Wednesday, July 22, 2020
Tuesday, July 21, 2020
Naibu Katibu Mkuu Dkt Haji akaribishwa rasmi Wizarani
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Dkt Mwinyi Talib Haji katika ofisi za Wizara Mtumba, Dodoma, mara baada ya kuapishwa tarehe 20 Julai 2020.
Naibu Katibu Mkuu akisalimiana na sehemu ya Menejimenti
Naibu Katibu Mkuu akisalimiana na sehemu ya Wakurugenzi, kulia ni Katibu Mkuu Balozi Ibuge akiwa emeongozana nae.
Katibu Mkuu Balozi Ibuge akiwa katika mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu alipomkaribisha ofisini kwake Mtumba, Dodoma.
Thursday, July 16, 2020
DKT. NDUMBARO AFANYA MAZUNGUMZO NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA MKOA WA RUVUMA
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Wilaya hiyo Mhe. Christina Mndeme ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
Mazungumzo hayo yamefanyika baada kuhitimisha ziara iliyofanywa na Dkt. Ndumbaro ya kutembelea mipaka inayoinganisha Tanzania na nchi jirani ya Msumbiji iliyopo katika Mkoa wa Ruvuma.
Dkt. Ndumbaro kwa nyakati tofauti katika mwaka huu amefanya ziara maalumu katika mpaka wa Magazini uliopo Wilayani Namtumbo-Ruvuma, Wenje uliopo Wilayani Tunduru-Ruvuma, Chiwindi uliopo Wilayani Nyasa-Ruvuma na baadaye mpaka wa Mkenda uliopo Wilaya ya Songea Vijijini. Mipaka yote inaiunganisha Tanzania na Nchi jirani ya Msumbiji.
Lengo la kufanya ziara ilikuwa ni kubaini na kutatua changamoto zinazokabili maeneo ya mipakani sambamba na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. Katika ziara hizo Dkt. Ndumbaro alikutana na kuafanya mazungumzo na baadhi ya wananchi na watumishi katika mipaka husika. Sambamba na changamoto kadhaa alizozibaini aliridhishwa na utendaji wa Watumishi waliopo mpakani na kuwahimiza kundelea kufanyakazi kwa bidii,ubunifu na kwa kuzingatia maadali.
Aidha, Dkt. Ndumbaro katika kikao chake na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa wa Ruma amebainisha kuwa changamoto nyingi zilizoelezwa mipakani zikiwemo ukosefu wa umeme, barabara za kiwango cha lami, mawasiliano na Vituo vya kutoa huduma Pamoja Mpakani (OSBP), Serikali chini ya usimamizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tayari zimeanza kufanyiwa kazi.
Dkt. Ndumbaro kwa upande wake amehimiza umuhimu wa Mamlaka za Mkoa hasa zilizopo maeneo ya Mipakani kuendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi, kudumisha na kulinda uhusiano wa kidiplomasia na nchi jirani.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mhe. Christina Mndeme kwa niaba ya Kamati ya Ulinzi ya Mkoa, amempongeza Naibu Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro kwa ziara hiyo na jitihada anazifanya katika kuhakikisha Diplomasia ya Uchumi inaendelea kutekelezwa kwa mafanikio makubwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisaini kitabu cha Wageni alipo wasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mideme |
|
Wednesday, July 15, 2020
DKT. NDUMBARO AFANYA ZIARA KATIKA MPAKA WA MKENDA, RUVUMA
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Wafanyakaozi wanahudumu katika mpaka wa Mkenda. Kushoto ni Mhe. Pololet Mgema Mkuu wa Wilaya ya Songea Vijijini. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Mkuu wa Wilaya ya Songea Vijijini Mhe. Pololet Mgema wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wakazi wa mpakani Mkenda |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akipokelewa na Maafisa Uhamiaji wa upande wa Msumbiji alipotembelea ofisi za mpakani Mkenda za nchi hiyo wakati wa ziara. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisaini kitabu cha Wageni alipotembelea Ofisi ya Uhamiaji za Msumbiji zilizopo mpakani Mkenda, Ruvuma |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Mkuu wa Wilaya ya Songea Vijijini Mhe. Pololet Mgema wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya Watumishi wa Mpakani kutoka Tanzania na Msumbiji |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akiendelea na ziara katika maeneo mbalimbali ya mpaka |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisisitiza jambo wakati wa mazunguzo na daadhi Wananchi waliojitokeza wakati wa ziara |
Friday, July 10, 2020
TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO, KUKUZA MAENDELEO
Tanzania
na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa
nchi hizo zinakuwa na maendeleo endelevu.
