Friday, December 8, 2023

NCHI WANACHAMA WA EAC ZAHIMIZWA KUWAUNGA MKONO WAJASIRIAMALI KUPUNGUZA CHANGAMOTO YA AJIRA

Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimehimizwa kuendelea kuunga mkono jitihada za kujikwamua kiuchumi zinazofanywa na wajasiriamali wadogo na wa kati ili kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana na wanawake na kukuza uchumi wa nchi hizo.

 

Rai hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Burundi, Mhe. Prosper Bazombaza leo tarehe 08 Desemba 2023 jijini Bujumbura, Burundi wakati akifungua rasmi Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini hapa kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023.

 

Amesema Nchi Wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaweza kujikwamua katika  changamoto ya ajira kwa vijana na wanawake kwa kuandaa mazingira yanawezesha makundi hayo kujiajiri ikiwa ni pamoja na kuendelea kuimarisha na kuboresha  Maonesho ya Wajasiriamali wadogo na wakati maarufu kama Nguvu Kazi/Jua Kali ili kuwa na tija zaidi kwa maslahi mapana ya wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

 Ameongeza kusema kuwa maonesho hayo  ambayo yalianza kufanyika mwaka 1999 pamoja na mambo mengine yanalenga kupunguza umaskini kwa kutengeneza ajira kwa vijana na wanawake pamoja na kukuza uchumi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati kutumia jukwaa hilo kukutana, kubadilishana uzoefu, kuuza bidhaa zao na kukuza ujuzi na teknolojia.

 

Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maoenesho hayo, Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha Wajasiriamali 259 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania kushiriki Maonesho hayo ambayo yamewawezesha kutambulika kimataifa na kupata soko kwa bidhaa na huduma mbalimbali walizo nazo.

 

Ameongeza kuwa, Serikali ya Tanzania itaendelea kuwawezesha Wajasiriamali wadogo kuendelea kushiriki katika fursa maonesho ya aina hiyo ili kuwa sehemu ya kuboresha mazingira yao ya biashara na kuongeza ajira.

 

“Nimezungumza na wajasiriamali wengi wa Tanzania waliopo hapa Burundi na wengi wao wamenieleza kuwa wamepata kazi ya kuuza bidhaa zao katika baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki ikiwemo kina mama kutoka Kigoma wanaotengeza Chaki wamepata zabuni ya kupeleka Chaki hizo nchini Congo na Uganda. Hivyo kupitia maonesho haya tunawaonesha Watanzania wenzetu kwamba fursa ni nyingi na wazichangamkie amesema Mhandisi Luhemeja.

 

Naye Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa amewapongeza na kuwashukuru Wajasiriamali walioshiriki maonesho hayo na kutoka wito kwa wajasiriamali wengine kuendelea  kushiriki maonesho hayo kwani ni fursa ya kuyafikia masoko na kupata uzoefu na kujifunza ubunifu kutoka kwa wajasiriamali wengine wanaoshiriki.

 

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na Biashara, Bi. Annette Mutaawe ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo kwenye ufunguzi wa maonesho hayo amesema kuwa Sekretarieti ya Jumuiya hiyo itaendelea kuboresha maonesho hayo ambapo wajasiriamali hao wanachangia kupunguza changamoto ya ajira kwa asilimia 65 na pato la kanda kwa asilimia 15.

 

Akizungumza kwa niaba ya Wajasiriamali hao, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati Afrika Mashariki,  Bw. Josephat Rweyemamu amezishukuru Serikali zinazounda Nchi Wanachama kwa kuwewawezesha kushiriki na kusisitiza umuhimu wa nchi  hizo  wanachama kufanyia kazi changamoto chache zilizopo ili kuboresha biashara miongoni mwa watu wake ikiwemo kuwa na sarafu moja ili kurahisisha biashara pamoja na kuendelea kukuza lugha ya Kiswahili kwa kukifanya kuwa lugha ya biashara.

 

Wakati wa ufunguzi huo, washiriki walishuhudia uzinduzi rasmi wa Mfumo wa Kielektroniki  wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Kutoa taarifa na kufuatilia uondoaji wa Vikwazo Visivyo vya Forodha ambao pamoja na mambo mengine unalenga kurahisisha ufanyaji biashara baina ya nchi wanachama hususan kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.

