbwa Ally

Tanzania and Pakistan enjoyed notable growth in bilateral trade and economic cooperation in the last three years, with the Asian country expanding participation in the Dar Es Salaam International Trade Fair, said Hon. Angela Kairuki, the Deputy Minister for Justice and Constitutional Affairs.

She commended H.E. Tajammul Altaf, the outgoing Pakistan High Commissioner to Tanzania, for his role in fostering relations between the two countries. "You have been an outstanding diplomat," she told him at a farewell dinner hosted by the Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Hon. Bernard K. Membe on 23 October, 2013.

Hon. Kairuki, who represented Minister Membe, said during Ambassador Altaf's tour of duty, three Pakistan naval ships visited Tanzania and negotiations started to waive visa requirement for Tanzanian diplomatic passport holders visiting Pakistan as a step towards full visa waiver.

The Pakistan High Commission in Tanzania, which was opened in 1967, was closed in 2000 up to 2009, when Ambassador Altaf was appointed to reopen it. "I have enjoyed non-stop hospitality since my arrival in Tanzania and unwavering cooperation from the Ministry of Foreign Affairs," said the envoy, who is being transferred to Prague, Czech Republic.

He accepted Hon. Kairuki's request to be Tanzania's good ambassador and promote the country's tourist attractions in Czech.

Monday, October 21, 2013

Membe revisits the ICC symphony


Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister for Foreign Affairs and International Co-operation revisits the International Criminal Court (ICC) matter against the Kenyan President Uhuru Kenyatta and his deputy William Ruto during his interview with the Clouds FM Radio Station today located in Mikocheni, Dar es Salaam. 

Listening on are Mr. Gerald Hando (left) and Mr. Paul James "PJ" of the Clouds FM Radio Station. 

Hon. Minister Membe reiterates Africa’s view that the ICC was biased against African leaders and that the African Union (AU) has ruled that no sitting African president or anyone with the mandate to act as president should stand trial before the ICC.  Right is Ms. Barbara Hassan of the Clouds FM Radio Station.


Membe revisits the ICC symphony

By TAGIE DAISY MWAKAWAGO

Tanzania’s Minister for Foreign Affairs and International Co-operation says that he expects the United Nations Security Council to defer the cases facing Kenyan President Uhuru Kenyatta, and his deputy, at the International Criminal Court, before November12, when H.E. Kenyatta is due to stand trial.  

Hon. Bernard K. Membe (MP) said in an interview with Clouds FM Radio in Dar es Salaam today, that Africa as a bloc will not understand failure by the UN to endorse the demand for deferral of the cases raised by African Leaders in Addis Ababa, Ethiopia last week.

Minister Membe reiterated Africa’s view that the ICC was biased against African Leaders. The African Union (AU) has ruled that no sitting African president or anyone with the mandate to act as president should stand trial before the ICC. Any charges against such leaders should be deferred until they retire.  

“We were under the impression that ICC would be fair to all accused persons, but it has been sorely targeting African Leaders,” said the Minister, wondering: “To which court are the Western suspects taken?”

The Minister rejected the notion that deferring the cases facing President Kenyatta and his deputy, Hon. William Ruto undermined the 1,200 Kenyans killed in post election violence for which they have been indicted.

“More than 600,000 South Africans were killed during the apartheid era, but the matter was settled through reconciliation, not at The Hague,” he explained.

He said that although President Kenyatta was indicted by the ICC when he was an ordinary citizen, the Court is duty bound to respect his status as Head of State and be sensitive to his responsibility to serve the people of Kenya.
  
Out of 30 cases brought before the ICC so far, 27 are from African Continent.    

Meanwhile, Hon. Membe said the so-called coalition of the willing, under which the other East African Community (EAC) members were convening to fast track political federation, was questionable because it was not endorsed by a formal meeting of all members.

The process was, therefore, clandestine, he said, adding:
“They should invite or at least notify us of their meetings, because leaving us out will not add or diminish anything.”

Uganda, Rwanda, Kenya and Burundi have been meeting without Tanzania to prepare a constitution for political federation, which Hon. Membe said was anomalous because the customs union remained shaky and the monetary union was not yet in place.

The Minister maintained that there could be no EAC without Tanzania. “Let me assure you that Tanzania is strategically located with all kind of resources and food surplus to feed neighboring countries.”

Hon. Membe said that Tanzania has been and will remain the pioneer of peace and security in the region.


End.




Mhe. Membe akutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bibi Ana Teresita Gonzalez Fraga (kushoto) kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba alipofika Wizarani kwa ziara yake ya kikazi hapa nchini.


Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano, Bibi Dora Msechu akifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe.Fraga (hawapo pichani). Wengine ni Bw. Greyson Ishengoma (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Thobias Makoba, Msaidizi wa Waziri Membe.

Mkutano ukiendelea. Mwenye suti nyeusi ni Balozi wa Cuba hapa nchini, Mhe. Jorge Luis Lopes Tormo.



Balozi Msechu akiagana na Mhe. Fraga.


