Monday, August 11, 2014

Kaimu Katibu Mkuu azungumza na Mkurugenzi wa masuala ya Afrika na Mashariki ya Kati wa Jamhuri ya Korea

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akizungumza na Bw. KWON Hee-seog, Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Afrika na Masharikiriki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Korea ambaye ametembelea nchini kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea.
Bw. KWON akizungumza.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki akiwa na Maafisa Mambo ya Nje, Bw. Cosato Chumi (katikati) na Emmanuel Luangisa wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Yahya na Bw. KWON ( hawapo pichani).
Ujumbe kutoka Jamhuri ya Korea uliofuatana na Bw. KWON.
Mazungumzo yakiendelea.

Picha na Reginald Philip

Watanzania waishio Visiwa vya Comoro waanzisha rasmi jumuiya yao.

Mhe. Balozi Kilumanga pamoja na watendaji wa Ubalozi wakifuatilia mkutano.

Sehemu ya Watanzania wanaoishi Comoro wakifuatilia hotuba ya Mhe. Balozi Kilumanga.

Viongozi wapya wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Kilumanga. Mwenye kanzu kushoto mwa Balozi, ni Bw. Salum Ali Abdallah (Mwenyekiti), wakulia kutoka alipo Balozi ni Bw. Khalfan Salum Khalifan (Makamu Mwenyekiti), anayefuatia kulia ni Bibi Rukia Selemani (Katibu).


Jana tarehe 10 Agost 2014, Watanzania wanaoishi katika Muungano wa Visiwa vya Comoro walianzisha rasmi Jumuiya yao. Lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ni kuwaunganisha wanachama wake, kuwawezesha kushirikiana katika kutambua fursa za maendeleo na kutoa mchango kwa taifa lao la Tanzania.

Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ubalozi wa Tanzania, Moroni. Wakati akifungua mkutano huo, Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania nchini Comoro aliwaeleza Watanzania hao kwamba Serikali ya Tanzania inathamini sana na kutambua umuhimu wao Serikali imeanzisha Idara inayoshughulikia Watanzania wanaoishi Ughaibuni katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aidha, Kitengo kama hicho kimeanzishwa katika Ofisi ya Rais wa Zanzibar. Sambamba na hilo, Viongozi wote wamekuwa wakikutana na Watanzania wanaoishi Ughaibuni, kila wanapopata fursa ya kufanya hivyo, wanapokuwa nje ya nchi. Mkuu wa Utawala wa Ubalozi, Nd. Ali Jabir Mwadini alitoa mada kuhusu misingi ya uanzishaji wa Jumuiya za Kiraia na kubainisha vipengele muhimu vinavyopaswa kuzingatiwa hususani katika katiba ya Jumuiya.
Mwisho, ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa muda waliopewa jukumu la kuandaa katiba.

Sunday, August 10, 2014

Balozi Chabaka afanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Exim Bank

Mhe. Chabaka Kilumanga (wa pili kushoto), Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya mazungumzo na Bw. Yogesh Manek, Mwenyekiti wa Bodi ya Exim Bank, kwenye Makazi ya Balozi, mjini Moroni. Maudhui ya mazungumzo hayo yalihusu azma ya Ubalozi ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wenzao wa Comoro kwa lengo la kuwezesha kila upande kutambua wafanyabiasha wanaotambulika na kuaminika  na pia kuwahamasisha kufanya biashara kwa kutumia taratibu rasmi. Uongozi wa Exim Bank umekubali kusaidia kifanyanikisha azma hiyo. Mhe. Balozi na Bw. Manek walizungumzia pia uwezekano wa Exim Bank kudhamini mradi mkubwa wa umeme ambao unategemewa kuanzishwa kati ya Shirika la Umeme la Comoro na Kampuni ya DACC Global ya Marekani kwa kushirikiana na Kampuni ya NSI Energy ya Tanzania.

