Tuesday, July 8, 2014

Viongozi mbalimbali watembelea banda la Mambo ya Nje sabasaba

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova  akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Maonesho la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Viwanja vya Sabasaba
Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Janeth Widambe akipata maelezo alipotembelea Banda la Mambo ya Nje katika Viwanja vya Sabasaba
Wananchi wakiwa wamefurika katika Banda la Maonesho la Mambo ya Nje katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mambo ya Nje na Taasisi zake.

Picha na Reginald Philip

Sunday, July 6, 2014

Mwanamfalme Akishino wa Japan amaliza ziara yake rasmi nchini

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angela Kairuki (Mb.) akizungumza na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino kabla ya kuondoka. Prince Akishino amemaliza ziara yake aliyo ifanya hapa nchini kuanzia tarehe 3 hadi 6 Julai 2014
Naibu waziri Angela Kairuki akimsindikiza Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino tayari kwa kuanza safari, kushoto pichani Afisa Mambo ya Nje Ramadhani Ditopile
Naibu Waziri Angela Kairuki akiagana na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino kabla ya kuanza safari yake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.

Picha na Reginald Philip

Saturday, July 5, 2014

Rais Kikwete Atembelea Banda la Mambo ya Nje, Sabasaba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye viwanja vya Sabasaba
Rais Dkt. Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje
Rais Kikwete (Mwenye Koti la Blue) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Taasisi zake.
Mtumishi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mbwana Msingwa akiweka saini katika kitabu cha wageni alipokuja na familia yake kwenye banda la Mambo ya nje lililopo kwenye viwanja vya sabasaba
Mpiga Picha wa Rais Muhidin Issa Michuzi (Ankal) akisalimiana na Afisa Mawasiliano Ally kondo, alitembelea Banda la Mambo ya Nje katika Viwanja vya Sabasaba

Picha na Reginald Philip

Waziri Membe ahudhuria msiba wa Mzazi wa Felista Rugambwa

Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa heshima za mwisho kwenye Kanisa la Anlikana la Mt. Joseph, kumuaga Mzee Rugambwa ambaye ni baba wa mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Idara ya Ulaya na Marekani Bi. Felista Rugambwa leo Julai 5, 2014.  
Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara John Haule na Mkurugenzi wa Idaho ya Ulaya na Marekani Balozi Joseph Sokoine, wakifuatilia misa iliyofanyika kwenye kanisa la Mt. Josefu, Dar es salaam leo tarehe 5 Julai 2014. 

Felista Rugambwa (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na ndugu zake wakifuatilia misa.
Familia ya Marehemu Mzee Rugambwa wakitoa shukrani (pichani juu)                        

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akitoa shukrani kwa niaba ya Wizara (pichani chini)


Friday, July 4, 2014

Dkt. Shein akutana na Mwana Mfalme wa Japan

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mwana Mfalme wa Japani Prince Akishino alipowasili Ikulu Mjini Zanzibar leo akiambatana na Mkewe Princess Akishino na baadae kufanya Mzazungumzo.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (kushushoto) akizungumza na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Ali Mohamed Shein (katikati) akiwapa maelezo Mwana Mfalme wa Japani Prince Akishino na Mkewe juu ya moja ya mti uliopo mbele yao
Picha ya pamoja


Picha na Reginald Philip

Waziri Membe apokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa UNFPA nchini

Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisalimiana na Mwakilishi mpya wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) hapa nchini, Dkt. Natalia Kanem alipofika Ofisini kwake kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
Mhe. Membe akipokea Hati za Utambulisho za Dkt. Kanem.
Mhe. Membe akizungumza na Dkt. Natalia kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu idadi ya watu na maendeleo. Kwa upande wake Dkt. Kanem aliahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala ya idadi ya watu ambapo pia aliipongeza Tanzania hususan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwa mstari wa mbele katika kutetea Afya ya Mama na Mtoto duniani. 
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Membe na Dkt. Kanem. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa pili kutoka kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi Mindi Kasiga (wa pili kutoka kulia), Afisa Mambo ya Nje, Bibi Samira Diria (wa kwanza kulia) na Mtaalam wa Mawasiliano kutoka UNFPA, Bi. Sawiche Wamunza.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

Waziri Membe apokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa IFAD nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Chakula na Kilimo (IFAD) hapa nchini, Bw. Francisco Javier Pichou Angulo.  Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofisini kwa Mhe. Membe tarehe 04 Julai, 2014.
Mhe. Membe akimsikiliza Bw. Angulo alipozungumza nae baada ya kupokea hati zake za Utambulisho. Miongoni mwa masuala aliyoahidi Mwakilishi huyo ni pamoja na kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Tanzania katika Sekta ya Kilimo na Chakula.
Mhe. Membe nae akizungumza huku akisikilizwa na Mwakilishi huyo pamoja na Afisa aliyefuatana nae pamoja Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa kwanza kushoto)
Picha ya pamoja.


Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali


Courtesy Call

Hon. Bernard K. Membe, Minister for Foreign Affairs and International Cooperation pays a courtesy call  to His Eminence Polycarp Cardinal Pengo, Archbishop of the Dar es salaam Archdiocese of the Roman Catholic Church at his residence in Kurasini, Dar es salaam.


Rais Kikwete apokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Malaysia na Cote d'Ivoire nchini


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hati za Utambulisho za Balozi wa Malaysia nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Ismail Salem. Haf;la hiyo fupi ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 4 Julai, 2014.
Mhe. Rais akimtambulisha Balozi Salem kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule.
Mhe. Balozi Salem akisalimiana na Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Balozi Salem akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Khatib Makenga.
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Balozi Salem mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho
Balozi Salem akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kukabidhi hati zake za Utambulisho.
Balozi Salem akisikiliza Wimbo wa Taifa lake mara baada ya kuwasili Ikulu. Wengine katika picha ni Balozi Mohammed Maharage Juma, Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki na Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo.
Bendi ya Polisi ikipiga wimbo wa taifa la Malaysia kwa heshima ya Balozi wake (hayupo pichani). 

....Balozi wa Cote d'Ivoire nae awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais

Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage Juma (katikati) akimtambulisha Balozi wa Cote d'Ivoire nchini mwenye makazi yake mjini Nairobi, Kenya, Mhe. Georges Aboua kwa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla Balozi huyo hajawasilisha Hati za Utambulisho
Balozi Aboua akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Kikwete.
Mhe. Rais Kikwete akimtambulisha kwa Balozi Aboua Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule.
Balozi Aboua akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana.
Balozi Aboua akisalimiana na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Selestine Kakele.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Balozi Aboua (kushoto) na Afisa aliyefuatana na Balozi huyo.
Rais Kikwete akizungumza na Balozi Aboua.
Balozi Aboua akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu.
Balozi Aboua akisikiliza wimbo wa taifa lake mara baada ya kuwasili Ikulu. Wengine katika picha ni Balozi Mohammed Maharage Juma, Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki pamoja na Mnikulu, Bw. Shaaban Gurumo.
Bendi ya Polisi ikiongozwa na ASP Kulwa ikipiga wimbo wa taifa kwa heshima ya Balozi Aboua wa Cote d'Ivoire nchini (hayupo pichani)

Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.


Thursday, July 3, 2014

PRESS RELEASE

Hon. Bernard K. Membe, Minister for Foreign Affairs and International Cooperation giving country's position during the joint SADC/ICGLR Ministerial Meeting held in Luanda, Angola July 2, 2014. Left to the Minister is the Tanzanian Army Chief of Staff, Lt. Gen. Samuel Ndomba.



SADC/ICGLR MINISTERIAL MEETING PRESS RELEASE



The second joint ministerial meeting of the Southern Africa Development Cooperation (SADC) and the International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR) countries was concluded in Luanda July 2, 2014 with concrete steps to finding sustainable peace in the region.


The well attended meeting by all country members represented by foreign and defence ministers deliberated heavily on a single agenda of voluntarily disarmament of the Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR).

Hon. Bernard Membe, Minister for Foreign Affairs and International Cooperation, led the Tanzania delegation whereby the Tanzania Defence Minister was represented by the Tanzanian Army Chief of Staff Lt. Gen. Samuel Ndomba.  


FDLR a politico-military organization whose combatants are exclusively freedom fighters originally from Rwanda settled in DRC, wrote an appeal letter to SADC secretariat expressing their readiness to surrender and hand over their weaponry to African relevant authorities. The letter also requested assistance from the organ to oversee the process of Disarm, Demobilize, Repatriate, Resettle and Re-integrate (DDRRR) in accordance to the directives of other neighbouring countries including Tanzania.

Apart from accepting the said letter, SADC member states welcomed the FDLR willingly surrender and adherence to the DDRRR process. They however strongly suggested other stakeholders such as AU, UN and ICGLR to oversee the process while Rwanda and DRC were urged to take part in the process.  

In a joint session, delegates discussed the provisional six-month time frame given to the FDLR to complete the DDRRR process as proposed by the technical experts meeting prior to ministerial meeting. Democratic Republic of Congo (DRC) supported by majority countries including Tanzania insisted that the allocated timeframe was right while Rwanda claimed the past experiences proved 3 months to be enough.


However the chair and the host of the said meeting, Angola, ruled out for the six months proposal but should be revised by the third month to gauge progress.


It is the expectation of all countries in attendance that the DDRRR process is implemented within the given time frame with full engagement of both DRC and Rwanda.

The ICGLR/SADC member countries also urged international community and neighbouring countries to join hands with DRC and Rwanda in this historical peace - making process.  
The third meeting of this nature is expected to take place within the next three months.


Issued by:
Government Communication Unit;
Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

03rd July, 2014