Friday, April 25, 2014

Waziri Membe ampokea Mfalme Mswati III kwa ajili ya Muungano

Ndege iliyombeba Mfalme Mswati  III wa Swaziland ikiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Mfalme Mswati ni miongoni mwa Viongozi kutoka mataifa mbalimbali duniani watakaoshiriki maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mfalme Mswati III akishuka kwenye Ndege mara baada ya kuwasili nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akiwa pamoja na Mke wake Mama Dorcas Membe (katikati) pamoja na Balozi wetu nchini Msumbiji ambaye anawakilisha pia Swaziland Mhe. Shamim Nyanduga wakishuhudia kuwasili kwa Mfalme Mswati IIi
Waziri Membe akisalimiana na Mfalme Mswati mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere.
Waziri Membe akisalimiana na Mke wa Mfalme Mswati III.
Mfalme Mswati III akisalimiana na viongozi mbalimbali waliokuwepo Uwanjani hapo kwa mapokezi.
Mh. Membe akiongozana  na Mfalme Mswati III mara baada kumpokea
Mama Membe akiongozana na Mama Mswati III


Waziri Membe akizungumza na Mfalme Mswati III walipokuwa wakiangalia burudani iliyokuwa ikitolewa na kikundi cha matarumbeta (hakipo pichani).
Mfalme Mswati III pamoja na Waziri Membe wakiangalia burudani ya kikundi cha matarumbeta.


Picha na Reginald Philip.

Viongozi waanza kuwasili nchini kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim  akimpokea Waziri Mkuu wa Msumbiji,  Mhe. Dr. Alberto Antonio Vaquina mara baada ya kuwasili  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Waziri Mkuu huyo ambaye ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Eduardo Coloma ni miongoni mwa viongozi wengi kutoka duaniani kote watakaoshiriki Maadhimisho ya kilele cha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika tarehe 26 Aprili, 2014.
Mhe. Vaquina akiwa na mwenyeji wake Naibu Waziri Mambo ya Nje Dkt. Maalim wakitizama burudani ya ngoma iliokuwa ikitolewa Viwanjani hapo.
Mhe. Dkt. Maalim akizungumza na Dkt. Alberto Antonio Vaquina, Waziri Mkuu wa Msumbiji mara baada ya mgeni huyo kuwasili.

Picha na Reginald Philip.

Wednesday, April 23, 2014

Mhe. Naibu Waziri azindua Kambi ya Airtel Rising Stars International Soccer

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Kambi Maalum ya Kimataifa ya Mafunzo ya Mpira wa Miguu kwa vijana wa kike na kiume wenye umri chini ya miaka 17 kutoka nchi 12 za Afrika ikiwemo Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika Viwanja vya Azam vilivyopo Chamazi jijini Dar es Salaam tarehe 23 Aprili, 2014. Kambi hiyo inadhaminiwa kwa ushirikiano kati ya kati ya Kampuni ya Simu ya Airtel-Tanzania na Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza.
Baadhi ya vijana hao wakimsikiliza kwa makini Mhe. Naibu Waziri (hayupo pichani).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso ambao ni wadhamini wa kambi hiyo kwa kushirikiana na Manchester United akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mhe. Mahadhi akimsikiliza Bw. Colaso, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel-Tamnzania (hayupo pichani wakati wa uzinduzi huo.
Mmoja wa Walimu kutoka Manchester United Bw. Neil Scott akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Adam Isara akiwa na mmoja wa wadau wa michezo wakati wa uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Ayoub Nyenzi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso kwa pamoja na Walimu wa Vijana hao chini ya miaka 17 wakimsikiliza Bw. Nyenzi (hayupo pichani) kutoka TFF alipokuwa akizungumza. Kulia ni Bw. Andrew Stokes na katikati ni Bw. Neil Scott.
Wanamichezo na wageni waalikwa wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri.
Mshereheshaji Bw. Ephraim Kibonde akiendelea na kazi
Mhe. Maalim akipongezwa na Bw. Colaso baada ya kutoa hotuba.
Mhe. Maalim akielekea kuzindua rasmi kambi hiyo kwa kupiga mpira.
Mmoja wa vijana hao ambaye ni mlinda mlango akiwa tayari kudaka mpira kutoka kwa Naibu Waziri.

