Thursday, June 26, 2014

Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika, Malabo Equatorial Guinea

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika akiwa amesimama na kupiga makofi baada ya kuimba wimbo wa taifa wa Umoja wa Afrika kuashiria kuanza rasmi kwa mkutano huo. 

Ujumbe wa Tanzania: Kutoka kushoto ni Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Christopher Chiza, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika; (Mstari unaofuatia nyuma kutoka kulia kwenda kushoto) Mhe. Binilith Mahenge, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira; Mhe. Ummy Mwalimu, Naibu Waziri - Mazingira; na Mhe. Haji Sereweji, Mmbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mhe. Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwasilisha salamu zake rasmi wakati wa ufunguzi wa mkutano huo ambapo moja ya masuala aliyozungumzia ni mabadiliko ya tabia nchi na athari zake. Aidha alizisifu nchi za Afrika tisa zinazounda Kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi chini ya uenyekiti wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania.
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Membe wakifanya majadiliano kabla ya ufunguzi wa mkutano huo.
Meza kuu wakiwa wamesimama wakati Wimbo wa Taifa wa Umoja wa Afrika ukiimbwa. 
Mhe. Abdul Fatah el-Sisi, Rais wa Misri akielekea kwenye kipaza sauti kabla ya kuhutubia kwa Mara ya kwanza tangu atwae madaraka nchini Misri, ambapo Umoja wa Afrika umeirudisha nchi hiyo kwenye Umoja baada ya uchaguzi kufanyika.

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Afrika na Addis Ababa Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz; wakielekea Nje ya ukumbi kwa picha ya pamoja ya viongozi waliohudhuria mkutano huo (chini )

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.