Monday, December 8, 2014

Waziri Membe azungumza na Mwakilishi wa EU nchini

Waziri wa Mambo wa Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Balozi Filberto Ceriani Sebregondi ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano pamoja na amani na usalama katika Ukanda wa Maziwa Makuu.
Balozi Sebregondi akimweleza jambo Mhe. Membe wakati wa mazungumzo yao.
Baadhi ya Mabalozi kutoka nchi za Umoja wa Ulaya waliopo hapa nchini wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Balozi Sebregondi (hawapo pichani). Kulia ni Balozi Diana Melrose wa Uingereza akifuatiwa na Balozi Malika  Berak wa Ufaransa.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo  ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine akiwa  na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (kulia)  pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Samira Diria (katikati) wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Balozi Sebregondi (hawapo pichani)
Katibu wa Waziri Membe, Bw. Thobias Makoba (kulia) na Maafisa Mambo ya Nje, Bw. Anthony Mtafya na Bi. Ngusekela Nyerere wakati wa mazungumzo hayo ya Waziri Membe na Balozi Sebregondi.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.