Monday, September 3, 2018

Tanzania na China zasaini Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano kwenye sekta ya kilimo na uvuvi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa kwenye mazungumzo rasmi na Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo wa China, Mhe. Han Changfu alipotembelea Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Beijing tarehe 03 Septemba, 2018. Katika mazungumzo yao Mhe. Majaliwa alimweleza Waziri Han nia ya Tanzania ya kushirikiana na China katika kuendeleza sekta za kilimo, uvuvi na mifugo. Naye Waziri Han alimhakikishia Waziri Mkuu ushirikiano wa hali ya juu kati ya Tanzania na China ambapo nchi hiyo ipo tayari kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa wataalam wa kilimo kutoaka Tanzania. Mhe. Waziri Mkuu yupo nchini China kwa niaba ya Mhe. Rais kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la shirikiano kati Afrika na China.
Mazungumzo ya pande mbili yakiendelea na kuhudhuriwa na viongozi wengine mbalimbali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu, Prof. Adolf Mkenda na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Khatibu Kazungu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bibi Justa Nyange akifuatilia mazungumzo
Waziri wa Kilimo, Maliasili na Uvuvi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Rashid Ali Juma kwa pamoja na mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo ya China wakisaini kwa niaba ya Serikali zao Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano kwenye sekta za kilimo na uvuvi. Wanaoshuhudia ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Kilimo wa China, Mhe. Han Changfu
Wakibadilishana mkataba mara baada ya kuusaini




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.