Invitation for admission into various programmes at the Centre for Foreign Relation for Academec year 2014/2015



CENTRE FOR FOREIGN RELATIONS
DAR ES SALAAM
(FULL ACCREDITED BY NACTE)

(Established by the 1978 Tanzania/Mozambique Agreement, Incorporated in the
Consular and Diplomatic Immunities and Privileges Act. No. 5, 1986)


INVITATION FOR ADMISSION INTO CERTIFICATE (NTA LEVEL 4), ORDINARY DIPLOMA (NTA LEVEL 5 & 6), DEGREE (NTA LEVEL 7 & 8) AND POSTGRADUATE DIPLOMA PROGRAMMES FOR THE ACADEMIC YEAR 2014/2015

A: IMPORTANT INFORMATION FOR ALL APPLICANTS

i)            THE CENTRE HAS INTRODUCED A BACHELORS DEGREE IN INTERNATIONAL RELATIONS AND DIPLOMACY (BDIRD) BEGINNING IN THE 2014/15 ACADEMIC YEAR.

ii)            Applicants aspiring to pursue Bachelors Degree in International Relations and Diplomacy should lodge their applications through the Central Admission System (CAS) under TCU and NACTE.

iii)           Applicants for Certificate, Ordinary Diploma and Postgraduate Diploma programmes should lodge their applications directly to the Centre not later than 29th August 2014.

B: PROGRAMMES OFFERED AND REQUIRED QUALIFICATIONS:

1. A BASIC CERTIFICATE IN INTERNATIONAL RELATIONS AND DIPLOMACY (NTA LEVEL 4)

            Regular and Evening Sessions
This is a one year programme aimed at equipping students to apply basic knowledge and skills in the field of International Relations and Diplomacy at work places. The graduands normally work under close supervision of qualified professionals in public, private and Non-governmental Organizations (NGOs).

          Entry Qualifications:
All applicants of the Certificate programme must have an Ordinary Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) with at least FOUR passes, OR equivalent qualifications.

2. AN ORDINARY DIPLOMA IN INTERNATIONAL RELATIONS AND DIPLOMACY (NTA LEVEL 5 AND 6)

Regular and Evening Sessions
This is a two-year programme aimed at enabling students to apply knowledge and skills in International Relations and Diplomacy at work places. The graduands are trained to work independently under the supervision of qualified professionals in public, private and Non-governmental Organizations (NGOs).

          Entry Qualifications:

i)            Direct Entry
A candidate must have an Advanced Certificate of Secondary Education Examination (CSEE), with ONE principal pass and TWO subsidiaries obtained at the same sitting and Certificate of Secondary Education (CSEE) with credit passes in THREE subjects.

          ii)        Equivalent Entry Scheme
A candidate must have a certificate from any institution recognized by NACTE with at least a second class or an average of B and above. 

3. A BACHELORS DEGREE IN INTERNATIONAL RELATIONS AND DIPLOMACY (BDIRD)

Regular and Evening Sessions
This is a three-year programme aimed at producing qualified and competent graduands to work in the field of International Relations and Diplomacy. The graduands are trained to work independently under the supervision of qualified professionals in public, private and Non-governmental Organizations (NGOs).

          Entry Qualifications:

ii)           Direct Entry
A candidate must have an Advanced Certificate of Secondary Education Examination (CSEE), with two principal passes excluding religious subjects and Certificate of Secondary Education (CSEE) with credit passes in THREE subjects.

          ii)        Equivalent Entry Scheme
A candidate must possess an Ordinary Diploma in International Relations and Diplomacy or related field from any institution recognized by NACTE with at least a second class or an average of B and above. 

