Thursday, June 5, 2014

Wizara ya Mambo ya Nje yaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akipanda mti katika kuashiria kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani katika eneo la Kituo wa Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kilichopo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo iliadhimishwa duniani kote tarehe 05 Juni, 2014.  
Afisa Mambo ya Nje, Bi. Naomi Zegezege akipanda mti kwa niaba ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
Bw. John Haule akiongozana na Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  Bw. Deus Kulwa (kulia) baada ya kupanda miti katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani. Kushoto ni Bi Naomi Zegezege, Afisa Mambo ya Nje
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.
Baadhi Wafanyakazi wa Wizara  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Katibu Mkuu  (hayupo pichani)
Katibu Mkuu, Bw. John Haule na Mkurugenzi wa JNICC, Bw. Kulwa katika picha ya pamoja.
Katibu Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya Wizara kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti.
Bw. John Haule akizungumza na waandishi wa habari



Picha na Habari na Reginald Philip

Wizara ya Mambo ya Nje yaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule, amewataka wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na watanzania wote kwa ujumla kutumia nishati endelevu badala ya kuni na mkaa, kuunga mkono juhudi za serikali za kunusuru mazingira.

Akiongea katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyoandaliwa na wizara kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, Bw. Haule alisema hatua nyingine za kutunza mazingira ni kupanda miti; kutolima kwenye miteremko ya milima; kupunguza matumizi makubwa ya mbolea na kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki isiyiteketezeka kwa urahisi.
Wawekezaji katika viwanda watumie teknolojia ya kisasa isiyoongeza gesi joto, alishauri.

Katika maadhimisho hayo chini ya kauli mbiu isemayo  “Sayari ya dunia ni kisiwa chetu wote kwa hivyo tuunganishe nguvu zetu kulinda kisiwa hiki,” Bw. Haule alipanda mti kuanzisha mpango wa wizara wa kupanda miti kutunza mazingira. Miti saba ilipandwa nje ya ukumbi wa Julius Nyerere leo kwa kuanzia.


Maadhimisho hayo pia yalishirikisha wafanyakazi wa AICC na ukumbi wa Julius Nyerere.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.