Thursday, June 20, 2019

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akimsikiliza Mwakilishi wa Kaimu Balozi wa Marekani hapa Nchini Bi Janine S. Young  alipomwita Wizarani kutoa ufafanuzi kuhusu angalizo la kiusalama lilitolewa na ubalozi huo kupitia tovuti ya Ubalozi wa Marekani hapa Nchini. June 20,2019. 


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKI WAMWITA KAIMU BALOZI WA MAREKANI WIZARANI

Tarehe 19 June, 2019, Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania ulitoa taarifa katika mitandao ya kijamii “Twitter” kuhusu angalizo la kiusalama “security alert”. Angalizo hilo la kiusalama lilitokana na uvumi unaodaiwa na ubalozi huo kusambaa kuhusu uwezekano wa kutokea kwa shambulio katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulimwita katika ofisi ndogo za Wizara zilizopo Jijini Dar es Salaam, Kaimu Balozi wa Marekani Bi Janine S. Young ili kutoa ufafanuzi wa “twitter” yao. 

Ubalozi wa Marekani ulimtuma Mwakilishi wa Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Janine S. Young kuonana na uongozi wa Wizara ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe.  

Bi Janine S. Young ameutambua ujumbe huo na kukiri kuwa  umetumwa na ubalozi wa Marekani hapa nchini.

Katika ufafanuzi wake amekiri kuwa Ubalozi umefanya makosa ya kutoa tetesi ambazo hazikuwalenga raia wa Marekani pekee bali raia wote wakitambua kuwa Ubalozi hauna mamlaka ya kufanya hivyo jambo lililosababisha taharuki kwa wananchi na wageni wanaotarajia kuitembelea Tanzania. 

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeukumbusha Ubalozi wa Marekani umuhimu wa kuzingatia sheria za nchi na taratibu za kidiplomasia zinazokubalika duniani kote katika utoaji wa taarifa za aina hii.

 Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe amewataka wananchi na Jumuiya za Kimataifa pamoja na wageni mbalimbali waliopo  nchini na wanaotarajia kuitembelea Tanzania kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani mpaka sasa hakuna taarifa yeyote iliyothibitishwa ya kuwepo kwa tishio la aina hiyo hapa nchini na kwamba Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimejizatiti kukabiliana na matishio yeyote.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar Es Salaam.
20 Juni, 2019



Wednesday, June 19, 2019

Wizara inaendelea kuhudumia wananchi Wiki ya Utumishi wa Umma

Bw. Hassan Mnondwa,  Mtumishi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoa ufafanuzi kwa Bw. Abdullatif kuhusu majukumu ya Wizara  alipofika kwenye Dawati la Wizara wakati wa kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma. Mwingine katika picha ni Mtumishi wa Wizara, Bi. Roxana Kagero. Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo ipo kwa mujibu wa Kalenda ya Umoja wa Afrika, Wizara imefungua madawati maalum kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo kusikiliza na kujibu hoja zao kuhusu Wizara pamoja na kueleza majukumu yanayotekelezwa na Wizara.
Mtumishi wa Wizara akimhudumia mgeni, Bi.Eunice Mmari kutoka Ofisi ya Kamishna wa Kazi aliyefika kwenye Dawati la Wizara katika Ofisi za Wizara zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza tarehe 16 hadi 23 Juni 2019.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Macha na Deogratius wakiwa tayari kuwapokea na kuwahudumia wadau mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Jenipher akiwa kwenye dawati lililopo Ofisi za Wizara za Mtumba tayari kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2019
Mtumishi wa Wizara akiwa tayari kwenye dawati lilopo Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar kwa ajili ya kuwahudumia wananchi katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma

Tuesday, June 18, 2019

Waziri Kabudi akutana na Balozi Al - Mashaan

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait anayeshughulikia masuala ya Afrika, Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan.

Pamoja na mambo mengine walizungumzia kuhusu jinsi ya kuboresha mahusiano yaliyopo katika kati ya Tanzania na Kuwait, nchi ya Kuwait imekuwa ni kati ya wadau muhimu wa Maendeleo hapa nchini kupitia mradi wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait(Kuwait Fund). 


Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimwelezea jambo Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan
Balozi Mubarak Mohamed Al -Sehaijan pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwait nchini wakisikiliza kwa makini mazungumzo hayo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan (hawapo pichani)
Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan naye akimweleza jambo  Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.)
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan (hawapo pichani)
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan, Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohamed AlSehaijan (wa pili kutoka kulia) pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwaiti na Afisa Mambo ya Nje Bw. Odilo Fidelis (wa pili kutoka kushoto)









TANZANIA YAWAHAKIKISHIA MAZINGIRA BORA WAWEKEZAJI WA KIMAREKANI NCHINI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akihutubia wakati wakufunga Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani, ulioandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji, Ubalozi wa Marekani, Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa wa afrika mashariki na Wizara ya Viwanda na Biashara  pamoja na Chemba ya wafanyabiashara wa kimarekani nchini Tanzania ikiwa ni juhudi za serikali ya Tanzania kupitia Wizara na taasisi za Serikali kusikiliza na kutatua changamoto za wawekezaji na wafanyabiashara wa Ndani na Nje. Ambapo Prof. Palamagamba alieleza kuwa Tanzania kwa sasa kuna mazingira mazuri ya kuvutia uwekezaji. 