 

Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo yamebeba Kaulimbiu isemayo “Kuunganisha Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki kufanya biashara katika Eneo la Afrika Mashariki” yamehudhuriwa na zaidi ya wajasiriamali 1,000 kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Makamu wa Rais wa Burundi, Mhe. Prosper Bazombaza akitoa hotuba tarehe 08 Desemba 2023 wakati wa ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Bujumbura tarehe 08 Desemba 2023. Maonesho hayo ambayo yamewashirikisha wajasiriamali zaidi ya 1,000 kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanafanyika kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023.

Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali wadodgo na wa kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo yanayofanyika jijini Bujumbura, Burundi kuanzia tarehe 05 hadi 15 Desemba 2023
Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Byakanwa akishiriki  hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati yanayofanyika jijini Bujumbura
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania wakishiriki hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati yanayofanyika jijini Bujumbura

Makamu wa Rais wa Burundi, Mhe. Prosper Bazombaza  akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Tanzania mara baada ya kufungua rasmi Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika ijini Bujumbur. Wanaoshuhudia ni Mhandisi Luhemeja (kushoto) na Mhe. Balozi Byakanwa

Makamu wa Rais wa Burundi, Mhe. Prosper Bazombaza akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Mhandisi Luhemeja, Mhe. Balozi Byakanwa na wageni wengine walioshiriki ufunguzi rasmi wa Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mhe. Mhandisi Luhemeja akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati Afrika Mashariki,  Bw. Josephat Rweyemamu alipotembelea Banda la Tanzania

Mhe. Balozi Byakanwa akiteta jambo na Mhe. Mhandisi Luhemeja

Mhe. Mhandisi Luhemeja akizungumza na mmoja wa wajasiriamali kutoka Tanzania anayeshiriki Maonesho ya 23 ya Wajasiriamali wadogo na wa kati maarfu kama Nguvu Kazi/Jua Kali alipotembelea mabanda ya wajasiriamali hao jijini Bujumbura


Mhe. Mhandisi Luhemeja akiwa na Mhe. Balozi Byakanwa wakizungumza na mmoja wa wajasiriamali anayeshiriki Maonesho ya 23 ya ajasiriamali wadogo na wa kati yanayoendelea jijini Bujumbura

Mhe. Balozi Byakanwa akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Maonesho la Mfuko wa Taifa wa Jamii (NSSF). Mfuko huo unashiriki ili kuhamasisha Diaspora wa Tanzania waliopo Burundi kujiunga na huduma mbalimbali zinazotolewa kwao na mfuko huo

Picha ya pamoja











 

WAZIRI MAKAMBA ATETA NA KATIBU MKUU AfCFTA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Secretarieti ya Soko Huru la Pamoja Barani Afrika (AfCFTA) Bw. Wamkele Mene walipokutana katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akizungumza na Katibu Mkuu wa Secretarieti ya Soko Huru la Pamoja Barani Afrika (AfCFTA) Bw. Wamkele Mene walipokutana katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Secretarieti ya Soko Huru la Pamoja Barani Afrika (AfCFTA) Bw. Wamkele Mene walipokutana katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam

Katibu Mkuu wa Secretarieti ya Soko Huru la Pamoja Barani Afrika (AfCFTA) Bw. Wamkele Mene akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba walipokutana katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akizungumza alipokutana na  Katibu Mkuu wa Secretarieti ya Soko Huru la Pamoja Barani Afrika (AfCFTA) Bw. Wamkele Mene walipokutana katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam

Katibu Mkuu wa Secretarieti ya Soko Huru la Pamoja Barani Afrika (AfCFTA) Bw. Wamkele Mene akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba walipokutana katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam



Katibu Mkuu wa Secretarieti ya Soko Huru la Pamoja Barani Afrika (AfCFTA) Bw. Wamkele Mene yupo nchini kuhudhuria Kongamano la Pili la AfCFTA la Wanawake katika Biashara lililofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 6-8 Disemba, 2023 na kukutanisha wanawake walioko katika biashara kutoka nchi mbalimbali barani Afrika .


Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili juu ya namna bora ya kuendesha biashara katika bara la Afrika kupitia soko hilo la AfCFTA.

 

Mhe. Waziri Makamba amemuhakikishia Bw. Wamkele Mene kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana na AfCFTA katika kuhakikisha soko hilo linaleta manufaa yaliyokusudiwa.




