Prof. Mkenda na Balozi Kazungu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo yao. |
Friday, September 14, 2018
Prof. Mkenda na Balozi wa Kenya wakutana kujadili utatuzi wa changamoto za biashara mipakani
Thursday, September 13, 2018
Waziri Mahiga afungua rasmi Ofisi za Uwakilishi wa Ubalozi wa Ujerumani jijini Dodoma
Mhe. Waziri Mahiga kwa pamoja na Balozi Waechter wakifungua kitambaa kuashiria kuwa Ofisi Ndogo za Uwakilishi wa Ubalozi wa Ujerumani zimefunguliwa rasmi jijini Dodoma |
Mhe. Balozi Waechter nae akizungumza ambapo alisema wamefungua Ofisi hizo ili kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Ujerumani |
Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika picha na Mhe. Balozi Waechter pamoja na viongozi wengine walioshiriki hafla hiyo |
Mhe. Waziri Mahiga akimpongeza Balozi Waechter ufunguzi wa Ofisi Ndogo za Uwakilishi wa Ubalozi wa Ujerumani jijini Dodoma |
Wageni waalikwa walioshiriki ufunguzi wa Ofisi hizo wakifuatilia matukio mbalimbali |
Mhe. Waziri Mahiga akizungumza na vyombo vya habari |
Awali Mhe. Waziri Mahiga alisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi Ndogo za Uwakilishi wa Ubalozi wa Ujerumani zilizopo jijini Dodoma. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini, Mhe. Detlef Waechter. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Binilith Mahenge na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga |
Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi wa Ujerumani nchini |
Wednesday, September 12, 2018
Tanzania ilivyoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara nchini Msumbiji
Mheshimiwa Balozi Rajabu Luhwavi akitoa maelezo mafupi wakati
wa ufunguzi wa Maonyesho ya Biashara Nampula yaliyohusisha wafanyabiashara
kutoka Tanzania. Kwa upande wake Balozi Luhwavi, alieleza kuwa
maonesho haya ni ya kimkakati kwa ajili ya kukuza na kuimarisha umoja,
mshikamano na mahusiano ya kiuchumi yaliyojengwa na waasisi wetu hayati Mwalimu
Julius Nyerere, aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
hayati Sheikh Abeid Amani Karume, aliyekuwa rais wa kwanza wa Zanzibar na
hayati Samora Moises Machel, aliyekuwa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Msumbiji.
Maonesho haya yalifungua fursa za masoko kwa bidhaa za viwanda vya Tanzania
pamoja na kuendeleza juhudi za utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kwa vitendo
na kukuza uchumi, hususan uchumi wa viwanda.
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ndugu Juma Ali Juma aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kilele cha maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania mjini Nampula akiwa pamoja na Balozi Rajabu Luhwavi na Katibu Mkuu wa Jimbo la Nampula, Bi. Veronica Langa wakipata maelezo kuhusu teknolojia ya ufugaji samaki kutoka kampuni ya Dokaman ya nchini Tanzania. |
Kutoka kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mheshimiwa Rajabu Luhwavi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ndugu Juma Ali Juma, Mkurugenzi wa Ukuzaji Biashara TanTrade, Bi. Anna Bulondo wakipata maelezo kutoka kwa wawakilishi wa kampuni ya A - Z Textile Mills. |
Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mheshimiwa Rajabu Luhwavi akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Ndugu Juma Ali Juma wakipokea maelezo kuhusu bidhaa zinazotengenezwa na Kampuni ya Tanzania M/s Darsh Industries wakati wa maonesho ya bidhaa za viwanda mjini Nampula, Msumbiji. |
Monday, September 3, 2018
Tanzania na China zasaini Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano kwenye sekta ya kilimo na uvuvi
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa kwenye mazungumzo rasmi na Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo wa China, Mhe. Han Changfu alipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Beijing tarehe 03 Septemba, 2018. Katika mazungumzo yao Mhe. Majaliwa alimweleza Waziri Han nia ya Tanzania ya kushirikiana na China katika kuendeleza sekta za kilimo, uvuvi na mifugo. Naye Waziri Han alimhakikishia Waziri Mkuu ushirikiano wa hali ya juu kati ya Tanzania na China ambapo nchi hiyo ipo tayari kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa wataalam wa kilimo kutoaka Tanzania. Mhe. Waziri Mkuu yupo nchini China kwa niaba ya Mhe. Rais kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la shirikiano kati Afrika na China. |
