Tuesday, April 24, 2012

Rais Kikwete ahudhuria mazishi ya Rais Bingu wa Mutharika nchini Malawi



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za rambirambi kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Malawi, Prof. Bingu wa Mutharika


 




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Malawi marehemu Prof. Bingu wa Mutharika, kijijini Ndata, wilayani Thyolo, nje ya jiji la Blantyre, nchini Malawi jana.  Pembeni yake ni Mhe. Waziri Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa aliyekuwa Rais wa Malawi, marehemu Bingu wa Mutharika, Bi. Calista Mutharika wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini Ndata, katika mji wa Blantyre, Malawi tarehe 23 Aprili, 2012.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionge na Rais wa Malawi, Bi. Joyce Banda, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Prof. Bingu wa Mutharika aliyefarika April 6 mwaka huu.  Mazishi hayo yalifanyika tarehe 23 Aprili, 2012 kijijini Ndata, wilayani Thyolo, katika mji wa Blantyre, Malawi.

Picha zote na:  FREDDY MARO, IKULU

Thursday, April 19, 2012

Relief food to Somalia to be shipped soon, says minister

About 3000 tonnes of relief food to hunger-stricken Horn of Africa will be dispatched on the designated place as soon as the South African ship under SADC flag docks at the Dar es Salaam Harbour.

Foreign Affairs and International Cooperation Minister Bernard Membe told the National Assembly in Dodoma yesterday that the vessel would deliver all consignments of relief food pledged by the members of the SOuthern African Development Cooperation.

"The ship is expected in Dar es Salaam anytime now," said the minister, attributing the delay in shipment to, insecurity off the Somalia Coast in the Indian Ocean.

He ruled out any further delay as security situation in the region had improved tremendeously of late.  He added that the government also pledged 200,000 US Dollars to the war and hunger ravaged Somalia.

The minister was reacting to Chambani Member of Parliament (CUF) Salim Hemed Khamis who had sought to know how the government was living up to the Africa Union's slogan "One Africa One Vote Against Hunger" adopted last year, requiring African countries to come to the rescue of the troubled region.

The AU had observed that food insecurity remained at emergency levels across parts of the Horn of Africa, with famine declared in two regions of Southern Somalia and humanitarian organizations struggled to cope with the influx of Somalia refugees in Ethiopia and Kenya.

Mr. Membe said the AU members during their special meeting in Addis Ababa, Ethiopia last August pledged 350m US Dollars for the cause.

He however, observed that as of February of this year, it emerged that some 1 bn US Dollars was needed to address the situation.

Quoting United Nations statistics, the minister said the disaster affected more than 12 million people, and deaths associated with famine reached an average of six people (five children and one adult) daily last year.

Source:  Daily News, Tanzania

Wednesday, April 18, 2012

Rais Kikwete akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tano nchini Brazil

   


Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia katika mkutano wa Open Government Partnership, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil tarehe 17 Aprili 2012.  


  
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu wa Georgie Mh Nika Gilauri katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil,baada ya kuhudhuria mkutano wa Open Government Partnership.  Wengine kwenye picha ni Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb) (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.



Ujumbe wa Tanzania ukibadilishana mawazo kabla ya ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil.  Kutoka kushoto ni Waziri katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. Mathias Chikawe, Waziri wa Kazi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi Juma Maalim na Mshauri wa Rais (Masuala ya Siasa) Dkt Laurian Ndumbaro.



Ujumbe wa Tanzania, akiwemo Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Mshauri Mkuu Mwandamizi wa Rais katika masuala ya kidiplomasia, wakiwa kwenye mkutano wa Open Government Partnership katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil. 



Wajumbe wa Tanzania, akiwemo Bi. Grace Shangali (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Europe na America kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, pamoja na Wajumbe wengine kutoka taasisi mbalimbali za kiraia na serikali wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil,wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership.


Picha zote na maelezo -   http://www.ikulublog.com/



Monday, April 16, 2012

Mhe. Membe aongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa CMAG mjini London




Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiongea jambo na Mhe. Surujrattan Rambachan (katikati), Waziri wa Mambo ya Nje wa Trinidad and Tobago ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Kikosi Kazi cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Ministerial Action Group - CMAG), na Mhe. Bob Carr, Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CMAG.  Mkutano huo ulifanyika katika Malborough House, mjini London tarehe 16 April, 2012.


