Tuesday, February 13, 2018

Ziara ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Wizara ya Mambo ya Nje

 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda  akifungua Mafunzo ya siku moja kwa wanachuo wa chuo cha Taifa cha Ulinzi yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, tarehe 12 Februari,2018. Lengo la mafunzo hayo ilikuwa kuwapa uelewa wanachuo hao kuhusu majukumu ya Wizara.


Major General Yacoob Mohamed  Commandant, Mkuu wa chuo cha Taifa cha Ulinzi akitoa hotuba baada ya ufunguzi wa Mafunzo

 Wajumbe wakifuatilia mada katika mafunzo hayo

Sehemu ya Wajumbe wakifuatilia mafunzo hayo


Balozi Innocent Shiyo akitoa mada katika ziara hiyo kuhusu baadhi ya majukumu ya Wizara 

 Sehemu ya Wanachuo wakifuatilia mafunzo

 Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizarani wakifutialia mafunzo hayo

 Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Wizarani akitoa mada katika mafunzo hayo Mafunzo yakiendelea.
 Mafunzo yakiendelea


Katibu Mkuu Prof. Adolf Mkenda na Balozi Peter Kalaghe wakifuatilia mafunzo hayo 

Baadhi ya  Wakurugenzi kutoka Wizarani wakifuatilia mafunzo hayo

Baadhi ya wajumbe wa mafunzo hayo wakifuatilia mada

Major General Mohamed akikabidhi zawadi kwa Katibu Mkuu Prof Mkenda

Bi. Robi Bwiru Afisa Habari kutoka Wizarani akielezea ratiba ya Mafunzo hayo.

Picha ya Pamoja  baada ya Mkutano

Monday, February 12, 2018

Katibu Mkuu afanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke, alipomtembelea Wizarani tarehe 12 Februari,2018, Dar es Salaam
Prof. Mkenda akizungumza na Mhe. Balozi Cooke,katika mazungumzo hayo Prof. Mkenda  alisema Mahusiano ya Uingereza na Tanzania yana historia ndefu, nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana katika maeneo mbalimbali kama vile biashara, uwekezaji, utalii na elimu.

Naye Mhe. Balozi Cooke alimweleza Prof Mkenda namna yeye na Wanadiplomasia wenzake  walivyofurahishwa na maandalizi ya hafla ya mwanzo wa mwaka kwa Mabalozi (Sherry Party), vilevile Mhe. Cooke alisema Serikali yake inaunga mkono Serikali ya Tanzania kwa juhudi inazofanya ili kufikia uchumi wa viwanda, alisema Uingereza  itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali ya maendeleo. 

Balozi Cooke naye akielezea jambo kwa Prof. Mkenda
Mazungumzo yakiendelea, wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika na Ulaya Bw. Salvatory Mbilinyi, na wa kwanza kushoto ni Naibu Balozi Ubalozi wa Uingereza Bw. Matt Sutherland 



Hafla ya chakula cha jioni kwa Wajumbe wa Baraza la Wakimbizi Duniani yafana

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akizungumza kwenye hafla ya chakula cha jioni na Wajumbe wa Baraza la Wakimbizi Duniani. Hafla hiyo iliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuhudhuriwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne na Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Wakimbizi Duniani, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wakimbizi Duniani Mhe. Lloyd Axworthy, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani,  Balozi Simba Yahaya (hawapo pichani).  Hafla hiyo imefanyika katika Hotel ya Hyatt Regancy, Jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.
Katibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Gerald Mbwafu (wa kwanza kushoto), Afisa Mambo ya Nje, Bi.Ramla Hamis (wa pili kutoka  kushoto) pamoja na Mjumbe wa Baraza la  Wakimbizi Duniani nao wakiwa katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wakimbizi Duniani, Mhe. Lloyd Axworthy naye akitoa neno la shukrani kwa Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mapokezi yao hapa nchini.
Mhe. Axworthy akiendelea kuzungumza huku meza kuu wakimsikiliza kwa makini
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza hilo nao wakiendelea kumsikiliza Mhe. Axworthy (hayupo pichani).
Sehemu nyingine ya wageni waalikwa wakiendelea kumsikiliza Mhe. Axworthy alipokuwa akizungumza.  
Bi. Nguse Nyerere, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa akisherehesha kwenye hafla hiyo
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati), Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (wa kwanza kulia), pamoja na Mhe. Lloyd Axworthy wakifurahia jambo kwa pamoja.










