Thursday, March 2, 2017

Waziri Mahiga akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Arkadia Ltd

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ARKADIA Ltd.  Dr. Ezio Copat walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma 

Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akimsikiliza Dr. Copat walipokutana kwa mazungumzo mjini Dodoma
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akifafanua jambo wakati wa mazungumzo

Mazungumzo yakiendelea

Kamati ya Kusimamia Soko la Pamoja la EAC yakutana jijini Dar Es Salaam

Mkurugenzi wa Ajira kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bw. Amir Amir aliyeshika kipaza sauti ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya kusimamia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki akifungua kikao hicho jana kwenye ukumbi wa hoteli ya Holiday In jijini Dar Es Salaam.

Bi. Agatha Nderitu akiwasilisha matokeo ya utafiti wa namna nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zilivyotekeleza Itifaki ya Soko la Pamoja kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2014 hadi 2016. Utafiti huo ulilenga maeneo ya Soko huru la bidhaa, mitaji na uhuru wa watu kusafiri ndani ya Jumuiya. Utafiti huo ulionesha kuwa nchi za EAC zimejitahidi kutekeleza Itifaki hiyo ingawa bado kuna vikwazo na sheria zinazozuia utekelezaji wa soko hilo kikamilifu hususan kwenye vikwazo visivyo vya kibiashara.

Baadhi ya washiriki wakifuatiliwa mada kuhusu tathmini ya utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la EAC

Wednesday, March 1, 2017

Naibu Waziri Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Singapore nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (kulia) akizungumza na Balozi wa Singapore nchini, Mhe. Tan Puay Hiang, alipomtembelea Wizarani Jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo yao Mhe. Dkt. Kolimba alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili sambamba na kutambua mchango wa Serikali ya Singapore kwa Tanzania katika sekta ya Elimu sambamba na kuwajengea uwezo Watumishi wa Umma.
Mhe. Tan Puay Hiang nae akizungumza ambapo alieleza Serikali ya Singapore itaendelea kudumisha ushirikiano wa kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Singapore pamoja na kuongeza maeneo ya ushirikiano hususan uwekezaji katika masuala ya nishati na miundombinu.
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo. Kulia ni Bw. Charles Faini na pembeni yake ni Bw. Emmanuel Luangisa.
Mazungumzo yakiendelea.Kushoto ni ujumbe alioambatana nao Mhe. Tan Puay Hiang.

Picha ya pamoja.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa DPRK nchini

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) nchini, Mhe. Kim Yong Su, alipomtembelea leo katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kuzungumzia historia ya ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzinia na DPRK pia walizungumzia ushirikiano katika masuala ya uchumi, hususan katika ujenzi wa miundombinu na kilimo chenye tija.
Mhe. Balozi Kim Yong Su nae akimweleza jambo Mhe. Dkt. Susan ambapo alitumia fursa hiyo kueleza namna Serikali DPRK ilivyojidhatiti katika kuhakikisha ushirikiano unazidi kuimarika kwa faida ya mataifa hayo mawili.
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo.Kushoto ni Bw. Benedict Msuya na pembeni yake ni Bw. Charles Faini.

Mazungumzo yakiendelea.
Picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo.

Monday, February 27, 2017

Wizara ya Mambo ya Nje yahamia Dodoma Rasmi


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ofisini kwake Mjini Dodoma. Waziri Mahiga leo ameutangazia Umma wa Watanzania kuwa Wizara imehamia Dodoma rasmi.



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUHUSU WIZARA KUHAMIA DODOMA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kuwa tayari imeshahamia Dodoma kuanzia tarehe 17 Februari, 2017.  Hatua hiyo imehusisha Awamu Mbili, awamu ya kwanza imetekelezwa tarehe 28 Januari, 2017 na awamu ya pili imetekelezwa tarehe 17 Februari, 2017.

Miongoni mwa Watumishi waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza ni pamoja na Viongozi Wakuu na Watumishi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.  Dkt. Augustine P. Mahiga na Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba pamoja na Watumishi Kumi (10) waliofuatana nao.

Awamu ya pili iliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan M. Mwinyi ambao waliongozana na Watumishi 33 wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Katika Uhamisho huu, jumla ya Watumishi 43 wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameungana na Viongozi wao Wakuu kwenye ofisi za Makao Makuu ya Wizara na Serikali Dodoma.

Mawasiliano ya Wizara yatakayotumika kuanzia sasa ni kama ifuatavyo:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Barabara ya Makole,
S.L.P 2933,
Jengo la LAPF, Ghorofaya6,
DODOMA.

Namba za Simu: +255 (0) 262323201-7,
Nukushi           :  +255-26-2323208,
Barua pepe      :   nje@nje.go.tz
 Tovuti             : www.foreign.go.tz


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 27 Februari, 2017.

Mhe. Waziri Mahiga na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi wakijadili jambo kabla ya kuanza kwa mkutano Ofisini Mjini Dodoma.

Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Mahiga kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje kuhamia Dodoma.

Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika picha na baadhi ya watendaji wa Wizara mjini Dodoma. 
Walioketi ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa pili kulia), Naibu Katibu Mkuu,  Balozi Ramadhani Mwinyi (wa kwanza kulia) Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Nigel Msangi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw.Hamid Mbegu wakiwa katika picha ya pamoja na  watumishi wa Wizara Mjini Dodoma. 

