Wednesday, April 26, 2023

UHOLANZI YARIDHISHWA NA MAZINGIRA YA BIASHARA, DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA

Uholanzi imeoneshwa kuridhishwa na mazingira ya biashara na uwekezaji, demokrasia, haki za binadamu na utawala bora nchini.

Hayo yamebainishwa na Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Wiebe de Boer wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku maalum ya Mfalme wa Uholanzi iliyofanyika tarehe 25 Aprili 2023 Jijini Dar es Salaam.

Balozi Boer alisema mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji nchini wafanyabiashara wengi kutoka Uholanzi wamewekeza Tanzania. “Kadhalika tumefurahishwa na kuridhishwa na demokrasia nchini, haki za binadamu na utawala bora pamoja na kufunguliwa kwa majukwaa na mikutano ya kisiasa nchini,” Alisema Balozi Boer.

Mbali na kuwekeza katika biashara na uwekezaji pia wafanyabiashara wa Uholanzi wamewekeza pia katika sekta za utalii pamoja na kilimo.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) alieleza dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kuendeleza uhusiano wa karibu na ushirikiano uliopo kati ya pande zote mbili.

Dkt. Tax alisema kuwa Uholanzi imeendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwamo kilimo, mifugo, uvuvi, elimu, nishati, afya, miundombinu, mawasiliano, utalii, usafiri pamoja na mafuta na gesi.

“Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji nchini, (TIC) hadi kufikia mwezi Machi, 2023 Kampuni kadhaa za Uholanzi zimewekeza Tanzania kwa kiasi cha (USD milioni 1,079.78), na kutengeneza ajira zaidi ya 15,607 katika sekta za kilimo, ujenzi, nishati, maendeleo ya rasilimali watu, mafuta na gesi, mawasiliano, utalii na usafiri,” alisema Dkt. Tax

“Naomba kutumia fursa hii kuzialika Kampuni na wawekezaji kutoka Uholanzi kuwekeza katika fursa zilizopo na kuwekeza nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika miradi ya kimkakati na yenye maslahi mapana ya pande zote mbili,” alisema Dkt. Tax

“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imepata mafanikio makubwa katika kuweka mazingira rafiki na mazuri ya biashara kupitia mageuzi ya kiutawala na kisheria na uwekezaji mkubwa katika maendeleo ya miundombinu,” alisema Dkt. Tax 

Pamoja na mambo mengine Dkt. Tax aliongeza kuwa juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Sita zimewezesha kupungua kwa gharama za kufanya biashara nchini Tanzania na kuwezesha ufanisi na uundaji wa huduma rahisi, msingi wa kuchochea shughuli za kiuchumi, na hivyo kuongeza uwekezaji, na kuimarishwa kwa biashara nchini.

Baadhi ya washiriki walioshiriki katika hafla ya maadhimisho ya Siku maalum ya Mfalme wa Uholanzi iliyofanyika tarehe 25 Aprili 2023 Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya washiriki walioshiriki katika hafla ya maadhimisho ya Siku maalum ya Mfalme wa Uholanzi iliyofanyika tarehe 25 Aprili 2023 Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Uholanzi nchini, Mhe. Wiebe de Boer akizungumza na washiriki walioshiriki katika hafla ya kuadhimisha Siku maalum ya Mfalme wa Uholanzi iliyofanyika tarehe 25 Aprili 2023 Jijini Dar es Salaam

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akihutubia katika hafla ya kuadhimisha Siku maalum ya Mfalme wa Uholanzi iliyofanyika tarehe 25 Aprili 2023 Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akihutubia katika hafla ya kuadhimisha Siku maalum ya Mfalme wa Uholanzi iliyofanyika tarehe 25 Aprili 2023 Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Mhe. Manfredo Fanti katika hafla ya maadhimisho Siku maalum ya Mfalme wa Uholanzi iliyofanyika tarehe 25 Aprili 2023 Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar katika hafla ya maadhimisho ya Siku maalum ya Mfalme wa Uholanzi iliyofanyika tarehe 25 Aprili 2023 Jijini Dar es Salaam


TIMU YA KUVUTA KAMBA KWA UPANDE WA WANAWAKE YA NJE SPORTS YAKWAMA KUVUKA ROBO FAINALI

Timu ya wanawake ya kuvuta kamba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jana tarehe 25 Aprili 2023, imemenyana vikali na timu ya Wizara ya Uchukuzi kwenye mchezo wa kuvuta kamba katika hatua ya robo fainali uliofanyika mjini Morogoro, katika mashindano ya kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Mei Mosi yanayoendelea mjini humo.