Mhe. Membe, ambaye aliongoza Ujumbe wa Tanzania, akiwa katika Chumba cha Mkutano wa CMAG.  Wengineo katika picha ni wajumbe kutoka Tanzania, akiwemo Bi. Dora Msechu (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  Tanzania ni mojawapo ya nchi mwanachama wa CMAG, zikiwemo nchi za Australia, Bangladesh, Canada, Jamaica, Maldives, Sierra Leone, Trinidad and Tobago na Vanuatu.



Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Bob Carr, Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CMAG.

Saturday, April 14, 2012

President Kikwete sends a Condolence Message to the President of Algeria

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, the President of the United Republic of Tanzania sends a condolence message to H.E. Abdelaziz Bouteflika, the President of the People’s Democratic Republic of Algeria following the death of H.E Ahmed Ben Bella, First President of the People’s Democratic Republic of Algeria.  The message reads as follows:   

“H. E. Abdelaziz Bouteflika 
President of the People’s Democratic Republic of Algeria
ALGIERS

Your Excellency and Dear Brother,

I am deeply saddened by the sad news of the untimely death of the founding Father of your great Nation that took place on 11th April, 2012.

On behalf of the Government and People of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf, I wish to convey our deepest sympathies and condolences to Your Excellency and, through you, to the bereaved family and relatives as well as the Government and the entire brotherly People of Algeria for this untimely death.

Tanzania will always remember the late Ahmed Ben Bella for the important role he played in cementing the relations between our two countries that so happily exists to-date.

 He will also be remembered as a truly son of Africa who stood for unity and dignity of the African people. Africa has indeed lost one of the charismatic and revolutionary leaders who dedicated his life not only for the struggle for the independence of Algeria but also for the other African countries that were still suffering under colonialism.  He also contributed positively to the peace and stability of Africa in his capacity as the Chairperson of the Panel of the Wise of the African Union. 

At this difficult moment of agony and distress, we share your grief and pray to the Almighty God to give the bereaved family, relatives and all the people of Algeria strength and courage to endure the agony resulting from this great loss.  May the Almighty God rest the soul of the deceased in eternal peace. 

Please accept, Your Excellency and Dear Brother, the assurances of my highest consideration.

Jakaya Mrisho Kikwete
President of the United Republic of Tanzania



Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation

DAR ES SALAAM
14th April, 2012

Wednesday, April 11, 2012

UTEUZI WA MKUU WA CHUO NA MWENYEKITI WA TAASISI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA NELSON MANDELA‏



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kuwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo, Jumatano, Aprili 11, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imesema Rais Kikwete pia amemteua Profesa David Homeli Mwakyusa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha chuo hicho cha Nelson Mandela.
Taarifa imesema kuwa uteuzi wa Dkt. Bilal ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Profesa Mwakyusa aliyepata kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii katika Serikali ya Rais Kikwete ulianza Alhamisi iliyopita, Aprili 5, 2012.
Chuo cha Nelson Mandela ambacho kiko Arusha ni moja ya vyuo vikuu vinne vinavyolenga kuendeleza sayansi na teknolojia katika Bara la Afrika.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
11 Aprili, 2012

Sunday, April 8, 2012

Mhe. Membe mgeni rasmi Tamasha la Pasaka

View FOTO1.JPG in slide show

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akihutubia umati wa watu uliofika kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika hivi karibuni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Mhe. Waziri ni Mke wake Mama Dorcas Membe.


View FOTO2.JPG in slide show

Mhe. Membe (wa pili kutoka kushoto) akiwa na viongozi wa dini waliohudhuria Tamasha la Pasaka. Kutoka kushoto ni Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO Missions akifuatiwa na Mtume Fernandes wa Agape Missions na mwisho ni Mama Membe.
View FOTO3.JPG in slide show

Mhe. Waziri Membe akizindua albamu mpya ya nyimbo za injili iitwayo Kwa Utukufu wa Mungu ya mwimbaji wa nyimbo za injili Solomon Mukubwa kutoka Kenya wakati wa Tamasha la Pasaka.


