Waandishi wa habari wakimsikiliza Balozi wa China nchini,Lu Youqing (hayupo pichani). |
Tuesday, June 17, 2014
Balozi wa China nchini, Lu Youqing akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya watu wa China Li Yuanchao.
mahojiano baina ya Bw. Omar Mjenga na Cloudstv.
mahojiano kati ya Bw. Omar Mjenga Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai na CloudsTv yaliyofanyika wakati wa Mkutano wa uwekezaji tarehe 11 Juni 2014.
Thursday, June 12, 2014
Mhe. Membe akutana na Mhe. Mark Simmonds Waziri wa Uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika
Wednesday, June 11, 2014
Uteuzi wa Naibu Mabalozi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi
wa Naibu Mabalozi wawili.
Walioteuliwa
ni Bw. Robert Kahendaguza (pichani juu) anayekuwa Naibu Balozi, Ubalozi wa Kudumu kwenye
Ofisi za Umoja wa Mataifa, Geneva, Uswisi, na Bw. Msafiri Marwa (pichani chini) anayekuwa Naibu
Balozi wa Tanzania London, Uingereza.
Kabla
ya uteuzi huu, Bw. Kahendaguza alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa
Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bw. Marwa alikuwa
Ofisa Mambo ya Nje Mkuu.
Uteuzi
huu unaanza tarehe 25 Mei, 2014.
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
JUNI 11, 2014
Misri yapata Rais Mpya
Na Ally Kondo, Cairo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe.
Bernard K. Membe (Mb) amemwakilisha Rais Kikwete katika sherehe za kumuapisha Mkuu
wa Majeshi wa zamani, Field Marshal Abdel Fattah al Sisi kuwa Rais mpya wa
Misri. Rais Sisi aliapishwa na Jaji Mkuu katika viwanja vya Mahakama Kuu ya
Misri siku ya Jumapili tarehe 08 Juni, 2014 ambayo ilitangazwa kuwa ni siku ya
mapunziko.
Sherehe za uapisho zilihudhuriwa na Viongozi wa nchi
mbalimbali duniani, hususan kutoka nchi za Kiarabu na Afrika. Nchi za Kiarabu
ziliwakilishwa vizuri katika sherehe hizo kwa kutuma Viongozi wa ngazi ya Juu
ukilinganisha na nchi za Afrika ambazo nyingi zilituma Mawaziri wa Mambo ya Nje
isipokuwa chache kama vile Somalia, Chadi na Equatorial Guinea ambazo Marais
wao walishiriki wenyewe.
Sherehe za uapisho zilipambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo
gwaride la kijeshi, hotuba za Rais anayengia madarakani na anayetoka na kila
mwakilishi kupata fursa ya kusalimiana na kufanya mazungumzo ya muda mfupi na Rais
Sisi.
Sherehe hizo ambazo zilifanyika huku kukiwa na ulinzi mkali
zilishuhudiwa pia, wafuasi wa Rais Sisi wakizunguka katika mitaa ya jiji la
Cairo wakiwa katika magari, pikipiki au kutembea kwa miguu wakiwa wamebeba
bendera za nchi hiyo huku wakifyatua fataki, kupiga mayowe na honi.
Wachambuzi wa mambo walieleza kuwa Rais mpya wa Misri
anatarajiwa kuituliza nchi hiyo ambayo imekuwa ikikumbwa na machafuko ya
kisiasa ya mara kwa mara tangu mapinduzi ya wananchi yaliyomuondoa madarakani
Rais Hosni Mubarak mwaka 2011.
Hata hivyo, walikiri kuwa Rais Sisi anakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufufua uchumi wa nchi hiyo ambao umedorora kwa
kiasi kikubwa kutokana na machafuko hayo. Changamoto nyingine ambayo Rais Sisi
anakabiliwa nayo ni kurejesha mshikamano na umoja wa wananchi wa Misri ambao
kwa kiasi kikubwa wametofautiana mitazamo kutokana na hali ya mambo inavyokwenda
katika nchi hiyo.
Taswira ya Ushiriki wa Mhe. Membe katika Sherehe za Kumuapisha Rais wa Misri
Waziri wa Mambo ya Nje (kulia) akipokea taarifa fupi kutoka kwa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Misri, Bw. Jestas Nyamanga katika Hoteli aliyofikia Mhe. Waziri ya Fairmont. |
Balozi Kibwana (kushoto) akijadili jambo na Afisa wake, Bw. Celestine Kakere |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) kushoto akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Mhe. Nabil Fahmy. |
Waziri Membe akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mawaziri wenzake baada ya kushiriki katika chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshima yao na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri |
Waziri Membe akibadilishana mawazo na watu mbalimbali kabla ya kupata Chakula cha Jioni. |
Sehemu ya mto Nile ambapo kando yake ndiyo kuna Hoteli ambayo Waheshimiwa Mawaziri waliandaliwa chakula cha jioni. Angani ni helikopta ikiwa katika doria kuhakikisha kuwa hakuna mtu anadhurika. |
Tuesday, June 10, 2014
Waziri Membe kushiriki Mkutano kuhusu Ukomeshaji Udhalilishaji wa Kijinsia mjini London
Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali ya Uingereza
imemwalika Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K.
Membe (Mb.) kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa kuhusu Ukomeshwaji wa Udhalilishaji
wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro (“End Sexual Violence in Conflict”) utakaofanyika
mjini London, Uingereza kuanzia tarehe 10 hadi13 Juni, 2014.
Mwaliko huo unakuja
kufuatia mchango mkubwa wa Tanzania katika kufanikisha kuwepo kwa Tamko la
Umoja wa Mataifa linalohusu suala hilo (Declaration of Commitment to End Sexual
Violence in Conflict).Vile vile itakumbukwa kuwa, Tanzania imekuwa mstari wa
mbele katika kuchangia vikosi vya kulinda amani katika maeneo yenye migogoro
Barani Afrika ambayo pia yana wahanga wengi wa udhalilishwaji wa kijinsia.