Mhe. Naibu Waziri akijiandaa kupiga mpira kuashiria kuzindua kambi hiyo ya vijana.
Mhe. Maalim akimsikiliza Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bibi Juliana Yasoda ambaye pia alishiriki uzinduzi huo.

Mhe. Naibu Waziri akizungumza na Waandishi wa Habari
Vijana hao wakiwa kwenye mazoezi
Mhe. Naibu Waziri katika picha ya pamoja na viongozi walioambatana na wanamichezo.
Mhe. Maalim katika picha ya pamoja  na wanamichezo.
Picha na Reginald Philip




Naibu Waziri wa Mambo ya Nje azindua Airtel Rising Stars International Soccer

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) amezindua rasmi Kambi Maalum ya Kimataifa ya Mafunzo ya Mpira wa Miguu kwa vijana wa kike na wa kiume wenye umri chini ya miaka 17 kutoka nchi 12 za Afrika ikiwemo Tanzania.

Uzinduzi wa Kambi hiyo umefanyika katika Viwanja vya Azam vilivyopo Chamazi Jijiji Dar es Salaam tarehe 23 Aprili, 2014 na inadhaminiwa kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya Simu ya Airtel-Tanzania na Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United ya Uingereza. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mhe. Dkt. Maalim amesema kuwa, kambi hiyo inalenga kuwapatia mafunzo maalum vijana hao wadogo ili kuwawezesha kuwa wachezaji mahiri katika mchezo huo ambao unapendwa na watu wengi duniani ikiwemo Tanzania.

“Mimi binafsi kama ilivyo kwa mamilioni ya Watanzania, mpira wa miguu una nafasi maalum katika mioyo yetu na tunazitambua na kuzipongeza jitihada zinazofanywa na Kampuni ya Simu ya Airtel kwa ushirikiano na Manchester United katika kusaidia maendeleo ya mchezo huo hapa Tanzania na sehemu nyingine za Bara la Afrika. Asanteni sana Airtel na Manchester United” alishukuru Mhe. Maalim.

Mhe. Maalim alieleza kuwa, mafunzo hayo ambayo yatasimamiwa na Waalimu kutoka Shule za Mpira wa Miguu za Timu kubwa ya Manchester United, yanalenga kuwaandaa vijana hao wadogo na kukuza vipaji vyao katika mafanikio ya mpira wa miguu Afrika kwani watu wanahitaji kuona mapinduzi katika mchezo huo na kuondokana na matokeo mabaya katika mashindano ya kimataifa.

“Ushiriki wa watoto wetu kwenye mafunzo haya ambayo yatajikita katika kuwajengea uwezo kiakili, kimwili na kisaikolojia, yatawasaidia kuwa na umoja, yatawapa kujiaamini na hatimaye kuwawezesha kufanya vizuri katika masomo yao kutokana na afya njema na pia kuwa wachezaji wa kulipwa Barani Afrika na duniani hapo baadaye”, alisema Mhe. Maalim.

Mhe. Maalim aliongeza kuwa, anaona fahari kubwa kama mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuwepo kwenye uzinduzi huo ikiwa ni katika kuhamasisha Diplomasia ya Michezo ambayo kwa sasa ni muhimu katika kukuza urafiki, undugu, ushirikiano na uhusiano mzuri kati ya mtu mmoja mmoja kwa maana ya wachezaji na pia kwa nchi na nchi kama ilivyo kwa vijana hao ambao wametoka mataifa ya nje 11.

“Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa sasa inahamasisha Diplomasia ya Michezo ikiwa ni njia mojawapo za kuimarisha mahusiano na mataifa mengine kupitia michezo. Wizara inaunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na Wizara yenye dhamana ya michezo na Taasisi nyingine zote za michezo na kitendo cha mimi kuwepo hapa leo ni katika kuongeza nguvu kwenye jitihada hizo ili nchi yetu iendelee kimichezo,” alisisitiza Mhe. Maalim.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ya kuwekeza kwenye michezo.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Ayoub Nyenzi ambaye alimwakilisha Rais wa Shirikisho hilo,  alimshukuru Naibu Waziri kwa kuzindua Kambi hiyo ambayo ni ya pili kwa Tanzania baada ya ile ya mwaka 2011. Aidha, aliwaasa vijana hao kuzingatia mafunzo watakayopewa kwani ndio msingi wa maisha yao hapo baadaye.

