Friday, May 26, 2023

WAZIRI TAX ASISITIZA UBORA WA KAZI KWA WATUMISHI WA WIZARA


Meza Kuu wakiwa katika hali ya furaha walipojumuika na Watumishi wa Wizara (hawapo pichani) kuimba wimbo wa mshikamano daima kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amewasisitiza watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa kujituma na kuzingatia ubora wa kazi wanapotekeleza majukumu yao.

Waziri Tax ameyasema hayo alipokuwa akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma tarehe 26 Mei, 2023.

Pia akawaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa wanawajibu wa kuelewa kwa ufasaha bajeti na mipango iliyowekwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 ili kujipanga kutekeleza vipaumbele vya Wizara kikamilifu.

‘’Pamoja na kuielewa mipango ni jukumu lenu pia kupendekeza mipango na mikakati mizuri zaidi katika kutekeleza vipaumbele vya Wizara katika utekelezaji wa majukumu hususan, kufanikisha utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi na uwekezaji,” alisema Dkt. Tax.

Kwa upande wa Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Samwel Shelukindo katika hotuba yake ya ufunguzi ameeleza kuwa baraza la wafanyakazi ni takwa la kisheria na pia linaleta fursa ya ushirikishwaji kwa watumishi hasa katika mipango ya uendeshaji wa Wizara na hivyo huchangia ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

"Hivyo, ni matumani yangu kuwa wajumbe wa mkutano huu mtatoa michango yenye tija ambayo itaboresha Rasimu ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kabla ya kusomwa Bungeni” alisema Balozi Shelukindo.


Naye Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa, Bw. Samuel Nyungwa akizungumza, ameushukuru uongozi wa Wizara kwa kuendelea kuthamini umuhimu na tija ya baraza hilo pamoja na kutoa nafasi ya ushirikishwaji wa mipango ya Wizara kwa watumishi.

Lengo la Mkutano wa Baraza la wafanyakazi ni kupitia taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/2023, na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2023/2024, bajeti ambayo inatarajiwa kuwasilishwa Bungeni tarehe 30 Mei 2023. 

Mkutano huu ulihudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samweli Shelukindo akitoa neno la utangulizi kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.
Meza Kuu wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wakifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma
Meza Kuu wakishirikiana na Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) kuimba wimbo wa mshikamano daima
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bi. Chiku Kiguhe akifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (katikati) akiwasili katika ukumbi wa St. Gapar kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa, Bw. Samuel Nyungwa akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga akifuatilia Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma.

SERIKALI YA TANZANIA YAPEWA TUZO NA DRC

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kupitia kwa Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama, Mhe  Peter Kazadi ameikabidhi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tuzo ya Heshima (Gardons notre amitiĆ©) - inayohusu KUDUMISHA UHUSIANO baina ya Nchi hizo mbili .Tuzo hiyo imepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini DRC, Mhe. Said J Mshana wakati wa Sherehe za Miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyoandaliwa kwa ajili ya Mawaziri wa SADC waliohudhuria Mkutano kuhusu Udhibiti wa Maafa.

Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe Said J Mshana akiongea jambo baada ya kukabidhiwa Tuzo na Serikali ya DRC

Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe Said J Mshana alimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge na Uratibu katika kikao cha Mawaziri wa SADC kilichohusu udhibiti wa maafa kilichofanyika jijini Kinshasa.
Hadi kufikia tarehe 25 Mei 2023, Nchi Wanachama sita kati ya kumi na sita zilikuwa zimesaini Mkataba wa Uendeshaji wa Kituo cha Operesheni na Huduma za Kibinadamu cha SADC.
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe Said J Mshana katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano wa Mawaziri wa SADC uliohusu udhibiti wa maafa uliofanyika jijini Kinshasa






