Monday, August 21, 2023

RAIS WA INDONESIA KUANZA ZIARA YA KIKAZI LEO NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo anatarajia kuanza ziara ya Kitaifa ya siku mbili nchini Tanzania kuanzia tarehe 21 hadi 22 Agosti 2023

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesema ziara hiyo ni matokeo ya kazi kubwa anayoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine.

 “Ziara ya Mheshimiwa Widodo itakuwa ni ziara ya pili kwa kiongozi wa taifa hilo kutembelea nchini. Ziara ya kwanza ilifanywa na Mheshimiwa Soeharto, Rais wa Pili wa Indonesia mwaka 1991, ikiwa ni miaka 32 iliyopita,” alisema Dkt. Tax. 

“Mheshimiwa Rais Widodo atawasili Leo tarehe 21 Agosti 2023 na atapokelewa rasmi na Mwenyeji wake, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 22 Agosti, 2023, Ikulu Jijini Dar es Salaam,” aliongeza Waziri Tax.

Waziri Tax ameongeza kuwa, baada ya mapokezi viongozi hao watakuwa na mazungumzo ya faragha na baadaye mazungumzo rasmi na kufuatiwa na hafla ya utiaji saini Hati za Makubaliano ya Ushirikiano kwenye sekta mbalimbali.

“Tanzania na Indonesia zina uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria. Uhusiano huo uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Indonesia Mheshimiwa Soekarno. Uhusiano wa kidiplomasia ulianza mwaka 1964, ambapo mwaka huohuo Indonesia ilifungua Ubalozi wake nchini na kuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa kufungua Ubalozi wake nchini miaka michache baada ya uhuru. Aidha, Tanzania ilifungua Ubalozi wake nchini Indonesia Agosti, 2022, na kuzinduliwa rasmi mwezi Juni 2023,” aliongeza Dkt. Tax 

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tax amesema kuwa Tanzania na Indonesia zimekuwa zikishirikiana katika sekta za Uwekezaji ambapo hadi kufikia mwaka 2023, Indonesia imewekeza nchini miradi ipatayo mitano (5) katika sekta za Kilimo, uzalishaji wa viwandani, ujenzi. 

Sekta nyingine za ushirikiano ni pamoja na kilimo ambapo mwaka 1996 Indonesia ilianzisha Kituo cha Mafunzo ya Kilimo kwa Wakulima Vijijini (Farmers’ Agriculture and Rural Training Centre-FARTC), kilichopo Mikindo mkoani Morogoro. Kituo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima. 

“Ziara hii inatarajiwa kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali kama itakavyoonekana katika Hati za Makubaliano zitakazosainiwa, na matokeo ya mazungumzo kati ya Viongozi wetu yatakayojikita katika diplomasia, biashara, kilimo, uvuvi, elimu, nishati, madini, uchumi wa buluu na uhamiaji,” alisema Dkt. Tax.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dk. Stergomena Tax akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo anayetarajia kuanza ziara ya Kitaifa ya siku mbili nchini Tanzania kuanzia tarehe 21 - 22 Agosti 2023

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dk. Stergomena Tax akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa Joko Widodo anayetarajia kuanza ziara ya Kitaifa ya siku mbili nchini Tanzania kuanzia tarehe 21 - 22 Agosti 2023. wwengine pichaani (kulia) ni Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Mhe. Balozi Macocha Tembele, (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Namibia, Mhe. Balozi Ceaser Waitara.







Sunday, August 20, 2023

BALOZI SHELUKINDO AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE YA INDONESIA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amekutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia Bw. Cecep Herawan katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Pamoja na Mambo mengine, mazungumzo ya viongozi hao yamejikita katika kujadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Indonesia katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, kilimo, afya, elimu na nishati.

Balozi Shelukindo amemhakikishia Katibu Mkuu huyo ushirikiano wa dhati katika kuendelea kuimarisha uhusiano wa muda mrefu na na Indonesia. Aidha,  amemueleza kwamba mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ni mazuri na salama na kuwasihi wawekezaji kutoka Indonesia kuchangamkia fursa zilizopo.