4. POST-GRADUATE DIPLOMA PROGRAMMES: Evening Session Only

i)        POSTGRADUATE DIPLOMA IN MANAGEMENT OF FOREIGN RELATIONS
This is a one year programme aimed at enabling students to acquire higher professional knowledge and skills in International Relations and Diplomacy and apply them in work places. The graduands can handle complex and newly emerging problems related to the course in the community. 


ii)       POSTGRADUATE DIPLOMA IN ECONOMIC DIPLOMACY
This is a one year programme which aims at enabling graduates to acquire higher professional knowledge and skills in Economic Diplomacy and apply them in work places. The graduands can handle complex and newly emerging problems related to the course in the community.

Minimum Qualifications:

·         A good First Degree or its Equivalent, OR
·         A good Advanced Diploma from recognized institutions.
·         Masters Degree holders are also encouraged to apply.

C: APPLICATION PROCEDURES

·         Non-refundable application fee of Tshs. 30,000/=.
·         Payments should be made through the Centre for Foreign Relations - A/C No. 20101100061 - NMB Bank.
·         Photocopies of certificates and testimonials should be attached.
·         The deadline for applicants for Certificate, Ordinary Diploma and Postgraduate Diploma is Friday 29th August, 2014.
·         Academic Year 2014/2015 commences on 29th September, 2014.

All enquires should be addressed to:

          The Deputy Director Academic, Research and Consultancy (Admissions),
          Centre for Foreign Relations,
          P.O. Box 2824,
          DAR ES SALAAM.
         
Tel: +255-22-2851007.
Mobile: +255-755 544119/786 258372/713 258372
Fax: +255-22-2851007.
Website: www.cfr.ac.tz

          

Thursday, August 7, 2014

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa azungumza na Mwakilishi wa UNFPA nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) hapa nchini, Dkt. Nathalia Kanem alipofika Ofisini kwake kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu idadi ya watu na maendeleo. 
Dkt. Kanem  akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Balozi Mushy.
Bibi Samira Diria, Afisa Mambo ya Nje akinukuu mazungumzo kati ya Balozi Mushy na Dkt. Kanem (hawapo pichani). Mwingine katika picha ni Afisa kutoka UNFPA nchini.

Picha na Reginald Philip

Monday, August 4, 2014

PRESS RELEASE

H.E. Xi Jinping, President of the People's Republic of China


PRESS RELEASE

H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a condolence message to H.E. Xi Jinping, President of the People’s Republic of China following a 6.5 magnitude earthquake that hit the South West China’s Yunnan Province on Sunday 3rd August, 2014 claiming at least 398 lives. 

The message reads as follows:

“H.E. Xi Jinping,
President of the People’s Republic of China,
BEIJING,
PEOPLE’S REPUBLIC OF CHINA.

I have learnt with profound shock and deep sorrow the sad news of a 6.5 magnitude earthquake that hit the South West China’s Yunnan Province this Sunday afternoon 3rd August, 2014 claiming at least 398 lives, leaving nearly 2000 injured and homeless as well as causing severe destruction of properties and infrastructure.

On behalf of the Government and the People’s of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf, I would like to convey my deepest condolences and sympathy to you and through you to the Government and the people of the People’s Republic of China and particularly to the bereaved families.

The Government and the people of the United Republic of Tanzania join with the families of the deceased, the victims and the people of the People’s Republic of China in this period of pain and agony. We also pray to the Almighty God to rest the souls of the departed in eternal peace while granting quick recovery to the injured.

Please accept, Your Excellency the assurances of my highest consideration”.


Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam.

4th August 2014

President Jakaya Mrisho Kikwete meets MCC's New Chief Executive Officer, Dana J. Hyde

President Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with MCC's new Chief Executive Officer, Dana J. Hyde and her delegation at the Ritz Carlton hotel in  George Town Washington DC. Second left is Energy and Mineral Minister Prof Sospete Muhongo and right is Tanzani'a envoys to the US Ambassador Liberata Mulamula. STATE HOUSE PHOTO.        
President Jakaya Mrisho Kikwete in talks with MCCs new Chief Executive Officer Dana J. Hyde and her delegation at the Ritz Carlton hotel in George Town Washington DC.