DKT. TAX ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UMOJA WA AFRIKA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023
Balozi wa Visiwa  vya Comoro na Mkuu wa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (katikati) na Balozi wa Visiwa  vya Comoro na Mkuu wa Mabalozi wa Nchi za Afrika nchini (kushoto) wakiimba wimbo wa Afrika wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelikindo (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Afrika Bi Ellen Maduhu waliposhiriki hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023
Baadhi ya washiriki wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023
Bw. Ahmed Salim Ahmed Salim, Mtoto wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika (OAU -(1989-2001) Mhe. Balozi Dkt. Salim Ahmed Salim ) akiangalia tuzo maalum ya Baba yake kabla ya kukabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (katikati) na Balozi wa Visiwa  vya Comoro na Mkuu wa Mabalozi wa nchi za Afrika nchini (wa pili kulia) iliyotolewa na Mabalozi wa Nchi za Afrika walioko nchini wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Nchi za Afrika walioko nchini wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) (katikati) katika picha ya pamoja na wenza wa Mabalozi wa Nchi za Afrika walioko nchini wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023

 

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) ameshiriki maadhimisho ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika. Maadhimisho hayo ya miaka 60 ya Umoja wa Afrika yalifanyika jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2023 na kuhudhuriwa na Jumuiya ya Mabalozi wa nchi za Afrika na Taasisi za Kimataifa za Afrika zilizoko nchini.

 

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mhe. Dkt. Tax alitoa rai  kwa nchi za Afrika kuungana ili kukua na kuwa na uchumi imara na kuongozwa na misingi na mawazo ya kuunganisha waafrika na hivyo kudumisha amani na usalama na kupata maendeleo ambayo yatatokana na utambulisho wake , urithi wa pamoja, maadili ya pamoja, mitazamo na ubunifu wa watu wake.

 

“Afrika lazima ijengwe kwa kuungana ili ishamiri, iwe na uchumi imara na kuongozwa na misingi ya kuunganisha waafrika ili kulinda amani na usalama ambayo maendeleo yake yanatokana na utambulisho wake yenyewe, urithi wa pamoja, maadili ya pamoja, mitazamo na ubunifu wa watu wake,” alisema Mhe. Waziri.

 

Dkt. Tax pia amezisihi nchi za Afrka kutumia vizuri fursa za kiuchumi zilizopo ili  kwa kuchochea ufanyaji biashara miongoni mwao na kufikia azma ya utekelezaji wa malengo ya Agenda 2063.

 

Amesema Afrika ni bara la pili kwa ukubwa likiwa na watu zaidi ya bilioni 1.2 na hivyo kuwa na fursa mbalimbali ambazo zikitumiwa vizuri zitawezesha waafrika kufikia azma ya utekelezaji wa Agenda 2063.

 

“Bara la Afrika ni la pili kwa ukubwa duniani likiwa na watu zaidi ya bilioni 1.2, tuna fursa nyingi, naomba nichukue fursa hii nisisitize katika kutumia fursa hizo zikiwemo za biashara, naamini kuwa  kama sisi wote tutafanya biashara miongoni mwetu tutafanikiwa kutekeleza malengo tuliyojiwekea katika agenda 2063,” alisisitiza.

 

Alisema wakati Afrika inaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake ni muhimu ikaangalia kauli mbiu ya mwaka huu isemayo “Uharakishaji na Utekelezaji wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika” na kuongeza kuwa Umoja wa Afrika umechukua hatua kwa kushirikiana na taasisi zake na zile za kikanda kuharakisha utekelezaji wa Soko hilo unafanyika kwa manufaa ya waafrika.

 

Amesema Soko la Eneo Huru la Bara Afrika (AfCFTA) ni chombo muhimu katika kukuza na kuchochea ufanyaji wa biashara miongoni mwa waafrika na hivyo kukuza maeneo mbalimbali ya uchumi ikiwa ni moja ya mafanikio ya muingiliano wa kiuchumi na maendeleo kwa watu wake

 

Amesema wakati wananchi wa Afrika wanaangalia fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo ni wakati muafaka pia kuangalia changamoto zinazolikabili bara la Afrika ambazo zinazuia kushamiri kwa bara hilo.

 

Ametaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni mabadiliko ya serikali yasiyofuata demokrasia, migogoro ya kivita, mabadiliko ya hali ya hewa, umasikini na ukosefu wa ajira  na kuongeza kuwa viongozi wa Afrika lazima waunganishe jitihada zao na kuja na mikakati ya pamoja kama njia za kutatua changamoto hizo.

