Wednesday, June 11, 2014

Taswira ya Ushiriki wa Mhe. Membe katika Sherehe za Kumuapisha Rais wa Misri

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) (kulia) akiwa katiika Kiwanja cha Ndege cha Addis Ababa  akiwa njiani kuelekea Cairo, Misri katika sherehe za kumuapisha Rais Mteule, Mhe. Abdel Fattah al Sisi. Mwingine katika picha ni Bw, Shelukindo, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.

Waziri Membe (kushoto)  akiongea na Msaidizi wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ambaye ana ngazi ya Ukurugenzi kwenye chumba cha Wageni Maalum katika Uwanja wa Ndege wa Cairo alipowasili kwa ajili ya kushiriki sherehe za kumuapisha Rais wa nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje (kulia) akipokea taarifa fupi kutoka kwa Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Misri, Bw. Jestas Nyamanga katika Hoteli aliyofikia Mhe. Waziri ya Fairmont.

Mhe. Waziri Membe mwenye miwani akiwa amesimama mbele ya Hoteli ili kuingia katika gari maalum kwa ajili ya kumpeleka eneo lililofanyika sherehe za uapisho. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana.


Balozi Kibwana (kushoto) akijadili jambo na Afisa wake, Bw. Celestine Kakere

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) kushoto akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Mhe. Nabil Fahmy.

Mhe. Membe na Mhe. Fahmy walifanya mazungumzo katika Hoteli aliyofikia Waziri Membe. Mazungumzo yao yalihusu kuimarisha ushirikiano, Misri kurejea katika Umoja wa Afrika na matumizi ya maji ya mto Nile.

Waziri Membe akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mawaziri wenzake baada ya kushiriki katika chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshima yao na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri

Waziri Membe akibadilishana mawazo na watu mbalimbali kabla ya kupata Chakula cha Jioni.

Sehemu ya mto Nile ambapo kando yake ndiyo kuna Hoteli ambayo Waheshimiwa Mawaziri waliandaliwa chakula cha jioni. Angani ni helikopta ikiwa katika doria kuhakikisha kuwa hakuna mtu anadhurika.

Waziri Membe akiwa na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wa Misri, Bi. Fatma. Bi. Fatma ambaye alishawahi kufanya kazi katika Ubalozi wa Misri nchini Tanzania ndio alikuwa Afisa Itifaki anayemuhudumia Mhe. Waziri na ujumbe wake.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.