Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia majadiliano |
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia, Bw. Humphrey Shangarai na Afisa Ubalozi Bw. Sunday Iddi wakifuatilia majadiliano. |
Ujumbe wa Tanzania. |
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia majadiliano |
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia, Bw. Humphrey Shangarai na Afisa Ubalozi Bw. Sunday Iddi wakifuatilia majadiliano. |
Ujumbe wa Tanzania. |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab (kulia) akiwa katika mazungumzo na na Bi. Josephine Etima kiongozi wa ujumbe wa Wataalam wa Umoja wa Afrika wa Kutathimini utekelezaji wa Agenda 2063, yaliyofanyika jijini Dodoma |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab (kulia) akisalimiana na Bi. Josephine Etima kiongozi wa ujumbe wa Wataalam wa Umoja wa Afrika wa Kutathimini utekelezaji wa Agenda 2063 walipowasili Wizarani jijini Dodoma |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab (mwenye kilemba) akiwa katika mazungumzo na ujumbe wa Wataalam wa Umoja wa Afrika wa Kutathimini utekelezaji wa Agenda 2063 |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab (mwenye kilemba) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Wataalam wa Umoja wa Afrika wa Kutathimini utekelezaji wa Agenda 2063 (kulia kwa Balozi Fatma) na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje (kushoto kwa Balozi Fatma) |
Mazungumzo yakiendelea |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yake na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto Ikulu jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yake na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto Ikulu jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto akimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipozungumza katika Mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yao Ikulu jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yake na Mhe. Rais Samia Ikulu jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati yake na Mhe. Rais Samia Ikulu jijini Dar es Salaam. |
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax kabla ya kuanza kwa Mkutano wa waandishi wa habari na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Mhe. Dkt William Ruto baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. |
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Camilius Wambura akifuatilia Mkutano wa waandishi wa habari na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Mhe. Dkt William Ruto baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yao Ikulu jijini Dar es Salaam. |
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman (kulia) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine wakifuatilia Mkutano wa waandishi wa habari na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Mhe. Dkt William Ruto Ikulu jijini Dar es Salaam. |
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga akifuatilia Mkutano wa waandishi wa habari na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Mhe. Dkt William Ruto Ikulu jijini Dar es Salaam. |
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kenya zimekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi zao kwa manufaa ya pande zote mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema hayo Ikulu jijini Dar wa Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuelezea walichojadili katika mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto aliyekuwa na ziara ya kikazi ya siku mbili nchini .
“Ziara hii ya Mhe. Ruto nchini, imetuwezesha kujadili na kuhuisha mahusiano yetu na kutupa nafasi ya kujitathmini mashirikiano baina ya Tanzania na Kenya, na tumekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano baina yan chi zetu,” alisema Mhe. Rais
Amesema katika mazungumzo yao wamejadili masuala ya kimkakati kuhusiana na ushirikiano baina ya nchi hizo, kikanda na kimataifa na kuongeza kuwa wamekubaliana kukuza na kuimarisha uhusiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Kenya.
Mhe. Rais Samia amesema Tanzania inajivunia kuondolewa kwa vikwazo visivyo vya kodi ambavyo vilikuwa vinazuia ufanyaji wa Biashara kati ya Tanzania na Kenya.
“Wakati naingia madarakani kulikuwa na vikwazo visivyo vya kodi 68, lakini sasa vimefanyiwa kazi na kubaki 14, ni matarajio yetu kuwa vikwazo vilivyobaki navyo vitamalizwa na hivyo kurahisisha ufanyaji biashara baina ya nchi zetu”, alisema Mhe. Rais.
Amesema wamekubaliana kuanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa Kenya kupitia Nairobi.
Amesema kuwa wamejadili jinsi ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa lengo la kuzifanya nchi zao kuwa sehemu salama na kuongeza kuwa wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika masuala ya kikanda na kimataifa na kukuza Jumuiya ya Afrika Mashariki Kama viongozi waanzilishi wa Jumuiya hiyo pamoja na nchi ya Uganda
Akizungumza katika mkutano huo Rais wa Kenya Mhe. William Ruto amesema amedhamiria kuyafikisha mahusiano kati ya Tanzania na Kenya katika levo nyingine na dhamira hiyo itafanikiwa kutokana na utayari uliopo baina ya nchi hizo.
Amesema biashara kati ya Tanzania imekuwa ikiongezeka na viongozi hao wanadhamira ya kuongeza ufanyaji wa biashara baina ya Kenya na Tanzania na kufafanua kuwa biashara kati ya nchi hizo imeongezeka na kuifanya Tanzania kuwa mnufaika mkubwa kuliko ilivyokuwa awali.
“Mauzo ya Tanzania nchini Kenya yamekuwa yakiongezeka kwa kasi , kabla ya kuondolewa vikwazo visivyo vya kodi, sasa Kenya wananunua zaidi Tanzania kuliko ilivyo kuwa,” alisema
Amesema mauzo yameongezeka kutoka shilingi bilioni 31 hadi shilingi bilioni 41 na biashara imekuwa kutoka shilingi bilioni 27 hadi shilingi bilioni 51 na hivyo kuleta picha kuwa Tanzania sasa inanufaika sana na ufanyaji wa biashara na Kenya.