Naye, Bw. Herawan amepongeza uhusiano imara uliopo baina ya serikali hizi mbili (Tanzania na Indonesia) na kuongeza kuwa Indonesia itaendelea kushirikina na Tanzania katika sekta mbalimbali kwa maslahi ya nchi zote mbili.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Bw. Cecep Herawan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Bw. Cecep Herawan katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Bw. Cecep Herawan (aliyevaa miwani kushoto) akizungumza wakati wa kikao chake na mwenyeji wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo (katikati kulia) akimsikilza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Bw. Cecep Herawan wakati wa mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumza baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Bw. Cecep Herawan yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam




Thursday, August 17, 2023

BALOZI WA TANZANIA NCHINI UMOJA WA FALME ZA KIARABU(UAE) AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Lt. Jen. (Mst) Yacoub Hassan Mohamed akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Mohammed Bin Zayed Al Nahyan katika Ikulu ya nchi hiyo (Qasr Al Watan) iliyopo mjini Abu Dhabi.


==============================================

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Lt. Jen. (Mst) Yacoub Hassan Mohamed mapema wiki hii amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Mohammed Bin Zayed Al Nahyan katika Ikulu ya nchi hiyo (Qasr Al Watan) iliyopo mjini Abu Dhabi.

Viongozi hao pia walipata wasaa wa mazungumzo ambapo Mheshimiwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu alimhakikishia Mhe. Mohamed ushirikiano wa Serikali yake katika kutekeleza majukumu yake nchini UAE kwa manufaa ya pande zote mbili hususan kiuchumi.

Kwa upande wa Balozi Mohamed alimuahidi Mheshimiwa Rais kuwa atahakikisha Watanzania na Waemirati wananufaika na fursa za uchumi zilizopo pande zote mbili.

Tanzania na UAE zina fursa nyingi za kushirikiana kiuchumi hususan katika sekta za nishati ambayo UAE ni miongoni mwa nchi tajiri katika uzalishaji wa mafuta. Kadhalika Tanzania ina eneo kubwa la kilimo hivyo ina soko kubwa la bidhaa za Kilimo na Mifugo ambapo ushirikiano huo utawezesha uzalishaji wa kisasa na kuongeza thamani ya bidhaa.

Bidhaa zenye soko kubwa kwa Tanzania nchini UAE ni pamoja na mbogamboga, matunda, nyama, korosho, karafuu, chai, karanga, asali, samaki na kahawa. Hivyo Ubalozi unaendelea na jitihada za kuwashawishi wawekezaji wa UAE kuja kushirikiana na Watanzania kuwekeza kwenye sekta ambazo zitatoa ajira kwa Watanzania wengi na zenye soko kubwa UAE kwa manufaa ya pande zote mbili.

Pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu ubalozi huo pia unawakilisha nchi za Bahrain, Pakistan na Iran. 

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Lt. Jen. (Mst) Yacoub Hassan Mohamed akiteta na Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Mhe. Sheikh Mohammed Bin Zayed Al Nahyan katika Ikulu ya nchi hiyo (Qasr Al Watan) iliyopo mjini Abu Dhabi.

Picha ya pamoja.

 

Monday, August 14, 2023

SADC YAJADILI UMUHIMU WA RASILIMALI WATU NA FEDHA KATIKA MAENDELEO YA VIWANDA





Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stegomena Tax (Mb) akifuatilia hotuba za ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambao ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Luanda, Angola tarehe 17 Agosti 2023.

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa SADC aliyemaliza muda wake ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Antipas Nyamwisi akikabidhi uenyekiti wa baraza hilo kwa Waziri wa Uhusiano wa Nje wa Angola, Mhe. Téte António 

Waheshimiwa Mawaziri wa SADC wakiendelea na mkutano wao ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Luanda, Angola tarehe 17 Agosti 2023

Saturday, August 12, 2023

DKT. KIKWETE AHIMIZA AMANI KATIKA NCHI ZA SADC

 
Rais Mstaafu wa Awamu ya NNne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasilisha mada kuhusu Amani na Usalama kama msingi wa kufikia maendeleo ya kweli katika nchi za Kusini mwa Afrika. Mada hiyo iliwasilishwa kwenye Chuo cha Diplomasia cha Angola ikiwa ni moja ya matukio ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Luanda, Angola kuanzia tarehe 08 hadi 17 Agosti 2023. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Msumbiji, Mhe. Luisa Diogo (kulia) na Katibu Mtendaji wa Zamani wa SADC, Mhe. Tomaz Salomão 

