Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zambia zinakutana jijini Lusaka, Zambia kujadili masuala ya ushirikiano yaliyokubaliwa baina ya nchi hizo mbili.
Majadiliano hayo yanafanyika katika ngazi ya Wataalam ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Kumi wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia unaofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 14 Oktoba 2022.
Mkutano wa Wataalam utafuatiwa na mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 12 Oktoba 2022 na kumalizika na mkutano ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 14 Oktoba 2022 jijini Lusaka Zambia.
Mkutano huu unajadili na kutathimini utekelezaji wa maazimio katika sekta mbalimbali za ushirikiano zilizokubaliwa katika mkutano wa tisa uliofanyika tarehe 25 hadi 26 Februari 2016 jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Maeneo ya ushirikiano ni pamoja na; Siasa, Ulinzi na Usalama, Mambo ya Nje, Uhamiaji, Fedha na Uchumi, Sheria, Nishati, Habari na Mawasiliano, Kilimo, Miundombinu, Uchukuzi na Usafirishaji, Elimu, Sayansi na Teknolojia, Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Utalii, Kilimo, Uvuvi, Mazingira na Maliaasili, Afya, Elimu, Vijana na Michezo na jinsia.
Mkutano huu unafanyika kufuatia maagizo ya Marais wa pande zote mbili wakati wa ziara ya kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Zambia nchini Tanzania, Mhe. Hakainde Hichilema mapema mwezi Agosti 2022.
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia majadiliano |
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Utawala na Fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia, Bw. Humphrey Shangarai na Afisa Ubalozi Bw. Sunday Iddi wakifuatilia majadiliano. |
Ujumbe wa Tanzania. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.