View FOTO4.JPG in slide show

Mhe. Membe kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa na waimbaji wa nyimbo za injili waliohudhuria Tamasha la Pasaka.

View FOTO5.JPG in slide show

Mhe. Membe na Mkewe (kulia) wakiwa na Rebecca Malope mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za injili kutoka Afrika Kusini wakati wa Tamasha la Pasaka.


View FOTO6.JPG in slide show

Baadhi ya Wabunge na Balozi Liberata Mulamula kwenye Tamasha la Pasaka.

Saturday, April 7, 2012

Kumbukumbu za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda‏


View FOT01.JPG in slide show

Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa hotuba wakati wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 18 ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City.
 
View FOTO2.JPG in slide show

Mhe. Naibu Waziri akiwasha mshumaa kama ishara ya kuwakumbuka mamia ya watu waliouawa nchini Rwanda mwaka 1994.


View FOTO3.JPG in slide show

Mhe. Naibu Waziri (wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na wawakilishi mbalimbali wakati wa kumbukumbu hizo. Kutoka kushoto kwa Naibu Waziri ni Bw. Alexio Musindo, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini anayefuata ni Bw.Lambert Sano, Kaimu Balozi wa Rwanda hapa nchini na mwisho ni Bw. Roland Amoussouga, Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyopo Arusha.


Wizara yamuaga Balozi wa Ireland nchini


View FOTO1.JPG in slide show

Mhe. Balozi Liberatta Mulamula, Msaidizi Mwandamizi wa Rais katika Masuala Diplomasia akitoa hotuba kwa niaba ya Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana kilichoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga Mhe. Lorcan Fullam, Balozi wa Ireland aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Double Tree.


View FOTO2.JPG in slide show

Balozi  Mulamula akiwa pamoja na Mhe. Fullam wakati wa hafla ya kumuaga Balozi huyo.


View FOTO3.JPG in slide show 
  
Mhe. Lorcan Fullam, Balozi wa Ireland aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini akizungumza machache wakati wa hafla ya kumuaga.
 
 
View FOTO4.JPG in slide show
 
Balozi Fullam akifurahia zawadi ya Picha ya Wanyama aliyokabidhiwa na Balozi Mulamula kama kumbukumbu ya Tanzania atakapoondoka.
 
 
View FOTO5.JPG in slide show
 
Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walioshiriki hafla ya kumuaga Balozi Fullam


Rais Kikwete atuma salamu za rambirambi kwa Makamu wa Rais wa Malawi

 

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA SERIKALI YA MALAWI KUFUATIA KIFO CHA ALIYEKUWA RAIS WA NCHI HIYO HAYATI BINGU WA MUTHARIKA


Hayati Bingu wa Mutharika
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Makamu wa Rais wa Malawi, Mheshimiwa Joyce Banda kuomboleza kifo cha kiongozi wa nchi hiyo, Mheshimiwa Rais Bingu wa Mutharika.

Katika salamu zake hizo, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Banda kuwa Tanzania imepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Rais Bingu wa Mutharika ambaye Rais Kikwete amemwelezea kama kiongozi wa karibu na rafiki mkubwa wa Tanzania.

Amesema Rais Kikwete katika salamu hizo, “Sisi katika Tanzania tumepokea taarifa za kifo cha Rais Bingu wa Mutharika kwa mshtuko na majonzi. Alikuwa kiongozi na rafiki wa karibu wa Tanzania na rafiki yangu. Alikuwa kiongozi wa kutumainiwa miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Bara la Afrika lote.”

Ameongeza Rais Kikwete: “ Kwa hakika, Afrika imempoteza kiongozi imara, aliyeamini katika maslahi ya Bara letu na watu wake. Siku zote tutamkumbuka kwa dhamira yake na moyo wake katika kupigania umoja, amani, utulivu na ustawi wa mataifa yetu mawili na Afrika nzima.”

Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa niaba yangu mwenyewe, nakutumia wewe Mheshimiwa, familia ya marehemu na wananchi wote wa Malawi salamu za rambirambi za dhati ya mioyo yetu kufuatia kifo cha ghafla cha Mheshimiwa Rais Bingu wa Mutharika,” amesema Rais Kikwete katika salamu zake.

