Thursday, November 5, 2015

Marais 7 wawasili asubuhi ya leo kuwahi uapisho wa Dkt. Magufuli


Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame (kulia) akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kushiriki sherehe za uapisho wa Rais Mteule, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame akisindikizwa na Waziri wa Mambo ya Nje kwenda kukagua gwaride.
Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame akikagua gwaride.
Mhe. Paul Kagame akikangalia kikundi cha wapiga tarumbeta
========================
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn (kulia) akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Bernard Membe alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kushiriki sherehe za uapisho za Rais Mteule, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Waziri Mkuu wa Ethiopia akikagua gwaride

===========================
Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kushuhudia sherehe za uapisho wa Rais Mteule, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Nyusi akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Mhe. Shamimu Nyanduga.
Rais Nyusi akikagua gwaride

================================
Rais wa Zambia, Mhe. Edger Lungu akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kushuhudia sherehe za uapisho wa Rais Mteule, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mhe. Lungu akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace Mujuma.
Rais wa Zambia akifurahia kikundi cha tarumbeta.

==========================
Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kushuhudia sherehe za uapisho wa Rais Mteule, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Kenya akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule.

===========================
Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kushuhudia sherehe za uapisho wa Rais Mteule, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mhe. Museveni akisalimiana na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Ngusekera Nyerere.
Rais Museveni akikagua gwaride.


Picha na Reginald Philip

Viongozi mbalimbali waendelea kuwasili kwaajili ya sherehe za Uapisho wa Rais Mteule

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (kushoto) akimpokea Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma (anayeshuka kwenye ngazi), Rais Zuma amewasili nchini kwaajili ya kuudhuria sherehe za uapisho wa Rais Mteule Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli zitakazofanyika hapo kesho katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam  
Waziri Membe akisalimiana na Rais Zuma
Rais Zuma akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Radhia Msuya (wa kwanza kulia).
Rais Zuma akitizama kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitoa burudani.
Balozi wa Tanzania nchini UAE Mhe. Mbarouk Nassoro Mbarouk (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii UAE.
Afisa Mambo ya Nje Bw. Hangi Mgaka naye akisalimiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii UAE

Picha na Reginald Philip.

Wednesday, November 4, 2015

Viongozi wawasili nchini Kushuhudia Uapisho wa Rais Mteule Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe (katikati chini) akimsubiria Rais wa Zimbabwe Mhe. Robert Mugabe (katikati juu kwenye ngazi) alipokuwa akiteremka kwenye Ndege, Rais Mugabe amewasili nchini kwaajili ya kuhudhuria Sherehe za uapisho wa Rais Mteule Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli zitakazofanyika hapo kesho katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 Waziri Membe akimpokea Rais Mugabe (mwenye Ua Mkononi) mara tu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mambo ya Nje Bi. Liliani Kimaro akisalimiana na Rais Mugabe.
 Rais Mugabe akikagua Gwaride la Heshima.
Rais Mugabe akiangalia kikundi cha wapiga Tarumbeta huku Waziri Membe akitoa ufafanuzi wa nyimbi iliyokuwa inachezwa.  


===============================

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (kushoto) akimlaki Naibu Waziri Mkuu wa Namibia Mhe. Netumbo Nandi - Ndaitwah mara baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kushuhudia Uapisho wa Rais Mteule Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Mhe. Netumbo Nandi - Ndaitwah (wa pili kutoka kulia) akifurahia kikundi cha ngoma kilichopo mbele yao.


================================

Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini pia anayeiwakilisha Tanzania nchini Botswana Mhe. Radhia Msuya (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Botswana Mhe. Olale Eric Mothibi alipo wasili nchini kwaajili ya kushiriki Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.


Picha na Reginald Philip

Katibu Mkuu akutana kwa mazungumzo na Msajili wa ICTR

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kulia), akisalimiana na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda  (ICTR), Bw. Bongani C. Majola (kushoto) alipofika Wizarani kwa mazungumzo kuhusu utendaji wa Mahakama hiyo iliyopo Jijini Arusha. 

Bw. Majola akimweleza Balozi Mulamula majukumu na namna wanavyoendesha kesi katika mahakama hiyo .
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Baraka Luvanda ( kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mindi Kasiga ( kulia) na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Mustafa Makame (katikati) nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo yaliyo kuwa yakiendelea kati ya Balozi Mulamula na Bw. Majola (hawapo pichani).
Balozi Mulamula kwa pamoja na Bw. Majola wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo yao.
Mazungumzo yakiendelea