Katika mtanange huo wa vuta nikuvute uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilipoteza mchezo huo dhidi ya Wizara ya Uchukuzi ambayo ilijinyakulia ushindi wa alama 2. Timu ya Wizara ya Uchukuzi ndiye bingwa mtetezi wa mchezo huo, ikishikilia rekodi ya kushinda kwa miaka 6 mfululizo.

Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imefanikiwa kufika katika hatua hiyo ya robo fainali baada ya kushinda michezo miwili katika ngazi ya makundi na 16 bora dhidi ya TAMISEMI na RAS Ruvuma. 

Akizungumzia mchezo huo mwalimu anayekinoa kikosi cha kuvuta kamba cha Wananawake cha Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Andrew Salia ameeleza kuwa licha ya kupungukiwa wachezaji wawili kwenye kikosi chake kwa sababu ya majeraha, bado kilikuwa imara kiasi cha kutoa upinzani mkali kwa bingwa huyo wa mara sita mfululizo.

Aidha Bw. Salia ametoa pongezi kwa kikosi chake kwa kufanikiwa kufuzu na kushiriki hatua ya robo fainali ya mashindano hayo yenye hamasa na ushindani mkubwa. Vilevile amehahidi kuwa ataendelea kukinoa kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo.
Timu ya wanawake ya kuvuta kamba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikijipanga kamkabili mpinzani wake timu ya Wizara ya Uchukuzi kwenye mchezo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro

Timu ya wanawake ya kuvuta kamba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikijitahidi kumshinda mpinzani wake Wizara ya Uchukuzi





Timu ya wanawake ya kuvuta kamba ya Wizara ya Uchukuzi ikiwa tayari kumkabili mpinzani wake Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye mchezo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro

Timu ya wanawake ya kuvuta kamba ya Wizara ya Uchukuzi ikionesha umahiri wake  katika mchezo huo dhidi ya mpinzani wake Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Tuesday, April 25, 2023

UJUMBE WA TANZANIA ULIVYOSHIRIKI MAANDALIZI YA MKUTANO MAALUM WA 48 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA EAC

Mkutano Maalum wa 48 wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki kwa ngazi ya Makatibu Wakuu umefanyika kwa njia ya mtandao tarehe 25 Aprili 2023 huku ujumbe wa Tanzania ukishiriki kutokea Dodoma.

 

Mkutano huo  ambao ulianza  kwa ngazi ya Wataalam tarehe 24 Aprili 2023 umejadili pamoja na mambo mengine Taarifa ya Mkutano wa Kamati ya Fedha na Utawala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mwezi Machi 2023 pamoja na  Taarifa ya Kamisheni ya Ukaguzi wa Fedha za Jumuiya kwa kipindi kilichoishia tarehe 30 Juni 2022.

 

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Mkatibu Wakuu umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi.

 

Vilevile, mkutano huo umehudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote Wanachama wa Jumuiya ambazo ni Burundi, Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na Sekretarieti ya Jumuiya hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 25 Aprili 2023 kuandaa Mkutano Maalum wa 48 wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki.
Mkutano ukiendelea
Balozi Mbumdi akiwa na Wajumbe wengine wa Tanzania kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mkutano ukiendelea

Wajumbe kutoka Tanzania katika Mkutano wa Makatibu Wakuu

Mkutano ukiendelea

Makatibu Wakuu kutoka Nchi wanachama wakishiriki Mkutano kwa njia ya mtandao

 

 

 