Mwisho.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

Tuesday, April 3, 2012

President Kikwete congratulates new President of the Republic of Senegal

Press Release

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E.  Macky SALL, President of the Republic of Senegal, following the swearing in to the office that took place on 2nd April, 2012.  The message reads as follows:

“His Excellency Macky Sally
President of the Republic of Senegal
DAKAR

Your Excellency and Dear Brother,

I have received with great pleasure the news of your swearing in as the new President of the Republic of Senegal, following your landslide victory during  the  second  run-off  Presidential  election  that  was  held  on 25th March, 2012.

On behalf of the Government and People of the United Republic of Tanzania, I would like therefore to extend to Your Excellency our profound and heartfelt congratulations for being sworn into office to assume the Presidency of your great country.  This is a clear testimony of the confidence reposed in you and your party by the people of the Republic of Senegal.  Also, it is a clear testimony of the maturity of democracy by the people of the Republic of Senegal and thus making Senegal to be hailed as one of Africa’s model democracies.

As you embark upon your new responsibilities of that high office, I look forward to working closely with you and the Government of the Republic of Senegal to further promote the bilateral relations that so-happily exist between our two countries, for the mutual benefit of our people.

I also look forward to working closely with you in the framework of the African Union and the United Nations in our common endeavour towards achieving economic and social prosperity not only for the people of our two countries but also for the people of the continent, as a whole.

While wishing you continued good health and success in your new responsibilities, please accept, Your Excellency and Dear Brother, the assurances of my highest consideration”.

  
ISSUED BY: MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES SALAAM

03RD APRIL, 2012
















Friday, March 30, 2012

Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje yakutana na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje


Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) walipokutana na uongozi wa Wizara chini ya Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara na Balozi Rajab Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara.  Kamati hiyo ilikutana na uongozi wa Wizara kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha kuanzia mwezi wa Januari hadi Machi mwaka huu 2012.



Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Machi 2012.  



Bw. John M. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akieleza changamoto na mafanikio mbalimbali ya Wizara katika kipindi cha miezi Januari had Machi 2012.  Pichani ni Mhe. Mahadhi Juma Maalim (kulia), Naibu Waziri wa Wizara na Balozi Rajab Gamaha (kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara.


Makaimu Wakurugenzi wa Idara na Vitengo wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara.


Makaimu Wakurugenzi wa Idara na Vitengo wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara.



Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Mhe. John Shibuda (Chadema-Maswa Magharibi) akichangia hoja.

Rais asikitishwa na kifo cha Balozi Lukindo



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe kufuatia taarifa za kifo cha Balozi Raphael Haji Lukindo kilichotokea tarehe 27 Machi, 2012 katika Hospitali ya Saisee iliyopo Mumbai nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Enzi za uhai wake, Balozi Lukindo alikuwa Mtumishi wa Umma aliyelitumikia Taifa letu katika nyadhifa mbalimbali kuanzia wadhifa wa Bwana Shauri yaani District Officer, na kwa muda mrefu amekuwa katika Balozi mbalimbali akiiwakilisha nchi yetu ambapo mara ya mwisho alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan kuanzia mwaka 1983 hadi 1988.

“Nimesikitishwa na kuhuzunishwa na kifo cha Balozi Raphael Haji Lukindo ambaye kwa hakika alikuwa Mtumishi wa Umma muadilifu na mchapakazi hodari tangu alipokuwa Bwana Shauri kati ya mwaka 1961 hadi 1962, alipokuwa Afisa katika Balozi zetu za Uingereza na Ujerumani, na hata alipoteuliwa kuwa Balozi akiiwakilisha nchi yetu katika nchi za uliokuwa Muungano wa nchi za Kisovieti za Urusi (USSR), Uingereza, Italia na hatimaye Balozi wa Tanzania nchini Japan kabla ya kustaafu”, amesema Rais Kikwete katika salamu zake.

Rais Kikwete amesema kutokana na utumishi wake uliotukuka, Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye, pamoja na kwamba alikuwa amekwisha kustaafu, lakini ushauri wake ulikuwa bado unahitajika sana hasa katika masuala ya kidiplomasia.  Kutokana na msiba huo, Rais Kikwete ametoa pole nyingi kwa familia ya Marehemu Balozi Lukindo kwa kupoteza kiongozi muhimu wa familia.

