Thursday, September 27, 2018

Prince William atembelea Bandari ya Dar es Salaam


Mjuu wa Malkia Elizabeth wa II wa Uingereza"Prince" William akisalimiana na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi mara baada ya kuwasili Bandari ya Dar es Salaam na kujionea utendaji kazi mzuri bandarini hapo, wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko na watatu kutoka kulia ni Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akisalimiana na "Prince" William mara baada ya kuwasili Bandarini kwaajili ya kujionea ufanisi na utendaji kazi mzuri wa Badari hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Kakoko akimwelezea namna bandari hiyo ilivyo na uwezo wa kuingiza mizigo mikubwa kutoka nje ya nchi na namna nchi jirani wanavyoitumia fursa ya bandari hiyo katika kusafirishia mizigo yao na kupokea.
Mhandisi Deusdedit Kakoko akimkabidhi "Prince" William kinyago cha mfano wa Twiga kilichotengenezwa kwa ufanisi mkubwa kwa kutumia Mti.
"Prince" William akiagana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamis Kigwangala (Mb.) ambapo anaelekea Mkoani Kilimanjaro kuendelea na ziara yake, akiwa huko atatembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo mkoani Tanga na Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro.


 





No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.