SERIKALI YAENDELEA KUWAREJESHA WATANZANIA KUTOKA SUDAN

 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Monday, April 24, 2023

CALL FOR APPLICATION: QUEEN'S COMMONWEALTH ESSAY COMPETITION 2023


 

NJE SPORTS HOI MBELE YA WAKUSANYA MAPATO


Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuingia dimbani kuwakabili wapinzani wao timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) kwa mara nyingine jana tarehe 23 Aprili 2023 ilishuka dimbani kucheza na timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika hatua ya timu 16 bora kwenye michuano ya kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) yanayoendelea mjini Morogoro 

Katika mtanange huo ulionza majira ya saa 10.30 jioni kwenye uwanja uliopo Solomon Mahlangu Kampas – Mazimbu, Nje Sports ambayo ilipewa nafasi kubwa ya ushindi kabla mchezo ilipoteza kwa goli 1-0 liliofungwa na mshambuliaji Erick Mwita katika dakika ya 20 ya kipindi cha kwanza, na kudumu hadi dakika ya mwisho wa mchezo. 

Katika hatua hiyo ya mashindano ya timu 16 bora ilihusisha timu ya TAMISEMI, Morogoro DC, Uchukuzi, Afya, Mahakama, TANROADS, HAZINA, Maliasili, TRA, Nje Sports, TANESCO, Kilimo, CRDB, Mambo ya Ndani, Wizara ya Ulinzi na TPDC.

Baada ya kufungwa katika mchezo huo Nje Sports imepoteza nafasi ya kuendelea kushiriki katika mashindano ya mpira wa miguu, hivyo wanamichezo wake wataendelea kushiriki katika mashindano ya michezo mingine ikiwemo kuvuta kamba, bao na drafti.

Mashindano hayo yanayohusisha michezo mbalimbali kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Dunia (Mei Mosi), itakayo adhimishwa kitaifa mjini Morogoro tarehe 1 Mei 2023.

Wachezaji wa Nje Sports na TRA wakiwania mpira katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja uliopo Solomon Mahlangu Kampas – Mazimbu.
                                           Mchezo ukiendelea
Safu ya ulinzi ya Nje Sports ikiwa imejipanga kuzima moja ya shambulizi lililofanywa na TRA 
Mshambuliaji wa Nje Sports akiwatoka walinzi wa TRA katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja uliopo Solomon Mahlangu Kampas – Mazimbu

Saturday, April 22, 2023

NJE SPORTS KUSONGA MBELE KWENYE MICHUANO YA MEI MOSI LICHA YA KUKUBALI KISASI CHA MAAFANDE

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) leo terehe 22 Aprili 2023, imeingia dimbani kucheza dhidi ya mpinzani wake timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa Sekondari ya Morogoro kuanzia majira ya saa 3.00 asubuhi.

Katika mchezo huo Nje Sports imepoteza kwa goli 1-0, lililofungwa katika dakika ya 37 ya kipindi cha pili (katika mashindano haya ya Mei Mosi mpira wa miguu unachezwa kwa dakika 60 badala 90 kama ilivyozoeleka) na kudumu hadi mwisho wa mchezo.

Hata hivyo licha ya kupoteza mchezo huo mbele ya Maafande, Nje Sports inasongo mbele kucheza hatua ya timu 16 bora ambazo zimefuzu katika hatua ya makundi baada ya kujikusanyia alama 7 katika kundi C, na kuwa miongozi mwa timu nne zilizofuzu katika kundi hilo. 

Kundi C lilijumuisha timu sita ambazo ni Wizara ya Ulinzi ambayo imejikusanyia alama 12 (kinala wa kundi), Wizara ya Fedha na Mipango –Hazina FC alama 10 (nafasi ya pili), Wizara ya Mambo ya Ndani alama 9 (nafasi ya tatu) Nje Sports alama 9 (nafasi ya nne) 21st Century alama 5 (nafasi ya 5) Ushirika alama 0 (nafasi ya 6)

Akizungumza muda mfupi baada ya mchezo huo Mwalimu wa Nje Sports Bw. Shaaban ameushukuru Uongozi wa Wizara kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa kikosi chake, ambao umewezesha kufunzu hatua ya 16 bora. Vilevile ametoa pongezi kwa wachezaji na uongozi wa timu kwa kufuzu hatua inayofuata katika mashindano hayo ya kuelekea Kilele cha Maadhimisho Mei Mosi yanaoyondelea mjini Morogoro.