 

Awali akizungumza katika Maadhimisho hayo Kiongozi wa Mabalozi wa na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini na  Mhe. El Badaoui Mohamed Fakih alisema Bara la Afrika linajivunia mafanikio makubwa ambayo limeyapata katika  siku za hivi karibuni.

 

Amesema mafanikio hayo yanatokana na kujipanga na kuanzishwa kwa mifumo wa utendaji kazi katika Umoja wa Afrika ambayo inashughulikia changamoto mbalimbali zitokanazo na matatizo yanayoikumba dunia na kutafuta njia za kukabiliana na matatizo hayo kwa pamoja.

 

Mhe. Balozi El Badaoui alipongeza kitendo cha Serikali kushirikiana na Jumuiya ya Mabalozi wa Afrika waliopo nchini katika kuadhimisha Siku ya Afrika ambayo imefikisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika mwaka 1963.

 

Katika hafla hiyo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Afrika (1989-2001) Mhe. Balozi Dkt. Salim Ahmed Salim alitunukiwa tuzo maalum na Umoja wa Mabalozi wa Afrika nchini ambayo ilipokelewa na mtoto wa Dkt. Salim Bw. Ahmed Salim Ahmed kwa niaba ya baba yake.

 

Hafla hiyo ya maadhimisho ya miaka 60 ya Siku ya Afrika iliandaliawa kwa pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Jumuiya ya Mabalozi wa Afrika waliopo nchini

 

 

 















Tuesday, May 23, 2023

DKT. TAX ATETA NA MABALOZI WA ITALIA NA UMOJA WA ULAYA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) nchini, Mhe. Manfredo Fanti katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. 

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika sekta mbalimbali hususan za elimu, afya, utalii, nishati, mitindo, utamaduni, uchumi wa buluu, mifugo na uvuvi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) nchini, Mhe. Manfredo Fanti pamoja na Balozi wa  Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) nchini, Mhe. Manfredo Fanti katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) nchini, Mhe. Manfredo Fanti katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Marco Lombardi pamoja na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) nchini, Mhe. Manfredo Fanti katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam




Monday, May 22, 2023

TAARIFA KWA DIASPORA WENYE ASILI YA TANZANIA


 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Mhe. Dkt. Stergomena L. Tax (Mb) amezindua rasmi Mfumo wa Kuwasajili Kidigitali Diaspora wote wenye asili ya Tanzania pamoja na wanafunzi wa kitanzania wanaosoma ughaibuni. Usajili huo utaiwezesha Serikali kuwa na kanzidata inayoonesha idadi yao, mahali walipo au ujuzi walionao.

SERIKALI YAZINDUA RASMI MFUMO WA KIDIGITALI KUSAJILI DIASPORA WENYE ASILI YA TANZANIA

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Mashariki, Mhe. Dkt Stergomena Tax (Mb.) akihutubia katika hafla ya uzinduzi rasmi wa mfumo wa kuwasajili Diaspora wenye asili ya Tanzania Kidigitali (Diaspora Digital Hub) Jijini Dar es Salaam  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Mashariki, Mhe. Dkt Stergomena Tax akizinduzi rasmi mfumo wa kuwasajili Diaspora wenye asili ya Tanzania Kidigitali (Diaspora Digital Hub) Jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela (kulia), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Dkt.Anna Makakala (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge – Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa (Mb).  
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akiwasilisha salamu za Wizara kwa Diaspora kabla ya uzinduzi rasmi wa DDH
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela akielezea faida za mfgumo wa kuwasajili Diaspora wenye asili ya Tanzania Kidigitali (Diaspora Digital Hub)
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba akieleza faida za Wanadiaspora kuchangia katika mifuko ya hifadhi ya jamii
Mwakilishi wa Mkuregenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Philbert Mponzi akiwaeleza washiriki fursa ambazo Diaspora watazipata kupitia Benki ya NMB watakapo jiunga na mfumo wa DDH 















