Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimtaifa, Mhe. Bernard Membe (Mb.) akisoma Hotuba ya kuwaaga Mawaziri wenzake katika mkutano wa Mawaziri wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. |
Saturday, June 13, 2015
Waziri Membe awaaga Mawaziri wa nchin wanachama wa Umoja wa Afrika
Friday, June 12, 2015
Watanzania wengine 13 warejea kutoka nchini Yemen
Kiongozi wa msafara wa Watanzania kumi na tatu waliorejea leo nchini wakitokea nchini Yemeni, Bw.Faiz Abdulsheikh Said akizungumza na Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi.Asha Mkuja wakati wa mapokezi ya Watanzania hao walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Shirika la Ndege la Qatar. Serikali imefanikiwa kuwarejesha nchini zaidi ya Watanzania 100 kutoka Yemen baada ya nchi hiyo kukumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe. Zoezi la kuwarejesha Watanzania hao linaratibiwa na kusimamiwa na Wizara kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Oman. Watanzania wengine 15 wanatarajiwa kuwasili nchini kesho tarehe 13 Juni, 2015.
Bi. Asha Mkuja akiendelea kupata maelezo kutoka kwa mmoja wa Watanzania hao Mzee Bader Saleh Omar kuhusu hali ilivyo nchini Yemen.
Mazungumzo yakiendelea
Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi.Asha akimsikiliza kwa makini mzee Bader, akimpa maelezo ya hali ilivyo huko Nchini Yemen.
Watanzania hao wakijiandaa kuondoka ndani ya Uwanja wa Ndege baada ya kukamilisha taratibu zote.
Picha na Reuben Mchome
Picha na Reuben Mchome
Wednesday, June 10, 2015
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje aongoza maadhimisho ya siku ya Taifa la Sweden
Mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Taifa la Sweden, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi wa Sweden hapa nchini. Mhe. Lennarth Hjelmaker (hayupo pichani).
Balozi wa Sweden hapa nchini, Mhe.Balozi Lennarth Hjelmaker akifungua hafla hiyo iliyofanyika usiku wa tarehe 09/06/2015 katika Makazi ya Balozi huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
Balozi Lennarth akimkaribisha Balozi Mulamula katika hafla hiyo.
Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Filberto Cerian Sebregondi akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula huku Afisa wa Wizara hiyo Bi.Asha Mkuja (kushoto mwenye kilemba).
Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini Mhe.Balozi Juma Halifan Mpango akisalimiana na Balozi Liberata Mulamula.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Balozi Mulamula (hayupo pichani)
Katibu Mkuu Mulamula akiendelea na hotuba yake,kushoto ni Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe.Lennarth
Balozi Lennarth na Katibu Mkuu Balozi Mulamula pamoja na wageni waalikwa wakinyanyua glasi kutakiana kheri katika ushirikiano wa nchi hizi mbili.
Balozi wa Sweden Mhe.Lennarth akicheza kwa furaha pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi huo hapa nchini kama ishara ya kufurahia maadhimisho ya siku ya Taifa lao la Sweden sherehe zilizofanyika katika makazi ya balozi huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha watoto wa Maafisa wa Ubalozi wa Sweden hapa nchini walioshiriki hafla hiyo kwa wakiimba kwa ufasaha nyimbo za Mataifa ya Sweden na Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waandishi wa abari katika hafla hiyo.
===================
Picha na Reuben Mchome.
Tuesday, June 9, 2015
Balozi Mulamula akutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa EU hapa nchini
Maafisa Mambo ya Nje Waandamizi wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Sebregondi (hawapo pichani). |
Balozi Mulamula na Balozi Sebregondi wakimsikiliza Balozi Melrose akifafanua jambo |
Kikao kikiendelea
Picha na Reginald Philip
|
Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje azungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress pamoja na ujumbe ulioambatana na Mhe. Thomas - Greenfield nao wakifuatilia mazungumzo. |
Balozi Linda akitoa ufafanuzi wa jambo huku Balozi Mulamula akimsikiliza kwa makini. |
Balozi Mulamula (katikati) akimsikiliza Mhe. Linda alipokuwa akizungumza naye kulia ni Afisa Mambo ya Nje Bwa. Lucas Mayenga. |
Picha na Reginald Philip.
Monday, June 8, 2015
Balozi wa China amtembelea Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu Youquig alipomtembelea Wizarani kwa mazungumzo ya kudumisha ushirikiano wa nchi hizi mbili.
Mkalimani wa Balozi wa China Bi.Wang Fang akisalimiana na Katibu Mkuu
Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu Youqing akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula.
Katibu Mkuu, Balozi Mulamula akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa China huku Maafisa wa pande zote mbili wakinukuu kile kinachozungumzwa.
Balozi wa China, Mhe.Lu akifurahia jambo na Balozi Mulamula
Balozi Lu Youqing akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Maafisa kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Mr.Dong (kulia), Mr.Lin Liang (katikati) na Bi.Wang Fang wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Lu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw.Nathaniel Kaaya (wa kwanza kushoto) kwa pamoja na Maafisa Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza (wa kwanza kulia) pamoja na Bi.Ramla Hamis wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Lu (hawapo pichani).
