Saturday, October 4, 2014

Mada mbalimbali za uelimishaji zawasilishwa kwenye Mkutano wa DICOTA

Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula akiwasilisha mada kuhusu Nafasi ya Ubalozi wa Tanzania katika kutoa Huduma kwa Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora). Katika mada hiyo Balozi Mulamula alizungumzia umuhimu wa mawasiliano kati ya Ubalozi na Diaspora na matumizi ya Teknolojia katika kurahisisha mawasiliano hayo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue katika meza kuu na Balozi Mulamula na wajumbe wengine waliohudhuria mkutano wa DICOTA akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Rosemary Jairo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akiwasilisha mada wakati wa Mkutano wa DICOTA kuhusu Nafasi ya Wizara katika kuwashirikisha Diaspora kuchangia Maendeleo ya Nchi".
Bi. Susan Mzee kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Diaspora akiwasilisha Mada kuhusu  Serikali katika kuwashirikisha Diaspora na nini kimefanyika hadi sasa.
Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Gesi Asili katika Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Norbert Kahyoza akiwasilisha Mada kuhusu Usimamizi wa Gesi katika kukuza Uchumi wa nchi wakati wa Mkutano wa DICOTA
Bi Jamila Ilomo kutoka Uhamiaji, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwasilisha mada kuhusu Uraia ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dkt. Mariam Ongara kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akiwasilisha mada kuhusu Hali ya sasa nchini kuhusu Afya ya kina Mama Wajawazito na Watoto wakati wa Mkutano wa DICOTA mjini Durham
Bw. Kofi Anani kutoka Benki ya Dunia nae akiwasilisha mada wakati wa Mkutano wa DICOTA.
Bi. Lulu Mengele, Afisa Mwandamizi kutoka Mfuko wa PPF akiwasilisha mada kuhusu Mfuko huo na umuhimu wake kwa Diaspora wakati wa mkutano wa DICOTA
Dkt. Joe Masawe kutoka Benki Kuu ya Tanzania akiwasilisha mada kuhusu Uchumi na umuhimu wa fedha zinazotumwa na Diaspora katika kuchangia uchumi wa nchi.
Bw. Dickson Ernest kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) akiwasilisha mada wakati wa mkutano wa DICOTA
Bw. Charles Singili kutoka Benki ya Azania nae akiwasilisha mada wakati wa mkutano wa DICOTA
Afisa kutoka EPZA, Bi. Grace Lemunge akiwasilisha mada kuhusu Fursa za Uwekezaji ndani ya EPZA wakati wa mkutano wa DICOTA.
Wajumbe wakifurahia jambo wakati wa mkutano wa DICOTA

Friday, October 3, 2014

Mkutano wa DICOTA wafunguliwa rasmi mjini Durham

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifungua rasmi Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA 2014) Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika Hoteli ya Millenium mjini Durham, North Carolina. Washiriki kwenye mkutano huo ni pamoja na Watanzania kutoka Majimbo mbalimbali ya Marekani, Wajumbe kutoka Serikalini na Sekta Binafsi na Serikali ya Marekani. Katika hotuba yake ya ufunguzi Balozi Sefue alilipongeza Baraza la DICOTA kwa juhudi na mafanikio mbalimbali na pia alisema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi hizo.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula (mwenye scarf) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo, Mwalimu Christopher Mwakasege na Wajumbe wengine wakimsikiliza Balozi Sefue (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa DICOTA 2014
Balozi Mulamula akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa DICOTA 2014


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Alphayo Kidata (wa kwanza kushoto) pamoja na wajumbe wengine akiwemoo Dkt. Joe Masawe (wa kwanza kulia) kutoka Benki Kuu ya Tanzania wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani)
Meya wa Mji wa Durham, Mhe. William Bell akiwakaribisha Wajumbe wa Mkutano wa DCOTA 2014 mjini hapo wakati wa sherehe za ufunguzi


Meya wa Durham Mhe. Bell akimkabidhi Balozi Sefue Cheti Maalum cha kuitambua DICOTA mjini Durham.
Rais wa DICOTA, Dkt. Ndaga Mwakabuta nae akikaribisha Wajumbe kwenye ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Mwaka wa DICOTA 2014
Wajumbe kwenye mkutano wakifuatilia matukio
Sehemu nyingine ya Wajumbe kwenye mkutano
Wajumbe wengine akiwemo Bi. Susan Mzee kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hafla ya ufunguzi
Wajumbe mbalimbali kwenye ufunguzi wa mkutano

