Tuesday, June 24, 2014

Balozi Sokoine apokelewa kwa shangwe Wizara ya Mambo ya Nje

Balozi Joseph Sokoine ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika akisalimiana na Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uswisi,  Robert Kahendaguza huku Wafanayakazi wengine wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakishangilia mara baada ya Balozi Sokoine kuwasili Wizarani baada ya kuapishwa.
Balozi Sokoine akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bi. Glory Mboya mara baada ya kuwasili Wizarani baada ya kuapishwa.


Balozi Sokoine akisalimiana kwa furaha na Bw. Kelvin Kheri mmoja wa Wafanayakazi Wizarani.

Mapokezi yakiendelea.

Balozi Sokoine akisalimiana na Wafanyakazi wa Wizara walipompokea kwa furaha 
Balozi Sokoine akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Irene Kasyanju mara baada kuwasili.

Picha na Reginald Philip



Monday, June 23, 2014

Makamu wa Rais wa China afungua rasmi Kongamano la Uwekezaji

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe Li Yuanchao akifungua rasmi Kongamano la Pili la Uwekazaji kati ya Tanzania na China. Ufunguzi wa Kongamano hilo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Juni, 2014. Ufunguzi huo ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwekezaji, Mhe. Mary Nagu, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Abdallah Kigoda, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bi. Julieth Kairuki, Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini na Taasisi Binafsi na wadau mbalimbali.
Wajumbe mbalimbali wakifurahia hotuba ya ufunguzi ya  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (hayupo pichani).
Mhe. Pinda, Mawaziri na wajumbe wengine wakimsikiliza Makamu wa Rais wa China, Mhe. Li Yuanchao (hayupo pichani) alipokuwa akifungua Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na China
Wajumbe wakifuatilia ufunguzi
Mhe. Li Yuanchao (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na  Mhe. Pinda (mwenye tai nyekundu), Mhe. Nagu (wa pili kushoto), Mhe. George Mkuchika (wa kwanza kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Balozi wa China nchini, Mhe. Lu Youqing (wa kwanza kulia) na Bi. Kairuki. Mkurugenzi wa TIC.
Picha ya pamoja na Wajumbe wa Kongamano

Picha na Reginald Philip

Sunday, June 22, 2014

Makamu wa Rais wa China awasili nchini kwa ziara ya kikazi



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimlaki kwa furaha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2014 kwa ajili ya kuanza rasmi ziara yake ya kikazi  ya siku tano hapa nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju aliyekuwepo Uwanjani hapo kwa ajili ya mapokezi ya Makamu huyo wa Rais.
Mhe. Li Yuanchao akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki mara baada ya kuwasili Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa China Mhe. Li Yuanchao akipita  katikati ya Gwaride la Heshima wakati wa mapokezi yakehuku  akisindikizwa na Mwenyeji wake Mhe. Dkt. Bilal.
Mhe. Li akifurahia kikundi cha burudani kilichokuwa uwanjani hapo (hawapo pichani) wakati wa mapokezi yake.
Moja ya vikundi vya burudani vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais wa China alipowasili hapa nchini.
Picha na Reginald Philip

Friday, June 20, 2014

Waziri Membe azungumza na Balozi wa Oman nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe (Mb), akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Soud Al Mohammed Al-Ruqaish alipofika kwa ajili ya mazungumzo yaliyojikita katika kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizi mbili mapema leo tarehe 20 Juni, 2014, Jijini Dar es Salaam.
Waziri Membe akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Oman nchini
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga na Afisa Mambo ya Nje, Batholomeo Jungu wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Balozi wa Oman  hapa nchini (hawapo pichani)
Waziri Membe pamoja na Balozi wa Omani wikifurahia jambo wakati wa mazungumzo yao wa kwanza kushoto ni Afisa aliyeambatana na na Balozi wa Oman.
Picha ya pamoja.


Picha na Reginald Philip



Thursday, June 19, 2014

Balozi mpya wa Marekani nchini ajitambulisha rasmi kwa Waziri Membe


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimkaribisha kwa furaha na kwa mara ya kwanza ofisini kwake Balozi wa Marekani hapa nchini, Mhe. Mark Childress alipofika e kwa ajili ya kujitambulishana pia kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani.
Mhe. Membe na Mhe. Childress katika picha ya pamoja.
Mhe. Childress akisaini Kitabu cha Wageni alipowasili Ofisini kwa Mhe. Membe
Mhe. Membe na Balozi Childress wakiwa katika mazungumzo
Mhe. Childress na ujumbe aliofuatana nao wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)
Picha ya pamoja kati ya Mkhe. Membe na Mhe. Childress pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Marekani na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia).

Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Mabalozi wa China, Cuba, Japan, Msumbiji na Kaimu Balozi wa Ujerumani

......Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa China


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimkaribisha Ofisini kwake Balozi wa China hapa nchini,  Mhe. Lu Youqing alipofika kwa ajili ya mazungumzo ambayo yalihusu pia ziara ya Makamu wa Rais wa China atakayoifanya hapa nchini kuanzia tarehe 21 hadi 26 Juni, 2014.
Mhe. Balozi Lu akimweleza jambo Mhe. Membe wakati wa mazungumzo yao.
Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Balozi LU (hawapo pichani)

 Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa Cuba

Mhe. Waziri akimkaribisha Ofisini kwake Balozi wa Cuba hapa nchini, Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo alipofika kwa ajili ya mazungumzo kuhusu kuimarisha ushrikiano kati ya Tanzania na Cuba. Tanzania na Cuba zinashirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya na siasa.
Mhe. Membe akimsikiliza kwa makini Balozi Tormo.

Mazungumzo yakiendelea huku Afisa Mambo ya Nje, Bw. Lucas Mayenga akinukuu.

Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa Japan

Mhe. Membe akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaki Okada alipofika kwa ajili ya mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.

Mhe. Balozi Okada akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Mhe. Membe.

Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Nathaniel Kaaya akifuatili mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Mhe. Okada (hawapo pichani)

Mkutano wa Mhe. Membe na Kaimu Balozi wa Ujerumani

Mhe. Membe akimkaribisha ofisini kwake Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Bw. Hans Koeppel alipofika kwa mazungumzo na Mhe. Waziri  kuhusu salamu za shukrani kwa Serikali ya Tanzania kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Frank-Walter Steinmeir kufuatia ziara yake ya mafanikio aliyoifanya hapa nchini mwezi Machi 2014

Mhe. Membe akipokea barua ya salamu hizo kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa nchini (hawapo pichani)

Mkutano wa Mhe. Membe na Balozi wa Msumbiji

Mhe. Membe akizungumza na Balozi wa Msumbiji hapa nchini, Mhe. Vicente M. Veloso alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
Balozi Veloso na ujumbe aliofuatana nao wakimsikiliza Mhe. Membe alipozungumza nao.

Press Release

Queen Elizabeth II


PRESS RELEASE
H.E Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to her Majesty Queen Elizabeth II on the occasion of her 88th birthday.

The message reads as follows:-
“Your Majesty Queen Elizabeth II,
Buckingham Palace,
London,
UNITED KINGDOM.

On behalf of the people and the Government of the United Republic of Tanzania, I extend sincere congratulations on the occasion of your 88th birthday.

As you celebrate your birthday allow me to take this opportunity to express my appreciation on the good relations that exist between our two countries and peoples.

The celebration of your birthday offers us yet another opportunity to reaffirm our commitment to continue working closely together in strengthening further the relations between our two countries.

Please accept, Your Majesty, my best wishes for your continued good health and peace and prosperity for the people of the United Kingdom.”

Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

18th June 2014


Wednesday, June 18, 2014

Makamu wa Rais atembelea mradi wa Dubai Sports City

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Ghalib Bilali, leo ametembelea mradi mpya wa Dubai Sports City, kujionea ramani ya mradi huo mkubwa wa kijiji cha michezo cha Dubai. kulia kwa makamu wa Rais, ni Bw. MOhamed Sharif, Mtanzania ambaye ni mtendaji Mkuu wa Mradi wa Dubai Sports City, na kushoto ni Balozi Mdogo Dubai, Omar Mjenga 

Ujumbe ulio ambatana na Makamu wa Rais nao wakitazama ramani ya mradi huo.

Tuesday, June 17, 2014

Balozi wa China nchini, Lu Youqing akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya watu wa China Li Yuanchao.

Balozi wa China nchini,Lu Youqing (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Watu wa China Mhe. Li Yuanchao katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini China ,Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo .

Balozi wa China nchini,Lu Youqing(kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Watu wa China Mhe. Li Yuanchao katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini China ,Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo na wakwanza kutoka kushoto ni  Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiruikiano wa Kimataifa Balozi Mbelwa Kairuki.