Picha na Reuben Mchome
Friday, June 5, 2015
Tanzania yachaguliwa Mjumbe Baraza la Shirika la Hali ya Hewa Duniani
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (mwenye suti nyeusi) akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano Mkuu wa 17 wa Shririka la Hali ya Hewa Duniani unaofanyika Mjini Geneva, Uswisi. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Celestine Mushy (Kulia) =================================== |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TANZANIA YACHAGULIWA KUWA MJUMBE KATIKA BARAZA LA UTENDAJI (EXECUTIVE COUNCIL) LA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI–WORLD METEOROLOGICAL ORGANIZATION (WMO).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi, amechaguliwa kuwa Mjumbe katika Baraza la Utendaji (Executive Council) la Shirika la Hali ya Hewa Duniani–World Meteorological Organization (WMO) kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2015 hadi 2019. Dr. Kijazi amechaguliwa tarehe 4 June 2015 wakati wa Mkutano Mkuu wa Kumi na Saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO-Congress wa 17) ulioanza tarehe 25 Mei 2015 na unatarajiwa kumalizika tarehe 12 Juni, 2015 Jijini Geneva, Uswisi.
Kuchaguliwa kwa Dr. Agnes Kijazi kumetokana na jitihada zilizofanywa na Ubalozi wetu wa Kudumu Umoja wa Mataifa wa Geneva na Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambazo kwa pamoja zilisimamia zoezi la kuomba kura kutoka kwa wanachama na kampeni wakati wa uchaguzi.
Dr. Kijazi ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika ushiriki Mkutano huo ambao una washiriki kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Maji na Ubalozi wa Tanzania Nchini Uswisi.
WMO ni Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya hali ya hewa duniani na mabadiliko ya tabianchi. WMO inatekeleza majukumu na maamuzi kuhusu maendeleo ya sayansi ya hali ya hewa na uboreshaji wake ikiwa ni pamoja na kusimamia viwango katika upimaji na utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa nchi wanachama.
Hadi wakati wa Mkutano huu huko nchini Uswisi, WMO ilikuwa na nchi wanachama 191. Katika Mkutano huu nchi za Sudan Kusini na Tuvalu zilikaribishwa rasmi kama wanachama wapya wa WMO. Kati ya nchi hizi 191 ni nchi 37 tu ambazo zina wajumbe katika Baraza hilo kuu. Hivyo hii ni nafasi adhimu na heshima kwa Tanzania, TMA na Dr Kijazi ambaye ni msomi mwenye utaalamu wa kutosha akiwa na Shahada ya Uzamivu (Ph.D) katika Sayansi ya Hali ya hewa.
Kazi kuu ya Baraza la Utendaji la WMO, ambalo Tanzania imefanikiwa kuwa mjumbe ni kuchukua hatua zinazostahili, kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa Shirika hilo kutekeleza maamuzi yanayotolewa na Mkutano Mkuu (WMO-Congress) ambao hukutana mara moja kila baada ya miaka minne.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alielezea sababu ya Tanzania kugombea nafasi hiyo muhimu kuwa ni pamoja na kuwa ndani ya chombo cha maamuzi na hivyo kushawishi maamuzi yatakayoinufaisha jamii nzima ya kimataifa ikiwemo Tanzania katika masuala ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kutoa mwelekeo wa kisayansi katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea katika maeneo mengi Duniani.
Kwa upande wake, Dkt. Kijazi alieleza kuridhishwa kwake na jinsi ambavyo nchi wanachama 190 walivyoridhishwa na utendaji wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu (2012-2015) ambacho alikuwa mjumbe wa Baraza hili na hivyo kumchagua tena katika kipindi kingine cha miaka minne. “Hii ni heshima kubwa kwa nchi yangu ya Tanzania na ninaahidi kutumia uwezo wangu wote kutekeleza majukumu ya nafasi hii” alisema Dkt. Kijazi.
Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam
05 Juni, 2015
Thursday, June 4, 2015
Balozi wa China Nchini amtembelea Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akimsikiliza Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu Youqing alipomtembelea Wizarani leo.
Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Lu akifurahia jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nje Balozi Simba huku Maofisa wa Ubalozi wa China waliofuatana na Balozi wakifuatilia mazungumzo hayo.
Balozi Simba akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea huku Maofisa wa Ubalozi wa China hapa nchini wakiendelea kunukuu kile kinachozungumzwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Asia na Australasia Bw.Nathaniel Kaaya (wa pili kushoto) akifuatilia mazungumzo hayo huku Maofisa Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza (wa kwanza kulia) pamoja na Bi.Ramla Hamis wakiendelea kunukuu kile kinachozungumzwa.
Mkutano ukiendelea
Monday, June 1, 2015
Balozi Mulamula akabidhiwa rasmi Ofisi
Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akikabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi John Haule. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mulamula alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mhe. Haule kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya. Makabidhiano hayo yalifanyika Wizarani leo tarehe 01 Juni, 2015. |
Balozi Mulamula akizungumza huku Naibu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya, (kulia kwa Balozi Mulamula), Mhasibu Mkuu Bw. Paul Kabale (wa tatu kutoka kushoto), Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Mambo ya Nje, Bw. Mathias Abisai na Afisa Habari wa Mambo ya Nje Bw. Ally Kondo |
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Nigel Msangi (wa kwanza kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango Bw. James Lugaganya na Balozi Haule wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani) |
Katibu Mkuu, Balozi Mulamula akiwa kwenye Mkutano na baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo mara baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Balozi Haule. |
Picha na Reginald Philip
Subscribe to:
Posts (Atom)