Saturday, February 10, 2018

Waziri Mahiga awa mgeni rasmi maadhimisho ya miaka 39 ya Taifa la Iran

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akihutubia wakati wa maadhimisho ya 39 ya  Taifa la Iran. Mhe. Mahiga ambaye alikuwa alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alitumia fursa hiyo kuelezea mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Iran katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara na elimu. Aidha alilipongeza taifa hilo kwa hatua kubwa ya maendeleo wanayopiga hususan katika matumizi ya teknolojia.
Waziri Mahiga akiendelea kuzungumza kwenye maadhimisho hayo.
Sehemu ya Mabalozi wanao ziwakilisha nchi zao hapa nchini wakifuatilia hotuba ya Waziri Mahiga (hayupo pichani).
Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mhe.Mousa Farhang naye akitoa hotuba wakati wa maadhimisho hayo ya 39 ya taifa lao
Sehemu ya viongozi wa dini pamoja na wageni waalikwa nao kwa pamoja wakisikiliza hotuba kwenye maadhimisho hayo.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nao wakiwa katika hafla hiyo. 
Sehemu ya raia wa Iran wanaoishi nchini na wageni waalikwa wakifatilia matukio wakati wa maadhimisho hayo
Waziri Mahiga akizungumza jambo na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mhe.Mousa Farhang
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (kulia) pamoja na Katibu wa Waziri Bw. Gerald Mbwafu nao walihudhuria hafla hiyo
Waziri Mahiga akisalimiana na Sheikh al Hadi Musa Salim, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam walipokutana kwenye hafla hiyo.  
Waziri Mahiga akisalimiana na Balozi wa Algeria nchini Tanzania Mhe.Saad Belabed walipokutana nae kwenye hafla hiyo.
Picha ya pamoja.













Matukio ya Hafla ya Mwanzo wa Mwaka kwa Mabalozi ( Sherry Party)

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe.Balozi Augustine Mahiga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda,wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini katika sherehe ya kukaribisha Mwaka mpya 2018 kwa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, tarehe 10 Februari 2018.

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mhe. Balozi Mahiga na Katibu Mkuu Prof. Mkenda wakiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi Wakuu, Wawakilishi wa Heshima na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

 Waheshimwa Mabalozi wakiwa katika mchapalo kabla ya kuanza Tafrija
Katibu Mkuu, baadhi ya Wakurugenzi katika hafla hiyo

Balozi Grace Mujuma akibadilishana mawazo na baadhi ya Mabalozi waliohudhuria hafla hiyo

Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Wizarani waliohudhuria hafla hiyo

Sehemu ya Wakurugenzi na  Maafisa wa Wizara

Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa kutoka Wizarani


Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Mhe. Balozi Mahiga wakiwasalimia na kuwakaribisha Mabalozi 






Baadhi ya Wakurugenzi na Maafisa wa Wizara wakiwa katika hafla hiyo.

Waziri, Katibu Mkuu wafanya mazungumzo na Ujumbe wa EU

    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Augustine Mahiga akiwa katika mkutano na Mabalozi kutoka Umoja wa Ulaya na Marekani wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Wizara, Dar es Salaam, tarehe 9 Februari,2018. 
    
Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine Waheshimiwa Mabalozi  waliishukuru Tanzania kwa mchango mkubwa inaoutoa katika kutatua mgogoro wa Burundi na Congo, pia wametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kusaidia juhudi za kutatua migogoro hiyo kwani wanaamini Tanzania ina mchango mkubwa katika kutafuta utatuzi wa kudumu wa migogoro hiyo ili nchi hizi kujikita zaidi katika shughuli za kujiletea maendeleo.

 Sehemu ya Waheshimiwa Mabalozi wakifuatilia Mkutano huo

Mheshimiwa Waziri akifafanua jambo kwa Waheshimiwa Mabalozi, kushoto mbele ni Balozi Grace Mujuma, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika na kulia mbele ni Bw. Joseph Kapinga, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika.
    Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akizungumza na wawakilishi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini walipomtembelea Wizarani, Dar es Salaam tarehe 9 Februari,2018.
Katika mazungumzo hayo walizungumzia jinsi ya kuboresha zaidi mahusiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya na pia kuangalia jinsi Umoja wa Ulaya unavyoweza kuendelea kusaidia Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani Umoja wa Ulaya ni kati ya wadau muhimu wanaochangia miradi mbalimbali katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha, Wajumbe hawa kwa upande wao walisifia Serikali ya awamu ya 5 inavyotekeleza miradi mbalimbali inayowagusa moja kwa moja wananchi, pia walisifia muongozo wa utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Serikali katika Idara mbalimbali za Serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi ( Blue Print) na kusema utakapokamilika itakuwa ni njia nzuri ya kutekeleza kwa haraka masuala mablimbali  ya Serikali.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda na Wajumbe kutoka Umoja wa Ulaya hapa nchini pamoja na Maafisa wa Wizara wakiendelea na mazungumzo.
    Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika  Balozi Grace Mujuma,akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi msaidizi wa Masuala ya Afrika katika Wiazara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi ambaye pia ni Mjumbe maalum wa Ukanda wa Maziwa Makuu (Great Lakes Region), Bw. Robert - Jan Siegert alipomtembelea Wizarani tarehe 9 Februari,2018, Wengine katika Picha ni Naibu Balozi wa Uholanzi Bibi Lianne Houben, na Maafisa kutoka Ubalozi wa Uholanzi na wa kwanza kulia ni Bw. Ally Ubwa Afisa Mambo ya Nje kutoka Wizarani.