Amesema anamuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema ailaze mahala pema peponi roho ya Marehemu Balozi Lukindo na awape moyo wa uvumilivu na ujasiri wanafamilia, ndugu na jamaa wa Marehemu katika kipindi chote cha maombolezo.  Aidha Rais Kikwete amewahakikishia kuwa yupo pamoja nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa kwa kutambua kuwa yote ni mapenzi yake Mola.

Mwisho.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.


 

Wednesday, March 28, 2012

Deputy Minister Hon. Maalim attends Pakistan Independence Day Celebration


The High Commissioner of Pakistan to Tanzania, H.E. Ambassador Tajammul Altaf welcoming the guest of honor, Hon. Mahadhi Juma Maalim (MP), the Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, during the 72nd Independence Anniversary of Pakistan held recently in Dar es Salaam. 

The Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Hon. Mahadhi Juma Maalim (MP) (4th left) and other distinguished members of diplomatic community including the Dean of Diplomatic Corps and Ambassador of Democratic Republic of Congo to Tanzania, H.E. Ambassador Juma Khalfan Mpango (4th-right), standing in honor of the Pakistan National Anthem during the ceremonyHon. Maalim was attending the 72nd Independence Anniversary of Pakistan held recently in Dar es Salaam.

 
The Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Hon. Mahadhi Juma Maalim (MP) (center) proposing a toast together with the High Commissioner of Pakistan to Tanzania, H.E. Ambassador Tajammul Altaf (left) and the Dean of Diplomatic Corps and Ambassador of Democratic Republic of Congo to Tanzania, H.E. Ambassador Juma Khalfan Mpango (right). 


The Deputy Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, Hon. Mahadhi Juma Maalim (MP) cutting a cake as he graced the 72nd Independence Anniversary of Pakistan held recently in Dar es Salaam.  Looking on (left) is the High Commissioner of Pakistan to Tanzania, H.E. Ambassador Tajammul Altaf and the Dean of Diplomatic Corps and Ambassador of Democratic Republic of Congo to Tanzania, H.E. Ambassador Juma Khalfan Mpango (Photo by Robert Okanda of Daily News Tanzania)

Distinguished guests, including H.E. Sander Gurbuz (right), the Turkey's Ambassador to Tanzania, Acting Director of the Department of Ausia and Australasia, Mr. Shao (2nd right), Indian High Commissioner H.E. Kocheril Velayudhan Bhagirath (2nd left) and the Dean of Diplomatic Corps and Ambassador of Democratic Republic of Congo to Tanzania, H.E. Ambassador Juma Khalfan Mpango (left), enjoying the Pakistan traditional food during the 72nd Independence Anniversary of Pakistan held recently in Dar es Salaam. 

Sunday, March 25, 2012

Tanzania condemns Seizure of power in Mali


 
The Government of the United Republic of Tanzania has received with profound consternation, the news of the seizure of power, by force, from a democratically elected Government of the Republic of Mali under H.E. President Amadou Toumani Toure.
 
This forceful seizure of power from a democratically elected government is a serious set-back to the cause of entrenching constitutional rule, democracy and good governance on the African continent and Mali, in particular, which is unacceptable. For, it negates the will of the people of Mali and denies them of their basic right, which they were expecting to exercise during the general elections scheduled for April 2012, to elect the leaders of their own choice, democratically. It is also a reminder of Mali’s dark past history of coups that took place in 1968 and 1991, that had long been forgotten by the Malian people.
 
The Government of the United Republic of Tanzania therefore strongly condemns this act of the seizure of power by force, which is against the letter and spirit of the Constitutive Act of the African Union, the Protocol Establishing the Peace and Security Council of the African Union, the Lome Declaration of July 2002 and the African Charter on Democracy, Elections and Governance, all of which prohibit unconstitutional changes of Governments on the African continent.
 