Nje Sports inatarajiwa kushuka tena dimbani kucheza dhidi ya Mamlaka ya Pato Tanzania (TRA) siku ya Jumapili tarehe 23 Aprili 2023 saa 10.00 jioni. 
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuingia dimbani kuwakabili wapinzani wao Wizara ya Mambo ya Ndani 
Mechi ikiendelea
 Penati ikipigwa kuelekea lango Nje Sports. Penati hiyo haikufanikiwa kutengeneza goli baada ya kudakwa na kipa mahiri wa Nje FC.
Mlinzi mahiri wa Nje Sports Bw. Abbas Abdallah shuti lililoelekezwa langoni kwake.
Mchezaji wa Nje FC akiwatoka walinzi wa timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwenye mechi iliyochezwa katika uwanja wa Morogoro Sekondari.
Baadhi ya wachezaji wa Nje Sports wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mchezo wao dhidi ya Wizara ya Mambo ya Ndani

Friday, April 21, 2023

NJE SPORTS YA VUTWA SHATI MOROGORO

Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports) leo tarehe 21 Aprili 2023 imeshuka dimbani kucheza mchezo wake wa wanne dhidi ya timu ya Wizara ya Fedha na Mipango (Hazina FC) ambapo imepoteza kwa goli 1-0. 

Mchezo huo ulioanza majira ya saa 3.00 asubuhi katika uwanja wa Ujenzi uliopo mjini Morogoro, Nje Sports iliruhusu goli la mapema katika dakika ya 2’ ya kipindi cha kwanza cha mchezo ambapo lilidumu hadi mwishoni mwa mchezo. 

Baada ya kupoteza mchezo huo Nje Sports inasalia na alama zake 7 katika kundi C huku ikishika nafasi ya pili katika kindi hilo nyuma ya Ulinzi FC yenye alama 9.

Nje Sports kesho tarehe 22 Aprili 2023 inatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo wake wa tano (5) dhidi ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Michezo hii ni muendelezo wa mashindano yanayoendelea mjini Morogoro kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Mosi) yatakayo adhimishwa Kitaifa mjini humo tarehe 1 Mei 2023.

Katika hutua nyingine timu ya kuvuta kamba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeibuka na ushindi dhidi ya TAMISEMI katika mchezo uliochezwa saa 12.30 asuhuhi katika uwanja wa Jumhuri mjini Morogoro.

Wakati huohuo timu ya Wanawake inayoshiriki mashindano ya mpira wa pete ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki saa 1.00 asubuhi ilishuka dimbani kucheza dhidi ya mpinzani wake Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambapo imepoteza kwa magoli 47-5 kwenye mchezo iliochezwa Jamhuri mjini Morogoro.
Mshambuliaji machachari wa Nje Sports Bw. Mikidadi Magola akiwatoka walinzi wa Hazina FC katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Ujenzi mjini Morogoro
Timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla kuingia uwanjani kucheza dhidi ya Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Balozi James Bwana wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na baadhi wanamichezo wa Wizara alipowatembelea katika uwanja wa Ujenzi, mjini Morogoro kwa lengo la kuwahamashisha. 
Timu ya mpira wa pete ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (mawasiliano) zikiwa zimejipanga tayari kwa mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
Moja ya goli lililofungwa kwenye mchezo kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 
Moja ya goli lililofungwa kwenye mchezo kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 
Mchezo kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mawasiliano ukiendelea
Winga machachari wa Nje Sports akipiga shuti baada ya kuwatoka walinzi wa Hazina FC katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Ujenzi mjini Morogoro
Mechi kati ya Nje na Hazina FC ikiendelea katika uwanja wa Ujenzi mjini Morogoro
Wachezaji wa Nje FC wakipata nasaha za kocha Bw. Shaaban Maganga wakati wa mapunziko