Picha na Reginald Philip Kisaka.

 




Friday, October 18, 2013

Pakistan Ambassador visits Ministry of Foreign Affairs


Ambassador Rajabu Gamaha, Acting Permanent Secretary of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation welcomes H.E. Tajammul Altaf, the High Commissioner for Pakistan to the United Republic of Tanzania.  Ambassador Altaf has just finished his three-years tenure in the country.

Ambassador Gamaha in a discussion with the outgoing Pakistan Ambassador Altaf, who had paid a courtesy visit in the Ministry today in Dar es Salaam.  During their meeting, the two Ambassadors expressed their satisfaction in the areas of cooperation that happily exist between the two countries such as in education sector, business and trade sectors.  

Mr. Omary Mjenga, Acting Director of the Department of Asia and Australasia and Mr. Charles Faini, Foreign Service Officer both from the Ministry of Foreign Affairs were also present during the meeting. 

Ambassador Altaf also took time to thank the Government of Tanzania for its continued support and cooperation with Pakistan during his tenure.  He said that the three-years that he has spent in Dar es Salaam were memorable and he will continue to be a goodwill Ambassador of Tanzania to his future endeavors.  

Ambassador Altaf also took time to meet with Mr. Omary Mjenga prior to his meeting with Ambassador Rajabu Gamaha (not in the photo).   Also in the photo is Mr. Muhammad Iqbal (left), Second Secretary in the High Commission for Pakistan to the United Republic of Tanzania. 

Mr. Mjenga bids well wishes to the Pakistan outgoing Ambassador and assured him of cooperation for the upcoming new Ambassador.

The meeting continues, whereby Ambassador Altaf expressed the need to explore other areas of cooperation such as investment, health, insurance, banking and infrastructure.  He said that his successor will continue to bridge the foundation of the bilateral ties that continue to exist between the two countries. 



All photos by Tagie Daisy Mwakawago 


Thursday, October 17, 2013

Wiki ya Umoja wa Mataifa kuadhimisha miaka 68 yazinduliwa


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa  itakayoanza kuadhimishwa tarehe 17 hadi 24 Oktoba, 2014. Wiki hiyo ambayo huadhimishwa kila mwaka itajumuisha matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mjadala wa Wazi utakaofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 22 Oktoba, 2013 na maonesho ya shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje yakayofanyika Viwanja vya Karimjee tarehe 23 na 24 Oktoba, 2013 . Kilele cha maadhimisho hayo ni tarehe 24 Oktoba ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) atakagua Gwaride rasmi na kupandisha Bendera ya Umoja wa Mataifa. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni "Tanzania ya Kesho Tunayoitaka". Mwingine katika picha ni Alberic Kacou, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
 

Waandishi wa Habari kutoka mashirika mbalimbali ya habari hapa nchini wakimsikiliza kwa makini Bw. Kacou na Balozi Gamaha walipozungumza nao kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa.

Bw. Kacou akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Wiki ya Umoja wa Mataifa.
 
Sehemu ya Waandishi wa Habari pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Balozi Gamaha alipozungumza nao kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa. Kushoto ni Bi. Maulidah Hassan na Bw. Lucas Mayenga, Maafisa Mambo ya Nje.

 
Picha na Reginald Philip Kisaka

Sunday, October 13, 2013

Membe: Hakuna Kiongozi wa Afrika kupelekwa ICC


Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiongea na waandishi wa habari mapema leo kwenye ukumbi wa mkutano wa Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Dar es Salaam.  Kulia ni Balozi Rajabu Gamaha, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje. 

Waandishi wa habari waliokusanyika kumsikiliza Mhe. Waziri Membe. 

Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje ukijumuisha Balozi Irene Kasyanju (kushoto), Mkurugenzi wa Kikengo cha Sheria, Balozi Simba Yahya (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Mbelwa Kairuki (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia na Balozi Dora Msechu (wa nne kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika. 

Wengine waliohudhuria Mkutano huo ni Bw. Mkubwa Ally (kushoto), Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Thobias Makoba (katikati) na Bw. Togolani Mavura (kulia), Wasaidizi wa Mhe. Waziri Membe. 

Kwenye Mkutano pia alikuwepo Bw. Kaaya (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa  

Mmoja wa waandishi wa habari kutoka gazeti la The Citizen, Bw. Mkinga Mkinga akiuliza swali kwa Mhe. Waziri Membe.  

Mhe. Waziri Membe akifafanua ombi la Kenya kuhusu uhalali wa kuwafikisha Viongozi Wawili wa juu wa Serikali ya Kenya kwenye Mahakama ya Kimatafa (ICC) kujibu Makosa ya Jinai. Kulia ni Balozi Rajabu Gamaha na kushoto ni Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 

Wakurugenzi wakisikiliza kwa makini maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani).  Kulia ni Bw. Mndeme, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, na Bw. Ligaganya, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango.

