Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake cha Umoja wa Mataifa (UN Women) kwa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Izeduwa Derex-Briggs alipofika Wizarani tarehe 06 Aprili, 2017. Katika mazungumzo yao, Bi. Derex-Briggs alimweleza Mhe. Waziri maendeleo ya utendaji wa Kitengo hicho kwa Kanda na umuhimu wa uwepo wao hapa nchini. Pia alimtambulisha Bi. Hodan Addou, Afisa Msimamizi mpya wa Kitengo hicho hapa nchini. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.