Thursday, December 7, 2023

MABALOZI WAPONGEZA JUHUDI ZA SERIKALI UOKOAJI HANANG, WAAHIDI MISAADA ZAIDI YA KIBINADAMU

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akizungumza katika kikao kati yake na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa Jijini Dar es Salaam alipokutana nao na kuwaelezea kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga hilo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akizungumza na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa (hawapo pichani) alipokutana nao Jijini Dar es Salaam na kuwaelezea kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga hilo

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) akiongoza Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa kusimama kwa dakika moja kwa ajili ya kuwaombea wananchi waliopoteza maisha kutokana na maafa yaliyotokea Hanang mkoani Manyara alipokutana nao Jijini Dar es Salaam na kuwaelezea kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga hilo



Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Zlatan Milišić akichangia jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa Jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Makamba aliwaelezea kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga hilo

 

Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa nchini wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba alipokutana nao Jijini Dar es Salaam kuwaelezea kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga hilo

 



Balozi wa Somalia nchini, Mhe. Zahra Ali Hassan akichangia jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa Jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Makamba aliwaelezea kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga hilo



Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa nchini wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokutana nao Jijini Dar es Salaam kuwaelezea kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga hilo

 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akizungumza na Balozi wa Italia nnchini Mhe. Marco Lombardi alipokutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa nchini Jijini Dar es Salaam kuwaelezea kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga hilo

 





Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi (katikati) wakizungumza na mmoja wa washiriki wa kikao kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa jijini Dar es Salam kuelezea yaliyotokea mkoani Manyara na jinsi Serikali ilivyokabiliana na janga hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Battle alipokutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa nchini Jijini Dar es Salaam kuwaelezea kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga hilo

 





NaibuWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Mhe. Isack Njenga wakati wa Kikao kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe. January Makamba na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa nchini Jijini Dar es Salaam kuwaelezea kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga hilo

 

Mkurugenzi wa Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga akizungumza kuwakaribisha Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika wa Kimataifa nchini Jijini Dar es Salaam kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Januari Makamba

 


 

 

Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini wamepongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali katika zoezi la uokoaji Hanang, kutokana na maporomoko ya tope kutoka katika mlima Hanang kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Mkoani Manyara tarehe 02 Disemba, 2023.

 

Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika hayo wametoa pongezi hizo Jijini Dar es Salaam walipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) aliyewaita kuwaelezea kilichotokea Hanang mkoani Manyara na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kukabiliana na janga hilo.

 

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Waziri Makamba amesema maporomoko hayo ya tope yamesababisha vifo vya watu 72, kujeruhi watu 117, kuharibu mali za watu, makazi na miundombinu ya barabara, maji na umeme.

 

“Serikali ya Tanzania inaishukuru Jumuiya ya Kimataifa nchini kwa jinsi ilivyoikimbilia na kusaidia wahanga wa maporomoko hayo hasa katika kusaidia urejeshaji wa huduma za muhimu za kibinadamu kwa wananchi wa Katesh” alisema.

 

Amesema katika kukabiliana na janga hilo, Serikali iliunda Kamati ya Kitaifa ya Maafa iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshirikiana na mamlaka ya Mkoa wa Manyara na kufungua akaunti Maalum ya maafa kwa ajili ya kuratibu na upokeaji misaada mbalimbali ili kusaidia wahanga wa maporomoko hayo na kuwezesha maisha ya watu kuendelea kama kawaida.

 

“Wahanga bado wanahitaji misaada ya kibinadamu ya hali na mali, wengi wamepoteza makazi yao na kupoteza wapendwa wao pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya barabara, maji na umeme na kusababisha maisha kusimama katika eneo hilo” alisema.

 

Amesema Serikali imeandaa maeneo maalum kwa ajili ya kuwahifadhi na kuwahudumia wahanga kwa kuwapatia huduma muhimu za kibinadamu, kuwatibu majeruhi, na kuwaokoa na kuwaondoa watu katika maeneo yaliyoathiriwa.

 

Amesema Serikali inaendelea na zoezi la kutafuta miili ya watu katika matope, kuhudumia shughuli za mazishi ya watu waliofariki na kuwafariji watu waliopoteza wapendwa wao kutokana na maporomoko hayo ili waweze kurejea katika hali zao za kawaida.

 

Naye Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Mhe. Zlatan Milisick amepongeza hatua za haraka zilizochukuliwa na Serikali katika zoezi la uokoaji wa wananchi na mali zao huko Hanang na kuongeza kuwa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali na kwamba Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini yameungana na kuchanga misaada ya yao ya kibinadamu kwa ajili ya kusaidia wahanga hao ambayo wataikabidhi kwa Serikali.

 

Balozi wa Kenya amesema Kenya kama nchi jirani iko pamoja na Watanzania katika sala na maombi kuwaombea marehemu na kutoa pole kwa familia za marehemu.

