Friday, December 5, 2014

Naibu Katibu Mkuu afungua Mkutano wa Kamati ya Ukaguzi ya Nchi za Maziwa Makuu

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Rajabu Gamaha akifungua Mkutano wa 6 wa Kamati ya Ukaguzi kwa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika katika Hoteli Harbour View, Jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kudhibiti uvunaji haramu wa maliasili ikiwemo madini ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa kichocheo cha vikundi vya uasi na migogoro katika Eneo la Maziwa Mkuu hususan katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Sehemu ya Wajumbe  wakimsikiliza Balozi Gamaha alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo. Wajumbe hao wanahusisha Maafisa kutoka nchi wananchi, Vyama vya Kiraia na Wafanyabiashara.
Wajumbe wengine wakiwemo Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mkurugenzi wa Idara ya Demokrasia na Utawala Bora katika Sekretarieti ya Maziwa Makuu, Balozi Ambeyi Ligabo akizungumza wakati wa mkutano wa 6 wa Kamati ya Ukaguzi ya Nchi Wanachama wa Maziwa Makuu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Peter Karasila nae akisema jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
Kaimu Mkuugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Innocent Shiyo akiwakaribisha Wajumbe kwenye mkutano
Mkutano ukiendelea
Balozi Gamaha (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Ukaguzi ya Nchi za Maziwa Makuu

................Matukio kabla ya mkutano

Balozi Gamaha akisalimiana na Balozi Ligabo alipofika Wizarani kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa 6 wa Kamati ya Ukaguzi ya Nchi za Maziwa Makuu.
Balozi Gamaha akizungumza na Balozi Ligabo alipofika Wizarani
Ujumbe uliofuatana na Balozi Ligabo walipofika Wizarani akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya Nchi za Maziwa Makuu, Bw. Peter Karasila (mwenye tai nyekundu)
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Innocent Shiyo (kushoto) akiwa na Maafisa Mambo ya Nje, Bi. Upendo Mwasha na Bw. Amos Tengu wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Gamaha na Balozi Ligabo (hawapo pichani).


Picha na Reginald Philip



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.