Aidha, aliezea kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, imeweka usawa kwa kuwasikiliza wawekezaji wa Ndani na wawekezaji kutoka Nje. 

Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania (AMCHAM) Bw. Garry Friend akipokea nakala za vitabu vya bajeti ya serikali kutoka kwa Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ili kujionea mabadiliko ya uwekezaji nchini yalivyoboreshwa.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania (AMCHAM) Bw. Garry Friend akimsikiliza kwa makini Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda wakifuatilia kwa makini mambo yaliyokuwa yakielezwa na Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)
Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi K. Patterson naye akizungumza kwenye Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Sehemu ya wageni waliohudhuria kwenye mjadala huo, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Marekani na Ulaya Bw. Jestas Nyamanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki (Mb.) naye akihutubia kwenye Mjadala wa kwanza wa Kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Mhe. Godfrey Mwambe naye akielezea namna kituo hichi kilivyoboresha na kinavyoshirikiana na taasisi nyingine katika kuhakikisha mwekezaji anapokuja nchini hapati shida. 
Juu na Chini ni Sehemu ya wageni waalikwa wakimsikiliza Bw. Godfrey Mwambe (hayupo pichani).


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi K. Patterson 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akijadiliana jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (wa kwanza kilia)
Prof. Palamagamba John Kabudi, Mhe. Angela Kairuki pamoja na Dkt. Faraji Mnyepe wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa Mjadala wa kwanza wa kibiashara kati ya Tanzania na Marekani
Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Marekani hapa nchini pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria kwenye mjadala huo















Monday, June 17, 2019

Call to Design Corporate Logo for the EAC 20 Anniversary


East African Community

Consultancy ON DESIGN OF THE EAC 20TH ANNIVERSARY CORPORATE LOGO

1.0 Introduction

The EAC is set to mark its 20th Anniversary with various activities and events culminating into EAC Day on 30th November, 2019, the date of the 21st Ordinary Summit of the EAC Heads of State.

2.0 Objective

For purposes of publicity and branding, the Community requires a logo to brand its 20th Anniversary celebrations. The EAC Secretariat intends to engage a creative artist or graphic designer to come up with a logo for the anniversary.

The graphic designer will be required to provide the following:

i)   Three designs of the proposed 20th Anniversary Logo from which the Secretariat can select;
ii)  Three soft copies of the proposed 20th Anniversary Logo from which one will be selected for use during the 20th Anniversary;
iii) Three hard copies of the proposed logo; and
iv) Designs that are usable in multimedia channels (print, electronic, social media, etc.)

4.0 Qualification / Competencies required

(a)  A Senior Expert/Design Firm who has at least 10 years previous experience in graphics design, new brand creation and logos development
(b)  A Senior Expert/Design Firm who has directed or supported at least two re branding activities
(c)  A Senior Expert/Design Firm who has strong experience in creating visual campaigns 
(d)  Bachelor’s Degree in Graphics design, brand development, business administration or other relevant fields. A Master’s Degree will be preferred but is not mandatory. 
(e)  Must be an East African national/East African based Brand Design Firm

5.0 Submission Requirements

(a)  Application Letter/Expression of Interest
(b)  CV of key experts to be involved with references for previous assignments
(c)  Previous design portfolio (new logo/brand design development, not more than 20 pages)
(d)  Proof of minimum two previous similar assignments undertaken.

Interested Brand Design Experts/Firms should submit Technical and Financial proposals by email to Procurement@eachq.org not later than 26th June, 2019.

Wamiliki wa Hoteli wakutana na Prof. Kabudi Kuhusu SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akihutubia kwenye mkutano wa wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli (hawapo pichani) Mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.
  Baadhi ya Wafanyabiashara na Wamiliki wa Hoteli wakifuatilia kwa ukaribu mkutano baina yao na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)(hayupo pichani) Mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraji Mnyepe akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli (hawapo pichani) Mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraji Mnyepe wakati wa Mkutano wa wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli (hawapo pichani) Mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiendelea kuhutubia kwenye mkutano wa wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli (hawapo pichani) Mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.
 Sehemu ya Wafanyabiashara na Wamiliki wa Hoteli waliohudhuria mkutano wa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)(hayupo pichani). Mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019. 
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wamiliki wa Hoteli wakisubiri kupiga picha ya pamoja  na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)(hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli baada ya kumalizika mkutano baina yao uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.  Kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Bi. Agnes Kayola. 
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na baadhi ya wamiliki na wafanyabiashara wa Hoteli baada ya kumalizika mkutano baina yao katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.