Dragon Mart ya Dubai wakutana na Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, Mhe Omary Mjenga

Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe. Omar Mjenga akiwa katikati na uongozi wa Dragon Mart ya Dubai, ambao wameonyesha nia kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara, kujenga uwanja wa maonyesho ya biashara wa kisasa utakao kuwa unafanya maonyesho mfululizo kwa mwaka mzima.

Niao yao pamoja na Wizara, ni kujenga kituo cha ubora (Centre of Excellency) kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Saturday, August 2, 2014

Serikali haijawatelekeza Watanzania nchini Ukraine

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mkumbwa Ally akizungumza na  Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu hatua  zilizochukuliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi katika kuhakikisha Wanafunzi kutoka Tanzania wanaondoka katika Jimbo lenye machafuko la Lugansk huko Ukraine. Mwingine katika picha ni Bw. Ally Kondo, Afisa Habari.
Sehemu ya Waandishi kutoka Vyombo mbalimbali vya habari vya hapa nchini
Mkutano ukiendelea (Picha na Reginald Philip)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

SERIKALI HAIJAWATELEKEZA WATANZANIA WANAOSOMA UKRAINE

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kukanusha vikali taarifa iliyotangazwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), tarehe 30 Julai, 2014, iliyodaikuwa Serikali ya Tanzania imetelekeza wananchi wake wanaosoma Ukraine Mashariki, ambako kunarindima vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Taarifa hiyo ya upande mmoja, iliyomnukuu mtu anayeitwa Shamila, aliyedai ni mmoja wa wanafunzi Watanzania nchini Ukraine, ilisema eti wananchi hao wameachwa bila msaada wowote.

Wizara imesikitishwa na taarifa hiyo iliyotolewa bila kufanyiwa uchunguzi wa kutosha. Ukweli ni kwamba Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, ambao unatuwakilisha pia Ukraine, umechukua hatua za haraka tangu mwezi Juni, 2014, kuhakikisha wanafunzi Watanzania wote wanaondoka katika jimbo la Lugansk lililoko vitani.

Ubalozi ulishirikiana na Rais wa wanafunzi wa Tanzania katika mji wa Lugansk, Bwana Ahmad Juma, kufanikisha kuondoka kwa Watanzania wote 32 waliokuwepo huko kurudi nyumbani au kuhamia mji wa Kharkov, ambao ni salama zaidi.

Serikali kupitia Ubalozi wake Moscow iliwaombea wanafunzi hao malazi kwenye Chuo cha Kharkov Technical University ambacho kilikubali kutoa hosteli kwa wanafunzi hao. Hata hivyo, wengi wa wanafunzi hao waliondokea Lugansk kurudi nyumbani isipokuwa wanafunzi saba ambao walihamia Kharkov. Mpaka tarehe 31 Julai, 2014, ni wanafunzi watatu tu waliokuwa wamebaki mjini Kharkov. Wanafunzi 20 wamedhaminiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Bodi ya Mikopo.

Orodha ya wanafunzi iliyopo Ubalozini haijumuishi jina la Shamila anayedaiwa kuhojiwa na BBC. Inasemeka na mtu huyo alikwishamaliza masomo yake ya shahada ya kwanza na ya pili lakini akaamua kubakia Ukraine akifanya udalali wa kuleta wanafunzi kutoka Tanzania kwa kushirikiana na vijana wa Nigeria.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kuuhakikishia Umma kuwa inasimamia kikamilifu usalama na ustawi wa Watanzania walioko Ukraine na popote ulimwenguni, na inasikitishwa na taarifa ya uzushi, upotoshaji na uzandiki iliyomnukuu mtu anayeitwa Shamila.

IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA DAR ES SALAAM
02 AGOSTI, 2014


Serikali ya Comoro ya kabidhi Eneo kwa Ubalozi Tanzania nchini humo

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Commoro, Mhe. Chabaka F. Kilumanga (katikati) akionyesha funguo aliyokabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe El-Anrif Said Hassane (ikiwa) ni ishara ya kukabidhiwa eneo lililotolewa na Serikali ya Comoro kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaajili ya Ujenzi wa Ubalozi wa Tanzania mijini Moroni
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Chabaka F. Kilumanga (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa visiwa vya Comoro Mhe. El-Anrif Said Hassane.


Waziri wa mambo ya Nje wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. El-Anrif Said Hassane amekabidhi rasmi eneo lililotolewa na Serikali ya Comoro kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwaajili ya Ujenzi wa Ubalozi wa Tanzania Mjini Moroni.

Hafla ya makabidhiano hayo yamefanyika Wizara ya Mambo ya Nje ya Comoro ambapo Mhe. Waziri El-Anrif amemkabidhi Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Chabaka F. Kilumanga funguo zamajengo matatu yaliyopo katika eneo hilo. Tukio hilo limeshuhudiwa pia na Mhe Ahamada El-Badaoui Mohamed Fakih, Balozi wa  Comoro nchini Tanzania.

Sambamba na kukabidhiana eneo hilo, Mhe. Balozi Kilumanga na Mhe. Waziri El-Anrif walipata fursa ya kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Comoro kwa maslahi ya pande zote mbili. 

Friday, August 1, 2014

Mkurugenzi wa Habari atembelea Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali Wizara ya Mambo ya Nje

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Bw. Assah Mwambene akizungumza na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mkumbwa Ally alipotembelea Kitengo hicho kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika.
Bw. Mwambene akiangalia moja ya machapisho aliyopatiwa na Bw. Mkumbwa kuhusu Wizara.


Picha na Reginald Philip

Monday, July 28, 2014

Watanzania waishio Comoro waandaa futari kwa kushirikiana na Ubalozi

Baadhi ya Watanzania wanaoishi Visiwani Comoro wakiwa katika picha ya pamoja na Bw. Ali Mwadini (wa pili kutoka kushoto), Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Comoro ambaye alimwakilisha Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga wakati wa  futari ya pamoja iliyoandaliwa na Watanzania hao kwa kushirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Moroni. 
Jumuiya ya Watanzania waishio Comoro wakipata futari ya pamoja.


 WATANZANIA WANAOISHI VISIWANI COMORO WAANDAA FUTARI YA PAMOJA KWA KUSHIRIKIANA NA UBALOZI

Jamii ya Watanzania wanaoishi Visiwani Comoro wameandaa futari ya pamoja, kwa kushirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mjini Moroni. Lengo la futari hiyo lilikuwa ni kuwakutanisha Watanzania wanaoishi Comoro, hususan katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili wajumuike pamoja. 

Wakizunguza wakati wa hafla hiyo, Watanzania hao walielezea kufurahishwa na kufarijika kwao kutokana na kitendo cha Serikali ya Tanzania kufungua Ubalozi nchini Comoro. Walieleza pia utayari wao wa kushirikiana na Ubalozi ili kuhamasisha maendeleo yao na ya nchi kwa ujumla.

Akizungumza katika halfa hiyo kwa niaba ya Mhe. Balozi Chabaka Kilumanga, Bw. Ali Mwadini wa Ubalozi wa Tanzania Moroni, aliwashukuru Watanzania hao kwa kupata wazo zuri la kuandaa futari na kuushirikisha Ubalozi.

Aidha, aliwasihi waendelee na umoja huo kwa kusaidiana na kuwa raia wema kwa kutii sheria za nchi wanapoishi. Aliwakumbusha pia kufika Ubalozini na kujisajili kwa wale ambao bado walikuwa hawajafanya hivyo. Vile vile, aliwahimiza kushiriki katika Kongamano la Watanzania Wanaoishi Ughaibuni linalotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 14 na 15 Agosti 2014.