Mazungumzo ya pande mbili yakiendelea na kuhudhuriwa na viongozi wengine mbalimbali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu, Prof. Adolf Mkenda na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Khatibu Kazungu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bibi Justa Nyange akifuatilia mazungumzo |
Waziri wa Kilimo, Maliasili na Uvuvi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma kwa pamoja na mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo ya China wakisaini kwa niaba ya Serikali zao Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano kwenye sekta za kilimo na uvuvi. Wanaoshuhudia ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Kilimo wa China, Mhe. Han Changfu |
Wakibadilishana mkataba mara baada ya kuusaini |
Waziri Mkuu ahamasisha uwekezaji kutoka Jimbo la Jiangsu la China
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Meya wa Jimbo la Jiangsu la nchini China, Bw.Guo Yuan Qiung mara alpowasili kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini China kwa ajili ya mazungumzo rasmi. Mhe. Waziri Mkuu yupo nchini humo kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya Afrika Nna China (FOCAC) utakaofanyika tarehe 03 na 04 Septemba, 2018. |
Mhe. Waziri Mkuu akizungumza na Bw. Qiung mara baada ya kumkaribisha Ubalozini |
Mhe. Waziri Mkuu akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Augustine Mahiga kwa Naibu Meya Qiung wakati wa mazungumzo rasmi kati ya Waziri Mkuu na Naibu Meya |
Mhe. Waziri Mkuu na ujumbe wa Tanzania wakizungumza na Naibu Meya wa Jiangsu na ujumbe wake walipofika Ubalozini. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda. |
Naibu Meya Qiung (wa tatu kulia) akiwa na ujumbe aliofuatana nao wakimsikiliza Waziri Mkuu hayupo pichani |
Mazungumzo yakiendelea |
Mazungumzo yakiendelea. Wa pili kulia ni Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki ============================================================
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema Tanzania inahitaji wawekezaji wa
uhakika kwenye sekta ya kilimo hususan watakaowekeza kwenye viwanda vya
kuchakata mazao ya kilimo, kuongeza thamani na kutafuta masoko.
Mhe.
Majaliwa aliyasema hayo wakati wa mazugumzo yake na Naibu Meya wa Jimbo la Jiangsu
nchini China, Bw. Guo Yuan Qiung aliyoyafanya tarehe 03 Septemba, 2018 katika
Ubalozi wa Tanzania nchini humo ikiwa ni mwendelezo wa program yake ya kukutana
na wadau muhimu wa maendeleo kabla ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) utafanyika
jijini Beijing kuanzia tarehe 01 hadi 04 Septemba, 2018.
Katika
mazungumzo yao, Mhe. Waziri Mkuu alimweleza Naibu Meya huyo kuwa, Tanzania inaendelea
kuboresha sekta ya kilimo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na kwamba jimbo
la Jiangsu ni moja ya mdau muhimu ambaye anaweza kuchangia maendeleo ya
Tanzania kwa kutumia teknolojia ya viwanda vya uchakataji mazao ili kuongeza
thamani na kupata masoko ya uhakika kwa mazao hayo. Alisema kuwa kwa kuwa jimbo
la Jiangsu ni miongoni mwa majimbo yaliyopiga hatua kubwa ya maendeleo ya teknolojia
na viwanda duniani. Hivyo kushirikiana na Tanzania katika sekta za kilimo na
viwanda kutaiwezesha nchi kufikia malengo yake ya kuwa nchi ya nchi ya viwanda
ifikapo mwaka 2020 na nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Pia
alisema kuwa, anathamini mchango wa Jimbo hilo katika uchumi wa Tanzania ambapo
sasa kuna Kampuni mbili kubwa za uwekezaji kutoka jimboni humo ikiwemo kampuni
ya kuchambua pamba na kutengeneza nyuzi ya mjini Shinyangana na Kiwanda cha
Urafiki cha jijini Dar es Salaam. Hata hivyo alisema bado mchango wa jimbo hilo
unahitajika katika uendelezaji viwanda hususan katika masuala ya teknolojia ya
viwanda; kuimarisha utafiti kwenye sekta ya kilimo na kuisaidia Tanzania kupata
masoko ya mazao kama mbaazi, mhogo na soya.