Mkutano ukiendelea na wajumbe wakifuatilia
Sehemu ya Wajumbe wakijadiliana jambo
Wajumbe zaidi kutoka Tanzania wakifuatilia hafla ya ufunguzi
Balozi Sefue akishangiliwa na kina mama wa DICOTA waliokuwa wamevalia sare kumkaribisha kufungua mkutano wa DICOTA 2014
Balozi Sefue akizungumza na Meya wa Durham, Mhe. Bell
Kina mama wa DICOTA wakati wa shamrashamra za ufunguzi wa mkutano
Balozi Sefue, Balozi Mulamula, Mama Jairo, Mwalimu Mwakasege na Wajumbe wengine wakifurahia nyimbo kutoka kwa kina Mama wa DICOTA kabla hala ya ufunguzi haijaanza.
Kijana wa DICOTA, John Mmanywa akiimba kwa ufasaha kabisa Wimbo wa Taifa la Tanzania.

 ----------Matukio kabla ya ufunguzi wa Baraza la DICOTA

Balozi Sefue akipata maelezo kutoka kwa Mjumbe kutoka Benki ya CRDB kuhusu huduma yao ya Tanzanite Account maalum kwa Diaspora. Kulia ni Dkt. Sweetbert Mkama kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi Sefue akiendelea kupata maelezo katika meza za maonesho ya bidhaa mbalimbali kwa ajili ya Diaspora na nchi
Balozi Mulamula akisalimiana na Mwalimu Mwakasege huku Balozi Sefue akishuhudia.
Balozi Sefue katika picha ya pamoja na Mwalimu Mwakasege
Balozi Mulamula katika picha ya pamoja na Bibi Jairo

Zimbabwe yamzawadia Dola za Marekani 100,000.00 Brig. Jen. Hashim Mbita

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard K. Membe (Mb) (katikati) akikabidhi hundi yenye thamani ya Dola za Marekani laki moja kwa mtoto wa Brigedia Jen. Mstaafu Hashim Mbita, Bibi Shella Mbita. Bibi Mbita alipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Baba yake ambayo imetolewa na Rais wa Zimbabwe, Mhe. Robert Mugabe kutokana mchango mkubwa alioutoa Brig. Jen. Mbita katika harakati za ukombozi Kuisini mwa Afrika. Mwingine katika picha ni Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Edzai Chimonyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Tuzo iliyotolewa na Rais Mugabe kwa Brig. Jen. Hashim Mbita wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa SADC uliofanyika Victoria Falls nchini Zimbabwe mwezi Agosti 2014. Waziri Membe alieleza kuwa Rais Mugabe alitoa Tuzo ya Munhumutapa kwa Brig. Jen Hashim Mbita kutokana na mchango wake mkubwa katika harakati za kutafuta uhuru Kusini mwa Afrika. Brig. Jen. Mbita anakuwa mtu wa kwanza sio Mkuu wa Nchi kutunukiwa Tuzo hiyo ambayo kwa kawaida hutukiwa Wakuu wa Nchi pekee. Wengine katika picha ni Balozi wa Zimbawe nchini Tanzania na binti yake Brig. Jen. Mbita, Bibi Shella. 
Bibi Shella akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Zimbabwe kutokana na zawadi ya Dola 100,000.00 kwa Baba yake mzazi
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Shiyo Innocent (tai nyekundu) na Afisa wa Ubalozi wa Zimbabwe nchini Tanzania wakifuatilia kwa makini mkutano wa waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakiwa kazini.



Picha na Reginald Philip

Balozi Mbelwa kairuki afanya mazungumzo na Balozi wa China nchini

Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki (Kulia) kulia akimsikiliza Balozi wa China nchini Lu Youqing alipokutana nae na kufanya mazungumzo juu ya mahusiano juu kati ya Tanzania na China
Wakwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga, wakwanza kulia ni Bw. Imani Njalikai afisa Mambo ya Nje na wapili kutoka kulia ni Bw. Medadi Ngaiza afisa Mambo ya Nje wakinukuu mazungumzo hayo.
Maafisa kutoka Ubalozi wa China nchini walioambatana na Balozi Lu Youqing
Mazungumzo yakiendelea.