KUKUA KWA KISWAHILI DUNIANI NI FURSA KWA TANZANIA

Wizara imelieleza Bunge kuwa imekuwa ikizitumia Ofisi za Balozi zilizoenea duniani kukuza Kiswahili na kuchangia ongezeko la fursa za ajira kwa Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni leo tarehe 22 Aprili 2023 wakati wa kujibu swali la Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, Mhe.  Ameir Abdallah Ameir aliyetaka kujua namna Balozi zinavyotumia fursa ya kukua kwa Kiswahili duniani kutafuta ajira kwa Watanzania.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geofrey Pinda kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alisema kuwa Ofisi za Balozi zimeanzisha programu za kufundisha, kutafsiri na kufanya ukalimani wa Kiswahili duniani, hatua ambayo inatoa ajira kwa watanzania. Jumla ya balozi 13 zimeanzisha madarasa, vituo na club za Kiswahili. Kupitia programu hizo, zaidi ya watanzania 95 wamepata ajira katika maeneo hayo.

Vilevile, vyuo na vituo binafsi zaidi ya 150 vinafundisha Kiswahili duniani. Kwa sasa, Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) limepewa kazi ya kufundisha walimu kumi (10) wa Diaspora katika Ubalozi wetu wa Abu Dhabi ambao ulihitaji walimu wa kwenda kufundisha Kiswahili katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mhe. Naibu Waziri aliendelea kueleza kuwa Ofisi za Balozi zipo katika mazungumzo na vyuo vikuu kwenye maeneo yao ya uwakilishi ili Lugha ya Kiswahili iweze kujumuishwa katika mitaala ya vyuo hivyo ikiwa ni pamoja na kupata wahadhiri wa Kiswahili kutoka Tanzania.  Vyuo hivyo ni pamoja na Chuo Kikuu cha Kuwait, Chuo Kikuu cha Holon Institute of Technology nchini Israel na Chuo Kikuu cha Buraimi nchini Oman.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Geofrey Pinda akijibu Swali Bungeni kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuhusu Lugha ya Kiswahili inavyotoa fursa za ajira kwa Watanzania.



 

Saturday, May 20, 2023

ZAMANA: KUTOKA IRENTE HADI KASRI LA BUCKINGHAM


Bi. Zamana (kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro wakiwa na tuzo iliyotolewa na Mfalme Charles III
Bi. Zamana (wa kwanza kushoto) katika picha ya pamoja na Mfalme Charles III (wa kwanza kulia) wakati wa hafla ya kuwapongeza waliopata tuzo iliyoandaliwa na Mfalme huyo

Bi. Zamana (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro (wa pili kushoto) na maafisa wengine wa Ubalozi huo



Friday, May 19, 2023

DKT SAMIA AZINDUA MAANDALIZI YA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI AFRIKA KUHUSU RASILIMALI WATU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali watu (Africa Heads of State Human Capital Summit) utakaofanyika nchini tarehe 25 - 26 Julai, 2023. 

Mhe. Dkt. Samia ametoa wito kwa viongozi wa Afrika kuendelea kuchukua hatua kwa kuwekeza kwa watu na kutoa kipaumbele kwa vijana na wanawake.

Mhe. Rais pia amewataka viongozi wa Afrika kuchukua hatua zaidi ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili watu wengi kwa kuwekeza zaidi katika kuboresha afya za watu, maji safi na salama, elimu bora na ujuzi muhimu kwa maendeleo ya rasilimali watu.

“Viongozi wa Afrika lazima tuendelee kuchukua hatua kwa kuwekeza kwa watu na kutoa kipaumbele kwa vijana na wanawake. Nitoe wito kwa viongozi wa Afrika kuchukua hatua zaidi ili kukabiliana na changamoto zinazokabili rasilimali watu kwa kuwekeza zaidi katika kuboresha afya za watu, kuwaletea maji safi na salama, kutoa elimu bora na ujuzi muhimu kwa maendeleo ya rasilimali watu,” alisema Mhe. Samia 

Rais Samia amesema taarifa za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa nchi nyingi za Afrika ukitoa za Afrika Kaskazini zinakabiliwa na changamoto katika utekelezaji wa malengo ya milenia ya uendelezaji rasilimali watu hali ikiwa chini ya wastani hasa katika maeneo ya elimu, afya na ulinzi wa jamii. 