Waandishi wa habari wakimsikiliza Balozi wa China nchini,Lu Youqing (hayupo pichani).

Mazungumzo yakiendelea


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MKUTANO WA KATIBU MKUU, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU ZIARA YA MHE. LI YUANCHAO, MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA WATU WA CHINA, NCHINI TANZANIA, DAR ES SALAAM
TAREHE 18 JUNI, 2014


·       Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Vitengo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje,
·       Ndugu waandishi wa Habari wa vyombo vya habari vya umma na binafsi,
·       Mabibi na Mabwana,

Ndugu Waandishi,
Tumekutana hapa leo kwa lengo la kufahamishana kwa muhtasari kuhusu ziara ya Mheshimiwa, Li Yuanchao, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, nchini. Makamu huyo wa Rais wa China, anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini kuanzia tarehe 21 hadi 26 Juni 2014. Lengo la ziara hiyo, ni kuimarisha mahusiano ya karibu na ya kidugu kati ya nchi hizi mbili ambayo mwaka huu yamefikisha miaka hamsini tangu kuasisiwa rasmi mwaka 1964.



Ndugu Waandishi,
Mheshimiwa Li Yuanchao atawasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tarehe 21 Juni 2014 amnapo atatembelea vivutio vya utalii vilivyopo Mkoa wa Arusha hususan Bonde la Ngorongoro tarehe 22 Juni 2014 na jioni atawasili jijini Dar es Salaam kuendelea na ziara yake hiyo.

Ndugu Waandishi,
Kama mnavyofahamu, ziara hii inakuja wakati muafaka ambapo tunaelekea katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania. Kadhalika, huu ni mwendelezo wa ziara mbalimbali zinazofanywa na Viongozi wa ngazi za juu wa pande zote mbili ambazo zimekuwa ni chachu katika kufikiwa kwa makubaliano mbalimbali hususan ya kiuchumi kwa manufaa ya pande zote mbili. 

Ndugu Waandishi,
Akiwa jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Li Yuanchao, atakutana na kufanya mazungumzo na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa kati ya tarehe 23 na 26 Juni 2014 pamoja na kufungua Jukwaa la Kiuchumi kati ya Tanzania na China. Miongoni mwa Viongozi atakaokutana nao ni Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwenyeji wake Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vilevile, Mheshimiwa Li Yuanchao atatembelea Zanzibar tarehe 25 Juni 2014 ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Balozi Seif Idi, Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kurejea Dar es Salaam tarehe 26 Juni 2014 tayari kwa safari ya kuelekea nchini China.

Ndugu Waandishi,
Ikumbukwe kuwa, Tanzania na China si tu zimekuwa zikishirikiana katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kisiasa lakini wamekuwa ni marafiki wakati wa shida na wa raha. Hili linadhihirishwa na mikataba takribani 17 ambayo nchi hizi mbili zilikubaliana mwezi Machi 2013 wakati wa ziara ya Mhe. Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China nchini.

Hivyo, mazungumzo kati ya Mheshimiwa Li Yuanchao na viongozi wetu Wakuu wa Kitaifa yatajikita zaidi katika kuimarisha zaidi ushirikiano uliopo wa kiuchumi, kisiasa na kijamii kati ya nchi hizi mbili pamoja na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.





Ndugu Waandishi,
Ni matumaini yangu mimi binafsi, Wizara pamoja na Serikali kwa ujumla kwamba wakati wote Mheshimiwa Li Yuanchao atakapokuwa nchini tutapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwenu na wadau wengine.

Itoshe tu kusema kwamba Tanzania na China zitaendelea kufanya juhudi za pamoja katika kuimarisha ushirikiano wa kirafiki, katika sekta mbalimbali, na kuhimiza uhusiano na ushirikiano wa kiuchumi ili kunufaisha pande zote mbili.

Mwisho Ndugu Waandishi wa Habari, napenda kunukuu kauli ya Mwalimu Nyerere, Mwasisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba katika huu Ulimwengu tumekuwa na marafiki wengi sana lakini rafiki mmoja wa kweli ni Jamhuri ya Watu wa China.


……Ahsanteni Sana…


WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Juni 2014                                       Dar es Salaam.


mahojiano baina ya Bw. Omar Mjenga na Cloudstv.


mahojiano kati ya Bw.  Omar Mjenga Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai na CloudsTv yaliyofanyika wakati wa Mkutano wa uwekezaji tarehe 11 Juni 2014.