Makubaliano
hayo yamefanywa na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, wakati alipokutana kwa
mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge leo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Ibuge amesema kuwa wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo suala la
namna ya kutekeleza nia ya Viongozi Wakuu wa nchii za China na Tanzania (Rais
wa China, Mhe. Xi Jinping pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
John Joseph Pombe Maufuli) ya kupunguza madhara yatokanayo na ugonjwa wa COVID
19 ikiwemo kufutiwa na kusamehewa madeni.
Naishukuru
Serikali ya China kwa uhusiano na ushirikiano ambao imekuwa ikionesha kwa
Tanzania. Uhusiano huo umeendelezwa na viongozi wa pande zote mbili ambao
umekuwa ukiimarika siku hadi siku na kuahidi kuwa serikali ya Tanzania
itaendela kudumisha ushirikiano wake wa kidiplomasia kati yake na China.
Pamoja
na mambo mengine, mazungumzo yalijadili masuala ya biashara na uwekezaji, mradi
wa nyumba 25 za wataalum wa Afya zilizopo Osterbay jijini Dar es Salaam.
Kwa
upande wake Balozi Wang Ke pamoja na mambo mengine, ameipongeza Serikali ya
Tanzania kwa jitihada ilizochukua katika kukukuza uchumi wake hadi kufikia
uchumi wa kati, pamoja na mapambano dhidi ya COVID 19.
"Leo
nimekutana na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Balozi Brigedia Jenerali Ibuge na
kuongea mambo mbalimbali ya ushirikiano na tunaipongeza Serikali ya Tanzania
kwa jitihada ilizochukua katika kufanya
kazi kwa bidii na kukuza uchumi wake hadi kufikia uchumi wa kati, pamoja na hatua
ilizochukua katika kupambana na janga la COVID 19 ambapo tumefurahishwa kuona
janga la COVID 19 limeisha," Amesema Balozi Ke.
Balozi
Ke ameongeza kuwa wamekubaliana katika maongezi hayo pia kuendeleza ushirikiano
wa kufanya kazi kwa pamoja kwa manufaa ya mataifa mawili (Tanzania na China)
ili kuhakikisha uhusiano na ushirikiano unazidi kukua na kuimarika.
Tanzania na China zimekuwa zikishirikiana
katika sekta za kilimo, biashara na uwekezaji, miradi ya mikopo nafuu na misaada,
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Uchukuzi, Afya, Utalii na
utamaduni.
China
na Tanzania zilianzisha mahusiano rasmi ya kidiplomasia mwaka 1964.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert
Ibuge akiongea na Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, wakati walipokutana kwa
mazungumzo leo jijini Dar es Salaam
Thursday, July 9, 2020
Tuesday, July 7, 2020
NUMBER OF FRENCH TOURISTS SURGE TO 56,000
The number of French tourists visiting Tanzania increased from 21,000 in 2016 to 56,000 last year, thanks to the Tanganyika Expeditions Agency and Axium by Parker operators, who have been organising trips.
Speaking at a meeting with French tour operators and tourism professionals in Paris recently, Tanzanian Ambassador to France Samwel Shelukindo told participants that the government of Tanzania had lifted restrictions on commercial flights and quarantine measures imposed on travellers since May 18, this year.
He noted that international airlines, including Ethiopian Airlines, Qatar Airways and KLM had already resumed flights to Tanzania.
"As it is the case in other countries, Tanzania was also affected by the Covid-19 pandemic, but now coronavirus cases have dropped significantly, thanks to the commitment and efforts made by the government under the leadership of our President John Magufuli and Tanzanian people who understood the challenge and complied with preventive measures to fight against the covid-19 pandemic," said the ambassador.