“Tanzania
inapongeza kazi nzuri unayoifanya na tunathamini sana mchango wako katika
maendeleo ya nchi yetu. Hadi sasa tunavyo viwanda viwili kutoka Juangshu.
Tunaomba uendelee kuhamasisha kampuni nyingi zaidi kutoka jimboni kwako kuja
kuwekeza nchini kwenye maeneo mbalimbali pamoja na kutusaidia kupata masoko ya
mazao kama mbaazi, mhogo na soya” alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Katika
hatua nyingine walikubaliana na Naibu Meya huyo kuangalia uwezekano wa kufanya
mapitio kuhusu changamoto za uendeshaji wa
Kiwanda cha Urafiki ili kutafuta suluhu ya haraka kwa kiwanda hicho ikiwa ni
pamoja na kuwaagiza wataalam wa pande mbili kukutana kuainisha changamoto hizo.
Kwa
upande wake, Bw. Qiung alimhakikishia ushirikiano wa hali ya juu Mhe. Waziri
Mkuu hususan katika uwekezaji wa viwanda na kwamba ni Imani yake kuwa mkutano
wa FOCAC utatoa dira kwa maendeleo si kwa Tanzania pekee bali kwa Bara zima la Afrika.
Aidha
aliongeza kuwa, mbali na ushirikiano katika masuala ya kilimo na uendelezaji
viwanda, jimbo lake lipo tayari kushirikiana na Tanzania katika masuala ya
elimu ambapo jimbo hilo lina vyuo vikuu zaidi ya 60,000 vinvyotoa kozi
mbalimbali na kuwakaribisha wanafunzi kutoka Tanzania kwenda jimboni humo.
|
Sunday, September 2, 2018
Tanzania yapata Mwakilishi wa Heshima Hong Kong na Macao
Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki kwa pamoja na Bibi Annie Suk-Ching Wu wakisaini Mkataba kumwezesha Bibi Wu kuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania huko Hong Kong na Macao. Tukio hilo lilifanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Beijing, China na kushuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda pamoja viongozi wengine ambao wapo nchini China kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC). |
Balozi Mbelwa na Bibi Wu wakibadilishana mkataba mara baada ya kuusaini |
Mhe. Waziri Mahiga akitoa hotuba kumpongeza Bibi Wu kwa kukubali kuiwakilisha Tanzania kwenye maeneo hayo na kumtaka kuiwakilisha vema nchi |
Mhe. Waziri na viongozi wengine wakisubiri kuanza kwa ratiba |
Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Mbelwa na Bibi Wu mara baada ya kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa kumwezesha Bibi Wu kuiwakilisha Tanzania Hong Kong na Macao
|
Katibu Mkuu, Prof. Mkenda akiteta jambo na Mhe. Balozi Mbelwa |
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bibi Justa Nyange akiwa na Maafisa ambao walikuwepo kushuhudia uwekwaji saini wa mkataba wa kumwezesha Bibi Wu kuwa Mwakilishi wa Heshima kwenye majimbo ya Hong Kong na Macao ya nchini China |
Waziri Mkuu afungua Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na China
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na China ambapo zaidi ya Kampuni 80 kutoka nchi hizi mbili zilishiriki. Wakati wa Kongamano hilo Mhe. Waziri Mkuu alizialika kampuni za biashara na uwekezaji kutoka China kuja kuwekeza Tanzania na kusisitiza kuwa mazingira ya uwekezaji ni mazuri. Mhe. Waziri Mkuu yupo nchini China kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika tarehe 3 na 4 Septemba, 2018 jijini Beijing. |
Sehemu ya wageni waalikwa wakfuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Mkuu |
Sehemu ya wageni kutoka Tanzania akiwemo Mzee John Cheyo wakifuatilia mkutano |
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akitoa neno wakati wa Kongamano hilo |
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Geofrey Mwambe akiwa pamoja na wageni wengine walioshiriki kongamano hilo |
Mkurugenzi Mkuu wa Eneo Maalum la Uwekezaji (EPZA), Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia naye akifuatilia Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na China |
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wwang Ke naye alishiriki kongamano hilo |
Sehemu nyingine ya wageni waalikwa |
Mshereheshaji kwenye kongaano hilo Bw. Laizer Mollel akitoa ratiba kabla ya kuanza kwa kongamano |
Mhe. Balozi Kairuki akihojiwa na Mwandishi kutoka TBC, Bi. Anna Mwasyoke kuhusu umuhimu wa kongamano hilo kwa Tanzania
====================================================
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewakaribisha
wafanyabiasha na wawekezaji kutoka China kuja Tanzania kuwekeza kutokana na mazingira rafiki ya uwekezaji na hali ya amani
na utulivu iliyopo nchini.
