28 Machi 2019
TAARIFA KWA UMMA
TANGAZO LA MAFUNZO YA KILIMO NCHINI ISRAEL
UTANGULIZI
Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki inatangaza ufadhili wa mafunzo katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini
Israel. Mafunzo hayo ni ya miezi 11 kuanzia mwezi Septemba, 2019 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya Israel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mafunzo hayo yatahusisha pia vitendo (field attachment) kwenye mashamba
makubwa ya mazao mbali mbali yakiwemo ya matunda, mbogamboga, ufugaji, uvuvi na
mazao mengine ya biashara kwa ujira maalum.
SIFA NA VIGEZO VYA MWOMBAJI
- Awe ni raia wa Tanzania
mwenye umri wa kati ya miaka 20-35 pamoja na cheti cha kuzaliwa na Kitambulisho
cha Uraia.
- Awe amehitimu mafunzo ya
Kilimo katika ngazi ya shahada ya Chuo Kikuu,Stashahada au Astashahada ya Vyuo
vya kilimo vinavyotambulika nchini.
- Awe na afya njema.
- Awe na ujuzi wa kuandika
na kuongea lugha ya Kiingereza.
- Awe na uwezo wa kufanya kazi
na watu wa tamaduni mbalimbali.
- Awe tayari kurejea nchini
baada ya mafunzo yake.
UTARATIBU WA KUFANYA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kwa
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yakiwa
yameambatishwa na nakala za nyaraka zifuatazo:
i. Cheti cha kuzaliwa na
uraia.
ii. Vyeti vya kitaaluma.
iii.
Hati ya Kusafiria au
uthibitisho wa maombi ya pasipoti.
iv. Cheti cha kuthibitisha
afya kutoka hospitali inayotambulika.
v. Barua ya kuonesha sababu
za kushiriki mafunzo hayo (Motivation
letter) kwa lugha ya Kiingereza.
vi.
Wasifu (Curriculum Vitae).
vii.
Picha mbili ndogo
(Passport size).
viii.
Majina na anwani za
wadhamini watatu wanaoishi nchini akiwemo mwalimu wa Chuo ulichohitimu.
Maombi yote yatumwe kupitia
anwani ifuatayo: -
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,
Jengo
la LAPF
Ghorofa
ya 6,
Barabara
ya Makole,
S.L.P 2933,
DODOMA.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 12 Aprili, 2019
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Dodoma.