 

Akizungumza katika kikao hicho Balozi wa Somalia nchini Mhe. Zahra Ali Hassan amesema Umoja wa Mabalozi wa Afrika kwa umoja wao wameungana na kuwaingiza katika maombi wahanga wa maporomoko hayo na kuchanga misaada ya kibinadamu ambayo wataikabidhi kwa Serikali na kutoa pole kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wote kwa maafa hayo makubwa yaliyotokea nchini.

 

Balozi wa Msumbiji Mhe.  Ricardo Mtumbuida amesema Msumbiji inaungana na Tanzania na kutoa pole kwa Mhe. Rais, Watanzania na wahanga wote na kuwaombea marehemu wapumzike kwa amani.


 


BALOZI KIBESSE AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS RUTO

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dkt. Bernard Kibesse amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Ruto, katika hafla iliyofanyika Ikulu, Nairobi tarehe 7 Disemba 2023. 

Wakati akiwasilisha Hati zake za Utambulisho, Mhe. Balozi Kibesse alimshukuru Mhe. Rais Ruto kwa kuridhia uteuzi wake kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya na kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Kenya.

Kwa upande wa Mhe. Rais Ruto alimkaribisha Mhe. Balozi Kibesse na kueleza kwamba amekuwa na ushirikiano mzuri na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan katika masuala ya kitaifa na kimataifa. Amemtakia heri Balozi Kibesse na kueleza kwamba yupo tayari kushirikiana naye katika kufanikisha majukumu yake ya kuiwakilisha Tanzania nchini Kenya

Aidha, katika mazungumzo yao, viongozi hao wamekubaliana kuongeza juhudi katika kuboresha biashara kati ya Tanzania na Kenya zikiwa ni nchi majirani na rafiki zenye ushirikiano mkubwa wa kibiashara katika muktadha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dkt. Bernard Kibesse akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Ruto baada ya kuwasili Ikulu Jijini Nairobi, kuwasilisha Hati za Utambulisho


Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dkt. Bernard Kibesse akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Ruto Ikulu Jijini Nairobi

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Ruto katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Dkt. Bernard Kibesse pamoja na Mabalozi mbalimbali baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho Ikulu Jijini Nairobi



Wednesday, December 6, 2023

TANZANIA , UTURUKI KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA ELIMU

 


Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (kulia) akizungumza na Rais wa Taasisi ya Presidency For Turks Abroad and Related Communities ya Jamhuri ya Uturuki (YTB) Bw. Abdullah Eren (kushoto) walipokutana katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Taasisi ya Presidency For Turks Abroad and Related Communities ya Jamhuri ya Uturuki (YTB) Bw. Abdullah Eren (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (kulia)

Rais wa Taasisi ya Presidency For Turks Abroad and Related Communities ya Jamhuri ya Uturuki (YTB) Bw. Abdullah Eren (katikati) akizungumza na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (kulia) huku Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Dkt. Mehmet Gulluoglu (kushoto) akifuatilia mazungumzo hayo
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na Rais wa Taasisi ya Presidency For Turks Abroad and Related Communities ya Jamhuri ya Uturuki (YTB) Bw. Abdullah Eren (kushoto) walipokutana katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (katikati) katika picha ya pamoja na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Dkt. Mehmet Gulluoglu (kulia ) Rais wa Taasisi ya Presidency For Turks Abroad and Related Communities ya Jamhuri ya Uturuki (YTB) Bw. Abdullah Eren (kushoto) katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam

 

 

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana kwa mazungumzo na Rais wa Taasisi ya Presidency For Turks Abroad and Related Communities ya Jamhuri ya Uturuki (YTB) Bw. Abdullah Eren katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho, Balozi Mbarouk ameiahidi Taasisi hiyo kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Uturuki kuendelea kuimarisha uhusiano uliopo kwa manufaa ya pande zote mbili.

Amesema uhusiano kati ya Tanzania na Uturuki ni wa muda mrefu na unaoongoza hasa katika sekta za elimu, afya, biashara na uwekezaji na kuelezea matumaini yake kuwa uhusiano huo utaendelea kuimarika zaidi.

Naye Bw. Eren amesema YTB ni Taasisi ya Uturuki inayojihusisha na utoaji fedha za ufadhili katika ngazi ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa mataifa mengine na kusaidia juhudi za mtangamano za Diaspora wa Uturuki wanaoishi nje ya nchi hiyo.