Wahuriki wakisikiliza mada kuhusu Amani na Usalama kama msingi wa kufikia maendeleo ya kweli katika nchi za Kusini mwa Afrika iliyokuwa ikiwasilishwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya NNne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Chuo cha Diplomasia cha Angola ikiwa ni moja ya matukio ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Luanda, Angola kuanzia tarehe 08 hadi 17 Agosti 2023

Washiriki wakisikiliza mada

Rais Mstaafu wa Awamu ya NNne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (mwenye tai nyekundu) akiwa na ujumbe wa Tanzania ulioshiriki katika Mhadhara wa Umma ambao aliwasilisha mada kuhusu Amani na Usalama kama msingi wa kufikia maendeleo ya kweli katika nchi za Kusini mwa Afrika






Wednesday, August 9, 2023

DKT. TAX ATEMBELEA AICC ARUSHA AZUNGUMZA NA BODI NA WATUMISHI , NA KUZURU CHUMBA CHA ICTR

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea shada la maua alipowasili katika Ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) jijini Arusha

Watumishi wa AICC wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya AICC Balozi Ole Njolay na Mkurugenzi Mtendaji wa AICC wakimpokea Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipowasili katika Ofisi zao jijini Arusha kuwatembelea.

 Mkurugenzi Mtendaji wa AICC Bw. Emphraim Mafuru ( wa pili kulia) akitoa maelezo kwa  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipowasili katika Hospitali za AICC jijini Arusha


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax amembeba Mtoto wa kiume aliyezaliwa leo (tarehe 09 Agosti  2023)  katika Hospitali ya AICC alipotembelea hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Kituo cha AICC   jijini Arusha


 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisaini kitabu cha wageni  kwenye Chumba cha iliyokuwa Mahakama ya Kimatifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikiendesha shughuli zake katika jengo la AICC  jijini Arushaalipozuru chumba hicho



 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha AICC alipotembelea eneo ambalo kitajengwa Kituo kipya cha Mikutano cha Kimatifa cha Mlima Kilimanjari (MKICC) alipotembelea Ofisi AICC  jijini Arusha


Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya AICC Balozi Daniel Ole Njolay na Mkurugenzi Mtendaji wa AICC Bw. Ephraim Mafuru wakiwa na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax aliangalia kumbi mpya za mikutano zilizoongezwa katika Kituo hicho




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha AICC alipotembelea kituo hicho jijini Arusha


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na watumishi wa AICC jijini Arusha alipotembelea Ofisi za kituo hicho jijini Arusha

Watumishi wa AICC wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipozungumza nao katika ofisi zao jijini Arusha

Watumishi wa AICC wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipozungumza nao katika ofisi zao jijini Arusha

Watumishi wa AICC wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipozungumza nao katika ofisi zao jijini Arusha

mwakilishi wa Watumishi wa AICC Bi. Catherine Kilinda akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa AICC tayari kumkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax alipotembelea ofisi za AICC na kuzungumza nao katika ofisi zao jijini Arusha


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akionesha zawadi aliyopewa na watumishi wa AICC alipotembelea ofisi za AICC na kuzungumza na watumishi wa AICC katika ofisi zao jijini Arusha




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika picha ya pamoja na watumishi wa AICC alipotembelea ofisi za AICC jijini Arusha


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) atembelea ofisi za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kujionea utendaji kazi wa taasisi hiyo na kupanga kwa pamoja jinsi ya kutekeleza majukumu ya AICC kwa mwaka huu wa fedha na kuleta tija kwa Taifa.

 

Mhe Waziri katika ziara hiyo amezuru Chumba cha iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyokuwa ikiendesha shughuli zake katika jingo la AICC , hospitali ya AICC, eneo litakalojengwa Kituo kipya cha Mikutano cha Kimataifa cha Mlima Kilimanjaro (MKICC)  na kuzungumza na wajumbe wa bodi, menejimenti na watumishi wa AICC.

 

Akizungumza na watumishi hao Mhe. Dkt. Tax amewataka kuhakikisha huduma wanazotoa zinaendana na mahitaji ya wakati uliopo ili kuhimili ushindani wa soko la biashara ya utalii wa mikutano na kuiwezesha taasisi yao kupata mikutano mingi zaidi.

 

Mhe. Waziri pia amewapongeza watumishi hao kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuitangaza nchi pale wanapotokea kuandaa mikutano ya Kimataifa kama ilivyotokea kwa mkutano uliofanyika nchini hivi karibuni wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliojadili rasilimali watu.

