|
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Joseph Sokoine akizungumza katika kikao cha
makabidhiano ya Ofisi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na aliyekuwa Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.
Kushoto ni Mhe. Balozi Mbarouk, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
|
Aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula akizungumza katika
kikao cha makabidhiano ya Ofisi kati yake na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma
|
|
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza katika
kikao cha makabidhiano ya Ofisi kati yake na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kilichofanyika mtumba jijini Dodoma |
|
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Alex Mfungo akizungumza katika
kikao cha makabidhiano ya Ofisi kati ya Mhe. Dkt. Tax na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mulamula kilichofanyika Mtumba jijini Dodoma |
|
Aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula akikibidhi rasmi Ofisi kwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma |
|
Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar Bi Mariam Haji Mrisho akitoa neno la shukurani katika hafla ya Makabidhino ya Ofisi kwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma |
|
Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara wakifuatilia hafla ya Makabidhino ya Ofisi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mtangulizi wake Balozi Mulamula (hawapo pichani) iliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma |
|
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara wakifuatilia hafla ya Makabidhino
ya Ofisi kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mtangulizi
wake Balozi Mulamula (hawapo pichani) iliyofanyika katika Ofisi za
Wizara Mtumba jijini Dodoma |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mtangulizi
wake Balozi Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara baada ya kukamilika kwa hafla ya Makabidhino
ya Ofisi iliyofanyika katika Ofisi za
Wizara Mtumba jijini Dodoma |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na mtangulizi
wake Balozi Mulamula katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara baada ya kukamilika kwa hafla ya Makabidhino
ya Ofisi iliyofanyika katika Ofisi za
Wizara Mtumba jijini Dodoma |
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax
amewataka watumishi wa Wizara kuendelea kuchapa kazi kwa bidii, ufanisi na
kushirikiana ili kufikia matarajio ya serikali na wananchi kwa ujumla.
Dkt. Tax
ametoa rai hiyo leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma mara baada ya
kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.
Dkt. Tax
amesema watumishi wa Wizara wanatakiwa kuhakikisha wanatumia weledi na
kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu ya Wizara ili kuleta tija na ufanisi
wakati wote.
“Sisi ni
timu ya ushindi, tuendelee kuchapa kazi, nitashirikiana na watumishi wote wa
Wizara, kuhakikisha tunatekeleza majukumu yetu kwa viwango na kwa muda sahihi,
tuwe wabunifu na tujitahidi kufanya kazi kama timu ili kufikia matarajio ya
Serikali yetu na wananchi wote kwa ujumla,” alisema Dkt. Tax
Ameongeza
kuwa kazi ya kukuza uhusiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali, Jumuiya za
kikanda na kimataifa haiwezi kufanikiwa ikiwa watumishi hawatashirikiana na
kufanya kazi kwa pamoja kama timu huku wakizingatia weledi, uzalendo na ubunifu
kwa maslahi mapana ya taifa.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo, Balozi Liberata Mulamula amewashukuru Watumishi wa
Wizara kwa ushirikiano waliompatia alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao ulimuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa
ufanisi.
“Nimeacha
timu imara nawashukuru wote kwa ushirikiano mlionipatia na niwaombe muendelee
na moyo huohuo katika kufanikisha majukumu ya wizara,” alisema Balozi Mulamula.
Awali
akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Mbrouk Nassor Mbarouk amemshukuru Balozi Mulamula kwa
ushirikiano aliompatia katika kipindi chake na kumsihi aendelee kushirikiana
nao kwa kuzingatia hazina kubwa ya uzoefu na ujuzi alionao katika sekta ya
mambo ya nje.
Naye
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Joseph Sokoine alisema Wizara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi
na kumuahidi Dkt. Tax kuwa watumishi wako imara na wataendelea kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi zaidi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni na
hivyo kuleta tija kwa wizara na taifa kwa ujumla
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.