Kwa upande wao Walimu wa vijana hao kutoka Manchester United Bw. Andrew Stokes na Bw. Neil Scott walisema kwao ni upendeleo wa pekee kufundisha vijana hao na kwamba Manchester United imedhamiria kushirikiana na Tanzania katika masuala ya kuendeleza michezo.

Kambi hiyo ambayo ipo kwa siku tano itahusisha vijana 74 kutoka mataifa 12 ya Afrika ikiwemo Tanzania. Jina la nchi na idadi ya vijana kwenye mabano ni kama ifuatavyo; Tanzania (19), Niger (17), Chad (4), Kenya (4), Malawi (4), Shelisheli (2) na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (6). Nchi nyingine ni Burkina Faso (4), Congo Brazaville (2), Gabon (4), Madagascar (2) na Siera Leone (6).

-Mwisho-














Sunday, April 20, 2014

Waziri Membe awa Mgeni Rasmi Tamasha la Pasaka

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwa na mkewe Mama Dorcas Membe wakiwasili kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kushiriki Tamasha la Pasaka. Mhe. Membe alikuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha hilo lililofanyika siku ya Pasaka tarehe 20 Aprili, 2014.
Mhe. Membe na mkewe wakisalimiana na Waandaaji wa Tamasha la Pasaka akiwemo Kiongozi wao Bw. Alex Msama (wa  kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Taifa.
Mhe. Membe akiwa ameongozana na Mwandaaji wa Tamasha la Pasaka  Bw. Msama kuingia uwanjani.
Mhe. Membe akisalimia umati wa watu (hawapo pichani)  waliohudhuria Tamasha hilo.
Umati wa Watu waliohudhuria Tamasha la Pasaka.
Mwandaaji wa Tamsha la Pasaka Bw. Msama nae akisalimia watu waliohudhuria
Mama Membe akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Bibi Angela Kairuki ambaye pia alishiriki kwenye Tamasha la Pasaka.
Mmoja wa Waimbaji wa Nyimbo za Injili, Bi. Upendo Nkone akitumbuiza wakati wa Tamasha la Pasaka.
Mhe. Membe akimpongeza Bi. Nkone mara baada ya kutumbuiza.
Mmoja wa Wachungaji waliohudhuria Tamasha la Pasaka akisoma risala maalum kwa Mgeni Rasmi, Mhe. Membe.
Mhe. Membe akitoa hotuba wakati wa Tamasha la Pasaka.
Umati wa watu wakishangilia wakati Mhe. Membe (hayupo pichani) akihutubia.
Balozi Mbelwa Kairuki (katikati), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa naye pia alikuwepo kwenye Tamasha la Pasaka.
Mhe. Membe akiwa na Bw. Richard Kasesera ambaye pia alihudhuria Tamasha la Pasaka.

Picha na Reginald Philip.

Saturday, April 19, 2014

Waziri Mkuu ahitimisha Maonesho ya miaka 50 ya Muungano

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Mizengo Peter Kayanza Pinda akiongozana na Mhe. Ummy A. Mwalimu (Mb), Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais alipowasili katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufunga rasmi Maonesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar  rasmi
 19 Aprili, 2014
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda, akihutubia wananchi waliohudhuria sherehe za ufungaji wa Maonesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Wananchi kutoka  vitongoji mbalimbali vya Jiji la Dar es Salaam wakimsikiliza Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda alipokuwa akihutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mhe. Pinda akiangalia burudani iliyokuwa ikitolewa na moja ya kikundi cha ngoma (hawapo pichani) kilichokuwa kikitumbuiza wakati wa ufungaji wa maonesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Wengine katika picha ni Mhe.  Mwigulu Nchemba, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais na Mhe. Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Ilala  ambaye pia alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kikundi cha Ngoma kikitoa Burudani mbele ya mgeni rasmi Mhe. Pinda (hayupo pichani) wakati wa sherehe za ufungaji wa Maonesho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mkumbwa Ally akipokea Cheti cha Ushiriki wa Wizara kwenye Maonesho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akizungumza na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Taasisi zake alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
Wananchi wakiwa katika Banda la maonesho la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Picha na Reginald Philip.