Katika ziara hiyo Dkt. Tax aliambatana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa AICC walioongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Daniel Ole Njolay na Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Bw. Ephraim Mafuru. 

Mhe. Dkt. Tax amefanya ziara ya siku moja ya kutembelea AICC kwa ajili ya kujadiliana nao na kuona ni jinsi gani wanaendana na mikakatiitakyoiwezesha AICC kuendelea kuwa Kituo bora cha Mkitano katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Ziara hii ni ya kwanza kwa Mhe Waziri tangu ateuliwa kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mwezi Oktoba 2022

Kituo cha AICC ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Taasisi nyingine ni Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam (CFR) pamoja na Mpango wa Hiari wa Kujitathmini wa Afrika (APRM).

DKT. SHELUKINDO AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA VIETNAM

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Vietnam, nchini Mhe. Nguyen Nam Tien katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo maandalizi ya Mkutano wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika sekta za kipaumbele hususan utalii, kilimo, afya, TEHAMA, biashara na uwekezaji, uchumi wa buluu na maeneo mengine.

“Vietnam itaendelea kushirikiana na wafanyabiashara wa Tanzania katika kuhakikisha wanapata fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu wa kibiashara nchini Vietnam ili kukuza ushirikiano wa biashara na uwekezaji,” amesema Balozi Tien. 

Pamoja na mambo mengine, Balozi Tien amesifu uhusiano mzuri na wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Viet Nam. Pia, ameeleza kuwa Vietnam inafurahishwa na Uongozi imara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Shelukindo amesema kwamba Tanzania inajivunia kuwa na uhusiano imara na Vietnam uliodumu kwa zaidi ya miaka 60. 

Dkt. Shelukindo amezialika kampuni kutoka Vietnam kuja kuwekeza nchini katika miradi ya kimkakati kwa maslahi ya pande zote mbili. “Nawaalika wafanyabiashara na wewekezaji wa Vietnam kuja kuwekeza Tanzania kwa kuwa Serikali imeboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.” amesema Dkt. Shelukindo.

Dkt. Shelukindo ameongeza kuwa Vietnam imechangia vyema katika kukuza sekta ya mawasiliano kupitia Kampuni ya Halotel ambayo imetoa ajira kwa Watanzania. 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akisalimiana na Balozi wa Vietnam, nchini Mhe. Nguyen Nam Tien katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Balozi wa Vietnam, nchini Mhe. Nguyen Nam Tien akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akizungumza na Balozi wa Vietnam, nchini Mhe. Nguyen Nam Tien katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 







Tuesday, August 8, 2023

MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA SADC NGAZI YA WATAALAMU WAANZA NCHINI ANGOLA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Shaban (mwenye mtandio) akiwa na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ulioanza leo katika ngazi ya maafisa waandamizi jijini Luanda, Angola.
Mwenyekiti wa ngazi ya maafisa waandamizi aliyemaliza muda wake ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Kikanda wa DRC, Balozi Songhu Kayumba (kulia) akikabidhi uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya wa maafisa waandamizi kutoka Angola, Balozi Nazare Salvador ambaye ni Mkurugenzi wa Ofisi ya SADC nchini Angola katika Wizara ya Uhusiano wa Nje ya nchi hiyo.


Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ngazi ya maafisa waandamizi ukiendelea jijini Luanda, Angola.



Monday, August 7, 2023

WAZIRI TAX APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MWAKILISHI MKAZI WA UNICEF, AMUAGA MWAKILISHI MKAZI UNDP

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amepokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) nchini Tanzania, Bi. Elke Wisch katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Waziri Tax amemweleza Bi. Elke Wisch kuwa UNICEF imekuwa na mchango mkubwa kuiunga mkono Serikali kwa kukuza, kulinda na kutimiza haki za watoto. 

“UNICEF ni wadau wakubwa na wamekuwa wakishirikiana na Serikali katika maeneno mengi………..na madhumuni yake ni kulinda haki ya mtoto na katika hili ni wadau wetu katika sekta za afya na elimu pamoja kuangalia maendeleo ya watoto,” amesema Dkt. Tax.