Picha na Reginald Philip

Taarifa kwa vyombo vya Habari




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bwana Samwel William Shelukindo  kuwa Balozi na pia kuwa Msaidizi wa Rais (Diplomasia).

Kabla ya uteuzi huu, Bwana Samwel William Shelukindo alikuwa Mkuu wa Utawala kwenye Ubalozi wa Tanzania Mjini Addis Ababa Ethiopia.

Uteuzi huu unaanza tarehe 01 Oktoba, 2014.

“Mwisho”

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
02 Oktoba, 2014

Balozi Sefue kufungua rasmi Mkutano wa Baraza la DICOTA

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula  na Viongozi wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA) (hawapo pichani) mara baada ya kukutana nao Hotelini kwake kwa ajili ya kupata taarifa za maandalizi ya Mkutano wa Mwaka wa Baraza hilo atakaoufungua leo tarehe 03 Oktoba, 2014 mjini Durham, North Carolina.

Balozi Mulamula, Viongozi wa DICOTA pamoja na Maafisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakimsikiliza Balozi Sefue (hayupo pichani)


Mkutano wa Tano wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA 2014) kuanza rasmi mjini Durham
============================================

Na Mwandishi Wetu, Durham

Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA 2014) utafunguliwa rasmi na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue tarehe 03 Oktoba, 2014 mjini Durham nchini Marekani.

Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Kuwawezesha Watanzania waishio ughaibuni (Diasporas) kufikia Mabadiliko ya Kiuchumi na Kijamii Kule Waliko  na Nyumbani”.

Mkutano huu ambao utahudhuriwa na Watanzania kutoka Majimbo yote ya Marekani, Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Kimarekani, unalenga kuwakutanisha wadau hao na wajumbe kutoka Serikalini, Taasisi za Umma na Sekta Binafsi ili kubadilishana mawazo na uzoefu na kuangalia namna bora ya kutumia fursa na rasilimali zilizopo katika kukuza uchumi na kupata maendeleo endelevu ya Jumuiya hiyo ya Diaspora na Taifa kwa ujumla.

Wakati wa Mkutano huu mada mbalimbali za ueleimishaji zitatolewa  kwa lengo la kueleza kwa kina fursa mbalimbali za uwekezaji, biashara na utalii zilizopo nchini. Mada hizo ni pamoja na Uhamiaji na Uraia, Mchakato wa Katiba mpya, Vitambulisho vya Uraia kwa Dispora, Mifuko ya Hifadhi za Jamii na Pensheni, masuala ya Ardhi na Nyumba, umuhimu wa Bandari ya Dar es Salaam kwa Diaspora, Usajili wa Makampuni na upatikanaji wa Leseni za Biashara kwa Diaspora, masuala ya Kodi, Masoko ya Mitaji na Hisa, masuala ya Nishati ya Mafuta na Gesi, Bima, Uwekezaji katika Kilimo na mada kuhusu Uchumi na Fedha zinazotumwa kutoka nje na Diaspora (Remittances).
Baraza la DICOTA lilianzishwa rasmi mwaka 2008 na kikundi cha watu 30 wakiwa na lengo la kushirikiana na Serikali na Sekta Binafsi katika kuleta maendeleo endelevu kwa kutumia ujuzi, elimu, maarifa na mitaji waliyoipata wakiwa ughaibuni. Baraza hilo linaongozwa na Dkt. Ndaga Mwakabuta na Katibu wake ni Bi. Lyungai Mbilinyi.

Mkutano wa kwanza wa DICOTA ulifanyika mwaka 2009 mjini Houston, Texas ukifuatiwa na ule wa mwaka 2010 uliofanyika mjini Minneapolis, Minnesota. Mkutano wa Tatu ulifanyika mwaka 2011 mjini Dulles, Virginia ukifuatiwa na mkutano wa mwaka 2012 uliofanyika Chicago, Illinois.

Mbali na Balozi Sefue, Viongozi Waandamizi wengine kutoka Serikalini wanaohudhuria mkutano huu ni pamoja na Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Bw. Alphayo Kidata, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi Rosemary Jairo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bi. Susan Mzee, Mshauri wa masula ya Diaspora kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.

-mwisho-