Pamoja na masuala
mengine, Mkutano huo utajadili hatua za kuchukua ili kumaliza tatizo la
udhalilishaji wa kijinsia katika maeneo yenye migogoro; mchango au nafasi ya
vijana katika kupambana na udhalilishaji wa kijinsia katika maeneo yenye migogoro;
kiwango cha udhalilishaji wa kijinsia unatokea katika maeneo yenye migogoro na
kuweka makubaliano ya kimataifa ya namna ya kutekeleza mikakati iliyomo katika maazimio ya G8 na
Umoja wa Mataifa; na kusikia matatizo na athari za udhalilishaji wa kijinsia
katika migogoro moja kwa moja kutoka kwa Wahanga.
Pia washiriki watajadili
changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na udhaifu unaotokana na kutoadhibiwa kwa
wanaofanya vitendo hivyo.
Mkutano huo
utazikutanisha nchi zilizoathiriwa na migogoro, nchi wahisani, Umoja wa
Mataifa, Asasi zisizo za Kiserikali, Mashirika ya Kimataifa na Taasisi za
Kijamii na wadau wengine.
Aidha, wakati wa
ziara hiyo, Mhe. Membe atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Uingereza
anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. Mark Simmonds. Miongoni mwa masuala
watakayozungumza ni kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Uingereza.
IMETOLEWA
NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM
10
JUNI, 2014
Friday, June 6, 2014
PRESS RELEASE
King Carl XVI Gustav of Sweden |
PRESS RELEASE
H.E Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United
Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to His Majesty, King
Carl XVI Gustav of Sweden on the occasion to celebrate the Swedish National Day on 6th
June, 2014.
“Your Majesty King Carl XVI Gustav,
The King of Sweden,
Stockholm,
SWEDEN.
It
is my pleasure on behalf of the people and the Government of the United
Republic of Tanzania to extend to Your Majesty and through you to the people of
Sweden my heartfelt congratulations on the occasion to celebrate the Swedish
National Day.
The
celebration of your National Day offers us yet another opportunity to reaffirm
our commitment to continue working closely together in enhancing the existing
bilateral ties between our two countries. I am confident that the bonds of
friendship, co-operation and partnership that our two countries enjoy will
continue to grow in greater heights for our mutual benefit.
Please
accept, Your Majesty, my best wishes for your continued good health and peace
and prosperity for the people of Sweden”.
Issued by the Ministry of Foreign Affairs and
International Cooperation of the United Republic of Tanzania,
Dar es Salaam.
06TH JUNE, 2014
Waziri Mwandamizi wa Mambo ya Nje na Ndani wa Singapore ziarani nchini
Bw. Adam Isara (kushoto), Katibu wa Naibu Waziri na Bw. Khatib Makenga, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo |
Mhe. Dkt. Maalim akimsindikiza Mhe. Zulkifli na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao |
Mhe. Dkt. Maalim akiagana na Mhe. Zulkifli. |
Thursday, June 5, 2014
Wizara ya Mambo ya Nje yaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani
Afisa Mambo ya Nje, Bi. Naomi Zegezege akipanda mti kwa niaba ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani. |
Baadhi Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani) |
Katibu Mkuu, Bw. John Haule na Mkurugenzi wa JNICC, Bw. Kulwa katika picha ya pamoja. |
Katibu Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya Wizara kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti. |
PRESS RELEASE
Tuesday, June 3, 2014
Tanzania participates in the 17th NAM Ministerial Conference
TANZANIA PARTICIPATES IN THE 17TH
NON-ALIGNED MINISTERIAL CONFERENCE
Tanzania
participated in the 17th Non-Aligned Ministerial Conference, which
ended in the Algerian capital, Algiers, on May 29.
The
conference, which was opened by Algerian Prime Minister Abdelmalek Sellal on
behalf of President Abdelaziz Bouteflika, adopted a final document asserting
NAM’s position on global political, development and social issues, ranging from
reform of the United Nations, peacekeeping operations, terrorism, disarmament,
post-2015 development agenda to food security.
The
ministers also adopted the Algiers Declaration and five other specific
statements, including reaffirmation of support for Palestinian nationhood, nuclear
non-proliferation and a vote of thanks to Algerian Foreign Minister Ramtane
Lamamra and the host country.
The
conference, which was held at the Palace of Nations, was attended by almost all
the 120 members of the movement, many of whom made statements. Speaker after
speaker reaffirmed the relevance and validity of NAM in bringing the members
together to address emerging global challenges.
The
Tanzanian statement was read by Mr. Japhet Mwaisupule, Minister
Plenipotentiary, on behalf of the Deputy Minister for Foreign Affairs and
International Cooperation, Dr. Mahadhi Juma Maalim.
Tanzania
urged NAM to continue pressing for fair and just economic, financial and
trading multilateral institutions. Reform of these institutions “will not be
complete without involving the United Nations Security Council. We must stand
together in calling for early reform of the Council so as to make it more
effective and responsive to the aspirations of all members,” said the
statement.
It
also called for new trade and investment rules that work for the benefit of
developing countries to facilitate implementation of the global development
agenda.
The
Ministerial Conference, which was preceded by a Senior Officials Meeting, was
addressed by His Excellency Ivo Morales, President of Bolivia, in his capacity
as Chairman of G-77 plus China.
Monday, June 2, 2014
Tanzania na Qatar zasaini Mkataba wa ushirikiano wa kazi na ajira
Mazungumzo yakiendelea. |
Subscribe to:
Posts (Atom)