The Government of the United Republic of Tanzania also joins other members of the international community in demanding the immediate restoration of constitutional rule. Furthermore, Tanzania calls on mutineers to take all the necessary measures to ensure the safety and security of the President and his family as well as his associates.  Also, Tanzania calls upon them to ensure respect for individual and collective freedoms and refrain from any acts of violence which may lead to the deterioration of the security in the country.

 
Finally, the Government of the United Republic of Tanzania supports the decision of the African Union to temporarily suspend the membership of Mali from the continental organization and expresses its commitment to work together with other Member States of the African Union, under the aegis of the African Union, to ensure that constitutional rule is restored in Mali so as to allow the Malian people choose the leaders of their own choice during the elections that were scheduled to take place in April 2012.
 

          MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL CO-OPERATION                                            

Saturday, March 24, 2012

Taarifa kwa Watanzania wanaoishi nchini Mali


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kuwafahamisha Watanzania waliopo Mali kujiandikisha Wizarani kupitia email zifuatazo nje@foreign.go.tz au info@foreign.go.tz. Wakati wa kujiandisha tafadhali toa taarifa muhimu kuhusu Jina lako kamili, Umri wako,namba ya hati yako ya Kusafilia,mahali ulipo nchini Mali, simu yako pamoja na anuani ya barua pepe yako.

Aidha Wizara inapenda kuwashauri Watanzania popote walipo kutosafiri kwenda nchini Mali kutokana na kufungwa kwa mipaka ya nchi hiyo baada ya Kikundi cha Wanajeshi kupindua Serikali ya nchi hiyo na hivyo kusababisha Mipaka yote pamoja na Viwanja vya ndege.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Thursday, March 22, 2012

Hon. Membe bids farewell to APRM Tanzania's Country Review Mission Team

Hon. Bernard K. Membe (MP) gives few remarks during the Cocktail Party he hosted at the Hyatt Regency (Kilimanjaro) Hotel in Dar es Salaam to bid farewell to African Peer Review Mechanism (APRM) Tanzania's Country Review Mission Team.  The Team had just wrapped its one month tour in the country, assessed Zanzibar and other regions including Arusha, Pemba, Songea, Bukoba, Kigoma, Dodoma, Dar es Salaam, Mbeya and others.  Listening on are Prof. Hasa Mlawa (2nd left), Chairman of the APRM Tanzania, Hon. John Shibuda (3rd left) (MP Chadema-Maswa West), a member of the National Governing Council of APRM Tanzania and H.E. Barrister Akere Muna (2nd right), the Lead Panelist for African Peer Review Mechanism (APRM) Country Review Mission for Tanzania. 


Hon. Bernard K. Membe (MP), presents a gift to H.E. Barrister Akere Muna (right), the Lead Panelist for African Peer Review Mechanism (APRM) Country Review Mission for Tanzania.  Looking on is Hon. John Shibuda (MP Chadema Maswa-West).

Hon. Bernard K. Membe (MP), presents a gift to Prof. Adelle Jinadu of Nigeria.  Looking on is Prof. Hasa Mlawa, Chairman of the APRM Tanzania.


Hon. Membe presents a gift to Dr. Rachel Mukamunana.  Looking on is Prof. Mlawa, Chairman of the APRM Tanzania.


Hon. Membe presents a gift to Dr. Kojo Busia.


Hon. Membe presents a gift to Prof. Abdul Aziz Jalloh.  Looking on is Prof. Mlawa.


Hon. Membe presents a gift to Ms. Candy W. Okoboi.  Looking on are Prof. Mlawa and H.E. Barrister Muna.


A group photo with the APRM's Country Review Team in Tanzania. The CRM is expected to produce a country review report and the final national programme of action which will entail strategic actions aimed at addressing the governance challenges afflicting Tanzania.

Ms. Zuhura Bundala, Acting Director of the Department of Africa at the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, chatting with Dr. Kojo Busia.


Ms. Zuhura Bundala (right), Acting Director of the Department of Africa at the Ministry, in conversation with Mr. Ali Bujiku (2nd right), Foreign Service Officer at the Department of Africa, Mr. Assah Mwambene (2nd left), Acting Head of the Government Communication Unit at the Ministry and Mr. Togolani Mavura (left), the Private Assistant to the Minister of Foreign Affairs.  The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation fully participated throughout the CRM assessment tour in the country.