Mhe. Waziri Membe akihojiwa na Bw. Erick David Nampesya, Mwandishi/Mtangazaji kutoka Shirika la Habari la BBC. 



Membe: Hakuna Kiongozi wa Afrika kupelekwa ICC

Na TAGIE DAISY MWAKAWAGO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akutana na waandishi wa habari leo kujadili uhalali wa kuwafikisha Viongozi Wawili wa juu wa Serikali ya Kenya kwenye Mahakama ya Kimatafa kujibu Makosa ya Jinai. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya Nje, jijini Dar es Salaam.

Waziri Membe alikuwa akielezea yaliyojiri kwenye Kikao cha dharura cha Viongozi Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (UA) kilichomalizika mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia jana tarehe 12 Oktoba, 2013.  Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mfalme Mswati wa III, Rais wa Swaziland, na Viongozi Wakuu na Watendaji Wakuu wa Serikali barani Afrika.

Kikao hicho kiliitishwa kutokana na ombi la Serikali ya Jamhuri ya Kenya ya kutaka UA kujadili mahusiano yaliyopo kati ya nchi za Afrika na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) na iwapo ni sahihi kwa Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika kufikishwa katika Mahakama hiyo kujibu mashtaka wakati wakiwa madarakani.

“Viongozi hao wa Afrika waliazimia mambo makuu matano,” alieleza Waziri Membe, huku akiyataja mawili kuwa hakuna Kiongozi yoyote kutoka barani Afrika atakayepelekwa ICC au Mahakama yoyote kujibu mashtaka wakati akiwa madarakani hata akiwa anashika nafasi ya kukaimu. 

Mengine ni kuwa mashtaka yanayomkabili Kiongozi yoyote barani Afrika yasubiri hadi Kiongozi huyo atakapomaliza muda wa uongozi wake.  Aidha, Mhe. Waziri alieleza kusikitishwa kwa Viongozi wa Afrika na namna Mahakama ya ICC inavyoendesha shughuli zake kwa kile walichokiita “kuwaandama Viongozi wa Bara la Afrika kuliko Viongozi wa Mataifa mengine hata pale panapokuwa na ushahidi wa Viongozi hao wengine kufanya makosa ya Jinai.”

Waziri Membe alihoji inakuwaje kwamba kati ya kesi 30 zilizopelekwa ICC tangu mwaka 2004, ishirini na saba (27) zinatoka barani Afrika.  “Haya yote yalijadiliwa kwa kina, pamoja na pendekezo la kujitoa kwenye uanachama wa Mahakama ya ICC,” aliongeza Waziri Membe.

Alisema suala la kujitoa uanachama wa ICC limeachiwa kila nchi kuamua, ingawaje linategemewa kujadiliwa tena katika kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mawaziri wa Sheria wa nchi wanachama wa mahakama hiyo kitakachofanyika tarehe 29 Novemba mwaka huu nchini Uholanzi. Hivi sasa kuna nchi thelathini na nne (34) barani Afrika ambazo ni wananchama wa Mahakama hiyo.

Akiendelea kuzungumza katika Mkutano wake wa leo na waandishi wa habari ambao pia ulihudhuriwa na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri Membe amesema kuwa Umoja wa Afrika umepeleka ombi lake rasmi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) kuahirisha kesi inayowakabili viongozi hao wa Kenya.

Wakati huo huo, Mhe. Waziri Membe alitumia fursa ya mkutano wake na waandishi wa habari kutoa salamu za pole kwa Bibi Ufoo Saro, Mwandishi/Mtangazaji wa kituo cha televisheni ITV, na familia yake, kufuatia  taarifa iliyomfikia kuwa Bibi Saro amelazwa hospitali akiwa mahututi baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya. Mama yake mzazi, Anastazia Saro na mtoto wake waliuwawa katika shambulio hilo.  Taarifa zinasema mtuhumiwa ni   mchumba wa Bibi Saro, ambaye anadaiwa kufyatua risasi kwa familia hiyo na hatimaye kujipiga risasi na kufa.

Sambamba na taarifa hiyo, Mhe. Waziri Membe pia aliwatakiwa wananchi sikukuu njema ya Kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambayo itaadhimishwa Kitaifa kesho tarehe 14 Novemba 2013.


Mwisho.


Mkutano wa Ajira kwa Watoto Duniani wafanyika nchini Brazil


Bw. David Mwakanjuki (kushoto), Afisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Brazil akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Tanzania uliomjumuisha Bw. Mkama (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira na Maafisa, mara baada ya kumaliza Mkutano wa Tatu wa Ajira kwa Watoto Duniani "III Global Conference on Child Labor" uliofanyika mjini Brasilia kuanzia tarehe 8 had 10 Oktoba, 2013. 

Bw. David Mwakanjuki (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Mkama  (katikati) na Bw. E. Kibuta kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Brazil nje ya ukumbi uliofanyika Mkutano wa Tatu wa Ajira kwa Watoto Duniani. 

Bango la Mkutano huo.


Picha na maelezo kwa hisani ya Bw. David Makanjuki