He added that the Ministry of Natural Resources and Tourism had developed national standard operating procedures (SOPs) for the management of Covid-19 in tourism business and invited potential tourists to consult the embassy.
"In this respect, I would like to underline that Tanzania has started receiving tourists. All precautions and preventive measures are taken to receive tourists and enable them to have an unforgettable stay. The government has also created an enabling environment to attract tourists."
French tour operators listening to Tanzanian Ambassador's speech |
Monday, July 6, 2020
KATIBU MKUU BALOZI BRIGEDIA JENERALI IBUGE ATEMBELEA BANDA LA WIZARA SABASABA
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, ametembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika banda la Wizara Balozi Ibuge amewataka Watanzania kuendelea kuchapa kazi zaidi ili kuyaona matunda ya nchi kuwa katika kundi la uchumi wa kati.
''Sasa nchi yetu imeingia katika uchumi wa kati ambao unamaanisha kila mtu aendelee kupiga juhudi zaidi ya pale alivyokuwa anafanya ili tuendelee kupaa kuliko hivi ambavyo tumefikia sasa'' amesema Balozi Ibuge.
Amesema Tanzania sasa ina Balozi 43 na Balozi ndogo tatu na ni mwenyeji wa Balozi 63 na Mashirika ya Kimataifa 30 ikiwa ni namna ya kuipeleka Tanzania katika anga za kimataifa tukionyesha mafanikio vivutio vyetu na vitu vingine vyote tunavyovifanya ili kujiletea maendeleo huku tukiimarisha mahusiano ya kimataifa.
Akiwa katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Balozi Ibuge ametembelea banda la Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) na makampuni matatu ya Kigeni yanayoshiriki maonesho hayo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akizungumza na watumishi alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akiangalia jarida linaloelezea utekelezaji wa dipolomasia ya uchumi linalochapishwa na Wizara alipotembelea banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, katika picha ya pamoja na watumishi walioko kwenye banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akijadili jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt. Ave Maria Semakafu walipotembelea moja ya banda kwenye maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dkt. Ave Maria Semakafu wakimsikiliza mfanyabiashara kutoka Siria anayeshiriki maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam |
Sunday, July 5, 2020
DKT. NDUMBARO ATEMBELEA BANDA LA WIZARA SABASABA
Naibu Waziri wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, ametembelea
banda la Wizara katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020
yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika banda la Wizara
Dkt. Ndumbaro amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa
zaidi ili kuiletea sifa Serikali na kuendelea kuimarisha mahusiano ya kimataifa.
"Kwa kuwa sisi
tunafanya kazi ya kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Nje na kuhakikisha mahusiano
ya kimataifa yanaimarika hatuna budi kufanya kazi kwa bidii na maarifa yetu
yote, hili ni jukumu letu hivyo ni lazima tuhakikishe tunalitekeleza kwa
ufanisi na ufasaha," Amesema Dkt. Ndumbaro
Akiwa katika maonesho ya 44
ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Dkt. Ndumbaro ametembelea pia banda la Bunge,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania.
Watumishi wa Wizara
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, alipotembelea banda la Wizara katika maonesho
ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea jijini Dar es
Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dkt. Ndumbaro, akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara katika maonesho
ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) 2020 yanayoendelea jijini Dar es
Salaam.
Thursday, July 2, 2020
PROF. KABUDI ATETA NA MJUMBE MAALUM WA MAZIWA MAKUU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Prof.
Kabudi ateta na Mjumbe Maalum wa Maziwa Makuu
Dodoma, 2 Julai 2020
Tanzania inaamini katika
umoja wa jumuiya ya kimataifa kwenye kutafuta ufumbuzi wa changamoto
zinazoikabili dunia ikiwemo mlipuko wa ugonjwa wa Corona.
Kauli hiyo imetolewa leo na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb.) alipofanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Mjumbe Maalum wa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Maziwa Makuu, Balozi Huang Xia.