Sunday, February 26, 2017

Rais Museveni amaliza ziara yake nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini.
Rais Museveni akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga. Kushoto ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb.). Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi.
Rais Museveni akiagana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Innocent Shiyo.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Bw. Elibariki Maleko akiagana na Rais Museveni
Rais Museveni akipunga mkono wa kwa heri kwa Rais Magufuli na Viongozi wengine walioshiriki kumuaga mara baada ya kumaliza ziara yake nchini.
Kutoka kulia ni Balozi wa Uganda nchini Mhe. Dorothy Hyuha, Balozi Shiyo, Mkuu wa Itifaki, Balozi Grace Martin, Mnikulu, Bw. Ngusa Samike na Balozi Zuhura Bundala, Mshauri wa Rais Masuala ya Diplomasia wakimuaga Rais Museveni (hayupo pichani) mara baada ya kumaliza ziara yake nchini.

Rais Magufuli awaapisha mabalozi wanne

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Hazara Chana. Hafla za uapisho zimeanyika leo jijini Dar es Salaam
Mhe. Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Balozi Chana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi wa Tanzania nchini Khartoum, Sudan Mhe. Silima Kombo Haji. Hafla za uapisho zimeanyika leo jijini Dar es Salaam
Mhe. Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Balozi Silima
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi wa Tanzania nchini Mascut, Oman Mhe. Abdallha Abas Kilima. Hafla za uapisho zimeanyika leo jijini Dar es Salaam

Mhe. Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Balozi Kilima
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi wa Tanzania nchini Seoul, Korea Kusini, Mhe. Matilda Swila Masuka. Hafla za uapisho zimeanyika leo jijini Dar es Salaam
Mhe. Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Balozi Masuka
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (wa nne kutoka kushoto), Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassani Suluhu (wa tatu kutoka kushoto), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa (wa nne kutoka kulia), Katibu Mkuu Kiongozi Mhe Eng. John   Herbert Kijazi (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Azizi Mlima (wa tatu kutoka kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wateule mara baada ya kuapishwa, Ikulu jijini Dar es Salaam.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Mabalozi wapya wanne waapishwa na kupangiwa vituo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapangia vituo na kuwaapisha Mabalozi wapya wanne ambao uteuzi wao ulifanyika    tarehe 03 Desemba 2016. 

Mabalozi hao ambao waliapishwa leo na Mhe. Rais Ikulu jijini Dar Es Salaam ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dkt. Pindi Chana ambaye anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. John Haule. Mhe. Haule ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa  iliyokuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alistaafu kwa mujibu wa sheria mwaka 2016.

Mhe. Chana kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Unaibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto katika Serikali ya awamu ya nne.

Balozi mwingine aliyeapishwa ni Mhe. Silima Kombo Haji anayekwenda kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Jamhuri ya Sudan baada ya Mhe. Rais kuamua kuufungua upya Ubalozi huo ambao ulifungwa miaka ya nyuma kutokana na sababu za kiuchumi. Kabla ya uteuzi huo Balozi Silima alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Walioapishwa pia ni Mhe. Abdallah Kilima ambaye anakwenda nchini Oman kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Ali Saleh aliyestaafu kwa mujibu wa sheria. Balozi Kilima kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea, Mhe. Matilda Masuka naye aliapishwa na Mhe. Rais leo. Balozi Masuka kabla ya kukabidhiwa majukumu hayo mapya alikuwa Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania nchini China.   Jamhuri ya Korea ni moja kati ya nchi sita ambazo Mhe. Rais Magufuli amefungua Balozi mpya. Nchi nyingine ni Algeria, Jamhuri ya Sudan, Uturuki, Israel na Qatar.

  Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dar es Salaam, 26 Februari, 2017.




Saturday, February 25, 2017

Tanzania yaahidi kuimarisha Diplomasia ya Uchumi na Uganda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Uganda hapa nchini, Mhe. Yoweri Museveni (anayeonekana ameketi kulia). Katika hotuba yake Rais Magufuli aliahidi kuimarisha urafiki na undugu uliodumu kwa miaka mingi baina ya mataifa hayo mawili.
Mhe. Rais Museveni nae akihutubia katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa ziara yake nchini.
 Pamoja na kuzungumzia masuala ya ushirikiano wa kidiplomasia, Rais Museveni aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuikomboa  Uganda dhidi ya adui Nduli Idd Amin Dada na ukombozi wa kiuchumi kwa kujenga reli ya kati " standard gauge" ambayo itaenda sambamba na ujenzi wa bandari kavu "Dry Port" Jijini Mwanza ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo ya Uganda kutoka Bandari ya Dar es Salaam. 
Sehemu ya Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Serikali ya Tanzania waliohudhuria mkutano huo ambao ulitanguliwa na hafla ya utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano katika masuala ya Siasa na Diplomasia. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia masuala ya Kimataifa wa Uganda, Mhe. Okello Oryem wakisaini Mkataba wa Ushirikiano katika masuala ya Siasa na Diplomasia.
Wakibadilishana mkataba mara baada ya kuusaini.
Marais wakipongezana mara baada ya kutoa hotuba.