Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Balozi wa Kenya nchini, Mhe. Dan Kazungu walipokutana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya. Pamoja na mambo mengine walijadili changamoto za biashara hususan tukio la hivi karibuni la kukwamishwa kwa bidhaa za Tanzania kuingia Kenya kwa sababu mbalimbali ikiwemo vinywaji, mchele na unga wa ngano. Katika kikao hicho ilikubalika Tanzania kuitisha kikao cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki na Biashara na Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Tanzania na Kenya. Pia walikubaliana kuendelea kuratibu ziara za viongozi wa juu kati ya nchi hizi mbili kwa lengo la kukuza mahusiano. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.