Viongozi hao walitumia fursa
hiyo kubadilishana mawazo katika masuala mbalimbali yanayotokea duniani, ikiwa
ni pamoja na mikakati na mbinu bora za kukabiliana na janga la ugonjwa wa
Corona na athari zake katika uchumi kwenye eneo la Maziwa Makuu.
Balozi Huang alielezea hatua
mbalimbali anazozichukua zikiwemo kuongea na taasisi za kimataifa za fedha na
wadau wengine kwa ajili ya kuzihimiza kutoa misaada kwa nchi za Maziwa Makuu
ili ziweze kukabiliana na janga la ugonjwa wa Corona na athari zake za kiuchumi
na kijamii. Licha ya kukutana na taasisi hizo, Balozi Huang pia amefanya mashauriano
na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Maziwa Makuu kuhusu janga la Corona.
Kwenye mashauriano hayo Mawaziri wamesisitiza umuhimu wa kuandaa mkutano wa
Mawaziri kwa njia ya mtandao ili kujadili, pamoja na mambo mengine mikakati ya
kukabiliana na ugonjwa wa Corona na hali ya usalama katika eneo la Maziwa
Makuu.
Kwa upande wake, Prof.
Kabudi aliunga mkono wazo la kuwa na mkutano wa Mawaziri wa nchi za Maziwa
Makuu na kuelezea matumaini yake kuwa, mkutano huo utatoa mawazo mazuri
yatakayosaidia ufumbuzi katika changamoto zinazoikabili dunia ukiwemo ugonjwa
wa Corona.
Aidha, Prof. Kabudi alitoa
maelezo kuhusu mikakati iliyochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kudhibiti
ugonjwa wa Corona. Alisema moja ya mikakati hiyo ni tangazo la maombi ya siku
tatu kwa nchi nzima lililotolewa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, maombi ambayo yaliyohusisha imani zote. Tangazo hilo lilionekana ni jambo geni kwa watu wengi duniani
lakini kwa Tanzania, nchi yenye waislamu na wakristo takribani nusu kwa nusu, lilikuwa
ni muhimu na uamuzi huo haukuifanya Tanzania kupuuza maelekezo mengine
yanayotolewa na wataalam wa afya.
Mazungumzo hayo
yalihitimishwa kwa Mhe. Waziri kuahidi kuwa, Tanzania itashirikiana kwa karibu
na ofisi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika uamuzi wake wa kuandaa
mkakati maalum wa kuzuia migogoro na kuimarisha amani na utulivu kwenye eneo la
nchi za maziwa makuu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza kwa njia ya mtandao na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe. Balozi Huang Xia kuhusu ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona na masuala ya amani na usalama katika ukanda huo. Mazungumzo hayo yalifanyika Prof. Kabudi akiwa jijini Dodoma huku Balozi Huang Xia akiwa jijini Nairobi, Kenya. |
Sehemu ya ujumbe ulioambatana na Mhe. Prof. Kabudi ukifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Kabudi na Balozi Huang Xia (hawapo pichani). Kulia ni Bw. Magabilo Murobi, Katibu wa Waziri na Bw. Ali Ubwa, Afisa Mambo ya Nje. |
Monday, June 29, 2020
VACANCY ANNOUNCEMENT
PRESS RELEASE
VACANCY ANNOUNCEMENT
Dodoma, 29 June 2020
The
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy
notification from the Commonwealth Secretariat inviting qualified Tanzanians to
apply for the post of Assistant Research Officer-International Trade
Policy Section.
Application
details can be found through the Secretariat’s website, http://thecommonwealth.org/jobs. Closing date for application is Wednesday 8 July 2020.
“The
Ministry encourages qualified Tanzanians to apply”.
Issued by;
Government Communication Unit
Friday, June 26, 2020
MKUTANO WA MAWAZIRI WA KAMATI YA SADC YA ASASI YA USHIRIKIANO WA SIASA, ULINZI NA USALAMA (TROIKA) WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM
Mkutano wa Mawaziri wa
Kamati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Asasi ya Ushirikiano
wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa ngazi ya Mawaziri umefanyika kwa njia ya
Mtandao (Video Conferencing) na kujadili masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama.