Amesema wamekubaliana kuwa Mawaziri na wadau wengine wote wanaohusika na biashara wananakutana na kuzifanyia kazi changamoto zinazokabili sekta ya biashara baina ya nchi hizo ili wananchi waweze kufanya biashara .
Amesema uongozi wake utatilia mkazo na kuhakikisha ujenzi wa bomba la gesi kutoka Dar es salaam hadi Mombasa unaharakishwa na kukamilika kwa wakati.
“Tutahakikisha tunatumia fursa ya ujenzi wa bomba la gesi kwenda Mombasa ili kuhakikisha tunatumia maliasili zetu na kuongeza ufanisi wa biashara na kuboresha maisha ya watu wetu, kuongeza na kuimarisha ushindani wa viwanda na wawekezaji wetu ,nchi zetu na ukanda wetu kwa ujumla
Amesema kukamilika kwa bomba hilo kutasaidia kukuza mpango wa viwanda katika nchi hizo na kuongeza kuwa utekelezaji wa mpango wa kuwa na mtandao mmoja kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki kwani walishakubaliana na baadhi ya nchi kuwa na mtandao mmoja
“Tutahakikisha tunatekeleza mpango huo ili kuwafanya wananchi wetu waweze kufanya biashara na kuwasiliana kwa urahisi na kwa gharama nafuu na hivyo kuendelea kuimarisha mahusiano yetu,” alsiema
Amesema wamewaelekeza watendaji katika nchi zao kukutana na kuandaa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya kabla mwaka huu haujaisha ili kujadili namna ya kuendelea kutatua changamoto zilizopo na hivyo kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo
Amewaambia Watanzania wajue kuwa wana marafiki na ndugu kutoka Kenya na kuahidi kuwa watafanya kazi pamoja na kuongeza kuwa Tanzania na Kenya hawawezi gawana njaa bali watagawana utajiri na fursa ili kujenga umoja kwa manufaa ya nchi zote mbili na watu wake
Rais Ruto aliwasili nchini tarehe 09/10/2022 kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili na aliondoka nchini kurejea Kenya tarehe 10/10/2022
Mkuu wa Itifaki Tanzania Balozi Yusuph Mndolwa akiwa na Mkuu wa Itifaki Kenya Balozi Betty Cherwon wakiwa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto nchini |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akizungumza wakati wa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan walipokutana Ikulu Dar es Salam. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto walipokutana Ikulu jijini Dar es Salaam |
Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto (katikati) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Dkt. Alfred Mutua (kushoto) wakati wa mazungumzo rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akiwasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungno Mhe. Samia Suluhu Hassan. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan. |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe Haroun Ali Suleiman alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan. |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan. |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Simbachawene alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan. |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Naimi Azizi alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan. |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto amewasili Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Dkt. Ruto na mke wake Mama Rachel Ruto wako nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku mbili waliwasili nchini tarehe 09/10/2022 na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Akiwa Ikulu Mhe. Dkt. Ruto alifanya mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na baadaye walikuwa na mazungumzo rasmi ambayo yalihudhuriwa na wajumbe wa pande zote mbili.
Viongozi hao walipomaliza mazungumzo yao walikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia walichojadili kwa umoja wao.
Baadaye viongozi hao walielekea katika ukumbi maalum ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliandaa dhifa malum kwa ajili ya mgeni wake Mhe. Rais Ruto.
Baada ya dhifa hiyo Mhe. Rais Ruto na ujumbe wake waliondoka nchini kurejea Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akishuka kutoka katika ndege alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini. |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akishuka kutoka katika ndege akipokea shada la Maua kutoka kwa Mtoto Tracy-Chantelle Mmbando alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto na Mke wake Mama Rachel Ruto wakizungumza na watoto Joseph Mmbando na Tracy-Chantelle Mmbando baada ya kupokea maua walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini |
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na mmoja wa maafisa waliofika ukatika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kumpokea alipowasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu |
Rais wa Jamhuri ya
Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakielekea katika chumba cha mapumziko katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto (kulia) Mama Rachel Ruto (wa pili kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Alfred Mutua (wa kwanza kushoto) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchin. |
Rais
wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto amewasili nchini kwa
ziara ya kikazi ya Siku mbili. Mhe. Dkt. Ruto ambaye ameambatana na mke
wake Mama Rachel Ruto, amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wa jijini Dar es Salaam.
Baada
ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa
Dar es Salaam Mhe. Dkt. Ruto alikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima
yake na kuelekea hotelini kwa mapumziko.
Tarehe 10 Oktoba 2022
asubuhi, Mhe. Dkt. Ruto atawasili katika Ikulu ya Dar es salam ambapo
atpokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao
watakuwa na mazungumzo rasmi ambayo yatakayohusisha wajumbe wa pande
zote mbili.
Baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo rasmi
viongozi hao watazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na
walichojadili katika ziara hiyo na baadaye watahudhuria dhifa ya kitaifa
ambayo Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuandalia mgeni
wake Mhe. Dkt. Ruto.
baada ya kumalizika kwa Dhifa hiyo ya Kitaifa, Mhe. Dkt. Ruto na ujumbe wake wanatarajiwa kuondoka kurejea nchini Kenya.