Mazungumzo ya viongozi hao yamelenga kuimarisha uhusiano zaidi katika sekta ya elimu kati ya Tanzania na Uturuki na Mkutano huo umewezesha kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa pande mbili ikiwa ni pamoja na kuona jinsi ushirikishwaji wa diaspora unavyovyoweza kuchangia maendeleo ya kisiasa, kijamii na kiutamaduni katika nchi husika.
 

Monday, December 4, 2023

BALOZI SAID AFUNGUA SEMINA YA NGAZI YA JUU KUJADILI MAENDELEO BARANI AFRIKA


 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Mussa Shaib akizungumza wakati wa kufungua Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Mussa Shaib akizungumza wakati wa kufungua Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam.   

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Mhe. Milisick Milovan (kulia) akifuatilia ufunguzi wa Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Comoro nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ahamada El- Badaoui akipiga makofi kushangilia kitu wakati wa ufunguzi wa Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi na Mwakilishi wa Tanzania nchini Ethiopia na katika Umoja wa Afrika Addiss Ababa, Mhe. Innocent Shio akishiriki ufunguzi wa Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam.



Washiriki wa Tanzania katika  Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam wakifuatilia ufunguzi wa Semina hiyo.

Washiriki wa Semina ya siku tatu ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo inayofanyika jijini Dar es Salaam katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Semina hiyo.

 

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Said Mussa Shaib amefungua Semina ya Ngazi ya Juu kuhusu Afrika tunayoitaka inayojadili fursa na changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya maendeleo.

Akifungua semina hiyo Balozi Said amesema Tanzania imejidhatiti kutekeleza Ajenda 2063 na Ajenda 2030 kwakuwa imeziweka katika mipango ya maendeleo ya kitaifa na kufanya ajenda hizo kutekelezwa kwa vitendo kupitia mipango ya maendeleo.


“Bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo umasikini, ukosefu wa maendeleo, ajira, amani na usalama, kutokuwa na sauti moja katika majukwaa ya kimataifa, nchi za Afrika lazima ziendelee kupambana ili kuhakikisha Afrika inayotakiwa inafikiwa” alisema Balozi Said Mussa
Shaib.


Amesema Tanzania imepiga hatua katika kutekeleza malengo ya Ajenda ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2063 na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 na hivyo kuendelea kuimarika kwa kiwango cha ukuaji ambacho alisema kuwa kinatarajiwa kuendelea kukua kwa zaidi ya asilimia 5 kwa mwaka 2024 na kuendelea. 


Amesema Kiwango hicho cha ukuaji kimechochewa na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ya miundombinu na uwekezaji inayotekelezwa na Serikali katika sekta mbalimbali. Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, Barabara, Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere pamoja na urekebishaji wa miundombinu ya bandari na viwanja vya ndege nchini.


Amesema Tanzania imeendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na kutokomeza njaa nchini na kuongeza kuwa hatua kadhaa zimechukuliwa kuimarisha upatikanaji na usawa katika Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Ufundi (TVET) na elimu ya juu. 


Amesema Tanzania pia imefanikiwa kupunguza viwango vya vifo vya mama na watoto wachanga na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano huku ikiendelea kufurahia amani na utulivu kwa kuboresha demokrasia, utawala bora, haki za binadamu na kuzingatia utawala wa sheria.


“Mbali na mafanikio niliyoyaeleza, bado nchi wanachama zinakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza Ajenda ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2063 na Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 na hivyo taarifa za tathmini katika nchi mbalimbali zinaonyesha utendaji wa jumla uko katika kiwango cha wastani” alisema Balozi Mussa.


Ametaja baadhi ya sababu zinazochangia utekelezaji wa ajenda hizo kuwa wa kiwango cha wastani kuwa ni pamoja na utawala dhaifu, mifumo mibovu ya usimamizi na uratibu kati ya wahusika wa maendeleo wa ndani na nje katika ngazi ya nchi, pamoja na rasilimali zisizotosha. 


Ameishukuru Ofisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha utekelezaji wa Malengo ya Milenia yanaendelea kufanyiwa kazi na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Ofisi hiyo  ili  kufikia  malengo hayo kwa ukamilifu.

Semina hiyo imeandaliwa na Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi Barani Afrika (UNECA) inajadili utekelezaji wa Agenda 2063 na Agenda 2030 katika ngazi ya Nchi  na Mpango wa utekelezaji wa Miaka 10 wa Ajenda 2063 ambao utatoa ramani ya mabadiliko ya Bara la Afrika ndani ya muongo mmoja kama ulivyopitishwa na Mawaziri wa Umoja wa Afrika mwezi Oktoba 2023