Friday, June 14, 2019

Prof. Kabudi amuaga Balozi wa India

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Balozi wa India anayemaliza muda wa uwakilishi nchini, Mhe. Sandeep Arya (wa pili baada ya aliyevaa tai nyekundu) jijini Dar Es Salaam. Mhe. Waziri alimuandalia chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Mhe. Balozi. Katika chakula hicho, Prof. Kabudi alishukuru misaada ya maendeleo inayotolewa na Serikali ya India katika sekta mbalimbali zikiwemo za maji, elimu, nishati na afya. Mhe. Waziri pia alimuhakikishia Mhe. Balozi kuwa Serikali itatoa ushirikiano kwa Balozi mpya atakayekuja kuchukua nafasi yake nchini.
Balozi wa India anayemaliza muda wa uwakilishi nchini (wa pili kutoka kulia) akiwa na ujumbe wake wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshima yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Prof. Kabudi akiwa na ujumbe wake wakati wa chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Balozi wa India anayemaliza muda wa uwakilishi nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimpa zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro na Mbuga ya Wanyama Balozi wa India anayemaliza muda wa uwakilishi nchini, Mhe. Sandeep Arya.

TANGAZO KUHUSU USHIRIKI WA WIZARA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


TANGAZO

            MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa, itashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuanzia tarehe 17 hadi 22 Juni 2019. Maadhimisho haya ni kwa mujibu wa kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu Utumishi wa Umma.

Wakati wa maadhimisho hayo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeandaa madawati maalum ya kutoa huduma kwa wananchi katika Ofisi za Wizara zilizopo Kata ya Mtumba jijini Dodoma na zile zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Huduma zitakazotolewa ni pamoja na kusikiliza na kutoa ufafafanuzi wa hoja mbalimbali za wananchi kuhusu Wizara pamoja na kutoa elimu kuhusu majukumu yanayotekelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika.

Madawati hayo yatakuwa wazi kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.


NYOTE MNAKARIBISHWA.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
14 Juni 2019




Kampuni 11 za Uturuki zatafuta fursa za Uwekezaji

Dodoma, 14 Juni 2019

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kampuni 11 za Uturuki zatafuta fursa za Uwekezaji 

Ujumbe wa kampuni 11  kutoka Uturuki upo nchini kwa ajili ya kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji, hususan kwenye sekta ya viwanda vya dawa za binadamu, vifaa vya maabara, vyombo vya ndani,  vifaa vya umeme, ujenzi pamoja na ununuzi wa korosho.

Ziara hiyo imetokana na uratibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Ujumbe huo ambao uliwasili nchini tarehe 10 Juni 2019 ulishiriki mkutano (B2B) uliondaliwa na TPSF tarehe 11 Juni 2019. Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine,  wawakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Ukanda  wa Uwekezaji (EPZA) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) walitoa maelezo kuhusu kanuni, taratibu na mazingira ya kufanya biashara hapa nchini.

Ujumbe huo utatembelea Zanzibar tarehe 13 Juni 2019 na baadaye Dodoma kwa ajili ya kuangalia maonyesho ya masuala ya ujenzi. Ujumbe huo utaondoka nchini tarehe 16 Juni 2019 kurejea Uturuki.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Majadiliano baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki yakiendelea katika ukumbi wa TPSF. Aliyesimama ni Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe Ali Davutoglu ambaye anatoa ufafanuzi kuhusu mazingira ya biashara Tanzania.

Mwenyekiti wa TPSF, Bw. Salum Shamte (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa kampuni hizo za Uturuki, Bw. Ali Engiz. Wengine ni Bw. Godfrey Simbeye (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF na Mhe. Ali Davutoglu, Balozi wa Uturuki hapa nchini.

Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Hassani Mwamweta (kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa wafanyabiashara wa Uturuki na Tanzania.


Thursday, June 13, 2019

Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Rwanda

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akisalimiana na mgeni wake ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille alipowasili katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 12 Juni 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille. Mazungumzo yao yalifanyika  katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 12 Juni 2019
Mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.)  na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille yakiendelea. Kushoto kwa Mhe. Kabudi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 12 Juni 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiagana na mgeni wake ambaye ni  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 12 Juni 2019
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille (kulia) akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe mara baada ya kuwasili  katika Ofisi ndogo za Wizara  zilizopo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi yaliyofanyika tarehe 12 Juni 2019.