Waziri
Mkuu alitoa rai hiyo wakati akifungua Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na
China lililowashirikisha wafanyabiashara zaidi ya 80 kutoka nchi hizi mbili.
Mhe. Majaliwa ambaye yupo nchini China kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jukwaa la
Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) alitumia fursa hiyo kukutana na
wafanyabiashara hao ili kuwaeleza hali ya uwekezaji nchini katika
Mhe.
Majaliwa alisema kuwa, Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuvutia
wawekezaji ambazo kwa kiasi kikubwa zimezaa matunda ambapo katika Ripoti ya
uwekezaji duniani kwa mwaka 2018 imeitaja Tanzania kuwa kitovu cha uwekezaji kwa
ukanda wa Afrika Mashariki ambapo imewekeza takribani dola za marekani bilioni
1.2.
Mhe.
Majaliwa aliongeza kuwa, Tanzania inamazingira mazuri sana ya uwekezaji ikiwemo
ardhi nzuri kwa kilimo cha mazao mbalimbali kama miwa, mpunga, ngano, mahindi,
Mhogo na katani. Alisema kuwa, jumla ya hekta milioni 44 za ardhi zinafaa kwa
kilimo na zaidi ya hekta milioni 29 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.
Akizungumzia
sekta ya madini, Mhe. Majaliwa alisema kuwa ni moja ya sekta muhimu
inayochangia pato la taifa na kuwahamashisha wawekezaji kuchangamkia sekta hiyo
hususan kwenye uchimbaji na uchakataji wa madini ya chuma na uchimbaji wa
madini ya urani.
Kuhusu
utalii, Mhe. Waziri Mkuu alisema kuwa Tanzania imekuwa ikifaidika kwa kiasi
kikubwa kutokana na kujaliwa vivutio vingi vya utalii ikiwemo fukwe zilizopo
Zanzibar, Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Ngororngoro. Hata hivyo alisema bado
sekta hii inahitaji wawekezaji hususan kwenye ujenzi wa miundombinu ya utalii
kama vile hoteli na sekta ya huduma kwa watalii kwa ujumla.
Masuala
mengine aliyowaeleza wawekezaji hao ambayo ni fursa kwao ni pamoja na eneo la
teknolojia ya habari na mawasiliano ambapo kwa sasa soko ni kubwa kutokana na ongezeko la watumiaji wa simu na
mitandao hususan watu wanaoishi vijijini. Aliwakaribisha wawekezaji kuwekeza
katika sekta hii katika maeneo ya ukarabati na utengenezaji wa vifaa vya
mawasiliano na kujenga viwanda vya kuunganisha simu.
Mhe.
Waziri Mkuu alihitimisha kwa kuhimiza wawekezaji kuja nchini na kusisitiza
kuwa, “ukitaka kuwekeza Afrika karibu Tanzania”
|
Subscribe to:
Posts (Atom)