Picha ya Pamoja



Picha na Reginald Philip

Friday, October 30, 2015

BALOZI ZOKA AWASILISHA HATI ZA UWAKILISHI KWA MAKAMU WA RAIS WA CUBA

Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka pamoja na ujumbe wake wakiwasili katika Ikulu ya Makamu wa Rais ijulikanayo kama Revolutionary Palace.
Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka akikabidhi Hati za Uwakilishi kwa Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa katika Ikulu ijulikanayo kama Revolutionary Palace.
Mara baada ya kukabidhi hati, yalifuata mazungumzo ya pamoja kuhusu ushirikiano wa nchi za Tanzania na Cuba. Kutoka kushoto ni Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka, Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa, na maafisa wa Ikulu ya Cuba. 
Picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Makamu wa Rais wa Cuba, Mhe. Salvador Valdes Mesa, Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka na mshauri wa Makamu wa Rais wa Cuba.
Mhe. Balozi Jack Mugendi Zoka akiweka shada la maua katika eneo la kumbukumbu (memorial square) kwa heshima ya mwanamapindizu, Jose Marti, shujaa na mhasisis wa Cuba.
Picha ya kumbukumbu mara baada ya kuweka shada la maua. Kutoka kushoto ni askari wa Cuba mwenye mkumbulu, Balozi wa Tanzania Ottawa-Canada na Mwakilishi nchini Cuba, Mhe. Jack Mugendi Zoka, Mama Balozi, Esther Nyanzila Zoka, Afisa wa Mambo ya Nje, Bw. Paul James Makelele na mshauri wa Makamu wa Rais wa Cuba. Wa nyuma ni maaskari wa Cuba.

*******************************
Balozi wa Tanzania nchini Canada na Cuba Mhe. Jack Mugendi Zoka aliwasilisha Hati za Uwakilishi kwa Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Valdes Mesa katika Ikulu ya nchi hiyo ijulikanayo kama ´Revolutionary Palace´. 

Mhe. Balozi aliambatana na Mama Balozi Bibi Esther Zoka na Afisa wa Ubalozi Bw. Paul Makelele. Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Cuba, Mhe. Balozi Miguel Lamazares Puello na Maafisa wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na ofisi ya Makamu wa Rais.
Baada ya zoezi hilo, Mhe. Balozi Zoka alipata fursa ya kuwa na mazungumzo na Mhe. Makamu wa Rais.
Baada ya zoezi la kuwasilisha Hati na mazungumzo, Balozi alitembelea eneo la kumbukumbu - Memorial Square ijulikanayo kama Jose Marti ambapo aliweka Shada la Maua, kutembezwa na kupewa maelezo ya historia kuhusu ukombozi wa nchi hiyo inayomtambua Jose Marti kama shujaa na muasisi wa ukombozi wa Cuba.

APOKEA UONGOZI WA KILIMANJARO FC UBALOZINI NA KUKUBALI KUWA MLEZI WA TIMU HIYO

Mhe. Balozi Dora Msechu ameupokea Ubalozini  Ujumbe wa timu maarufu  ya soka ya watanzania waishio Sweden,  Kilimanjaro FC, ambao walikuja kumkabidhi Mhe. Balozi makombe waliyoshinda kwenye mashindano mbalimbali hapa Sweden. Mhe. Balozi Dora Msechu ameipongeza na kuishukuru Kilimanjaro FC kwa kuiwakilisha vyema nchi yetu kwenue fani ya michezo hapa Sweden na kuwahamasisha waongezee bidii zaidi na wasibweteke na mafanikio wanayoyapata.

Aidha, Mhe. Balozi Dora Msechu amekubali ombi la Kilimanjaro FC la kuwa Mlezi wa timu hiyo na kuahidi ushirikiano wake pale itakapowezekana.


BALOZI DORA MSECHU ASHIRIKI KWENYE SHEREHE YA MIAKA 10 YA JUMUIYA YA WATANZANIA JIMBO LA FYN, DENMARK

Balozi Dora Msechu  amekutana na watanzania wanaoishi kwenye Jimbo la Fyn nchini Denmark na kuwapongeza kwa kutimiza miaka 10 ya Umoja wao. na kuwashukuru kwa mchango mkubwa wanaotoa kwenye maendeleo ya nchi yetu. Amewaasa waendeleze mshikamano wao na kuwahakikishia kuwa  milango ya Ubalozi ipo wazi katika kuwahudumia na kushirikiana kwa  karibu na watanzania wote wanaoishi kwenye nchi za Nordic na Baltic.

Sherehe hiyo iliandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Jimbo la Fyn kwa kushirikiana na familia ya Bibi Dorthe Nielsen, rafiki mkubwa wa Tanzania na mtoto wa aliyekuwa Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Denmark, marehemu Robert Andersson.





Katibu Mkuu akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Sudan nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Sudan hapa nchini, Mhe. Dkt. Yasir Mohammed Ali alipofika Wizarani kwa mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Sudan. 
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Samwel Shelukindo (kushoto) akifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Ali (hawapo pichani). Kulia ni Afisa Mambo ya Nje. 
Balozi Ali nae akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Balozi Mulamula
Mazungumzo yakiendelea
Balozi Mulamula akiagana na  Balozi Ali mara baada ya kumaliza mazungumzo baina yao.