Waziri Tax ameongeza kuwa UNICEF wamekuwa pia wakisaidia katika kuhakikisha vifo vya watoto wadogo nchini vinapungua na wamekuwa na msaada mkubwa katika hilo.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi UNICEF nchini, Bi. Elke Wisch amesema kuwa UNICEF itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha kuwa haki za watoto zinalindwa na kuimarishwa kuanzia katika ngazi ya jamii na Tanzania nzima kwa ujumla.

 “UNICEF tunaahidi kuendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa haki za watoto zinalindwa na kuimarishwa kuanzia katika ngazi ya jamii na Tanzania nzima kwa ujumla.” amesema Bi. Wisch

Aidha, Bi Wisch ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kufanikisha vizuri Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali watu (Africa Heads of States Human Capital Summit) ulifanyika mwezi Julai. Ambapo amesema mkutano huo ulikuwa njia sahihi ya kujadili misingi ya ushirikiano pamoja na masuala mbalilmbali ya Watoto na vijana ambao ndiyo rasimali za kukuza na kuendeleza maendelea ya nchi.

 Katika tukio jingine, Waziri Tax amemuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Bi. Christine Musisi baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini.

Bi. Musisi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akiifanya tangu alipoinga madarakani licha ya kuingia madarakani katika kipindi kigumu cha janga la Uviko 19.

“Nimekuwa na wakati mzuri kuona nchi ikikuwa, ikiwa na ustahimilivu hata katika kipindi cha janga la Uviko 19, nimeona pia maendeleo ya watu yakiwa imara kutokana na uongozi thabiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanalindwa,” alisema Bi. Musisi

Bi. Musisi ameongeza kuwa ilikuwa faraja kubwa kufanya kazi Tanzania kama mwakilishi mkazi wa UNDP ambapo alishirikiana vyema na Serikali katika kuhakikisha kuwa mpango wa maendeleo wa miaka mitano na malengo ya milenia yanatekelezwa na kutimia kama ilivyopangwa.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) nchini Tanzania, Bi. Elke Wisch katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Bi. Christine Musisi katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Bi Musisi amemuaga Dkt. Tax baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimkabidhi zawadi ya picha Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Bi. Christine Musisi katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaamb baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi nchini






Thursday, August 3, 2023

WAZIRI TAX AFANYA MAZUNGUMZO NA SPIKA WA BUNGE LA ALGERIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Mhe. Brahim Boughali alipomtembelea katika Ofisi za Bunge tarehe 2 Agosti 2023 jijini Algiers, Algeria.

Katika mazungumzo yao Waziri Tax alieleza kuwa uhusiano kati ya Tanzania  na Algeria ni wa kirafiki na kindugu tangu enzi za kupigania ukombozi wa bara la Afrika. 

Pia kupitia ziara yake ya kikazi nchini humo pamoja na kuhuishwa kwa maeneo ya ushirikiano katika Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Algeria ni wazi kwamba nchi zetu zimejidhatiti kupiga hatua za kimaendeleo katika ushirikiano uliopo.

 ‘’Kuhitimishwa kwa mkutano  wa JPC kwa mafanikio ni hatua muhimu katika kuendelea kuimarisha ushirikiano wetu kwenye sekta za kiuchumi kwa maslahi ya pande zote’’ alisema Dkt. Tax.

Naye Spika wa Bunge la Algeria, Mhe. Brahim Boughali ameeleza kuwa Serikali ya Algeria ipo tayari kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kibunge ili kwa pamoja tuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazoendelea duniani.

‘’ Ni vema Bunge la Tanzania na la Algeria tukajenga mfumo rasmi wa ushirikiano ili kuweka utaratibu rasmi wa kushirikishana katika masuala mbalimbali ya kitaifa, kikanda na dunia kwa ujumla,’’ alisema Mhe. Boughali.

Aidha, Mhe. Spika Boughali amemhakikishia Mhe. Waziri Tax kuwa kwenye Kikao cha Bunge la Algeria la mwezi Septemba, suala la ushirikiano na Tanzania litakuwa ni moja ya eneo la  Kipaumbele katika mijadala ya Bunge hilo.

===================================


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria, Mhe. Brahim Boughali alipomtembelea katika ofisi za Bunge jijini Algiers, Algeria tarehe 2 Agosti 2023

Mazungumzo yakiendelea.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax akiwasili katika Ofisi za Bunge la Algeria jijini Algiers.

Picha ya pamoja