TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Ziara ya Mjukuu wa Malkia wa
Uingereza nchini, (Prince William)
Mjukuu wa Malkia wa
Uingereza “Prince” William anatarajiwa kufanya ziara nchini kuanzia tarehe 26
hadi 29 Septemba 2018. Ziara hiyo
inakuja kufuatia maombi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan alipofanya naye mazungumzo wakati wa mkutano wa Wakuu
wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Uingereza mwezi Aprili
2018.
“Prince” William
atakapowasili nchini pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Aidha,
atatembelea kikosi cha Maji cha Jeshi la Polisi; Bandari ya Dar es Salaam;
Jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii (Mpingo House); Hifadhi ya Taifa ya
Mkomazi iliyopo mkoani Tanga na Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka
kilichopo mkoani Kilimanjaro.
“Prince” William ni
mmoja wa wanaharakati duniani wanaopinga biashara haramu ya bidhaa za
wanyamapori na Uingereza imekuwa ikisifu juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya
Tanzania katika kupambana na vitendo vya ujangili.
“Prince” William
ataondoka nchini tarehe 29 Septemba 2018 kuelekea nchini Kenya.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 21 Septemba 2018
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.