Mkutano huo umefanyika chini
ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Jamhuri ya
Zimbabwe, Mhe. Sibusiso Busi Moyo na utakutanisha Mawaziri wenye dhamana ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mambo ya Ndani, Ulinzi pamoja na
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka nchi wanachama wa SADC. Ujumbe wa
Tanzania umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi.
Mkutano huo umehudhuriwa
na nchi 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, Comoro,
DRC, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia,
Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi
(katikati), kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nchi George Simbachawene na mwisho
kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi, Dkt. Faraji Mnyepe wakifuatilia
mkutano kwa njia ya video conference, Jijini Dar es salaam
|
Mawaziri pamoja
na baadhi ya Makatibu Wakuu/Maafisa waandamizi kutoka Tanzania wakifuatilia
mkutano kwa njia ya Video Conference, jijini Dar es Salaam
|
Mkutano
ukiendelea
|
IMF YAAHIDI KUIPATIA TANZANIA FEDHA ITAKAYOIHITAJI
Shirika la
Fedha Duniani (IMF) limeahidi kuipatia Tanzania fedha itakayoihitaji ili iweze
kuendelea kukabiliana na athari zitokanazo na janga la Covid 19 kwa ajili ya kuimarisha
uchumi wake.
Mkurugenzi
Mkazi wa IMF nchini Tanzania Bw. Jens Reinke ameyasema hayo wakati alipokutana
na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi leo katika ofisi ndogo za wizara jijini
Dar es Salaam.
Pia Bw. Reinke
ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua madhubuti inazozichukua
katika kukabiliana na janga la Covid 19
ili kuepusha madhara ya kiuchumi na kijamii.
Mazungumzo hayo
pia yamelenga miradi ya maendeleo, msamaha wa madeni kwa nchi zinazoendelea
ikiwemo Tanzania, ushirikiano baina ya IFM na Tanzania, biasara na utalii.
Kwa upande
wake, Prof. Kabudi ameishukuru (IMF) kwa msamaha wa madeni ambao umetolewa kwa Tanzania
na nchi nyingine, fedha zitakazoziwezesha nchi hizo kuendelea kukabiliana na Covid
19.
"Tumeongelea
mambo mbalimbali yanayohusu ushirikiano hasa katika kuimarisha uchumi wetu
baada ya janga la covid 19, usirikiano kati ya Tanzania na IMF unafahamika na tumekubaliana
baadhi ya mambo ambayo tutayafanyia kazi kwa kina ili tuweze kuimarisha uchumi wetu
baada ya corona hasa katika sekta ya utalii, biashara na miundombinu,"
amesema Prof. Kabudi.
Katika hatua
nyingine, Waziri Kabudi amekutana
na kumuaga Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh ambaye amemaliza
muda wake wa utumishi na amemtakia maisha mema na kumsihi kuendelea kuwa balozi
mwema kwa Tanzania nchini Vietnam na duniani kwa ujumla.
"Kwa niaba ya Serikali napenda
kukuhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Vietnam katika nyanja mbalimbali
za kimataifa ikiwemo kuiunga mkono Vietnum katika kugombea nafasi mbalimbali
katika Masirika ya KImataifa," Amesema Prof. Kabudi.
Nae Balozi Doanh ameishukuru Tanzania
kwa ushirikiano ambao imekuwa ikimpatia alipokuwa akitekeleza majukumu yake
nchini wakati wote na kuahidi kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili
utaendelea kuimarishwa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa IMF nchini Tanzania Bw. Jens Reinke |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akimuelezea jambo Mkurugenzi Mkazi wa IMF nchini Tanzania Bw. Jens Reinke leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam |
Mkurugenzi Mkazi wa IMF nchini Tanzania Bw. Jens
Reinke akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Prof. Palamagamba John Kabudi leo katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es
Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akiongea na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh ambaye
amemaliza muda wake wa utumishi nchini Tanzania
Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi |
Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh akimkabidhi
zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi
Subscribe to:
Posts (Atom)