“Hali ya afya ya uzazi, uwepo wa maji safi na salama na usimamizi wa maji taka bado ni changamoto kwa nchi nyingi huku ujumuishi wa kijinsia ukiwa na kasi ndogo na utekelezaji wa sheria za kulinda wanawake na watoto wa kike dhidi ya ubaguzi, unyanyasaji wa kijinsia, ndoa za utotoni na ukeketaji ukiwa mdogo na kuongeza kuwa kuwa hali ya ukamilishaji wa malengo ya milenia namba , 4, 5, 6 na 8 kwa nchi za Afrika hairidhishi na inaonesha hatari ya kutokamilika kwa malengo hayo kufikia mwaka 2030,” alisema Dkt. Samia.

Akizungumza katika uzinduzi wa Mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax (Mb.) alisema kuwa kufanyika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Rasilimali Watu mwezi Julai 2023, kunatokana na jitihada za Serikali kuboresha ushirikiano na kuzingatia umuhimu wa rasilimali watu katika kukuza uchumi na umuhimu wa kuwekeza kwa watu.

 “Kufanyika kwa mkutano huo hapa nchini, kunatokana na jitihada za serikali katika kuboresha ushirikiano na kuzingatia umuhimu wa rasilimali watu katika kukuza uchumi wa na kuona umuhimu wa kuwekeza kwa watu,” 

Alisema kufanyika kwa mkutano huo kutatoa fursa kwa wakuu wa nchi kubadilishana ujuzi na uzoefu kuhusu rasilimali watu na kutoka na maazimio madhubuti kuhusu cha kufanya kuendeleza rasilimali watu.

Dkt. Tax aliongeza kuwa Azma ya agenda 2063 inalenga kuzibadilisha nchi za Afrika na kuwa na nguvu za kiuchumi lakini azma hiyo inahitaji uwekezaji wa makusudi katika ujuzi na uwezo ili kutumia fursa za kijamii na kiuchumi katika bara la Afrika.

Naye Waziri wa Fedha na Mipango  Dk. Mwigulu Nchemba (Mb.) alisema Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na vipaumbele vya Rais Dkt. Samia alivyoweka katika maeneo ya afya na  makundi mbalimbali ya vijana na wanawake.

Alisema mbali ya Rais kufanya mabadiliko mbali mbali yaliyofanyika nchini lakini pia tumeshuhudia uwekezaji mkubwa wa fedha ukielekezwa katika eneo la elimu ili watoto wengi zaidi wanufaike kwa kupata elimu.

Awali Mkurugenzi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Zambia na Zimbabwe, Bw. Nathan Belete alisema Bara la Afrika lina nguvu kazi kubwa ambapo zaidi ya asilimia 75 ya watu wake wanafanya kazi katika sekta rasmi na kwamba nchi za Afrika zinapaswa kuungana na kufanya kazi kwa pamoja ili kumaliza changamoto zinazokabili rasilimali watu.

“Bara la Afrika lina nguvu kazi kubwa, tunaona kuwa asilimia 75 ya watu katika bara hili wanafanya kazi katika sekta rasmi, hivyo Nchi  zinapaswa kuungana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuzimaliza changamoto zinazokabili rasilimali watu kwa urahisi katika ukanda huo,” alisema. 

Alisema nchi za Afrika lazima zifanyie kazi suala la unyanyasaji wa kijinsia kwa kuwekeza katika elimu, afya na kuwawezesha wananchi wake kupata maarifa, ujuzi na afya bora.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi, Mabalozi pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kabla ya kuzindua Mkutano wa Maandalizi kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali watu (Africa Heads of State Human Capital Summit), Jijini Dar es Salaam. Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu unatarajiwa kufanyika tarehe 25-26 Julai, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa Mkutano wa Maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali watu (Africa Heads of State Human Capital Summit), Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Viongozi, Mabalozi pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa wakifuatilia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa Mkutano wa Maandalizi kwa ajili ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali watu (Africa Heads of State Human Capital Summit), Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Balozi wa Canada nchini, Mhe. Kyle Nunas kabla ya uzinduzzi wa Mkutano wa Maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali watu (Africa Heads of State Human Capital Summit), Jijini Dar es Salaam